Mo Dewji - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 23 Apr 2025 17:18:13 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Mo Dewji - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mo amshukuru Rais Samia https://www.greensports.co.tz/2025/04/23/mo-amshukuru-rais-samia/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/23/mo-amshukuru-rais-samia/#respond Wed, 23 Apr 2025 17:14:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13309 Na mwandishi wetuRais wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa msaada wake katika klabu hiyo inayoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika.Taarifa ya Mo iliyopatikana leo Jumatano Aprili 23, 2025 ilielezea shukrani za klabu hiyo kwa mchango wa usafiri na malazi kuelekea mchezo wao wa […]

The post Mo amshukuru Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa msaada wake katika klabu hiyo inayoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika.
Taarifa ya Mo iliyopatikana leo Jumatano Aprili 23, 2025 ilielezea shukrani za klabu hiyo kwa mchango wa usafiri na malazi kuelekea mchezo wao wa marudiano dhidi ya Stellenbosch ya Afrika Kusini.
Simba itarudiana na timu hiyo Jumapili ijayo katika mechi ya pili ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho ikiwa na faida ya ushindi wa bao 1-0 ilioupata Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Katika taarifa hiyo, Mo ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo, alisema Simba inatambua na kuthamini juhudi za Rais Samia katika sekta ya michezo nchini hasa mchezo wa soka.
Mo alitolea mfano wa goli la mama ambalo huhusisha zawadi ya Sh milioni 10 kwa kila goli linalofungwa kwenye mechi za kimataifa akisema jambo hilo limekuwa chanzo cha hamasa na ari kwa wachezaji na mashabiki.
Sambamba na Rais Samia, Mo pia alitoa shukrani zake kwa Wizara ya Fedha pamoja na Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo kwa namna wizara hizo zilivyoratibu safari ya Simba.
Mo pia alitoa shukran kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Shirika la Reli Tanzania (TRL).
Iwapo Simba itafanikiwa kuitoa Stellenbosch itaumana katika fainali na mshindi wa mechi kati ya RS Berkane na CS Constantine.

The post Mo amshukuru Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/23/mo-amshukuru-rais-samia/feed/ 0
Mo Dewji arejea Simba kwa nguvu, ari mpya https://www.greensports.co.tz/2024/06/12/mo-dewji-arejea-simba-na-nguvu-ari-mpya/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/12/mo-dewji-arejea-simba-na-nguvu-ari-mpya/#respond Wed, 12 Jun 2024 12:10:40 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11311 Na mwandishi wetuHatimaye mwekezaji wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ ameibuka na kueleza kukubali kuwa mwenyekiti mpya wa muda wa bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo na kujinasibu amerudi kwa ari na nguvu mpya.Dewji ambaye amesisitiza kuwa sambamba na Simba katika nyakati zote ikiwemo hali wanayoipitia sasa, ameeleza hilo leo Jumatano baada ya […]

The post Mo Dewji arejea Simba kwa nguvu, ari mpya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Hatimaye mwekezaji wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ ameibuka na kueleza kukubali kuwa mwenyekiti mpya wa muda wa bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo na kujinasibu amerudi kwa ari na nguvu mpya.
Dewji ambaye amesisitiza kuwa sambamba na Simba katika nyakati zote ikiwemo hali wanayoipitia sasa, ameeleza hilo leo Jumatano baada ya jana Salim Abdallah ‘Try Again’ kutangaza kujiuzulu nafasi ya mwenyekiti wa bodi na kumuomba Dewji achukue nafasi hiyo.
“Ndugu zangu Wanasimba huu sio muda wa malumbano, kupakana matope, ni muda wa kusimama na kutengeneza timu yetu ili iwe bora zaidi ya ilivyokuwa awali.
”Ni wakati wa kupambana, kubuni mbinu, kuweka mikakati na kutekeleza hiyo mipango ya kuandaa Simba mpya, simba itakayotisha tena.
“Hivi karibuni nilikua na kikao na Mwenyekiti wa Bodi, Salim kupokea ripoti ya klabu yetu, nilimchagua ndugu Salim kuwa mwenyekiti wa bodi kwa kuwa nilishafanya naye kazi muda mrefu, namjua ni mtu mwaminifu na mtulivu.
”Namshukuru sana yeye na wajumbe wote wa bodi kwa kazi kubwa waliyofanya mpaka sasa, ameonesha nia ya kutaka kupumzika na kuniomba mimi nirudi kuwa mwenyekiti wa bodi,” alisema Dewji.
Dewji amefunguka kuwa amekubali kuwa mwenyekiti baada ya kushauriana na viongozi mbalimbali pamoja na bodi ya ushauri kwa kipindi hiki mpaka Simba itakaporejea kwenye hali yake ya kawaida.
“Wanasimba pia nimemuomba Salim kubaki kwenye bodi kwa niaba ya mwekezaji na amekubali na hivi punde nitateua wajumbe wengine kujaza nafasi ili bodi iwe kamili kuanza kufanya kazi,” alieleza Dewji na kuongeza:
“Narejea nikiwa na nguvu na ari mpya, maarifa ya kuirejesha Simba ninayo, naongozwa zaidi na ushabiki wa Simba na wala sio uwekezaji wala ufadhili, wala udhamini.
“Sitaiacha Simba leo wala kesho, niwaombe sana Wanasimba wenzangu mtulie, mtupe nafasi ya kujenga Simba mpya, Simba yenye matarajio na mabadiliko ili kila mwanasimba awe na furaha na atembee kifua mbele.

“Ningependa sana kuona Simba yenye utulivu na umoja ili tupate mafanikio makubwa, naomba tuache kelele, vijembe, hasira na makundi tuyazike yote kwa sasa, maana klabu yetu ipo kwenye kazi kubwa ya kusajili, kuna ‘pre-season’, Simba Day, Ngao ya Jamii na hatimaye ligi kuu, klabu ndiyo klabu kubwa Afrika kutoka Tanzania, tusisahau hilo,” alisema Dewji.


Hivi karibuni, Simba imekuwa kwenye msuguano uliopelekea baadhi ya viongozi wa juu kujiuzulu kutokana na matokeo yasiyoridhisha ya timu hiyo katika michuano wanayoshiriki.
Mafanikio ya wapinzani wao, Yanga SC kwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu NBC, Kombe la FA la CRDB pia kuwafunga nje ndani Simba, vimechangia ‘mvurugiko’ huo kwa Wekundu hao.

The post Mo Dewji arejea Simba kwa nguvu, ari mpya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/12/mo-dewji-arejea-simba-na-nguvu-ari-mpya/feed/ 0
Mangungu akana Mo kuinunua Simba https://www.greensports.co.tz/2024/03/07/mangungu-akana-mo-kuinunua-simba/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/07/mangungu-akana-mo-kuinunua-simba/#respond Thu, 07 Mar 2024 18:37:57 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10070 Na mwandishi wetuMwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amesema si kweli kuwa mwekezaji wao, Mohammed Dewji ‘Mo’ aliinunua klabu hiyo miaka mitano iliyopita kama ilivyoelezwa hivi karibuni.Mangungu alipokuwa akizungumza na kituo cha redio cha EFM Jumatano hii, alisema: “Simba SC ipo, kitu ambacho kimejitokeza ni kwamba nadhani ni uelewa wa watu wengi hata Wanasimba […]

The post Mangungu akana Mo kuinunua Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amesema si kweli kuwa mwekezaji wao, Mohammed Dewji ‘Mo’ aliinunua klabu hiyo miaka mitano iliyopita kama ilivyoelezwa hivi karibuni.
Mangungu alipokuwa akizungumza na kituo cha redio cha EFM Jumatano hii, alisema: “Simba SC ipo, kitu ambacho kimejitokeza ni kwamba nadhani ni uelewa wa watu wengi hata Wanasimba wenyewe kuhusu mabadiliko yaliyofanyika ndani.
“Simba SC kama ilivyo kwa timu nyingine ilikuwa inaendeshwa kwa mfumo wa ridhaa baada ya mabadiliko ya maendeleo na changamoto nyingi za kiuendeshaji, Mohammed Dewji ni mmoja wa waliojitolea sana kuisaidia klabu,” alisema Mangungu.
Alieleza kuwa Dewji kipindi ambacho hakuwa sehemu ya Simba alikuwa anatoa michango yake kama watu wengine wanaochangia lakini baadaye akatoa wazo la kutengeneza mfumo ambao watawekeza ili klabu iwe ya kiushindani zaidi
“Hivyo kwa makubaliano ya awali tuliunda chombo ambacho kiliitwa Simba SC Company Limited, ambayo ndio ambayo imegawanya muundo wa shea wa asilimia 51/49 ambapo mwanzoni ilikuwa 50/50.
“Lakini masharti yaliyowekwa na serikali yalilazimisha kuwa lazima upande wa wanachama uwe wenye hisa nyingi chombo hicho kipo na kwa uelewa wangu na ndivyo ukweli ulivyo,” alisisitiza Mangungu.
Aliongeza kuwa kuna makubaliano ya uendeshaji na Simba SC imetoa mali zake na nguvu zake kuwekeza na mwekezaji amewekeza fedha ambazo zitakuwa mtaji unaounganishwa kwa pamoja kwa ajili ya kuendesha klabu na mambo mengine.
“Mchakato huo umeanza na umefikia hatua za mwisho kwa maana kwamba kwa kuwa klabu yetu ilikuwa inaendeshwa kwa ridhaa kuna taratibu zilikuwa zinapaswa kufikiwa kwa mujibu wa taratibu za kiserikali kwa upande wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ambayo ni Wizara pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na upande wa FCC (Tume ya Ushindani).
“Maana mtaji ukizidi Shilingi bilioni tano lazima FCC wasimamie huo mchakato, hivi sasa tuko hatua ya mwisho ya kuingiza mali zetu, Simba ina bodi ya udhamini ambao ndio walioingia mkataba na mwekezaji mwenza ambaye ni Dewji,” alisema Mangungu.
Alisema baada ya kukamilisha hayo ndio wanaenda FCC kuangalia kama kila kitu ambacho kilichotakiwa kimekamilika ndipo mchakato ukamilike.

The post Mangungu akana Mo kuinunua Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/07/mangungu-akana-mo-kuinunua-simba/feed/ 0
Mo Dewji atishia kukata tamaa https://www.greensports.co.tz/2023/07/11/mo-dewji-atishia-kukata-tamaa/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/11/mo-dewji-atishia-kukata-tamaa/#respond Tue, 11 Jul 2023 14:02:12 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6903 Na mwandishi wetuMwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ ameeleza kukaribia kukata tamaa ya kuwekeza katika klabu hiyo kutokana na kuchelewa kukamilika kwa mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji.Dewji ameyaeleza hayo leo Jumanne katika andiko aliloliweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter akibainisha kuwa ni miaka sita sasa mchakato huo unaendelea na haumaliziki.“Transformation (mabadiliko) […]

The post Mo Dewji atishia kukata tamaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ ameeleza kukaribia kukata tamaa ya kuwekeza katika klabu hiyo kutokana na kuchelewa kukamilika kwa mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji.
Dewji ameyaeleza hayo leo Jumanne katika andiko aliloliweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter akibainisha kuwa ni miaka sita sasa mchakato huo unaendelea na haumaliziki.
“Transformation (mabadiliko) ya Simba bado haijakamilika, huu ni mwaka wa sita, karibuni nitakata tamaa,” aliandika Dewji ambaye pia ni rais wa heshima wa klabu hiyo.
Simba ilianza mchakato huo tangu mwaka 2018 ikiwa ni mahsusi kwa ajili ya kuitoa timu hiyo kwenye mfumo wa wanachama na kwenda kwenye kampuni lakini hadi sasa mabadiliko hayo hayajakamilika.
Wekundu hao waliamua kufanya hivyo baada ya kubaini kuwa mfumo wa wanachama hautawapa mafanikio na maendeleo kulingana na mifumo ya soka na kiuendeshaji kidunia kwa sasa ilivyo.
Katika mabadiliko hayo, Dewji anawekeza kiasi cha Shilingi bilioni 20 ambazo ambazo ni sawa na umiliki wa hisa asilimia 49 na mmiliki mwenza ambaye ni wanachama wakimiliki asilimia 51.
Pamoja na hayo, hatua za awali za kubadilishwa kwa mfumo zilishaanza kuchukuliwa ikiwemo mabadiliko ya muundo wa uongozi wa klabu hiyo kwa kuundwa bodi ya wakurugenzi, uwepo wa mtendaji mkuu na mengineyo huku mchakato kamili ukiwa bado haujakamilika.
GreenSports ilifanya juhudi za kumtafuta Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula kutoa ufaftisanuzi walipofikia katika mabadiliko hayo lakini simu yake ya mkononi iliita bila ya kupokelewa, alipotafutwa meneja mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally simu yake ya mkononi haikuwa hewani.

The post Mo Dewji atishia kukata tamaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/11/mo-dewji-atishia-kukata-tamaa/feed/ 0
Mo Dewji amshukuru Rais Samia https://www.greensports.co.tz/2023/06/24/mo-dewji-amshukuru-rais-samia/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/24/mo-dewji-amshukuru-rais-samia/#respond Sat, 24 Jun 2023 19:39:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6713 Na mwandishi wetuRais wa heshima wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ amemshukuru na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya biashara nchini Tanzania yaliyompelekea kushinda tuzo ya All Africa Business Leaders Awards 2023 upande wa viwanda.Dewji ameshinda tuzo hiyo kwenye kipengele cha Industrialist of the Year usiku wa kuamkia leo Jumamosi […]

The post Mo Dewji amshukuru Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa heshima wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ amemshukuru na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya biashara nchini Tanzania yaliyompelekea kushinda tuzo ya All Africa Business Leaders Awards 2023 upande wa viwanda.
Dewji ameshinda tuzo hiyo kwenye kipengele cha Industrialist of the Year usiku wa kuamkia leo Jumamosi katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Sun City, Johannesburg, Afrika Kusini.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, mwekezaji huyo wa Simba SC alieleza furaha yake ya kushinda tuzo hiyo na kumshukuru Rais Samia kwa matunda hayo baada ya kuwarahisishia mazingira ya biashara nchini.
“Nimeheshimiwa na napokea kwa unyenyekevu Tuzo ya All Africa Business Leaders kwa Industrialist of the Year 2023. Naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa Rais wa Tanzania, mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kujenga mazingira mazuri ya biashara nchini ambayo yanawezesha maendeleo makubwa ya viwanda nchi nzima,” aliandika Dewji.
Mbali na tuzo hiyo, Februari, mwaka huu pia jarida la Forbes lilimuorodhesha Dewji kuwa tajiri namba 13 Afrika akifungana na wengine wawili katika nafasi hiyo kwa utajiri wa Dola za Marekani bilioni 1.5 (sawa na Sh 3.5 trilioni).

The post Mo Dewji amshukuru Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/24/mo-dewji-amshukuru-rais-samia/feed/ 0
Mo Dewji aahidi fungu la usajili Simba https://www.greensports.co.tz/2023/05/19/mo-dewji-aahidi-fungu-la-usajili-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/19/mo-dewji-aahidi-fungu-la-usajili-simba/#respond Fri, 19 May 2023 12:38:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6213 Na mwandishi wetuRais wa heshima wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji ameahidi kutoa fungu la kutosha kwa ajili ya kufanya usajili utakaoirudisha timu hiyo kwenye ushindani wa mataji ya ndani na nje ya nchi.Tajiri huyo juzi aliwapongeza watani zao Yanga, kwa kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika lakini mafanikio hayo yamemfanya kuingilia […]

The post Mo Dewji aahidi fungu la usajili Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa heshima wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji ameahidi kutoa fungu la kutosha kwa ajili ya kufanya usajili utakaoirudisha timu hiyo kwenye ushindani wa mataji ya ndani na nje ya nchi.
Tajiri huyo juzi aliwapongeza watani zao Yanga, kwa kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika lakini mafanikio hayo yamemfanya kuingilia kati suala la usajili wa timu yake kuelekea msimu ujao lengo likiwa ni kupata wachezaji wenye ubora unaoendana na malengo ya Simba.
Dewji ameeleza kuwa anafanya hivyo kwa kuwa hataki kuona makosa waliyofanya huko nyuma yakijirudia na hiyo inatokana na malengo waliyokuwa nayo ya kuwa miongoni mwa timu zinazopigania mataji na siyo kusindikiza wenzao.

“Natarajia kukutana na benchi la ufundi pamoja na mtendaji mkuu wa timu ili kujadili ninachotaka lazima tufanye maamuzi magumu ya kuachana na watu ambao hawana msaada kwenye timu na kuleta wachezaji ambao wataipigania timu na kutufikisha pale tunapopakusudia,” alisema Dewji.


Kiongozi huyo ameeleza kuwa zoezi hilo halitofanywa kwa wachezaji pekee bali watalifanya hata kwa baadhi ya viongozi ambao wataonekana hawana msaada ndani ya timu siyo mbaya wakawaweka pembeni ili kubaki na watu sahihi watakaoisaidia timu kufika wanapopataka.
Alisema mafanikio waliyokuwa nayo watani zao Yanga, yametokana na maamuzi magumu yaliyofanywa na uongozi ulioingia madarakani hivi karibuni hivyo hata wao kama wanataka kufanikiwa lazima wabadilike bila kumwonea huruma mtu yeyote.
Kwa mujibu wa ripoti ya Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, timu hiyo inatarajia kusajili wachezaji wapya wanane, wengi wao wakiwa wa kigeni ili kuboresha kikosi chao na kufanya vizuri pia kwenye michuano ya klabu Afrika mwakani.

The post Mo Dewji aahidi fungu la usajili Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/19/mo-dewji-aahidi-fungu-la-usajili-simba/feed/ 0
Forbes wamtaja tena Mo Dewji https://www.greensports.co.tz/2023/02/01/forbes-wamtaja-tena-mo-dewji/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/01/forbes-wamtaja-tena-mo-dewji/#respond Wed, 01 Feb 2023 07:01:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4929 Na mwandishi wetuRais wa heshima wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ ametajwa tena kwenye jarida la Forbes kuwa anashika namba 13 Afrika kwa utajiri akifungana na matajiri wengine wawili katika nafasi hiyo.Katika orodha hiyo mpya ya mwaka huu, Dewji ameelezwa kuwa na utajiri wa Dola za Marekani bilioni 1.5 (sawa na Sh 3.5 trilioni) […]

The post Forbes wamtaja tena Mo Dewji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa heshima wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ ametajwa tena kwenye jarida la Forbes kuwa anashika namba 13 Afrika kwa utajiri akifungana na matajiri wengine wawili katika nafasi hiyo.
Katika orodha hiyo mpya ya mwaka huu, Dewji ameelezwa kuwa na utajiri wa Dola za Marekani bilioni 1.5 (sawa na Sh 3.5 trilioni) kama ilivyo kwa Youssef Mansour raia wa Misri na Othman Benjelloun wa Morocco.
Dewji ambaye ametajwa kama bilionea mwenye umri mdogo zaidi kwa miaka sita mfululizo iliyopita pia kwenye orodha ya mwaka jana alitajwa kushika namba 15 akiwa na kiwango hicho hicho cha fedha.
Katika orodha hiyo yenye watu 19 ikiwa ni ongezeko la mtu mmoja tofauti na mwaka jana, Rais wa Shirikisho la Soka (Caf), Patrice Motsepe naye ametajwa akiwa namba tisa na utajiri wa Dola 3.2 bilioni.
Aliko Dangote raia wa Nigeria ameendelea kushikilia nafasi ya kwanza akiwa na utajiri wa Dola 13.5 bilioni, nafasi ya pili ni ya Johann Rupert na familia yake kwa utajiri wa Dola 10.7 bilioni huku Nicky Oppenheimer na familia yake wakikamilisha tatu bora kwa utajiri wa Dola 8.4 bilioni.

The post Forbes wamtaja tena Mo Dewji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/01/forbes-wamtaja-tena-mo-dewji/feed/ 0