Misitu Bonanza - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 16 Apr 2024 07:29:51 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Misitu Bonanza - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Ihefu kinara Sao Hill Bonanza 2023 https://www.greensports.co.tz/2023/12/18/ihefu-yangara-sao-hill-bonanza-2023/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/18/ihefu-yangara-sao-hill-bonanza-2023/#respond Mon, 18 Dec 2023 20:37:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8922 Na mwandishi wetuTimu ya soka ya Ihefu imeibuka mashindi wa soka wa bonanza la michezo la Misitu ya Sao Hill lililofanyika kuanzia Desemba 9 mwaka huu na kufikia tamati mwishoni mwa wiki kwenye Shamba la Miti la Sao Hill wilayani Mufindi.Katika mechi ya soka ya kufunga Bonanza hilo ambayo ilivuta hisia za mashabiki wengi, vinara […]

The post Ihefu kinara Sao Hill Bonanza 2023 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya soka ya Ihefu imeibuka mashindi wa soka wa bonanza la michezo la Misitu ya Sao Hill lililofanyika kuanzia Desemba 9 mwaka huu na kufikia tamati mwishoni mwa wiki kwenye Shamba la Miti la Sao Hill wilayani Mufindi.
Katika mechi ya soka ya kufunga Bonanza hilo ambayo ilivuta hisia za mashabiki wengi, vinara Ihefu waliibwaga Mgololo Misitu kwa penalti 4-3 baada ya sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za kawaida.
Kwa ushindi huo, Ihefu wanakuwa wametetea vyema taji hilo ambalo pia walilibeba katika mashindano hayo kwa msimu uliopita.
Mbali na soka, Bonanza hilo pia lilishirikisha michezo mbalimbali ikiwamo kuvuta kamba, kukimbia kwenye magunia, kucheza draft na bao, riadha mbio ndefu na fupi, mpira wa wavu na netiboli na washindi kupewa zawadi mbalimbali.
Bonanza hilo la kila mwaka na ambalo linafanyika kwa mara ya tisa sasa kwenye shamba la misitu la Sao Hill, lengo lake ni kuhimiza upandaji miti na kuimarisha ujirani mwema.
Bonanza hilo limeendelea kuwa mfano halisi wa kutumia michezo na burudani kuhamasisha upandaji miti, kauli mbiu yake inasema: ‘Panda miti kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.’

The post Ihefu kinara Sao Hill Bonanza 2023 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/18/ihefu-yangara-sao-hill-bonanza-2023/feed/ 0
Fainali Sao Hill Sport Bonanza Jumamosi https://www.greensports.co.tz/2023/12/15/fainali-sao-hill-sport-bonanza-jumamosi/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/15/fainali-sao-hill-sport-bonanza-jumamosi/#respond Fri, 15 Dec 2023 12:20:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8875 Na mwandishi wetuBonanza la Ujirani Mwema liloandaliwa na kudhaminiwa na Shamba la Miti la Sao Hill (Sao Hill Sport Bonanza) litafikia tamati kesho Jumamosi Desemba 16 kwa mechi ya soka ya fainali kati ya Ihefu FC na Mgololo Misitu.Mechi hiyo ya soka pamoja na michezo mingine itachezwa kwenye makao makuu ya shamba la Miti la […]

The post Fainali Sao Hill Sport Bonanza Jumamosi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Bonanza la Ujirani Mwema liloandaliwa na kudhaminiwa na Shamba la Miti la Sao Hill (Sao Hill Sport Bonanza) litafikia tamati kesho Jumamosi Desemba 16 kwa mechi ya soka ya fainali kati ya Ihefu FC na Mgololo Misitu.
Mechi hiyo ya soka pamoja na michezo mingine itachezwa kwenye makao makuu ya shamba la Miti la Sao Hill (Mafinga) Mufindi.
Timu 32 kutoka vijiji vyote vinavyozunguka msitu wa Shamba la Sao Hill kupitia tarafa nne ambazo ni Irundi, Ihefu, Ihalimba na Mgololo, zimeshiriki michuano hiyo kuanzia Desemba 9 mwaka huu.
Mbali na mechi hiyo ya soka pia kutakuwa na michezo mingine itakayopamba Bonanza hilo ambayo ni kufukuza kuku, kukimbia kwenye magunia, kucheza bao na draft, mashindano ya kula, riadha na kucheza muziki.
Pia kutakuwa na mechi za veterans toka Igowele na Misitu FC huku kauli mbiu ya mashindano hayo ikiwa ni Panda Miti Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi.

The post Fainali Sao Hill Sport Bonanza Jumamosi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/15/fainali-sao-hill-sport-bonanza-jumamosi/feed/ 0