miquissone - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 07 Sep 2023 19:16:34 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg miquissone - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Miquissone amkosha Robertinho https://www.greensports.co.tz/2023/09/07/miquissone-amkosha-robertinho/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/07/miquissone-amkosha-robertinho/#respond Thu, 07 Sep 2023 19:16:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7691 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, amempongeza kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Luis Miquissone kwa kupungua uzito akisema hilo ni jambo zuri kuelekea mchezo wa raundi ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos.Miquissone aliyetua Simba kwa mara ya pili mwanzoni mwa msimu huu akitokea Al Ahly ya Misri, […]

The post Miquissone amkosha Robertinho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, amempongeza kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Luis Miquissone kwa kupungua uzito akisema hilo ni jambo zuri kuelekea mchezo wa raundi ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos.
Miquissone aliyetua Simba kwa mara ya pili mwanzoni mwa msimu huu akitokea Al Ahly ya Misri, ameonekana kutokuwa kwenye kiwango chake kilichozoeleka kutokana na uzito alionao sasa tofauti na awali.

“Miquissone alikuja akiwa na uzito wa kilo 77, lakini kumpa program maalumu ya kupunguza uzito na mwili kwa sasa amepungua mapaka kilo 73, amekuwa mwepesi kuliko kawaida na amerudi kwenye kiwango chake kile cha zamani, naamini atakuwa msaada mkubwa kwenye mechi za kimataifa zinazotukabili,” alisema Robertinho.


Mbali na Miquissone, kocha huyo pia alifurahishwa kupona majeraha kwa Aubin Kramo, sanjari na kipa namba moja wa timu hiyo, Aishi Manula ambaye naye ameanza mazoezi mepesi wiki iliyopita akitarajiwa kujiunga na mazoezi ya kikosi siku chache za usoni.

The post Miquissone amkosha Robertinho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/07/miquissone-amkosha-robertinho/feed/ 0
Miquissone ahisi ana deni Simba https://www.greensports.co.tz/2023/07/26/miquissone-ahisi-ana-deni-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/26/miquissone-ahisi-ana-deni-simba/#respond Wed, 26 Jul 2023 19:32:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7139 Na mwandishi wetuWinga mpya wa Simba, Luis Miquissone (pichani) amesema anahisi ana deni kubwa na timu hiyo kutokana na mapokezi makubwa aliyopewa na kuahidi kuipigania mpaka mwisho.Miquissone raia wa Msumbiji ametua Simba kwa mara ya pili baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Al Ahly ya Misri hivi karibuni. Miquissone alienda Al Ahly misimu miwili […]

The post Miquissone ahisi ana deni Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Winga mpya wa Simba, Luis Miquissone (pichani) amesema anahisi ana deni kubwa na timu hiyo kutokana na mapokezi makubwa aliyopewa na kuahidi kuipigania mpaka mwisho.
Miquissone raia wa Msumbiji ametua Simba kwa mara ya pili baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Al Ahly ya Misri hivi karibuni. Miquissone alienda Al Ahly misimu miwili iliyopita akitokea Simba.
Mchezaji huyo ambaye ametua kwenye kambi ya maandalizi ya timu hiyo iliyopo Uturuki jana Jumanne, amesema pia anaamini kwa kushirikiana pamoja, timu hiyo itafikia malengo yake msimu ujao.

“Ningependa kuwashukuru Simba na mashabiki wote kwa mapokezi mazuri niliyoyapata. Mmenifanya nihisi nina majukumu makubwa ya kuipigania klabu hii kwa kweli. Kwa kushirikiana na kufanya kazi pamoja, naamini tutafikia malengo yetu,” alisema Miquissone.


Miquissone ni miongoni mwa wachezaji pendwa wa Simba ambaye hata baada ya kuondoka kwake, pengo lake liliendelea kuonekana na sasa amerejea kwa ajili ya kuirejeshea makali timu hiyo iliyokosa makombe kwa msimu wa pili mfululizo.

The post Miquissone ahisi ana deni Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/26/miquissone-ahisi-ana-deni-simba/feed/ 0
Hatimaye Miquissone arejea Simba https://www.greensports.co.tz/2023/07/22/hatimaye-miquissone-arejea-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/22/hatimaye-miquissone-arejea-simba/#respond Sat, 22 Jul 2023 14:12:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7079 Na mwandishi wetuSimba imeendelea kuimarisha kikosi chake cha msimu ujao baada ya leo Jumamosi kumtambulisha winga Luis Miquissone ambaye amerejea katika timu hiyo na kusaini mkataba wa miaka miwili.Miquissone ambaye habari ya kurejea kwake imezua mjadala siku za hivi karibuni huku baadhi ya wadau wa soka wakiwadhihaki viongozi wa Simba waliojinadi kuhusu kurejea kwa mchezaji […]

The post Hatimaye Miquissone arejea Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba imeendelea kuimarisha kikosi chake cha msimu ujao baada ya leo Jumamosi kumtambulisha winga Luis Miquissone ambaye amerejea katika timu hiyo na kusaini mkataba wa miaka miwili.
Miquissone ambaye habari ya kurejea kwake imezua mjadala siku za hivi karibuni huku baadhi ya wadau wa soka wakiwadhihaki viongozi wa Simba waliojinadi kuhusu kurejea kwa mchezaji huyo.
Mchezaji huyo ambaye tayari amekabidhiwa jezi namba 11, kurejea kwake kunamaliza mabishano ya hivi karibuni yaliyotawala kwenye mitandao ya kijamii.
Miquissone anarejea Simba akiwa mchezaji huru baada ya hivi karibuni kuvunja mkataba na mabingwa wa Afrika, Al Ahly ambayo ilikuwa ikimmiliki tangu msimu wa 2019/20 ilipomnunua kutoka Simba.
Akiwa Ahly hata hivyo Miquissone Septemba mwaka jana aliuzwa kwa mkopo katika klabu ya Abha ya Saudi Arabia ambako pia mambo yake hayakuwa mazuri kabla ya kurejea Simba.
Meneja Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema baada ya kukamilisha usajili wa mchezaji huyo wamesalia na nafasi moja ambayo ni ya kipa na wanatarajia kumtambulisha leo usiku au kesho Jumapili.

“Tumejipanga kuhakikisha msimu ujao Simba inarudisha mataji yake, tumemrudisha Miquissone hakuna asiyejua uwezo wake, imani yetu atasaidia mapambano kuelekea mapambano ya kuirudisha Simba kwenye mafanikio msimu ujao,” alisema Ahmed.


Alisema Miquissone raia wa Msumbiji anatarajiwa kuondoka nchini kuelekea Uturuki kesho kwenda kuungana na wachezaji wenzake kwenye kambi ya maandalizi ya msimu ujao.
Kabla ya kujiunga na Al Ahly, Miquissone aliitumikia Simba kwa misimu miwili na kuipa mafanikio makubwa ikiwemo mataji mawili ya Ligi Kuu NBC.
Miquissone pia aliwahi kutamba na timu za UD Songo ya Msumbiji pamoja na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

The post Hatimaye Miquissone arejea Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/22/hatimaye-miquissone-arejea-simba/feed/ 0
Hatma ya Miquissone Simba mikononi mwa Pablo https://www.greensports.co.tz/2022/05/13/hatma-ya-miquissone-simba-mikononi-mwa-pablo/ https://www.greensports.co.tz/2022/05/13/hatma-ya-miquissone-simba-mikononi-mwa-pablo/#respond Fri, 13 May 2022 13:03:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=719 Na mwandishi wetuUongozi wa klabu ya Simba hauna pingamizi kuhusu kurejea kwa mkopo kwa mshambuliaji wao wa zamani Luis Miquissone anayekipiga Al Ahly ya Misri iwapo kocha Pablo Franco atakubaliana na hilo.Imeelezwa kuwa mchezaji huyo tangu atue Al Ahly mwanzoni mwa msimu huu hana furaha kutokana nakukosa nafasi kikosi cha kwanza na amekuwa akitajwa kutaka […]

The post Hatma ya Miquissone Simba mikononi mwa Pablo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Luis Miquissone

Na mwandishi wetu
Uongozi wa klabu ya Simba hauna pingamizi kuhusu kurejea kwa mkopo kwa mshambuliaji wao wa zamani Luis Miquissone anayekipiga Al Ahly ya Misri iwapo kocha Pablo Franco atakubaliana na hilo.
Imeelezwa kuwa mchezaji huyo tangu atue Al Ahly mwanzoni mwa msimu huu hana furaha kutokana nakukosa nafasi kikosi cha kwanza na amekuwa akitajwa kutaka kurejea Simba kabla ya hivi karibuni kuibuka taarifa kwamba Al Ahly imependekeza kumrejesha Miquissone Simba kwa mkopo.
Taarifa zaidi kutoka duru mbalimbali za Misri zinaeleza kuwa timu hiyo inajipanga kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao ikitaka si tu kutwaa taji la Klabu Bingwa Afrika bali kutwaa ubingwa wa klabu wa dunia, hivyo miongoni mwa majina ya watakaopunguzwa la Miquissone lipo pia.
Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu amefafanua kuwa wao hawana pingamizi la kurejea kwa Miquissone kwa kuwa wao si tatizo mchezaji mzuri anapoamua kurudi alipotoka na kwamba wao hawatakuwa wa kwanza kufanya hivyo.
“Miquissone ni kijana wetu na hawa wachezaji mara nyingi wanapotoka kwenda timu nyingine huwa wanategemea mambo kuongezeka zaidi lakini kama inakuwa tofauti tunaweza kumpokea na hatutakuwa wa kwanza kufanya hivyo.
“Kuhusu kama kuna mawasiliano baina yetu na Al Ahly kuhusu dili hilo siwezi kusema ndiyo au hapana lakini hizi timu huwa tunawasiliana kila wakati na kama kuna jambo kama hilo nadhani wakati muafaka wa kulizungumzia ni mwisho wa msimu na si sasa tukiwa katikati ya msimu.
“Na hiyo ikiwa baada ya kusikiliza maoni ya kocha yeye anaonaje kuelekea msimu ujao na anatakaje, kwa hiyo atatutambia ilivyo na sisi tutaona itakavyokuwa lakini kwa sasa bado,” alisema Mangungu.
Hivi karibuni Simba ilimrejesha kiungo wake, Clatous Chama akitokea RS Berkane ya Morocco alikodumu kwa nusu msimu hivyo huenda ikafanya uamuzi wa kumrejesha Miquissone pia ili irejee kwenye makali yake ya awali.

The post Hatma ya Miquissone Simba mikononi mwa Pablo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/05/13/hatma-ya-miquissone-simba-mikononi-mwa-pablo/feed/ 0