Mourinho - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 31 May 2026 08:46:25 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Mourinho - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mourinho asaini mkataba Real Madrid https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/mourinho-asaini-mkataba-real-madrid/ https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/mourinho-asaini-mkataba-real-madrid/#respond Sun, 31 May 2026 08:46:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14658 Madrid, HispaniaJose Mourinho au Speacial One anadaiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Real Madrid ingawa atatangazwa rasmi baada ya uchaguzi wa rais wa klabu hiyo utakaofanyika Juni 7, 2026.Hii itakuwa mara ya pili kwa Mourinho kuinoa timu hiyo ingawa uhalali wa mkataba wake upo njia panda na kila kitu kitajulikana rasmi baada […]

The post Mourinho asaini mkataba Real Madrid first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Jose Mourinho au Speacial One anadaiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Real Madrid ingawa atatangazwa rasmi baada ya uchaguzi wa rais wa klabu hiyo utakaofanyika Juni 7, 2026.
Hii itakuwa mara ya pili kwa Mourinho kuinoa timu hiyo ingawa uhalali wa mkataba wake upo njia panda na kila kitu kitajulikana rasmi baada ya rais wa sasa, Florentino Perez kuchaguliwa tena katika nafasi hiyo.
Mourinho, 63, amekuwa akihusishwa katika nafasi hiyo mara kadhaa tangu kuondoka kwa Xabi Alonso Januari mwaka huu na nafasi yake kukabidhiwa kocha wa muda, Alvaro Arbeloa.
Kwa kukubali kuinoa Real Madrid, Mourinho anaachana na klabu ya Benfica ambayo alianza kuinoa Septemba mwaka jana na ameiwezesha kushika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu Ureno maarufu Primera Liga msimu huu.
Akiwa na Real Madrid mara ya kwanza kati ya mwaka 2010 hadi 2013, kocha huyo kutoka Ureno aliiwezesha timu hiyo kutwaa mataji ya La Liga, Copa del Rey na Spanish Super Cup.
Mourinho pia amewahi kuzinoa timu za FC Porto, Chelsea, Inter Milan, Tottenham, Man United, AS Roma na Fenerbahce.
Msimu huu wa 2025-26 na msimu uliopita imekuwa migumu kwa Real Madrid ikimaliza bila taji lolote na msimu huu imeuaga kwa kichapo cha mabao 2-0 mbele ya mahasimu wao Barcelona katika El Clasico.
Perez, 79, anaamini Mourinho ana uwezo wa kurudisha heshima Real Madrid ingawa bado ana kazi ya kuchuana katika kiti cha urais wa klabu hiyo na Enrique Riquelme, bilionea aliyewekeza katika nishati jadidifu.
Tangu mwaka 2009, Perez amekuwa Real Madrid akikosa mpinzani tishio katika kiti cha urais na kabla ya hapo aliiongoza klabu hiyo kati ya mwaka 2000 na 2006, safari hii licha ya kupewa nafasi kubwa ya kushinda urais, ujasiri wa Riquelme unaacha maswali mengi.

The post Mourinho asaini mkataba Real Madrid first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/mourinho-asaini-mkataba-real-madrid/feed/ 0
Bosi La Liga amtaka Mourinho https://www.greensports.co.tz/2026/05/02/bosi-la-liga-amtaka-mourinho/ https://www.greensports.co.tz/2026/05/02/bosi-la-liga-amtaka-mourinho/#respond Sat, 02 May 2026 12:45:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14581 Madrid, HispaniaRais wa La Liga, Javier Tebas amesema anamkaribisha mara ya pili kocha Jose Mourinho katika soka la Hispania huku kukiwa na habari kwamba kocha huyo anaweza kurudi mara ya pili katika klabu ya Real Madrid.Rais wa Real Madrid, Florentino Pérez inadaiwa anamfikiria kocha huyo ambaye anainoa Benfica ili achukue nafasi ya kocha wa sasa […]

The post Bosi La Liga amtaka Mourinho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Rais wa La Liga, Javier Tebas amesema anamkaribisha mara ya pili kocha Jose Mourinho katika soka la Hispania huku kukiwa na habari kwamba kocha huyo anaweza kurudi mara ya pili katika klabu ya Real Madrid.
Rais wa Real Madrid, Florentino Pérez inadaiwa anamfikiria kocha huyo ambaye anainoa Benfica ili achukue nafasi ya kocha wa sasa Álvaro Arbeloa mara baada ya msimu huu kumalizika.
Tebas amenukuliwa akisema kwamba kama Real Madrid na viongozi wao wataamua hivyo hilo litakuwa jambo zuri kwa Real Madrid kwani Mourinho wakati wote ni mtu wa kujiweka juu na hilo ni jambo zuri kwa La Liga.
Katika misimu mitano ambayo Mourinho amekuwa kocha Real Madrid, ameiwezesha timu hiyo kubeba mataji ya La Liga, Spanish Supercup na Copa del Rey kabla ya kuachana nayo mwaka 2013 kwa makubaliano ya kiungwana na Perez.
Mourinho, 63, ana mkataba na Benfica unaofikia ukomo Juni 2027 lakini katika mkataba huo kuna kipengele ambacho kinairuhusu klabu au kocha huyo kuvunja mkataba mwishoni mwa msimu huu.
Januari mwaka huu baada ya kutimuliwa kwa Xabi Alonso, Madrid ilimpa majukumu ya ukocha Arbeloa, mchezaji wa zamani wa timu hiyo aliyewahi kufundishwa na Mourinho.
Kwa namna msimu huu wa 2025-26 unavyoendelea Madrid inasubiri kumaliza msimu wa pili bila taji hivyo moja ya mikakati yao msimu ujao ni kuwa na kocha wa hadhi na Mourinho ni kati ya makocha walio katika hesabu zao.

The post Bosi La Liga amtaka Mourinho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/05/02/bosi-la-liga-amtaka-mourinho/feed/ 0
Mourinho alimwa red card, alia kuitwa msaliti https://www.greensports.co.tz/2026/03/09/mourinho-alimwa-red-card-alia-kuitwa-msaliti/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/09/mourinho-alimwa-red-card-alia-kuitwa-msaliti/#respond Mon, 09 Mar 2026 20:09:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14415 Porto, UrenoKocha wa Benfica, Jose Mourinho amemshutumu kocha msaidizi wa FC Porto akidai kocha huyo alimuita msaliti mara 50 mara baada ya Mourinho kupewa kadi nyekundu katika mechi baina ya timu hizo.Mechi hiyo baina ya mahasimu hao wa soka nchini Ureno iliisha kwa sare ya mabao 2-2 huku Benfica ikipambana hadi kusawazisha mabao hayo baada […]

The post Mourinho alimwa red card, alia kuitwa msaliti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Porto, Ureno
Kocha wa Benfica, Jose Mourinho amemshutumu kocha msaidizi wa FC Porto akidai kocha huyo alimuita msaliti mara 50 mara baada ya Mourinho kupewa kadi nyekundu katika mechi baina ya timu hizo.
Mechi hiyo baina ya mahasimu hao wa soka nchini Ureno iliisha kwa sare ya mabao 2-2 huku Benfica ikipambana hadi kusawazisha mabao hayo baada ya kuwa nyuma kwa mabao 2-0.
Mkombozi wa Benfica katika mechi hiyo alikuwa Leandro Barreiro, mchezaji aliyeingia akitokea benchi na kufunga bao la kusawazisha dakika mbili kabla ya mpira kumalizika, bao ambalo lilisababisha kuzuka tafrani.
Katika tafrani hizo, Mourinho alijikuta akipewa kadi nyekundu baada ya kuonekana akiwa katika mzozo na watu wa kwenye benchi la timu ya FC Porto.
Alipoulizwa sababu ya kupewa kadi nyekundu na kutolewa nje, Mourinho alisema hajui ingawa mwamuzi alimwambia kwamba alipewa kadi hiyo kwa kosa la kuwapiga na mpira watu wa kwenye benchi la FC Porto.

“Mwamuzi ameniambia alinipa kadi kwa sababu niliwapiga na mpira watu wa FC Porto jambo ambalo ni uwongo, kwa sababu niliupiga mpira kwa mashabiki,” alisema Mourinho.


Mourinho kocha wa zamani wa timu za Chelsea, Real Madrid, Inter Milan, Tottenham, AS Roma, Man United na FC Porto, alifafanua kwamba huwa ana kawaida ya kufurahia goli kwa kuupiga mpira jukwaani kwa mashabiki kwa lengo la kumpa mpira huo shabiki mwenye bahati.
Kocha huyo mwingi wa vituko ambaye pia anajulikana kwa jina la Speacial One, hata hivyo alisema anajua yeye si mahiri katika mbinu za soka ingawa mpira ule aliupiga lengo lake ni uende jukwaani kwa mashabiki.
Kuhusu kocha msaidizi wa FC Porto, Mourinho alifafanua kuwa kocha huyo alimuita msaliti mara 50 na alimtaka amwambie yeye msaliti kwa lipi wakati kila timu alizokuwa alijitoa kwa moyo wote na maisha yake kwa saa 24.
“Kutukanwa na mashabiki hilo ni jambo jingine lakini kocha mtaalam mwenzangu ananiita mimi msaliti, kwa nini? Ninavyojitoa hapa Benfica? Mimi msaliti kwa lipi?,” alihoji Mourinho.

The post Mourinho alimwa red card, alia kuitwa msaliti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/09/mourinho-alimwa-red-card-alia-kuitwa-msaliti/feed/ 0
Mourinho atimuliwa Fenerbahce https://www.greensports.co.tz/2025/09/06/mourinho-atimuliwa-fenerbahce/ https://www.greensports.co.tz/2025/09/06/mourinho-atimuliwa-fenerbahce/#respond Sat, 06 Sep 2025 14:55:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13861 Fenerbahce, UturukiKocha Jose Mourinho ametimuliwa katika klabu ya Fenerbahce ya Uturuki baada ya kuinoa katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja.Kutimuliwa kwa Mourinho kumekuja siku chache baada ya timu hiyo kutolewa na Benfica kwenye mechi za play-off za Ligi ya Mabingwa Ulaya.Katika taarifa ya kumfuta kazi kocha huyo, klabu ya Fenerbahce ilimshukuru Mourinho kwa juhudi zake na […]

The post Mourinho atimuliwa Fenerbahce first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Fenerbahce, Uturuki
Kocha Jose Mourinho ametimuliwa katika klabu ya Fenerbahce ya Uturuki baada ya kuinoa katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja.
Kutimuliwa kwa Mourinho kumekuja siku chache baada ya timu hiyo kutolewa na Benfica kwenye mechi za play-off za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika taarifa ya kumfuta kazi kocha huyo, klabu ya Fenerbahce ilimshukuru Mourinho kwa juhudi zake na kumtakia kila la heri.
Mourinho, 62, ni kati ya makocha wenye jina kubwa barani Ulaya akiwa hadi sasa amezinoa timu za FC Porto, Chelsea, Man United, Tottenham, Inter Milan, Real Madrid na AS Roma.
Katika msimu uliopita, Mourinho aliiwezesha Fenerbahce kumaliza Ligi Kuu Uturuki akiwa nafasi ya pili lakini mara kadhaa alijikuta katika matukio yaliyojaa utata.
Februari mwaka huu, vinara wa ligi kuu nchini Uturuki, Galatasaray walitangaza nia ya kumfungulia kesi ya jinai kwa madai ya kutoa kauli za ubaguzi wa rangi baada ya timu hizo mbili kutoka sare ya bila kufunga.
Mourinho hata hivyo aliigeuzia kibao klabu hiyo akikana madai hayo na kusisitiza kwamba yeye ni mtu anayechukia ubaguzi wa rangi na badala yake akawafungulia mashtaka akitaka Galatasaray wamlipe fidia ya Euro 41,000 kwa kumharibia jina.
Katika mechi ya Europa Ligi dhidi ya United, mechi iliyochezwa Oktoba mwaka jana na kumalizika kwa sare ya bao 1-1, Mourinho alisema baada ya kuachana na Fenerbahce atainoa timu iliyo chini ya msimamo wa ligi ili asipate nafasi ya kushiriki michuano ya Uefa.
Nchini Uturuki, Mourinho aliwahi kufungiwa mechi nne ingawa baadaye zilipunguzwa na kuwa mbili baada ya kutoa kauli ya kulalamikia ubora wa waamuzi mara baada ya mechi yao dhidi ya Galatasaray.
Sambamba na mataji ya ligi za ndani barani Ulaya, Mourinho pia ana rekodi ya kubeba taji la ligi ya mabingwa mara mbili, kwanza na FC Porto na baadaye akiwa Inter Milan.

The post Mourinho atimuliwa Fenerbahce first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/09/06/mourinho-atimuliwa-fenerbahce/feed/ 0
Mourinho aitamani timu ya taifa Ureno https://www.greensports.co.tz/2025/07/19/mourinho-aitamani-timu-ya-taifa-ureno/ https://www.greensports.co.tz/2025/07/19/mourinho-aitamani-timu-ya-taifa-ureno/#respond Sat, 19 Jul 2025 12:53:08 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13757 Fenerbahce, UturukiKocha Jose Mourinho ameweka wazi kuhusu shauku yake ya kutaka kuwa kocha wa timu ya taifa lake la Ureno wakati akiwa kwenye ubora wake.Mourinho, 62, kwa sasa anainoa klabu ya Fenerbahce ya nchini Uturuki na amebakiwa na mwaka mmoja kwenye mkataba wake na timu hiyo.Mourinho aliondoka nchini Ureno mwaka 2004 baada ya kuiwezesha FC […]

The post Mourinho aitamani timu ya taifa Ureno first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Fenerbahce, Uturuki
Kocha Jose Mourinho ameweka wazi kuhusu shauku yake ya kutaka kuwa kocha wa timu ya taifa lake la Ureno wakati akiwa kwenye ubora wake.
Mourinho, 62, kwa sasa anainoa klabu ya Fenerbahce ya nchini Uturuki na amebakiwa na mwaka mmoja kwenye mkataba wake na timu hiyo.
Mourinho aliondoka nchini Ureno mwaka 2004 baada ya kuiwezesha FC Porto kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na kujiunga na Chelsea ambapo alianza kupata umaarufu hadi kubatizwa jina la utani la Special One.
Mbali na Chelsea na FC Porto, Mourinho pia amewahi kuzinoa timu za Tottenham, Inter Milan, Man United, Real Madrid na AS Roma na hadi sasa ana rekodi ya kubeba mataji 26 akiwa kocha wa timu alizopita.
Mourinho hata hivyo alipoulizwa kama angependa kuendelea kuwa kocha wa klabu au timu ya taifa, alisema lolote kwake sawa lakini hakuficha shauku yake ya kurudi Ureno.

“Ni hakika nitarudi Ureno, hilo halijatokea na si kwa sababu naelekea mwisho wa kazi ya ukocha, hapana huko bado ni mbali sana, sitaki kurudi Ureno kama mstaafu au katika miaka yangu ya mwisho ya kazi,” alisema Mourinho.


Mourinho aliongeza kuwa angependa arudi Ureno akiwa katika ubora wake, akiwa mwenye afya nzuri kimwili na kiakili na mwenye nguvu na kusisitiza kuwa ni lazima arudi.
Mourinho hata hivyo aliwahi kukanusha habari kwamba alifanya mazungumzo na viongozi wa Shirikisho la Soka Ureno ili awe kocha wa timu hiyo kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2026 ingawa pia aliwahi kusema kwamba alikataa mara mbili nafasi ya kuwa kocha wa timu ya Ureno.

The post Mourinho aitamani timu ya taifa Ureno first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/07/19/mourinho-aitamani-timu-ya-taifa-ureno/feed/ 0
Mourinho afurahia Amorim kubaki Man United https://www.greensports.co.tz/2025/06/02/mourinho-afurahia-amorim-kubaki-man-united/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/02/mourinho-afurahia-amorim-kubaki-man-united/#respond Mon, 02 Jun 2025 18:21:39 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13529 Fenerbahce, UturukiKocha wa zamani wa Man United, Jose Mourinho amesema timu hiyo imefanya jambo sahihi kuamua kuendelea na kocha wao Ruben Amorim licha ya kutopata mafanikio msimu huu.Man United chini ya Amorim msimu huu wa 2024-25 imemaliza Ligi Kuu England (EPL) ikiwa nafasi ya 15, rekodi ambayo ni mbaya na imewanyima nafasi kushiriki Ligi ya […]

The post Mourinho afurahia Amorim kubaki Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Fenerbahce, Uturuki
Kocha wa zamani wa Man United, Jose Mourinho amesema timu hiyo imefanya jambo sahihi kuamua kuendelea na kocha wao Ruben Amorim licha ya kutopata mafanikio msimu huu.
Man United chini ya Amorim msimu huu wa 2024-25 imemaliza Ligi Kuu England (EPL) ikiwa nafasi ya 15, rekodi ambayo ni mbaya na imewanyima nafasi kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Timu hiyo pia imekosa nafasi hiyo baada ya kushindwa kutamba mbele ya Tottenham katika fainali ya Europa Ligi baada ya kulala kwa bao 1-0 kwenye mechi ya fainali.
Akizungumzia mazingira hayo, Mourinho alisema anajua kitendo cha kukosa taji la Europa ni pigo kubwa kwa timu hiyo hasa kwa kuwa imepitia kipindi kirefu bila ya kubeba taji la Ulaya.
Mourinho ambaye mwaka 2017 aliiwezesha Man United kubeba taji la mwisho Ulaya hata hivyo alisema kwamba inaonekana Amorim anaungwa mkono na wanampa muda na mazingira ya kusonga mbele.
Amorim ambaye aliachana na Sporting CP ya Ureno, Novemba mwaka jana na kuanza kibarua cha kuinoa Man United, aliomba radhi kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya kumaliza EPL wakiwa nafasi ya chini.
Kocha huyo hata hivyo baada ya kupoteza taji la Europa alisema jambo hilo litakuwa sababu ya kuisaidia timu hiyo iwe bora msimu ujao.

“Nimesoma baadhi ya kauli zake (Amorim) akisema kwamba ana furaha kujiunga na timu hiyo na tayari amepitia katika miezi sita jambo ambalo naweza kulifananisha na kile nilichowahi kupitia,” alisema Mourinho.


Mourinho alisema alipojiunga na FC Porto alikutana na hali kama hiyo, “Nilikwenda Januari 2002 nilikuwa na miezi sita migumu, tulikuwa tunapambana japo tufuzu Kombe la Uefa na tukafanikiwa na baada ya hapo nini kilitokea?” Alisema Mourinho na kuhoji.
Mourinho baadaye aliiwezesha Porto kubeba mataji matatu (treble) akianzia taji la Ureno, Kombe la Uefa, baadaye akabeba taji la ligi kuu na kulitetea kabla ya kuongeza na taji la Ligi ya Mabingwa ulaya katika msimu wake wa kwanza wa 2003-04.
Mourinho ambaye kwa sasa ni kocha wa Fenerbahce pia amewahi kuzinoa timu za Chelsea, Inter Milan, Real Madrid, Tottenham na AS Roma.

The post Mourinho afurahia Amorim kubaki Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/02/mourinho-afurahia-amorim-kubaki-man-united/feed/ 0
Mourinho aikana timu ya taifa Ureno https://www.greensports.co.tz/2025/05/19/mourinho-aikana-timu-ya-taifa-ureno/ https://www.greensports.co.tz/2025/05/19/mourinho-aikana-timu-ya-taifa-ureno/#respond Mon, 19 May 2025 15:18:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13486 Fenerbahce, UturukiKocha wa Fenerbahce ya Uturuki, Jose Mourinho amekana kufanya mazungumzo na mabosi wa Shirikisho la Soka Ureno ili awe kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo.Kumekuwapo habari katika siku za karibuni kwamba kocha huyo Mreno ataachana na klabu ya Fenerbahce mwishoni mwa msimu huu na kwenda kuchukua nafasi ya Roberto Martinez kwenye timu […]

The post Mourinho aikana timu ya taifa Ureno first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Fenerbahce, Uturuki
Kocha wa Fenerbahce ya Uturuki, Jose Mourinho amekana kufanya mazungumzo na mabosi wa Shirikisho la Soka Ureno ili awe kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo.
Kumekuwapo habari katika siku za karibuni kwamba kocha huyo Mreno ataachana na klabu ya Fenerbahce mwishoni mwa msimu huu na kwenda kuchukua nafasi ya Roberto Martinez kwenye timu ya taifa ya Ureno.
Mourinho ambaye amewahi kuinoa timu ya FC Porto ya Ureno na kuiwezesha kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, majira ya kiangazi mwaka jana alisaini mkataba wa miaka miwili na Fenerbahce na bado hajasema lolote kama ataendelea na timu hiyo kwa msimu ujao.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo Mourinho hakulipinga badala yake alisema kitu pekee anachoweza kusema ni kukataa hoja ya kwamba amefanya vikao na mabosi wa Shirikisho la Soka Ureno kwa kuwa yeye ni mtu mtiifu.

“Wakati pekee ambao nilifanya mawasiliano ya moja kwa moja na klabu fulani niliwaarifu Fenerbahce, si sasa ilikuwa ni mwezi Januari, nilifanya kikao na klabu hiyo lakini sikukubali ofa yao na niliiarifu klabu yangu kabla hata ya kikao,” alisema Mourinho.


Rais wa klabu ya Fenerbahce, Ali Koc hivi karibuni alibainisha kwamba Mourinho alipata ofa ya Dola 40.6 milioni wakiwa katikati ya msimu ili aachane na Fenerbahce lakini aliikataa.
Mbali na timu za FC Porto na Fenerbahce, Mourinho pia amewahi kuzinoa timu za Chelsea, Inter Milan, Real Madrid, Man United na Tottenham Hotspur.

The post Mourinho aikana timu ya taifa Ureno first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/05/19/mourinho-aikana-timu-ya-taifa-ureno/feed/ 0
Mourinho afungiwa mechi tatu https://www.greensports.co.tz/2025/04/06/mourinho-afungiwa-mechi-tatu/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/06/mourinho-afungiwa-mechi-tatu/#respond Sun, 06 Apr 2025 18:57:56 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13222 Istanbul, UturukiKocha wa klabu ya Fenerbahce ya Uturuki, Jose Mourinho amefungiwa mechi tatu pamoja na kupigwa faini ya dola 7.735 baada ya kumminya pua kocha wa Galatasaray, Okan Buruk.Uamuzi huo umefikiwa na Shirikisho la Soka Uturuki (TFF) baada ya kujiridhisha na kosa hilo ambalo Mourinho anadaiwa kulifanya wakati wa mechi ya timu hizo mahasimu yaani […]

The post Mourinho afungiwa mechi tatu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Istanbul, Uturuki
Kocha wa klabu ya Fenerbahce ya Uturuki, Jose Mourinho amefungiwa mechi tatu pamoja na kupigwa faini ya dola 7.735 baada ya kumminya pua kocha wa Galatasaray, Okan Buruk.
Uamuzi huo umefikiwa na Shirikisho la Soka Uturuki (TFF) baada ya kujiridhisha na kosa hilo ambalo Mourinho anadaiwa kulifanya wakati wa mechi ya timu hizo mahasimu yaani Istanbul Derby.
Mourinho, 62, anadaiwa kufanya kitendo hicho Jumatano katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Uturuki iliyoisha kwa Fernerbahce anayoinoa Mourinho na iliyokuwa uwanja wa nyumbani kulala kwa mabao 2-1.
Hali ya tafrani iliibuka katika mechi hiyo baina ya wachezaji hadi mwamuzi kulazimika kuwapa kadi nyekundu wachezaji watatu, wawili wakiwa wa Galatasaray.
Baada ya mwamuzi kupuliza filimbi ya kumaliza mechi, Mourinho alionekana akimminya Buruk puani ambapo kocha huyo alianguka chini katika namna ambayo kwa tafsiri ya wengi ilikuwa kama kulikuza zaidi tukio hilo.

“Mourinho amelazimika kufungiwa kuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo na kwenye benchi kwa mechi tatu zilizo rasmi,” ilieleza taarifa ya TFF.


Kwa mantiki hiyo Mourinho ambaye timu yake inashika nafasi ya pili katika ligi ikiwa imetanguliwa na mahasimu wao, Galatasaray kwa tofauti ya pointi sita, atazikosa mechi dhidi ya Kayserispor, Trabzonspor na Sivasspor.

The post Mourinho afungiwa mechi tatu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/06/mourinho-afungiwa-mechi-tatu/feed/ 0
Mourinho aishitaki Galatasaray https://www.greensports.co.tz/2025/03/01/mourinho-aishitaki-galatasaray/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/01/mourinho-aishitaki-galatasaray/#respond Sat, 01 Mar 2025 20:58:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13066 Istanbul, UturukiKlabu ya Fenerbahce ya Uturuki na kocha wao Jose Mourinho wanajipanga kuwashitaki mahasimu wao Galatasaray kwa madai ya kushambulia na kuingilia haki binafsi za kocha huyo.Galatasaray inamtuhumu Mourinho kwa kutoa kauli za ubaguzi wa rangi wakati wa mechi baina ya timu hizo mahasimu wakidai kwamba kauli ya kocha huyo si ya kiungwana.Mourinho alinukuliwa akiwadhihaki […]

The post Mourinho aishitaki Galatasaray first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Istanbul, Uturuki
Klabu ya Fenerbahce ya Uturuki na kocha wao Jose Mourinho wanajipanga kuwashitaki mahasimu wao Galatasaray kwa madai ya kushambulia na kuingilia haki binafsi za kocha huyo.
Galatasaray inamtuhumu Mourinho kwa kutoa kauli za ubaguzi wa rangi wakati wa mechi baina ya timu hizo mahasimu wakidai kwamba kauli ya kocha huyo si ya kiungwana.
Mourinho alinukuliwa akiwadhihaki waliokuwa kwenye benchi la timu ya Galatasaray siku ya mechi akidai kwamba walishangilia kwa kuruka kama nyani.
Fenerbahce walikana kauli hiyo kuwa na viashiria vyovyote vya kibaguzi badala yake ilitafsiriwa ndivyo sivyo na kupotosha maana iliyokusudiwa.
Taarifa ya klabu ya Fenerbahce iliyopatikana jana Ijumaa ilidai kwamba inakusudia kulifikisha suala hilo kwenye vyombo vya sheria na kudai fidia ya Dola 52,000.
Shirikisho la Soka Uturuki limemfungia Mourinho mechi nne na kumtoza faini ya Dola 44,00 kwa kauli aliyoitoa dhidi ya waamuzi wa soka nchini Uturuki.
Mourinho baada ya mechi dhidi ya Galatasaray, iliyochezeshwa na mwamuzi wa Slovenia, alisema anaunga mkono kutumiwa waamuzi wa kigeni kauli ambayo imetafsiriwa kuwa ni kuwadhihaki waamuzi wa Uturuki.
Wakati huo huo, kiungo wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Ghana, Michael Essien ameibuka na kumtetea Mourinho katika tuhuma za ubaguzi wa rangi kama alivyofanya mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba.
Essien ambaye Mourinho aliwahi kuwa kocha wake katika klabu ya Chelsea alihusisha tuhuma zinazomkabili Mourinho na jambo baya la upotoshaji.

“Historia ya maisha yake kwa wakati wote amekuwa mtu mzuri kwa watu wote, duniani kote, na kwa watu wa mataifa tofauti, hilo liko wazi na linaeleweka,” alisema Essien.


Essien pia alisema kwamba kinachofanyika ni kujaribu kupotosha kauli ya Jose na mwisho watu wameona kitu kisicho sahihi na uwongo kutoka Galatasaray.

The post Mourinho aishitaki Galatasaray first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/01/mourinho-aishitaki-galatasaray/feed/ 0
Drogba: Mourinho si mbaguzi wa rangi https://www.greensports.co.tz/2025/02/26/drogba-mourinho-si-mbaguzi-wa-rangi/ https://www.greensports.co.tz/2025/02/26/drogba-mourinho-si-mbaguzi-wa-rangi/#respond Wed, 26 Feb 2025 20:05:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13058 Istanbul, UturukiMshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba amemtetea aliyekwua kocha wake katika timu hiyo, Jose Mourinho akisema kwamba kocha huyo si mbaguzi wa rangi.Klabu ya Galatasaray ya Uturuki imemtuhumu Mourinho ambaye kwa sasa anainoa Fenerbahce kwa kutoa kauli ya kibaguzi baada ya timu hizo mahasimu kutoka sare ya bila kufungana juzi Jumatatu.Akizungumza baada ya […]

The post Drogba: Mourinho si mbaguzi wa rangi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Istanbul, Uturuki
Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba amemtetea aliyekwua kocha wake katika timu hiyo, Jose Mourinho akisema kwamba kocha huyo si mbaguzi wa rangi.
Klabu ya Galatasaray ya Uturuki imemtuhumu Mourinho ambaye kwa sasa anainoa Fenerbahce kwa kutoa kauli ya kibaguzi baada ya timu hizo mahasimu kutoka sare ya bila kufungana juzi Jumatatu.
Akizungumza baada ya mechi hiyo maarufu Istanbul Derby, Mourinho alisema kwamba benchi la timu pinzani ambao ndio wenyeji wa mechi hiyo walikuwa wakiruka kama nyani.
Drogba (pichani chini) amewahi pia kuichezea Galatasaray katika msimu wa 2013-14 na kuifungia mabao 20 katika mechi 53, hakubaliani na tuhuma hizo na ameamua kumtetea bosi wake huyo wa zamani.
“Mnajua jinsi nilivyojivunia kuvaa jezi ya njano na nyekundu na mapenzi yangu kwa klabu yenye hadhi nchini Uturuki, sote tunajua jinsi hamasa na uhasama vinavyoweza kuwa na mimi ni mwenye bahati kukutana na mambo haya,” alisema Drogba.

“Nimesikia maoni ya hivi karibuni kuhusu Jose Mourinho, niamini mimi ninapokwambia namjua Jose kwa miaka 25 na si mbaguzi na historia ya siku za nyuma na ya sasa ipo kuthibitisha hilo, ‘baba’ yangu anawezaje kuwa mbaguzi, hapana jamani,” alisema Drogba.


Mourinho ambaye mbali na Chelsea pia amewahi kuzinoa Man United, Real Madrid, FC Porto na Inter Milan, alianza kibarua cha kuinoa Fenerbahce Juni mwaka jana baada ya kuachana na Roma ya Italia.


Mourinho aliwahi kutoa shutuma kwa waamuzi wa Uturuki akisema kwamba ingekuwa majanga kuwatumia waamuzi hao.
Mechi ya Fanarbahce na Galatasaray ilichezeshwa na mwamuzi Slavko Vincic ambaye anatokea nchini Slovenia baada ya timu zote kuomba mwamuzi kutoka nje ya Uturuki achezeshe mechi hiyo.
Inadaiwa Mourinho amekerwa na tuhuma hizo na anaangalia uwezekano wa kuchukua hatua za kisheria, amefanya kazi na wachezaji wengi weusi wenye asili ya Afrika na inaaminika hakuna anayeweza kuamini kocha huyo kujihusisha na ubaguzi wa rangi.

The post Drogba: Mourinho si mbaguzi wa rangi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/02/26/drogba-mourinho-si-mbaguzi-wa-rangi/feed/ 0