Michezo - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 23 Sep 2023 13:25:57 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Michezo - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Msigwa sasa katibu mkuu michezo https://www.greensports.co.tz/2023/09/23/msigwa-sasa-katibu-mkuu-michezo/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/23/msigwa-sasa-katibu-mkuu-michezo/#respond Sat, 23 Sep 2023 13:25:56 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7835 Na mwandishi wetuRais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Gerson Msigwa (pichani) kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo akichukua nafasi ya Said Yakubu ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.Uteuzi huo wa Msigwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali umetangazwa leo Jumamosi kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais […]

The post Msigwa sasa katibu mkuu michezo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Gerson Msigwa (pichani) kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo akichukua nafasi ya Said Yakubu ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
Uteuzi huo wa Msigwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali umetangazwa leo Jumamosi kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa nafasi iliyoachwa wazi na Msigwa ambaye ataapishwa Jumanne ya keshokutwa Ikulu ya Dar es Salaam, itatangazwa mrithi wake hapo baadaye.
Mabadiliko hayo yamekuja ikiwa ni wiki tatu zimepita tangu Rais Samia amteue Dk Damas Ndumbaro kuwa waziri wa wizara hiyo akichukua nafasi ya Dk Pindi Chana aliyehamishiwa Wizara ya Katiba na Sheria.
Kabla ya uteuzi huo, Msigwa amehudumu kamaar mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi (Ikulu) chini ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu na Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli.
Na baada ya kudumu kwa miaka mitano na nusu katika wadhifa huo, Aprili 4, mwaka juzi Msigwa aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.

The post Msigwa sasa katibu mkuu michezo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/23/msigwa-sasa-katibu-mkuu-michezo/feed/ 0