Mmombwa - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 04 Jun 2024 12:32:02 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Mmombwa - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mmombwa aachwa Australia https://www.greensports.co.tz/2024/06/04/mmombwa-aachwa-australia/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/04/mmombwa-aachwa-australia/#respond Tue, 04 Jun 2024 12:32:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11216 Na mwandishi wetyKlabu ya MacArthur ya Australia imeachana na mshambuliaji wa Tanzania, Charles Mmombwa baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya nchini humo hivi karibuni.Mmombwa ambaye kwa sasa yuko na kikosi cha Tanzania, Taifa Stars kinachojiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Zambia, ni miongoni mwa wachezaji wanane waliotemwa na timu […]

The post Mmombwa aachwa Australia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wety
Klabu ya MacArthur ya Australia imeachana na mshambuliaji wa Tanzania, Charles Mmombwa baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya nchini humo hivi karibuni.
Mmombwa ambaye kwa sasa yuko na kikosi cha Tanzania, Taifa Stars kinachojiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Zambia, ni miongoni mwa wachezaji wanane waliotemwa na timu hiyo.
Kupitia chapisho waliloliweka jana Jumatatu kwenye mitandao ya kijamii ya timu hiyo wameeleza wazi kuwatema wachezaji hao lakini leo Jumanne kipekee waliweka chapisho la video za Mmombwa akifunga mabao ya timu hiyo maarufu kama Bulls.
Video hiyo ilisindikizwa na maneno yaliyosomeka: “Kuanzia msimu wa uzinduzi wa Bulls hadi leo, tunakushukuru Charles, na tunakutakia kila la heri katika siku zijazo.”
Mmombwa alijiunga na MacArthur ya mjini Sydney mwaka 2020 akitokea Central Coast Mariners ambako alipata makuzi yake ya soka baada ya kutoka Mt Druit Town, zote za Australia.

The post Mmombwa aachwa Australia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/04/mmombwa-aachwa-australia/feed/ 0