Minziro - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 26 Feb 2024 18:49:34 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Minziro - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Minziro: Wachezaji walifuata melekezo https://www.greensports.co.tz/2024/02/26/minziro-wachezaji-walifuata-melekezo/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/26/minziro-wachezaji-walifuata-melekezo/#respond Mon, 26 Feb 2024 18:49:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9893 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Kagera Sugar, Fred Minziro amesema ushindi wa mabao 2-1 walioupata jana Jumapili dhidi ya Ihefu umetokana na wachezaji wake kufuata kikamilifu kile alichowaelekeza mazoezini.Minziro aliyewahi kuinoa Yanga, alisema walilazimika kubadili mfumo walioanza nao baada ya wapinzani wao Ihefu kuziba njia zote walizopanga kuzitumia na hiyo iliwasaidia kupata bao la ushindi.“Nawapongeza […]

The post Minziro: Wachezaji walifuata melekezo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Fred Minziro amesema ushindi wa mabao 2-1 walioupata jana Jumapili dhidi ya Ihefu umetokana na wachezaji wake kufuata kikamilifu kile alichowaelekeza mazoezini.
Minziro aliyewahi kuinoa Yanga, alisema walilazimika kubadili mfumo walioanza nao baada ya wapinzani wao Ihefu kuziba njia zote walizopanga kuzitumia na hiyo iliwasaidia kupata bao la ushindi.
“Nawapongeza wachezaji wangu kwa kufuata kile nilichowaelekeza na kupata ushindi, ulikuwa mchezo mgumu uliohitaji mbinu ili kupata ushindi na ndivyo tulivyofanya, malengo yetu ni kuendelea kufanya vizuri mechi zijazo,” alisema.
Naye kocha mkuu wa Ihefu, Mecky Maxime aliwapongeza wapinzani wao kwa ushindi huo lakini akaeleza kuvutiwa na ushindani ambao umeoneshwa na timu yake pia.

“Hongera kwa Kagera sababu wamepata pointi zote tatu lakini niseme mchezo ulikuwa ’50-50′ yoyote angeweza kushinda, pamoja na kupoteza mchezo huu lakini vijana wangu walicheza vizuri na kutoa upinzani mkubwa, tunakubali matokeo na sasa tunaangalia mechi zijazo,” alisema Maxime.


Kwa matokeo ya mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Kagera imepanda hadi nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC na kufikisha pointi 21.
Kipigo hicho kwa Ihefu kimeiacha katika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi zao 19 walizovuna kwenye michezo 17 waliyocheza hadi sasa.

The post Minziro: Wachezaji walifuata melekezo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/26/minziro-wachezaji-walifuata-melekezo/feed/ 0
Minziro kuondoa unyonge Kagera https://www.greensports.co.tz/2024/02/13/minziro-kuondoa-unyonge-kagera/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/13/minziro-kuondoa-unyonge-kagera/#respond Tue, 13 Feb 2024 19:39:03 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9716 Na mwandishi wetuKocha mkuu wa Kagera Sugar, Fred Minziro ameahidi kuiondolea timu hiyo unyonge na kuirudisha kwenye ushindani kama ilivyokuwa hapo awali.Akizungumza na GreenSports, Minziro alisema hiyo ni kutokana na wachezaji waliopo kuwa na uwezo mkubwa wa kushika haraka anachofundisha kwenye mazoezi.“Nataka kuirudisha Kagera Sugar ya zamani ambayo iliogopwa hata na timu vigogo na hilo […]

The post Minziro kuondoa unyonge Kagera first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Kagera Sugar, Fred Minziro ameahidi kuiondolea timu hiyo unyonge na kuirudisha kwenye ushindani kama ilivyokuwa hapo awali.
Akizungumza na GreenSports, Minziro alisema hiyo ni kutokana na wachezaji waliopo kuwa na uwezo mkubwa wa kushika haraka anachofundisha kwenye mazoezi.
“Nataka kuirudisha Kagera Sugar ya zamani ambayo iliogopwa hata na timu vigogo na hilo linawezekana kutokana na aina ya wachezaji nilionao kwenye kikosi changu, wana uwezo mkubwa wa kushika ninachowaelekeza,” alisema Minziro.
Alisema mechi mbili walizocheza katika uwanja wa nyumbani wa Kaitaba na kuvuna pointi nne zimempa mwanzo mzuri wa kutimiza kile ambacho amekiahidi kwa uongozi na mashabiki wa timu hiyo.
Alisema kwa kuwa ameichukua timu hiyo ikiwa nafasi za chini kwenye msimamo, mikakati yake ni kushinda mechi zote watakazocheza nyumbani huku wakitafuta sare au ushindi mechi za ugenini.
Kagera Sugar chini ya Minziro imepata ushindi wake wa kwanza wa bao 1-0 dhidi ya Singida Fountain Gate na kupanda hadi nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC wakiwa na pointi 17.

The post Minziro kuondoa unyonge Kagera first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/13/minziro-kuondoa-unyonge-kagera/feed/ 0
Kagera yaanika sifa za Minziro https://www.greensports.co.tz/2024/02/01/kagera-yaanika-sifa-za-minziro/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/01/kagera-yaanika-sifa-za-minziro/#respond Thu, 01 Feb 2024 19:15:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9552 Na mwandishi wetuUongozi wa timu ya Kagera Sugar umeeleza uzoefu na ubora wa kazi ya Fred Felix Minziro ndivyo vilivyopelekea wakampa ukocha mkuu wa timu hiyo kwa muda wa mwaka mmoja.Akizungumza na GreenSports, Katibu Mkuu wa Kagera Sugar, Ally Masoud alisema wamemchukua Minziro wakiamini kile alichonacho na rekodi alizonazo katika kuzifundisha timu mbalimbali za Ligi […]

The post Kagera yaanika sifa za Minziro first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Uongozi wa timu ya Kagera Sugar umeeleza uzoefu na ubora wa kazi ya Fred Felix Minziro ndivyo vilivyopelekea wakampa ukocha mkuu wa timu hiyo kwa muda wa mwaka mmoja.
Akizungumza na GreenSports, Katibu Mkuu wa Kagera Sugar, Ally Masoud alisema wamemchukua Minziro wakiamini kile alichonacho na rekodi alizonazo katika kuzifundisha timu mbalimbali za Ligi Kuu NBC.

“Minziro ni kocha mwenye rekodi nyingi na uzoefu wa kutosha katika kufundisha timu za Ligi Kuu Tanzania Bara, hicho ndio kimetuvutia na kuamua kumkabidhi kikosi chetu tukiamini atatufikisha tulipokusudia,” alisema Masoud.


Kiongozi huyo alisema kwa kutumia uwezo wake yeye na wenzake wanaamini ataitoa timu yao kwenye nafasi mbaya na kuwaweka nafasi za juu na salama kwao.
Naye Minziro alisema: “Nawashukuru viongozi wa Kagera Sugar kwa kuniona nafaa kuifundisha timu yao, naahidi kuitumia vizuri nafasi hii kwa kuirudisha kwenye mbio za ubingwa lakini ili tufanikiwe hayo naomba ushirikiano kuanzia viongozi hadi wachezaji,” alisema Minziro.
Minziro kabla ya kutambulishwa Kagera jana Jumatano, alikuwa akiinoa Tanzania Prisons ambayo ilimfuta kazi mwezi mmoja uliopita kutokana na matokeo mabaya iliyokuwa ikiyapata timu hiyo.

The post Kagera yaanika sifa za Minziro first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/01/kagera-yaanika-sifa-za-minziro/feed/ 0
Ratiba ligi kuu yamkera Minziro https://www.greensports.co.tz/2023/11/10/ratiba-ligi-kuu-yamkera-minziro/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/10/ratiba-ligi-kuu-yamkera-minziro/#respond Fri, 10 Nov 2023 19:25:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8426 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa timu ya Prisons, Fred Minziro ameeleza kuwa ratiba ya mechi zake imekuwa sababu kubwa ya kufanya vibaya kwenye michuano ya Ligi Kuu NBC msimu huu. Minziro ameiambia GreenSports leo Ijumaa kuwa hajaridhishwa na ratiba inayopangiwa timu yake akichukulia mfano wa mechi tatu za mwisho wamecheza ndani ya siku nane katika […]

The post Ratiba ligi kuu yamkera Minziro first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa timu ya Prisons, Fred Minziro ameeleza kuwa ratiba ya mechi zake imekuwa sababu kubwa ya kufanya vibaya kwenye michuano ya Ligi Kuu NBC msimu huu.

Minziro ameiambia GreenSports leo Ijumaa kuwa hajaridhishwa na ratiba inayopangiwa timu yake akichukulia mfano wa mechi tatu za mwisho wamecheza ndani ya siku nane katika mikoa mitatu tofauti.

“Hatujafanya vizuri lakini kuna sehemu ni kama ratiba inatukandamiza, sababu huwezi kucheza mechi tatu ndani ya siku nane, tumecheza na KMC tarehe 27 tukiwa Dar es Salaam kisha tukacheza na Geita (Gold) tukiwa Mbeya.

“Baada ya hapo tarehe 3 ikabidi tuifuate Kagera Sugar kwao, na wakati huo Kagera haina mchezo wowote, imepumzika muda mrefu kwao, sasa kulikuwa na ulazima gani wa kuwahisha mchezo kama huo?” Alihoji Minziro kocha wa zamani wa Yanga na Geita.

Minziro alisema kuwa uchovu wa mfululizo wa mechi hizo ambazo walipata pointi mbili pekee baada ya sare ya KMC na Geita kabla ya kufungwa na Kagera mabao 2-1, unachangia kuzorota kwa utendaji kazi wa wachezaji wake na kupelekea matokeo yasiyoridhisha.

Kocha huyo hata hivyo, alisisitiza kuwa sasa anakwenda kujipanga pia kurekebisha makosa machache aliyoyaona kuhakikisha wanaanza na ushindi katika mechi yao inayofuata dhidi ya Coastal Union, Novemba 23, mwaka huu ili kurejesha hali ya ushindani na matumaini ya kupambana.

Kwenye ligi hiyo inayoshirikisha jumla ya timu 16, Prisons kwa sasa inashika nafasi ya 14 baada ya kucheza mechi tisa.

The post Ratiba ligi kuu yamkera Minziro first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/10/ratiba-ligi-kuu-yamkera-minziro/feed/ 0
‘Nidhamu imetupa pointi Singida’ https://www.greensports.co.tz/2023/08/24/nidhamu-imetupa-pointi-singida/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/24/nidhamu-imetupa-pointi-singida/#respond Thu, 24 Aug 2023 05:43:06 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7503 Na mwandishi wetuKocha wa Tanzania Prisons, Fred Minziro amesema nidhamu iliyooneshwa na wachezaji wake katika mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate imewasaidia kuondoka na pointi moja katika mechi hiyo iliyoisha kwa suluhu.Katika mechi hiyo Prisons ilikuwa ugenini katika Uwanja wa Liti, Singida ambapo Minziro amekiri kulingana na ugumu wa mchezo pointi hiyo imekuwa halali kwao.“Singida […]

The post ‘Nidhamu imetupa pointi Singida’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha wa Tanzania Prisons, Fred Minziro amesema nidhamu iliyooneshwa na wachezaji wake katika mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate imewasaidia kuondoka na pointi moja katika mechi hiyo iliyoisha kwa suluhu.
Katika mechi hiyo Prisons ilikuwa ugenini katika Uwanja wa Liti, Singida ambapo Minziro amekiri kulingana na ugumu wa mchezo pointi hiyo imekuwa halali kwao.
“Singida wana timu nzuri, wamefanya usajili mzuri, wanacheza kitimu. Tulijaribu kuwaruhusu kucheza kutoka nyuma na vijana wangu walicheza kwa nidhamu wakafanikiwa kuwadhibiti,” alisema.
Kwa upande wa Kocha Msaidizi wa Singida, Mathias Lule alisema licha ya kumiliki mpira lakini walishindwa kupata ushindi akisema huenda ni kwa sababu wamechoka wakitoka kucheza mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya JKU ambao walishinda kwa mabao 4-2.

“Tumemaliza salama mchezo wetu, tulikosea kwa sababu hatujapumzika vizuri, tulifanya kila kitu lakini haikuwa bahati yetu, tulipoteza nafasi ambazo zingetupa ushindi lakini ndio soka lilivyo,” alisema Minziro.


Alisema wataendelea kujiimarisha zaidi kwa kuwa bado ni mwanzo wa ligi, wataendelea kujipanga kwa michezo ijayo kwa kufanyia kazi mapungufu yao kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi msimu huu.

The post ‘Nidhamu imetupa pointi Singida’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/24/nidhamu-imetupa-pointi-singida/feed/ 0
Minziro aomba ushirikiano Prisons https://www.greensports.co.tz/2023/07/25/minziro-aomba-ushirikiano-prisons/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/25/minziro-aomba-ushirikiano-prisons/#respond Tue, 25 Jul 2023 18:56:06 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7116 Na mwandishi wetuKocha mpya wa Tanzania Prisons, Fred Minziro ameomba ushirikiano kutoka kwa viongozi, wachezaji na mashabiki wa timu hiyo ili kufikia malengo waliyojipangia.Maafande hao mipango yao ni kumaliza ligi ndani ya nafasi nne za juu msimu ujao ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya klabu Afrika.Kocha huyo alieleza kuwa malengo hayo yanaweza kufikiwa lakini […]

The post Minziro aomba ushirikiano Prisons first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mpya wa Tanzania Prisons, Fred Minziro ameomba ushirikiano kutoka kwa viongozi, wachezaji na mashabiki wa timu hiyo ili kufikia malengo waliyojipangia.
Maafande hao mipango yao ni kumaliza ligi ndani ya nafasi nne za juu msimu ujao ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya klabu Afrika.
Kocha huyo alieleza kuwa malengo hayo yanaweza kufikiwa lakini kitu cha msingi anahitaji umoja na mshikamano kutoka kwa uongozi, wachezaji pamoja na mashabiki.
“Nataka kuirudisha Prisons ile ya zamani na kutoa upinzani kwenye ligi, hilo linawezekana endapo tutafanya usajili mzuri sababu ligi ya msimu ujao itakuwa ngumu, tunasikia wenzetu kila siku wanasajili wachezaji wakubwa lakini kama tutajipanga vizuri na tukawa na umoja sidhani kama kuna kitakachotusumbua,” alisema Minziro.
Alisema kwa sasa timu yake imeshaanza mazoezi lakini akiwa na wachezaji walioitumikia timu hiyo kwenye msimu uliopita na baada ya wiki moja anatarajia kuanza kuwapokea wachezaji wapya ambao wamewasajili kwa ajili ya msimu ujao.
Alisema baada ya wachezaji wote kukamilika wanatarajia kwenda Zanzibar au sehemu nyingine ambayo uongozi utaichagua kwenda kupiga kambi kujiandaa na msimu mpya ambao umepangwa kuanza Agosti 15, mwaka huu.
Minziro ametua Prisons akitokea Geita Gold, ambayo aliifundisha kwa mafanikio na kuiwezesha kumaliza nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi hiyo ambayo inashirikisha timu 16.

The post Minziro aomba ushirikiano Prisons first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/25/minziro-aomba-ushirikiano-prisons/feed/ 0
Minziro ajiweka kando Geita Gold https://www.greensports.co.tz/2023/06/06/minziro-ajiweka-kando-geita-gold/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/06/minziro-ajiweka-kando-geita-gold/#respond Tue, 06 Jun 2023 20:21:19 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6483 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Geita Gold, Fred Felix Minziro amejiweka kando na timu hiyo baada ya kile kilichoelezwa kuwa ni kushindwana kwa maslahi binafsi nje ya mkataba baina ya pande hizo.Minziro ameiambia GreenSports leo Jumanne kuwa amekaa kando kutokana na timu hiyo kumkatalia matakwa yake ya kumlipa kiasi cha pesa alichowatajia katika mechi mbili […]

The post Minziro ajiweka kando Geita Gold first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Geita Gold, Fred Felix Minziro amejiweka kando na timu hiyo baada ya kile kilichoelezwa kuwa ni kushindwana kwa maslahi binafsi nje ya mkataba baina ya pande hizo.
Minziro ameiambia GreenSports leo Jumanne kuwa amekaa kando kutokana na timu hiyo kumkatalia matakwa yake ya kumlipa kiasi cha pesa alichowatajia katika mechi mbili zilizosalia za Ligi Kuu NBC msimu huu.
“Mkataba wangu umeisha tangu Mei 28, niko nje ya mkataba nikijihudumia kwa kila kitu hivyo nikawaambia wanipe pesa kidogo kwa ajili ya kumaliza hizo mechi mbili na siwezi kuwatajia pesa kubwa sababu mimi niko na timu mwaka wa tatu sasa, lakini wakanijibu hawana kiasi hicho.

“Basi mimi nimeondoka zangu, niko Dar es Salaam naendelea na mambo mengine maana kwa tafsiri fupi unaweza kusema hawakutaka labda niendelee kwenye mechi hizi mbili na uzuri nimezungumza nao, tumemalizana vizuri,” alisema Minziro.


Alipotafutwa Ofisa Habari wa Geita, Samwel Dida alisema: “Hizi mechi mbili ziko nje ya mkataba wake, tukamwomba amalizie hizi dakika 180, akatupa utaratibu wake wa malipo, tuliona hatuwezi kumudu na yeye akawa na msimamo wake basi tukamalizana.”
Dida pia alisema mechi zao mbili zilizosalia ikiwemo ya leo dhidi ya Ihefu na ya Mei 9, mwaka huu dhidi ya Mtibwa Sugar, kikosi chao kitakuwa chini ya kocha wa timu ya vijana, Choke Abeid.
Dida aliongeza kuwa kulingana na hali iliyopo sasa baada ya kushindwana na Minziro, imekuwa ngumu kufahamu kama watakua na kocha huyo msimu ujao au la.

The post Minziro ajiweka kando Geita Gold first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/06/minziro-ajiweka-kando-geita-gold/feed/ 0
Minziro awapongeza wachezaji Geita https://www.greensports.co.tz/2023/05/26/minziro-awapongeza-wachezaji-geita/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/26/minziro-awapongeza-wachezaji-geita/#respond Fri, 26 May 2023 05:59:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6288 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Geita Gold, Fred Minziro amewapongeza wachezaji wake kwa kupambana kuifikisha timu hiyo hapo ilipo licha ya changamoto nyingi walizopitia msimu huu.Geita inashikilia nafasi ya sita kwa pointi 37 ikipambana kumaliza ndani ya tano bora katika michezo miwili iliyosalia kabla ya kufungwa pazia la Ligi Kuu NBC msimu wa 2022-23.Minziro (pichani […]

The post Minziro awapongeza wachezaji Geita first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Geita Gold, Fred Minziro amewapongeza wachezaji wake kwa kupambana kuifikisha timu hiyo hapo ilipo licha ya changamoto nyingi walizopitia msimu huu.
Geita inashikilia nafasi ya sita kwa pointi 37 ikipambana kumaliza ndani ya tano bora katika michezo miwili iliyosalia kabla ya kufungwa pazia la Ligi Kuu NBC msimu wa 2022-23.
Minziro (pichani juu) alifafanua kwamba haikuwa rahisi kwa timu hiyo kuendelea kupambana na kufika hapo licha ya kuondokewa na wachezaji wao wengi waliokuwa wakiunda kikosi cha kwanza cha timu hiyo ilioyoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza msimu huu.
“Kama ilivyoonekana wachezaji wengi waliondoka kwenye dirisha dogo la usajili na wengi walikuwa ni kikosi cha kwanza lakini wachezaji waliobaki walipambana, tukawa pamoja na tumefika hapa nawapongeza sana.

“Bado tunajipanga kuhakikisha tunamaliza ligi ndani ya tano bora, tunapishana pointi mbili na Namungo walio nafasi ya tano, hivyo bado tuna nafasi na wachezaji wapambanaji ninao pia,” alisema Minziro.


Miongoni mwa nyota walioihama timu hiyo katika dirisha dogo ni Saido Ntbazonkiza aliyeenda Simba, Yahya Mbegu aliyetua Ihefu, Kevin Nashon na Yusuf Kagoma waliotimkia Singida BS na George Mpole aliyesajiliwa FC Lupopo ya DR Congo.

The post Minziro awapongeza wachezaji Geita first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/26/minziro-awapongeza-wachezaji-geita/feed/ 0
Geita kupigania nne bora https://www.greensports.co.tz/2023/03/21/geita-kupigania-nne-bora/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/21/geita-kupigania-nne-bora/#respond Tue, 21 Mar 2023 18:24:57 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5549 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Geita Gold, Fredy Minziro ametamba kuwa atapambana kuhakikisha timu yake inakuwa kati ya timu nne zitakazopeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya kimataifa msimu ujao.Tanzania itapeleka timu nne kwenye michuano ya klabu Afrika baada ya timu za Simba na Yanga kufanya vizuri kwenye mechi za hatua ya makundi ya Ligi […]

The post Geita kupigania nne bora first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Geita Gold, Fredy Minziro ametamba kuwa atapambana kuhakikisha timu yake inakuwa kati ya timu nne zitakazopeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya kimataifa msimu ujao.
Tanzania itapeleka timu nne kwenye michuano ya klabu Afrika baada ya timu za Simba na Yanga kufanya vizuri kwenye mechi za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika ikiwemo timu zote mbili kutinga hatua ya robo fainali.
Kocha huyo ameeleza kuwa malengo yake ni kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mashindano yote mawili wanayoshiriki kwa maana ya Ligi Kuu NBC na Kombe la FA, ambayo ndio yanatoa nafasi za kushiriki michuano hiyo.

“Tunaitaka michuano ya kimataifa kwa mara nyingine tena baada ya mwaka huu kutolewa hatua ya awali, kitu kizuri nafasi ya kufanya hivyo bado ipo sababu kwenye msimamo wa ligi tupo nafasi ya tano na kwenye Kombe la FA tupo robo fainali na tutacheza na Yanga hilo halitupi presha,” alisema Minziro.


Minziro amesema kuwa wapinzani wao wakubwa katika kampeni ya kusaka nafasi ya kuwakilisha taifa kwenye michuano ya kimataifa ni Azam na Singida Big Stars ambazo zipo juu yao kwenye msimamo wa ligi na imani yake ni kushinda mechi zao tano zilizobaki kwenye ligi ili kupata nafasi hiyo.
Alisema kwenye Kombe la FA, anajua wanakwenda kukutana na bingwa mtetezi Yanga, anajua utakuwa mchezo mgumu lakini wamejipanga kuhakikisha wanapambana kuvuka kigingi hicho ili kuendelea kwenye hatua zinazofuata na kutinga fainali.
Geita msimu huu ilitolewa kwenye hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho na Hilal Alsahil ya Sudan, mechi ya kwanza Geita ikiwa ugenini ilifungwa bao 1-0 kabla ya kushinda 2-1 kwenye mechi ya nyumbani na hivyo kutolewa kwa bao la ugenini.

The post Geita kupigania nne bora first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/21/geita-kupigania-nne-bora/feed/ 0
Mkataba wa Minziro Geita wachelewa https://www.greensports.co.tz/2022/08/11/mkataba-wa-minziro-geita-wachelewa/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/11/mkataba-wa-minziro-geita-wachelewa/#respond Thu, 11 Aug 2022 15:11:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2337 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Geita Gold, Fred Minziro ameeleza hofu aliyonayo juu ya kuchelewa kuongeza mkataba mpya kuinoa timu hiyo namna inavyoweza kumkwamisha kwenye michuano watakayoshiriki msimu ujao.Imeelezwa kuwa leo au kesho ilitarajiwa kukamilika kwa dili hilo ambalo limechelewa kutokana na sababu mbalimbali ambazo Minziro hakutaka kuziweka wazi akidai ni majadiliano ya kimkataba.Minziro aliyeipandisha […]

The post Mkataba wa Minziro Geita wachelewa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Geita Gold, Fred Minziro ameeleza hofu aliyonayo juu ya kuchelewa kuongeza mkataba mpya kuinoa timu hiyo namna inavyoweza kumkwamisha kwenye michuano watakayoshiriki msimu ujao.
Imeelezwa kuwa leo au kesho ilitarajiwa kukamilika kwa dili hilo ambalo limechelewa kutokana na sababu mbalimbali ambazo Minziro hakutaka kuziweka wazi akidai ni majadiliano ya kimkataba.
Minziro aliyeipandisha timu hiyo kushiriki Ligi Kuu Bara mara ya kwanza msimu uliopita alisema kwa sasa yupo mbali na maandalizi ya timu mpaka amalizane na uongozi, ingawa benchi la ufundi linaendelea na kazi lakini bado haileti afya ya maandalizi ya timu.
“Ni kweli ligi inaanza wiki ijayo tu hapo, maandalizi yanaendelea lakini hasa nilihitaji kuwa na mechi hasa za kirafiki kuona mapungufu mapema lakini ni kama tumechelewa kwa sababu bado sijamalizana na uongozi juu ya mkataba.
“Pengine leo au kesho naweza nikaenda Geita kumaliza hilo maana hata leo tumewasiliana, mazungumzo yanakwenda vizuri lakini wasiwasi ni muda wa maandalizi ya timu na michuano tuliyonayo msimu ujao,” alisema Minziro kocha na mchezaji wa zamani wa Yanga.
Geita iliyomaliza nafasi ya nne msimu uliopita, msimu ujao mbali na michuano ya Ligi Kuu Bara na Kombe la FA lakini pia watakuwa na kibarua kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ikitarajia kuanza hatua ya awali dhidi ya Hilal Alsahil ya Sudan.
Katika mechi hizo za hatua ya awali, Geita itaanzia ugenini Septemba 9 kabla ya kurudiana kwenye mchezo watakaokuwa nyumbani mnamo Septemba 16, mwaka huu.

The post Mkataba wa Minziro Geita wachelewa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/11/mkataba-wa-minziro-geita-wachelewa/feed/ 0