mwamuzi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 01 Jun 2023 19:09:03 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg mwamuzi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mourinho amvaa mwamuzi nje ya uwanja https://www.greensports.co.tz/2023/06/01/mourinho-amvaa-mwamuzi-nje-ya-uwanja/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/01/mourinho-amvaa-mwamuzi-nje-ya-uwanja/#respond Thu, 01 Jun 2023 19:08:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6418 Budapest, HungaryKocha wa AS Roma, Jose Mourinho ameonekana akimvaa mwamuzi Anthony Taylor kwenye maegesho ya magari baada ya timu yake kushindwa kutamba kwenye fainali ya Europa Ligi jana Jumatano.Mourinho jana kwa mara ya kwanza alipoteza mechi ya fainali ya michuano ya klabu Ulaya ikiwa ni fainali yake ya saba akiwa ameshinda sita za awali baada […]

The post Mourinho amvaa mwamuzi nje ya uwanja first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Budapest, Hungary
Kocha wa AS Roma, Jose Mourinho ameonekana akimvaa mwamuzi Anthony Taylor kwenye maegesho ya magari baada ya timu yake kushindwa kutamba kwenye fainali ya Europa Ligi jana Jumatano.
Mourinho jana kwa mara ya kwanza alipoteza mechi ya fainali ya michuano ya klabu Ulaya ikiwa ni fainali yake ya saba akiwa ameshinda sita za awali baada ya Roma kushindwa kutamba kwa Sevilla. Katika mechi hiyo iliyopigwa mjini Budapest, timu hizo awali zilitoka sare ya bao 1-1 na katika penalti Roma ililala kwa mabao 4-1 jambo ambalo lilionekana kumvuruga mno Mourinho.
Mechi hiyo iliyoonekana kujaa ubabe wa kila aina, ilimfanya mwamuzi kuchukua uamuzi mgumu kwa kutoa jumla ya kadi za njano 13 ikiwa ni rekodi ya kipekee katika mechi ya Europa Ligi.
Baada ya mechi hiyo, video zilimuonesha Mourinho akiwa kwenye maegesho ya magari na kuanza kumkaripia mwamuzi huyo ambaye pia anachezesha mechi za Ligi Kuu England.
Mourinho alimlaumu mwamuzi huyo kwa kushindwa kuipa Roma penalti kipindi cha pili baada ya tukio la mchezaji kuunawa mpira pamoja na maamuzi mengine ambayo anadhani yalimshinda mwamuzi huyo.
“Mwamuzi alijiona kama yeye ni Mhispaniola, matokeo hayakuwa ya haki na kuna mengi ya kuyafanyia tathmini upya,” alisema Mourinho.


“Hii ni fainali ya Ulaya, na kwa aina hii ya uamuzi ni ngumu kukubali, kama tunazungumzia matukio ya mwamuzi, hayakuwa mawili au matatu, ni mengi ukiacha yale maamuzi makubwa, kwa sisi ambao tumekuwa kwenye soka muda mrefu tumebaini haraka kilichokuwa kikiendelea,” alisema Mourinho.

“(Lorenzo) Pellegrini anaanguka kwenye boksi anapewa kadi ya njano, Ocampos (Lucas) anafanya hivyo hivyo hapewi kadi, hii ni kashfa,” alisema Mourinho.


Mourinho ambaye pia alipewa kadi ya njano katika mechi hiyo huenda akakumbana na adhabu ya kufungiwa na Uefa kwa tukio lake la kupokea medali ya fedha kwa timu yake kushika nafasi ya pili lakini akairusha medali hiyo kwa shabiki mmoja kijana mdogo.
Baadaye kocha huyo wa zamani wa timu za FC Porto, Chelsea, Inter Milan, Real Madrid, Man United na Tottenham, alipoulizwa alisema kwamba yeye huwa anatunza medali za dhahabu tu.
Roma inashika nafasi ya sita katika Serie A na Jumapili itaumana na timu ya Spezia inayohaha kujitoa kwenye janga la kushuka daraja, mechi ambayo Roma inatakiwa kushinda ili kujiweka nafasi ya tano.
Iwapo itafanikiwa kushika nafasi ya tano timu hiyo itashiriki michuano ya Europa Ligi msimu ujao vinginevyo ikiangukia nafasi ya sita itashiriki Europa Conference Ligi, michuano ambayo ilibeba taji lake msimu uliopita.

The post Mourinho amvaa mwamuzi nje ya uwanja first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/01/mourinho-amvaa-mwamuzi-nje-ya-uwanja/feed/ 0
Mwamuzi aliyedaiwa kumpiga kiwiko beki asamehewa https://www.greensports.co.tz/2023/04/14/mwamuzi-aliyedaiwa-kumpiga-kiwiko-beki-asamehewa/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/14/mwamuzi-aliyedaiwa-kumpiga-kiwiko-beki-asamehewa/#respond Fri, 14 Apr 2023 20:14:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5814 London, EnglandMwamuzi msaidizi wa Ligi Kuu England (EPL) Constantine Hatzidakis hatochukuliwa hatua za kinidhamu baada ya kumuomba radhi beki wa Liverpool, Andy Robertson aliyedaiwa kumpiga kiwiko.Hatzidakis alidaiwa kumpiga kiwiko Robertson Jumapili iliyopita katika mechi kati ya Arsenal na Liverpool iliyopigwa kwenye dimba la Anfield na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.Chama cha Soka England (FA) […]

The post Mwamuzi aliyedaiwa kumpiga kiwiko beki asamehewa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Mwamuzi msaidizi wa Ligi Kuu England (EPL) Constantine Hatzidakis hatochukuliwa hatua za kinidhamu baada ya kumuomba radhi beki wa Liverpool, Andy Robertson aliyedaiwa kumpiga kiwiko.
Hatzidakis alidaiwa kumpiga kiwiko Robertson Jumapili iliyopita katika mechi kati ya Arsenal na Liverpool iliyopigwa kwenye dimba la Anfield na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Chama cha Soka England (FA) kilitarajiwa kumpa adhabu mwamuzi huyo ambaye ilidaiwa kwamba alimpiga kiwiko mchezaji huyo baada ya wawili hao kuzozana.
Tukio hilo lilitokea wakati wa mapumziko ambapo Robertson alimkusa mkononi mwamuzi huyo ambaye alijibu mapigo kwa kumpiga beki huyo wa kushoto sehemu ya usoni akitumia kiwiko.
Hata hivyo baada ya uchunguzi wa siku nne kwa kutumia video na taarifa kutoka kwa waamuzi, wachezaji na mashahidi wengine, FA ilithibitisha kwamba Hatzidakis hatopewa adhabu.

“Tumepitia ushahidi wote unaohusisha tukio zima lililotokea Anfield likimhusisha beki wa Liverpool, Andrew Robertson na mwamuzi Constantine Hatzidakis na hatutochukua hatua zozote,” alisema msemaji wa FA.


Inadaiwa kwamba jana Alhamisi Hatzidakis mwenyewe alimuomba radhi Robertson kwa tukio hilo na Robertson alikubali na kumsamehe bila kusita.
“Haikuwa dhamira yangu kumgusa Andy kwa namna yoyote wakati nikiuondoa mkono wangu karibu naye na kwa hilo namuomba msamaha. Kwa sasa najiandaa kuendelea na kazi yangu ya kusimamia mechi za soka,” alisema mwamuzi huyo.

The post Mwamuzi aliyedaiwa kumpiga kiwiko beki asamehewa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/14/mwamuzi-aliyedaiwa-kumpiga-kiwiko-beki-asamehewa/feed/ 0
Barca yadaiwa kuhonga mwamuzi https://www.greensports.co.tz/2023/03/09/barca-yadaiwa-kuhonga-mwamuzi/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/09/barca-yadaiwa-kuhonga-mwamuzi/#respond Thu, 09 Mar 2023 05:49:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5452 Madrid, HispaniaWaendesa mashitaka wa Hispania wanajiandaa kuwasilisha kesi ya rushwa dhidi ya klabu ya Barcelona na rais wa zamani wa klabu hiyo, Josep Maria Bartomeu kwa tuhuma za kutoa rushwa kwa mwamuzi.Habari zinadai kwamba Bartomeu anatuhumiwa kuidhinisha malipo kwa makamu wa rais wa zamani wa kamati ya waamuzi, Jose Maria Negreira kiasi cha Euro 1.4 […]

The post Barca yadaiwa kuhonga mwamuzi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Waendesa mashitaka wa Hispania wanajiandaa kuwasilisha kesi ya rushwa dhidi ya klabu ya Barcelona na rais wa zamani wa klabu hiyo, Josep Maria Bartomeu kwa tuhuma za kutoa rushwa kwa mwamuzi.
Habari zinadai kwamba Bartomeu anatuhumiwa kuidhinisha malipo kwa makamu wa rais wa zamani wa kamati ya waamuzi, Jose Maria Negreira kiasi cha Euro 1.4 milioni kati ya mwaka 2016 na 2018.
Hadi sasa uchunguzi wa waendesha mashtaka hao unamuangazia mwamuzi wa zamani, Jose Maria Enriquez ambaye ndiye anayedaiwa kupokea malipo hayo yaliyoidhinishwa na Bartomeu.
Klabu ya Barcelona au Barca pamoja na Bartomeu kwa pamoja watatakiwa kujitetea katika kesi hiyo na huenda wakajikuta wakikumbana na mkono wa sheria kutokana na fedha hizo zilizolipwa kwenye kampuni ya Negreira iitwayo, Dasnil 95 SL.
Marais wa zamani wa Barca, Joan Gaspart na Sandro Rosell pamoja na rais wa sasa wa klabu hiyo, Joan Laporta ambaye pia alikuwa kiongozi wa klabu hiyo kati ya mwaka 2003 hadi 2010 nao pia wataitwa kutoa ushahidi.
Akizungumza hivi karibuni, Laporta ambaye aliwahi kunukuliwa hapo kabla akisema kwamba malipo hayo ni kwa ajili ya taarifa ya kiufundi kuhusu waamuzi na uchezeshaji wao, alikana tuhuma hizo akidai klabu yake haijawahi kuwanunua waamuzi.

“Barca haijawahi kuwanunua au kuwashawishi waamuzi kwa namna yoyote, haikuwahi kuwapo dhamira hiyo, ukweli unakinzana na wale wanaojaribu kuja na habari tofauti,” aliongeza Laporta.


Inadaiwa kwamba Barca ilimlipa Negreira jumla ya Euro 7 milioni kati ya mwaka 2001 hadi 2018 kipindi ambacho klabu hiyo ilikuwa chini ya marais wanne kabla Bartomeu hajakata malipo hayo miaka mitano iliyopita.
Malipo yaliyozua utata na kuwa chanzo cha uchunguzi huo ni yale yaliyofanyika kati ya mwaka 2016 na 2018 baada ya kutiliwa shaka na maofisa wa ofisi ya ushuru.
Uefa au Fifa nao wana nafasi ya kuchukua hatua na tayari Shirikisho la Soka Hispania lilibainisha wiki iliyopita kwamba Uefa iliomba kupatiwa taarifa na nakala zote zinazohusu uchunguzi wa kashfa hiyo.

The post Barca yadaiwa kuhonga mwamuzi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/09/barca-yadaiwa-kuhonga-mwamuzi/feed/ 0