Michael Carrick - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 18 Apr 2026 19:51:15 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Michael Carrick - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Carrick ampigia hesabu Rashford https://www.greensports.co.tz/2026/04/18/carrick-ampigia-hesabu-rashford/ https://www.greensports.co.tz/2026/04/18/carrick-ampigia-hesabu-rashford/#respond Sat, 18 Apr 2026 19:51:12 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14535 Manchester, EnglandKocha wa Man United, Michael Carrick amekataa kufuta uwezekano wa kurejea kwa mshambuliaji wa timu hiyo, Marcus Rashdord ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika klabu ya Barcelona.Kauli ya kocha huyo wa muda imekuja wakati huu kukiwa na hali isiyoeleweka kuhusu mambo ya baadaye ya Rashford katika kikosi cha Barcelona.Rashford, 28, ambaye pia ni […]

The post Carrick ampigia hesabu Rashford first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kocha wa Man United, Michael Carrick amekataa kufuta uwezekano wa kurejea kwa mshambuliaji wa timu hiyo, Marcus Rashdord ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika klabu ya Barcelona.
Kauli ya kocha huyo wa muda imekuja wakati huu kukiwa na hali isiyoeleweka kuhusu mambo ya baadaye ya Rashford katika kikosi cha Barcelona.
Rashford, 28, ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya England mara ya mwisho kuichezea Man United, ilikuwa Desemba 2024 na kumalizia msimu uliopita akiwa Aston Villa kwa mkopo kabla ya kuhamia Barcelona katika msimu wa 2025-26.
Barcelona au Barca inaweza kumsajili Rashford kwa dau la Pauni 30 milioni wakati wa majira ya kiangazi kama sehemu ya makubaliano ambayo yatamfanya mshambuliaji huyo kubaki katika klabu hiyo.
Wakati huo huo Man United wanafuatilia kwa karibu habari za nchini Hispania zinazodai kwamba Barcelona wana nia ya kufanya mazungumzo mapya kuhusu mchezaji huyo ikiwamo kupunguza ada yake ili aendelee kuwa hapo kwa mkopo katika makubaliano mengine.
Kwa upande mwingine mabosi wa Man United wanadaiwa kutokuwa tayari kwa mazungumzo mengine kuhusu usajili wa mshambulijai huyo na badala yake wanataka kumrudisha katika klabu hiyo iwapo Barca hawatapanda dau.
Man United wanaamini kiwango cha Rashford katika La Liga kimekuwa juu hivyo wanaweza kuwa na nafasi ya kufanya mazungumzo na klabu nyingine ikiwamo kupandisha ada ya uhamisho iwapo Barca hawatakuwa tayari.

The post Carrick ampigia hesabu Rashford first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/04/18/carrick-ampigia-hesabu-rashford/feed/ 0
Carrick ampotezea Rooney https://www.greensports.co.tz/2026/03/17/carrick-ampotezea-rooney/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/17/carrick-ampotezea-rooney/#respond Tue, 17 Mar 2026 12:08:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14451 Manchester, EnglandKocha wa muda wa Man United, Michael Carrick amesisitiza kuwa hasikilizi kauli zikiwamo za mchezaji mwenzake wa zamani wa timu hiyo, Wayne Rooney kudai kwamba kocha huyo sasa anatakiwa kupewa mkataba wa kudumu.Ushindi wa mabao 3-1 ambao Man United iliupata Jumapili dhidi ya Aston Villa umezidi kumpaisha kocha huyo na hatimaye kuibua hoja ya […]

The post Carrick ampotezea Rooney first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kocha wa muda wa Man United, Michael Carrick amesisitiza kuwa hasikilizi kauli zikiwamo za mchezaji mwenzake wa zamani wa timu hiyo, Wayne Rooney kudai kwamba kocha huyo sasa anatakiwa kupewa mkataba wa kudumu.
Ushindi wa mabao 3-1 ambao Man United iliupata Jumapili dhidi ya Aston Villa umezidi kumpaisha kocha huyo na hatimaye kuibua hoja ya kuwataka mabosi wa klabu kumpa mkataba wa kudumu.
Huo ni ushindi wa saba katika mechi tisa za Carrick, ushindi ambao umeianya timu hiyo kuiacha Chelsea inayoshika nafasi ya sita kwa tofauti ya pointi sita na kujiweka katika nafasi nzuri ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Matokeo hayo yamemfanya Rooney katika mazungumzo yake na kituo kimoja cha redio kusema kwamba sasa ni kwa asilimia 100, Carrick anatakiwa kupewa mkataba wa kudumu Man United.
Rooney alifafanua kuwa anamjua vizuri Carrick na tabia zake na jinsi alivyo katika timu ambayo inahitaji mtu mwenye utulivu na ambaye anaijua timu hiyo na wachezaji ambao wanahitaji upendo na anawapa vyote hivyo.
Kwa upande wake Carrick alipoulizwa kuhusu hilo alicheka na kupuuza kila kinachozungumzwa na kusema kwamba hizo ni kelele tu za jumla na si Rooney pekee yake.

“Hazina madhara yoyote kwangu, kwa wakati huu nipo katika kazi ambayo naifanya kwa ubora wangu na tunaendelea kupambana zaidi na zaidi, tunataka kuifanya timu iwe bora kadri iwezekanavyo, lolote linaloweza kutokea tuache litokee,” alisema.


Nahodha wa timu hiyo, Bruno Fernandes ameendelea kuwa mtu muhimu kikosini akitoa pasi muhimu zinazozaa mabao, katika mechi na Villa alitoa pasi mbili ambazo Cunha na Casemiro walizitumia kuipatia Man United mabao.

The post Carrick ampotezea Rooney first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/17/carrick-ampotezea-rooney/feed/ 0
Carrick: Mashabiki hawanipi presha https://www.greensports.co.tz/2026/02/01/carrick-mashabiki-hawanipi-presha/ https://www.greensports.co.tz/2026/02/01/carrick-mashabiki-hawanipi-presha/#respond Sun, 01 Feb 2026 12:14:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14307 Manchester, EnglandKocha wa Man United, Michael Carrick amesema hatarajii mgomo wa mashabiki dhidi ya wamiliki wa klabu hiyo, Familia ya Glazer na Sir Jim Ratcliffe kuiathiri timu yake katika mechi dhidi ya Fulham Jumapili hii.Hali ya utulivu imeanza kurejea katika klabu hiyo ya Old Trafford chini ya Carrick aliyeanza kibarua kwa ushindi wa mabao 2-0 […]

The post Carrick: Mashabiki hawanipi presha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kocha wa Man United, Michael Carrick amesema hatarajii mgomo wa mashabiki dhidi ya wamiliki wa klabu hiyo, Familia ya Glazer na Sir Jim Ratcliffe kuiathiri timu yake katika mechi dhidi ya Fulham Jumapili hii.
Hali ya utulivu imeanza kurejea katika klabu hiyo ya Old Trafford chini ya Carrick aliyeanza kibarua kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mahasimu wao wa jiji la Manchster, Man City kisha kuichapa Arsenal mabao 3-2 wiki iliyopita.
Man United inatarajia kuendeleza wimbi la ushindi Jumapili hii Februari mosi, 2026 dhidi ya Fulham wakati huo huo kukiwa na utata kutoka maelfu ya mashabiki ambao inatarajiwa kabla ya mechi hiyo wataanika kero yao ya kuwapinga wamiliki wa klabu hiyo.
Familia ya Glazer ambayo iliinunua klabu hiyo mwaka 2005 imekuwa ikisakamwa na mashabiki kama ambavyo imekuwa kwa Sir Jim Ratcliffe ambaye alinunua sehemu ya hisa za klabu hiyo mapema mwaka 2024 naye amejikuta katika hali hiyo hasa katika miezi ya karibuni.

“Sidhani kama kuna uhusiano wowote wa hali hiyo na ushindi wa mechi mbili, niwe mkweli nadhani haina athari yoyote kwa timu, nawaheshimu mashabiki, ni watu wa kipekee, wamekuwa na timu hii kwa muda mrefu,” alisema Carrick ambaye alikabidhiwa timu hiyo Januari 8 mwaka huu baada ya kutimuliwa kwa Ruben Amorim.


Carrick ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa nafasi ya kiungo katika timu hiyo alisema mashabiki wana mambo yao mazuri na mabaya pia lakini hawamsemi yeye kwa ubaya na wachezaji pia hawana ubaya nao.
Alisema uhusiano wake na mashabiki katika wiki chache zilizopita umekuwa ni wa kipekee na kusisitiza kwamba mashabiki wamekuwa hivyo kwa wakati wote na anaamini wataendelea kuwa hivyo.

The post Carrick: Mashabiki hawanipi presha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/02/01/carrick-mashabiki-hawanipi-presha/feed/ 0