MwanaFA - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 21 May 2024 19:30:33 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg MwanaFA - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Viwanja vya Afcon kukamilika mwakani https://www.greensports.co.tz/2024/05/21/viwanja-vya-afcon-kukamilika-mwakani/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/21/viwanja-vya-afcon-kukamilika-mwakani/#respond Tue, 21 May 2024 19:30:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11060 Na mwandishi wetuSerikali ya Tanzania imesema ujenzi wa viwanja vipya vya michezo kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2027), unatarajiwa kukamilika mwakani ili kupisha ukaguzi wa kikanuni wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf).Hayo yameelezwa kutokana na uandaaji wa michuano hiyo kupitia nchi tatu za Tanzania, Kenya na Uganda zilizoomba kushiriki […]

The post Viwanja vya Afcon kukamilika mwakani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Serikali ya Tanzania imesema ujenzi wa viwanja vipya vya michezo kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2027), unatarajiwa kukamilika mwakani ili kupisha ukaguzi wa kikanuni wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf).
Hayo yameelezwa kutokana na uandaaji wa michuano hiyo kupitia nchi tatu za Tanzania, Kenya na Uganda zilizoomba kushiriki kwa kuandaa kwa pamoja michuano hiyo mikubwa Afrika ikiwa pia ni mara ya kwanza nchi hizo zinafanya hivyo.
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwijuma amefafanua kuhusiana hilo leo Jumanne wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Chakechake, Ramadhan Suleiman Ramadhan.
Mbunge huyo alihoji ni lini viwanja vipya ambavyo Serikali inatarajia kujenga kwa ajili ya matayarisho ya Afcon vitakamilika.
Akijibu swali hilo, Mwijuma alisema kwa mujibu wa ratiba na mahitaji, viwanja hivyo vinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka ujao na kwamba wanafanya hivyo ikiwa ni tayari kwa ajili ya ukaguzi wa kikanuni ambao utafanyika mwakani.
Mpaka sasa Tanzania inatarajia kutumia viwanja vitatu katika michuano hiyo ambavyo ni Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa New Amaan Complex wa Zanzibar na uwanja mpya wa kisasa unaojengwa jijini Arusha.

The post Viwanja vya Afcon kukamilika mwakani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/21/viwanja-vya-afcon-kukamilika-mwakani/feed/ 0
Serikali kuunda timu tatu za soka https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/serikali-kuunda-timu-tatu-za-soka/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/serikali-kuunda-timu-tatu-za-soka/#respond Wed, 01 May 2024 19:14:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10797 Na mwandishi wetuSerikali kupitia Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo ina mpango wa kuunda timu tatu imara za soka za taifa kulingana na umri ambazo zitashiriki fainali za Afcon 2027 na michuano mengine ambayo nchi itashiriki.Naibu Waziri wa wizara hiyo, Hamisi Mwinjuma ‘MwanaFA’ amesema hayo Jumatatu hii wakati akijibu maswali ya nyongeza ya Mbunge wa […]

The post Serikali kuunda timu tatu za soka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Serikali kupitia Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo ina mpango wa kuunda timu tatu imara za soka za taifa kulingana na umri ambazo zitashiriki fainali za Afcon 2027 na michuano mengine ambayo nchi itashiriki.
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Hamisi Mwinjuma ‘MwanaFA’ amesema hayo Jumatatu hii wakati akijibu maswali ya nyongeza ya Mbunge wa Jimbo la Magomeni, Mwanakhamisi Kassim Said (CCM).
Mbunge huyo alitaka kujua mkakati wa Serikali kuandaa timu ya Taifa ili ishindane kwenye michuano ya Afcon.
Katika ufafanuzi wake, Waziri Mwinjuma alisema Serikali imeandaa mkakati wa kuandaa timu si tu kwa ajili ya Afcon 2027, bali kwa mashindano mengine ambayo Tanzania itashiriki na zitagharamiwa na Serikali kwa asilimia 100.
Alisema miongoni mwa mkakati huo ni kutengeneza timu tatu za Taifa zitakazopishana umri. Ya kwanza itakuwa ni ya vijana chini ya miaka 17, itakayotokana na wanafunzi kupitia michezo ya Umiseta ya kila mwaka inayoshirikisha shule za sekondari.

“Tukishawapata wachezaji hawa tutawaweka kwenye shule moja ambayo tumeshaiteua na watasimamiwa na walimu magwiji. Itapata mechi za mazoezi ya kutosha za ndani na nje. Kila mwaka wachezaji hao tutakuwa tunawapeleka kwenye akademi zenye mafanikio nje ya nchi ili kuendeleza vipaji tayari kulitumikia Taifa,” alisema.


Alisema timu ya pili itakuwa inaundwa na vijana wa umri wa chini ya miaka 23 ambao wanacheza ligi mbalimbali ndani na nje ya nchi na watakuwa wakikutana wakati wakiwa kwenye mapumziko ya timu zao.
Alisema pia ili kuhakikisha timu ya Taifa inafanya vizuri katika mashindano hayo, Serikali imeweka mikakati mbalimbali ikiwemo ujenzi wa viwanja vya mpira katika majiji ya Dodoma na Arusha pia utafanyika ukarabati wa Viwanja vya Benjamin Mkapa na Uhuru vilivyopo Dar es Salaam.
Sambamba na hilo, serikali pia itakuwa ikiwatafuta na kuwaleta nchini wachezaji wenye asili ya Tanzania wanaoishi na kucheza nje ya nchi ili kuchezea timu ya Taifa.

The post Serikali kuunda timu tatu za soka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/serikali-kuunda-timu-tatu-za-soka/feed/ 0
MwanaFA aipa Simba ushindi kwa Asec https://www.greensports.co.tz/2023/12/21/mwanafa-aipa-simba-ushindi-kwa-asec/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/21/mwanafa-aipa-simba-ushindi-kwa-asec/#respond Thu, 21 Dec 2023 04:53:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8955 Na mwandishi wetuNaibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma ‘MwanaFA’ amesema anaamini kiwango ilichonacho Simba kwa sasa, itaifunga Asec Mimosas kwenye mchezo unaofuata wa Ligi ya Mabingwa Afrika.MwanaFA ameyasema hayo baada ya Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wydad AC, Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam na kupata ushindi wao […]

The post MwanaFA aipa Simba ushindi kwa Asec first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma ‘MwanaFA’ amesema anaamini kiwango ilichonacho Simba kwa sasa, itaifunga Asec Mimosas kwenye mchezo unaofuata wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
MwanaFA ameyasema hayo baada ya Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wydad AC, Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam na kupata ushindi wao wa kwanza wa hatua ya makundi ya michuano hiyo baada ya mechi nne.
Alisema sehemu iliyokuwa ngumu kupata ushindi kwa Simba ugenini ilikuwa ni Morocco dhidi ya Wydad ambapo Simba ilifungwa bao 1-0 lakini anaamini nchini Ivory Coast itakuwa rahisi dhidi ya Asec.
“Kiwango kikibaki hivihivi naamini Simba itapata alama tatu, mahali pagumu kupata alama tatu palikuwa Wydad, Morocco kule na ilikuwa chupuchupu ipatikane angalau moja ila tu mpira una matokeo yake na chochote kinatokea.

“Lakini sina wasiwasi kabisa na kiwango cha Simba dhidi ya Asec, naamini pointi tatu zitachukuliwa tu kulekule ugenini,” alisema Mwinjuma ambaye pia ni shabiki mkubwa wa Wekundu hao.


Simba inatarajia kukutana na upinzani mkubwa katika mchezo huo utakaopigwa Februari 23, mwaka huu kutokana na rekodi ya Asec ya kutopoteza mechi yoyote ya nyumbani katika michuano hiyo msimu huu mpaka sasa.
Katika Kundi B, Asec inaongoza kwa pointi 10, Simba ya pili ikiwa na pointi tano wakati Jwaneng Galaxy ya Botswana ni ya tatu kwa pointi nne na Wydad inaburuza mkia ikiwa na pointi tatu.

The post MwanaFA aipa Simba ushindi kwa Asec first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/21/mwanafa-aipa-simba-ushindi-kwa-asec/feed/ 0
MwanaFA aipa neno Pazi https://www.greensports.co.tz/2023/10/26/mwanafa-aipa-neno-pazi/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/26/mwanafa-aipa-neno-pazi/#respond Thu, 26 Oct 2023 20:18:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8244 Na mwandishi wetuNaibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ ameihimiza klabu ya mpira wa kikapu ya Pazi kujitahidi katika michuano ya Afrika kwa kufanya vizuri ikijua wazi kuwa imebeba jukumu la kitaifa.Pazi imefuzu kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Kikapu Afrika itakayofanyika Afrika Kusini kuanzia Novemba 14 hadi 19, mwaka huu baada ya […]

The post MwanaFA aipa neno Pazi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ ameihimiza klabu ya mpira wa kikapu ya Pazi kujitahidi katika michuano ya Afrika kwa kufanya vizuri ikijua wazi kuwa imebeba jukumu la kitaifa.
Pazi imefuzu kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Kikapu Afrika itakayofanyika Afrika Kusini kuanzia Novemba 14 hadi 19, mwaka huu baada ya kufanya vizuri katika michezo ya Kanda ya Afrika Mashariki hivi karibuni.

“Nilihudhuria katika mashindano hivi karibuni na kuona Pazi inacheza kama timu, niwatie moyo waendelee kufanya hivyo, wafahamu wana bendera ya nchi, na sisi tuna sababu ya kuishabikia kwa sababu ni timu bora,” alisema MwanaFA.


Alisema kinachohitajika kwa sasa ni mashabiki wa kikapu kurudisha mioyo yao katika mchezo huo kwa kujitokeza pindi yanapokuwepo mashindano ili kuwatia hamasa wachezaji.
MwanaFA alisema wao kama serikali wana maagizo kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kujenga viwanja viwili vya ndani Dar es Salaam na Dodoma kwa ajili ya kutoa nafasi ya kuandaa mashindano makubwa.

The post MwanaFA aipa neno Pazi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/26/mwanafa-aipa-neno-pazi/feed/ 0
MwanaFA ataka Simba, Yanga wasaidiane https://www.greensports.co.tz/2023/09/12/mwanafa-ataka-simba-yanga-wasaidiane/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/12/mwanafa-ataka-simba-yanga-wasaidiane/#respond Tue, 12 Sep 2023 16:09:19 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7723 Na mwandishi wetuNaibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma ‘MwanaFA’ (pichani) ameziomba Simba na Yanga kusaidiana katika michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa manufaa ya taifa kwa ujumla.Akizungumza Dar es Salaam leo Jumanne kwenye uzinduzi wa Bodi ya Cosota na Bodi ya Filamu Tanzania, Mwinjuma alisema hata kama timu hizo zinashindwa kusaidiana kutokana […]

The post MwanaFA ataka Simba, Yanga wasaidiane first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma ‘MwanaFA’ (pichani) ameziomba Simba na Yanga kusaidiana katika michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa manufaa ya taifa kwa ujumla.
Akizungumza Dar es Salaam leo Jumanne kwenye uzinduzi wa Bodi ya Cosota na Bodi ya Filamu Tanzania, Mwinjuma alisema hata kama timu hizo zinashindwa kusaidiana kutokana na utamaduni wao basi wasihujumiane wala kuumizana.
Alisema amesikia malalamiko ya chini kwa chini kwamba timu hizo zinahujumiana akisema afadhali wafanyiane figisu katika michezo ya ndani lakini sio ya nje kwa kuwa wote wanakwenda kuwakilisha nchi, hivyo wanatamani kuona mafanikio yao.

“Tujue tunaenda kuwakilisha nchi hivyo kama kuna lolote linatokana na kuhujumiana liishe, sifikiri kama ni kitu sahihi kufanyiana hujuma hasa kwa timu za kimataifa,” alisema MwanaFA.


Naibu Waziri huyo alisema serikali inawategemea kufikia mafanikio ya juu zaidi ya walikotoka, wakajitahidi na kuzitakia kila la heri katika michezo yao itakayochezwa mwishoni mwa wiki hii.
Yanga inatarajia kuondoka keshokutwa kuelekea Rwanda kwa ajili ya mchezo wa raundi ya kwanza ya ligi hiyo dhidi ya Al Merreikh ya Sudan na Simba itacheza nchini Zambia dhidi ya Power Dynamos ya Zambia. Mechi zote zikitarajiwa kuchezwa Jumamosi hii.
Katika hatua hiyo, endapo timu hizo zitafanikiwa kuondoka na ushindi wa jumla, zitafuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

The post MwanaFA ataka Simba, Yanga wasaidiane first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/12/mwanafa-ataka-simba-yanga-wasaidiane/feed/ 0
MwanaFA mgeni rasmi, Simba-Vipers https://www.greensports.co.tz/2023/03/03/mwanafa-mgeni-rasmi-simba-vipers/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/03/mwanafa-mgeni-rasmi-simba-vipers/#respond Fri, 03 Mar 2023 12:51:17 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5379 Na mwandishi wetuUongozi wa Simba umemtangaza Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma ‘MwanaFA’ kuwa mgeni rasmi katika mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers ya Uganda.Simba imemtaja MwanaFA kuwa mgeni rasmi wa mechi hiyo itakayopigwa Jumanne ya wiki ijayo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, ikiwa ni siku chache tangu […]

The post MwanaFA mgeni rasmi, Simba-Vipers first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Uongozi wa Simba umemtangaza Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma ‘MwanaFA’ kuwa mgeni rasmi katika mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers ya Uganda.
Simba imemtaja MwanaFA kuwa mgeni rasmi wa mechi hiyo itakayopigwa Jumanne ya wiki ijayo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, ikiwa ni siku chache tangu ateuliwe katika wadhifa huo.
Akizungumza jjini Dar es Salaam leo Ahamisi, Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema sababu ya kumpendekeza kiongozi huyo ni mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo kwa Simba.
“Mgeni rasmi katika mchezo wetu dhidi ya Vipers, tumemwalika Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma aje kumuona Simba ikimpelekea moto Vipers, tunaamini atakuwa chachu ya ushindi katika mchezo huo,” alisema Ally.
Kuhusu maandalizi ya timu hiyo kuelekea mchezo huo, Ally ameeleza kuwa kikosi chao kimeingia kambini jana mchana na jioni kilitarajiwa kuanza mazoezi kujiandaa na mchezo huo ambao wameupa uzito mkubwa.
Alisema wanahitaji pointi tatu nyingine kama walivyofanya kwenye mechi ya awali iliyochezwa wiki iliyopita nchini Uganda na Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Ally alisema lengo lao ni kujiweka katika mazingira mazuri ya kutinga robo fainali kutoka kwenye Kundi C ambalo linaongozwa na Raja Casablanca ya Morocco.
“Tulikwenda kufufukia Uganda, na kweli tumefufuka. Jumanne ni mechi ya marudiano, katika mechi hii tunakwenda kuamua hatma ya Simba kwenye michuano ya CAF. tukimpiga tutafikisha pointi sita na kuanza kuchungulia robo fainali,” alisema Ally.
Kuhusu ujio wa Vipers, Ally alisema timu hiyo inayoburuza mkia kwenye msimamo wa kundi hilo, itawasili nchini Jumatatu asubuhi huku waamuzi watakaochezesha mchezo huo wanaotoka Ethiopia wakitarajiwa kutua nchini Jumapili mchana.
Ameeleza kuwa kuelekea mchezo huo wamebadilisha mfumo wa kutembelea maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuwahamasisha mashabiki wao kwenda uwanjani kuipa sapoti timu.
“Tumekuwa tukizunguka kwenye maeneo mbalimbali ya wazi tukiwa na kispika, kutangaza mechi yetu, mechi hii tumekuja na kitu cha tofauti na chenye mvuto zaidi, kinaitwa Wenye Nchi Beach Party ambayo tutaifanya Jumapili hii kwenye ufukwe wa Coco,” alisema.
“Mashabiki wote tutakutana pale na kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wengi na tiketi za mchezo huo zitauzwa siku hiyo,” alisema Ally.
Tiketi za mchezo huo zimeanza kuuzwa, Sh 3,000 kwa mzunguko, Sh 10,000 VIP C wakati Sh 20,000 ni VIP B huku Sh 30,000 ikiwa ni VIP A na Sh 150,000 kwa Platinum.
Sambamba na tiketi hizo, pia kutakuwa na tiketi za Simba Executive kwa ajili ya wateja wa Simba walio maofisini, faida zake ni kupata kibali cha kupelekwa uwanjani na basi na kukaa eneo maalumu na kupata huduma ya vinywaji baridi wakiwa uwanjani.

The post MwanaFA mgeni rasmi, Simba-Vipers first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/03/mwanafa-mgeni-rasmi-simba-vipers/feed/ 0
MwanaFA amshukuru Rais Samia https://www.greensports.co.tz/2023/03/01/mwanafa-amshukuru-rais-samia/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/01/mwanafa-amshukuru-rais-samia/#respond Wed, 01 Mar 2023 06:15:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5339 Na mwandishi wetuMbunge wa Muheza, Hamis Mwinjuma au MwanaFA amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuwataka wasanii na wanamichezo kufanya kazi kwa mikono yao.MwanaFA ambaye ni mwanamuziki mkongwe nchini ni miongoni mwa uteuzi uliotangazwa Jumapili hii na Rais Samia kabla ya kula kiapo Jumatatu akichukua […]

The post MwanaFA amshukuru Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mbunge wa Muheza, Hamis Mwinjuma au MwanaFA amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuwataka wasanii na wanamichezo kufanya kazi kwa mikono yao.
MwanaFA ambaye ni mwanamuziki mkongwe nchini ni miongoni mwa uteuzi uliotangazwa Jumapili hii na Rais Samia kabla ya kula kiapo Jumatatu akichukua nafasi ya Pauline Gekul aliyehamishiwa Wizara ya Katiba na Sheria.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao kijamii wa Instagram, MwanaFA aliweka ujumbe huo wa shukrani kwa Rais sambamba na kuwasihi wadau wa wizara hiyo kwenda kufanya kazi kwa bidii.

“Wanautamaduni,wasanii na wanamichezo wa nchi hii, muda ndio huu jamaa zangu, twendeni tukafanye mambo yetu kwa mikono yetu wenyewe, Mungu ametoa kibali,” alisema MwanaFA


“Namshukuru sana Rais Samia kwa imani hii kubwa aliyonipa kijana wake, ina maana kubwa mno na naahidi kufanya kila lililo ndani ya uwezo wangu nisimuangushe.
“Nawashukuru pia wananchi wenzangu wa Muheza kwa imani na ushirikiano mkubwa wanaoendelea kunipatia. Muheza ni ya watu magwiji watupu,” aliandika FA.

The post MwanaFA amshukuru Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/01/mwanafa-amshukuru-rais-samia/feed/ 0
MwanaFA sasa waziri https://www.greensports.co.tz/2023/02/27/mwanafa-sasa-waziri/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/27/mwanafa-sasa-waziri/#respond Mon, 27 Feb 2023 13:40:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5315 Na mwandishi wetuUsiseme MwanaFA, sema mheshimiwa waziri. Kwa sasa ndilo jina sahihi la msanii wa muziki wa kizazi kipya, Hamis Mwinjuma ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo.MwanaFA ametangazwa Jumapili hii kushika wadhifa huo baada ya mabadiliko ya baraza la mawaziri na viongozi kadhaa yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa […]

The post MwanaFA sasa waziri first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Usiseme MwanaFA, sema mheshimiwa waziri. Kwa sasa ndilo jina sahihi la msanii wa muziki wa kizazi kipya, Hamis Mwinjuma ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo.
MwanaFA ametangazwa Jumapili hii kushika wadhifa huo baada ya mabadiliko ya baraza la mawaziri na viongozi kadhaa yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Msanii huyo ambaye ametamba na nyimbo kadhaa lakini zinazokumbukwa kwa miaka ya karibuni ni ‘Habari ndiyo hiyo’ na ‘Bado nipo nipo sana’, anachukua nafasi ya Pauline Gekul aliyehamishiwa wizara ya sheria na katiba.
MwanaFA ambaye ni mbunge wa jimbo la Muheza mkoani Tanga aliingia bungeni mwaka 2020 baada ya kuchuana kwenye kura za maoni na mkurugenzi wa zamani wa mashtaka, Adadi Rajab.
Na ingawa MwanaFA alishindwa kwenye kura hizo lakini jina la msanii huyo lilipitishwa na vikao vya juu vya chama chake CCM kabla ya kuchaguliwa kwa kura nyingi na wananchi wa jimbo la Muheza.
Mara baada ya uteuzi wa msanii huyo kutangazwa, maoni mbalimbali yamekuwa yakitolewa kwenye mitandao ya kijamii kwa baadhi ya watu kumpongeza, kumtakia heri wengine kuhoji na hata kukosoa.
Katika sanaa MwanaFA amefanikiwa kujipambanua kuwa miongoni mwa wasanii wanaoimba mashairi yenye ujumbe katika jamii na ambayo yamefanikiwa kuliteka soko la muziki ndani na nje ya nchi.
Mfano wa mashairi yake katika ‘Habari ndiyo hiyo’ yameendelea kuwa njia mojawapo ya kufikishiana ujumbe kwa namna tofauti katika maisha ya kawaida iwe kwa kukosoana, kusimangana au kukumbushana jambo.
Mashairi ya ‘Bado nipo nipo’ yameendelea kutumiwa katika jamii hasa kwa vijana wanaochelewa au ambao hawataki kuoa.
Nje ya hilo, MwanaFA ambaye amekuwa mjumbe wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata pia alionyesha kuwa na msimamo katika kukataa dhulma kutoka kwa mapromota ambao ilidaiwa wengi wao walikuwa wakineemeka kwa kuwadhulumu wasanii.
Msanii huyo na viongozi wengine walioteuliwa na Rais Samia wanatarajia kuapishwa rasmi Jumatatu hii jioni Ikulu mjini Dodoma.

The post MwanaFA sasa waziri first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/27/mwanafa-sasa-waziri/feed/ 0