Mwigulu Nchemba - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 04 Jun 2024 18:44:21 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Mwigulu Nchemba - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mwigulu aipongeza Yanga bungeni https://www.greensports.co.tz/2024/06/04/mwigulu-aipongeza-yanga-bungeni/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/04/mwigulu-aipongeza-yanga-bungeni/#respond Tue, 04 Jun 2024 18:44:18 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11222 Na mwandishi wetuWaziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (pichani) ameipongeza Yanga SC bungeni baada ya timu hiyo kufanikiwa kubeba Kombe la Shirikisho la CRDB.Pongezi hizo amezitoa leo Jumanne mjini Dodoma wakati wa vikao vya Bunge la Bajeti vikiendelea huku akieleza kuwa Yanga imejua kuwapa raha wafuasi wa timu hiyo.“Mheshimiwa Spika nashukuru kwa kunipa fursa hii lakini […]

The post Mwigulu aipongeza Yanga bungeni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (pichani) ameipongeza Yanga SC bungeni baada ya timu hiyo kufanikiwa kubeba Kombe la Shirikisho la CRDB.
Pongezi hizo amezitoa leo Jumanne mjini Dodoma wakati wa vikao vya Bunge la Bajeti vikiendelea huku akieleza kuwa Yanga imejua kuwapa raha wafuasi wa timu hiyo.
“Mheshimiwa Spika nashukuru kwa kunipa fursa hii lakini kabla sijaendelea ningependa nianze kwa kuipongeza sana timu ya Yanga kwa kupata makombe yote ikiwa imeongeza kombe jingine Jumapili. Yanga wamejua kutupa raha mwaka huu,” alisema Nchemba.
Yanga imetwaa taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuifunga Azam FC kwa penalti 6-5 baada ya suluhu ya dakika 120 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Yanga ambayo awali ilitolewa kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, pia imefanikiwa kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu NBC, ikitwaa kwa mara ya tatu mfululizo ukiwa ni ubingwa wao wa 30 wa ligi hiyo.

The post Mwigulu aipongeza Yanga bungeni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/04/mwigulu-aipongeza-yanga-bungeni/feed/ 0