Mgunda - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 04 Jun 2024 07:10:36 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Mgunda - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mgunda, Lusajo wang’ara mwezi Mei https://www.greensports.co.tz/2024/06/04/mgunda-lusajo-wangara-mwezi-mei/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/04/mgunda-lusajo-wangara-mwezi-mei/#respond Tue, 04 Jun 2024 07:10:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11212 Na mwandishi wetuKaimu kocha mkuu Simba, Juma Mgunda ameteuliwa kuwa kocha bora wa mwezi Mei huku mshambuliaji wa Mashujaa FC, Reliant Lusajo akiteuliwa mchezaji bora, wote kwa msimu huu wa 2023-24 wa Ligi Kuu NBC.Taarifa ya Idara ya habari, mawasiliano ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilimtaja Lusajo kuwa mshindi akiwabwaga, Stephane Aziz Ki […]

The post Mgunda, Lusajo wang’ara mwezi Mei first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kaimu kocha mkuu Simba, Juma Mgunda ameteuliwa kuwa kocha bora wa mwezi Mei huku mshambuliaji wa Mashujaa FC, Reliant Lusajo akiteuliwa mchezaji bora, wote kwa msimu huu wa 2023-24 wa Ligi Kuu NBC.
Taarifa ya Idara ya habari, mawasiliano ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilimtaja Lusajo kuwa mshindi akiwabwaga, Stephane Aziz Ki wa Yanga na Feisal Salum au Fei Toto wa Azam FC.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kamati ya tuzo hizo ya TFF ilimteua Lusajo kwa kuwa alikuwa msaada mkubwa kwa timu yake katika ushindi wa mechi nne kati ya sita za timu hiyo kwa kipindi cha mwezi Mei.
Mchango wa Lusajo uliiwezesha Mashujaa kukusanya pointi 12 na hivyo kupanda kutoka nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC hadi nafasi ya nane huku Lusajo akifunga mabao matano na kuwa ‘mpishi’ wa mabao mengine mawili.
Kwa upande wa Mgunda ambaye aliteuliwa kukaimu nafasi hiyo baada ya Abdelhak Benchikha kuamua kuachia ngazi, yeye ameiwezesha Simba katika kipindi hicho kushinda mechi zake dhidi ya Tabora United, Azam, Prisons, Geita, KMC, JKT na kutoka sare ya 1-1 na Kagera Sugar.
Mgunda katika kinyang’anyiro cha kocha bora wa mwezi Mei alikuwa akishindana na Miguel Gamondi wa Yanga na Bruno Ferry wa Azam.
Kamati ya tuzo pia imemteua meneja wa Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Juma Amir kuwa meneja bora wa mwezi Mei kutokana na usimamizi mzuri wa matukio ya uwanjani pamoja na masuala yanayohusu miundombinu ya uwanja

The post Mgunda, Lusajo wang’ara mwezi Mei first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/04/mgunda-lusajo-wangara-mwezi-mei/feed/ 0
Mgunda ataka kufunga hesabu vizuri Simba https://www.greensports.co.tz/2024/05/27/mgunda-ataka-kufunga-hesabu-vizuri-simba/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/27/mgunda-ataka-kufunga-hesabu-vizuri-simba/#respond Mon, 27 May 2024 18:41:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11135 Na mwandishi wetuKuelekea mechi ya kufunga msimu wa 2023-24, kaimu kocha mkuu Simba, Juma Mgunda amesema wanahitaji kufunga hesabu zao vizuri kwa kuhakikisha wanaibuka na ushindi dhidi ya JKT Tanzania kesho Jumanne.Akizungumza leo Jumatatu kocha huyo wa zamani wa Coastal Union alisema mechi yao hiyo itakayochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam itakuwa na ushindani […]

The post Mgunda ataka kufunga hesabu vizuri Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kuelekea mechi ya kufunga msimu wa 2023-24, kaimu kocha mkuu Simba, Juma Mgunda amesema wanahitaji kufunga hesabu zao vizuri kwa kuhakikisha wanaibuka na ushindi dhidi ya JKT Tanzania kesho Jumanne.
Akizungumza leo Jumatatu kocha huyo wa zamani wa Coastal Union alisema mechi yao hiyo itakayochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam itakuwa na ushindani mkubwa kwani wanafahamu JKT pia wanauhitaji ushindi wa kesho ili kusalia Ligi Kuu NBC.
“Mechi ya kesho ni ya maamuzi, na mechi yoyote yenye kuhitaji maamuzi inategemea ni mahitaji gani yanahitajika, kila mmoja ana mahitaji yake, Simba tuna mahitaji yetu ya mchezo huo na JKT pia wana mahitaji yao, kwa hiyo naamini itakua mechi yenye ushindani na mwisho lazima itoe maamuzi.

“Sababu kesho kama nilivyosema ndio kama tunafunga shule, unapofuga shule lazima ujue mtihani wako umekuwaje, matokeo yako kiujumla yakoje, lakini kubwa nataka niseme tunajua umuhimu wa mechi ya kesho, tumejiandaa kuhakikisha licha ya kufanya vizuri lakini pia tunapata matokeo mazuri,” alisema Mgunda.


Naye kocha msaidizi wa JKT, George Mketo alisema: “Tumejiandaa na mchezo wa simba hapo kesho, tunaamini hauwezi kuwa mchezo rahisi, utakuwa mgumu kulingana na mahitaji ya timu zote mbili, sisi tunahitaji kupata alama kwa ajili ya kubaki ligi kuu lakini Simba wanahitaji ushindi ili wamalize wa pili.
“Lakini tumeitazama Simba kwa timu yao, ubora wao na tunaamini ni timu kubwa na ina uzuri wa wachezaji waliokomaa kwa hiyo nasi kulingana na ugumu wa mchezo tutawaheshimu kulingana na mahitaji tunayoyahitaji kwa kuhakikisha tunapata alama tukiwa na mpango wetu kuhusiana na hilo.”
JKT inashika nafasi ya 12 kwa pointi 32, pointi moja zaidi ya Kagera Sugar inayoshika nafasi ya 13. JKT inahitaji ushindi ili kukimbia kushuka chini na kuwa miongoni mwa timu nne zitakazoanza mchakato wa kujinasua kutoshuka daraja.

The post Mgunda ataka kufunga hesabu vizuri Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/27/mgunda-ataka-kufunga-hesabu-vizuri-simba/feed/ 0
Mgunda: Geita walitupa wakati mgumu https://www.greensports.co.tz/2024/05/23/mgunda-geita-walitupa-wakati-mgumu/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/23/mgunda-geita-walitupa-wakati-mgumu/#respond Thu, 23 May 2024 09:24:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11086 Na mwandishi wetuKaimu kocha mkuu Simba, Juma Mgunda amesema licha ya kupata ushindi Jumanne wa mabao 4-1 dhidi ya Geita Gold lakini amekiri wapinzani wake hao walimpa wakati mgumu kutokana na malengo waliyonayo.Mgunda alisema tangu awali alibainisha kuwa hawezi kuwadharau Geita kulingana na nafasi waliyopo ya mkiani kwenye msimamo wa ligi kwani hilo ndilo linalofanya […]

The post Mgunda: Geita walitupa wakati mgumu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kaimu kocha mkuu Simba, Juma Mgunda amesema licha ya kupata ushindi Jumanne wa mabao 4-1 dhidi ya Geita Gold lakini amekiri wapinzani wake hao walimpa wakati mgumu kutokana na malengo waliyonayo.
Mgunda alisema tangu awali alibainisha kuwa hawezi kuwadharau Geita kulingana na nafasi waliyopo ya mkiani kwenye msimamo wa ligi kwani hilo ndilo linalofanya mchezo kuwa mgumu.
Alifafanua kwamba na hicho ndicho kilichotokea katika dakika 90 za mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Alisema bado hawajamaliza kazi kwani sasa wamebakisha mechi mbili za kuwania kumaliza ligi nafasi ya pili, hivyo wanarejea kikamilifu kwenye uwanja wa mazoezi kuhakikisha wanahitimisha shughuli kwa kuchukua pointi zote sita dhidi ya KMC na JKT Tanzania.
“Kikubwa ni kwamba mechi ilikuwa ngumu na siku zote lazima tuseme ukweli, huwezi kumdharau mtu sababu ya huko aliko au matokeo yake, nilisema tangu mapema mechi itakuwa ngumu na nzito sababu kila mmoja ana malengo yake.
“Lakini yote kwa yote tunamshukuru Mungu tumepata alama tatu na mabao manne, hii imeshakwisha tunajipanga na mchezo ujao kuangalia nini cha kufanya ili tuondoke na ushindi,” alisema Mgunda.
Simba iliyopo nafasi ya tatu inapambana kumaliza nafasi ya pili ikiwa imefikisha pointi 63 sawa na Azam iliyo nafasi ya pili kutokana na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na pia imebakiwa na mechi mbili za kufunga dimba dhidi ya Kagera Sugar na Geiga Gold.

The post Mgunda: Geita walitupa wakati mgumu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/23/mgunda-geita-walitupa-wakati-mgumu/feed/ 0
Mgunda akiri Geita si wepesi https://www.greensports.co.tz/2024/05/20/mgunda-akiri-geita-si-wepesi/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/20/mgunda-akiri-geita-si-wepesi/#respond Mon, 20 May 2024 18:02:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11048 Na mwandishi wetuKuelekea mchezo wao wa kesho Jumanne dhidi ya Geita Gold, kaimu kocha mkuu wa Simba, Juma Mgunda amesema maandalizi yamekamilika wakifahamu hautakuwa mchezo mwepesi.Mgunda alisema kwamba pia wanawategemea mashabiki wao kujitokeza kwa wingi kuwapa nguvu katika mchezo huo muhimu kwao katika kutafuta nafasi ya pili.Mgunda alisema hayo leo Jumatatu akieleza anafahamu timu hiyo […]

The post Mgunda akiri Geita si wepesi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kuelekea mchezo wao wa kesho Jumanne dhidi ya Geita Gold, kaimu kocha mkuu wa Simba, Juma Mgunda amesema maandalizi yamekamilika wakifahamu hautakuwa mchezo mwepesi.
Mgunda alisema kwamba pia wanawategemea mashabiki wao kujitokeza kwa wingi kuwapa nguvu katika mchezo huo muhimu kwao katika kutafuta nafasi ya pili.
Mgunda alisema hayo leo Jumatatu akieleza anafahamu timu hiyo ina wachezaji wazuri lakini pia ina kocha mzuri, Denis Kitambi hivyo wataingia wakifahamu uzito wa mchezo huo utakaopigwa kuanzia majira ya saa 1.00 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dae es Salaam.
“Maandalizi ya kucheza mchezo wa kesho ambao ni mgumu, wenye ushindani, yanakwenda vizuri kwa hiyo tuko tayari kabisa kushindana katika mchezo mgumu wa kesho lakini mwisho wa yote kupata matokeo.
“Tunafahamu kabisa (Geita) wana mwalimu mzuri, wana vijana wazuri kwa hiyo kikubwa sisi tumejiandaa vizuri kucheza na timu nzuri. Katika wachezaji 11 watakaokuwa uwanjani, nina mchezaji wangu muhimu sana wa 12 ambaye ndiye sapoti yetu kubwa.

“Wakifanya sehemu yao wakiungana na wachezaji wa uwanjani basi naamini kabisa tulichokusudia kukipata au kukifikia kwa uwezo wa Mungu tutakifanikisha,” alisema Mgunda.


Naye kocha mkuu wa Geita, Denis Kitambi alisema pamoja ya kuwaheshimu Simba kutokana na wachezaji walionao wenye ubora katika kutumia nafasi lakini wamejiandaa kupambana nao.
Zaidi ya hilo Kitambi alisema kwamba wamejiandaa pia katika kutengeneza, kumiliki mpira na kuhakikisha wanatumia vizuri nafasi wanazozipata ili wapate matokeo.

The post Mgunda akiri Geita si wepesi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/20/mgunda-akiri-geita-si-wepesi/feed/ 0
Mgunda azipigia hesabu pointi 9 https://www.greensports.co.tz/2024/05/18/mgunda-azipigia-hesabu-pointi-9/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/18/mgunda-azipigia-hesabu-pointi-9/#respond Sat, 18 May 2024 17:23:21 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11017 Na mwandishi wetuKaimu kocha mkuu wa timu hiyo, Juma Mgunda amesema wakijipanga sawasawa wataondoka na pointi zote tisa katika mechi tatu zilizobaki za Ligi Kuu NBC kwa kuwa mechi zote hizo watazicheza kwenye uwanja wao wa nyumbani.Mgunda alizungumza hayo baada ya jana Ijumaa kufanikiwa kuifunga Dodoma Jiji bao 1-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na […]

The post Mgunda azipigia hesabu pointi 9 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kaimu kocha mkuu wa timu hiyo, Juma Mgunda amesema wakijipanga sawasawa wataondoka na pointi zote tisa katika mechi tatu zilizobaki za Ligi Kuu NBC kwa kuwa mechi zote hizo watazicheza kwenye uwanja wao wa nyumbani.
Mgunda alizungumza hayo baada ya jana Ijumaa kufanikiwa kuifunga Dodoma Jiji bao 1-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na kuwa sawa na Azam FC kwa kufikisha pointi 60.
Azam hata hivyo bado inashikilia nafasi ya pili ikiwa juu kwa uwiano mzuri wa mabao ya kufunga ingawa timu zote hizo kila moja imecheza mechi 27.
“Tumemaliza salama mechi za ugenini na sasa zimesalia za nyumbani tu, ni kweli ugenini ugumu unakuwepo na nyumbani inakuwa na nafuu yake lakini kikubwa ni kwamba tuko nyumbani.

“Tunapata muda wa kupumzika, yaani ile kuzunguka inakuwa haipo sababu hatusafiri tena, kwa hiyo naamini tukijipanga sawa sawa tutapata matokeo yaliyo mazuri katika mechi hizi,” alisema Mgunda.


Kuhusu mechi yao na Dodoma, Mgunda alisema waliingia na mpango mkakati wa kutafuta ushindi mapema maana walishafahamu ubora na udhaifu wa Dodoma na hawakutaka mpaka timu zizoeane kwa kuhofia mambo kuwa magumu zaidi.
Alisema kutokana na malengo waliyokuwa nayo hatimaye walifanikiwa kuandika bao hilo pekee dakika ya saba kupitia kwa Freddy Koublan na kuwapa pointi tatu muhimu.
Katika mechi tatu zilizosalia ambazo zitachezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Simba wataumana na Geita Gold Mei 21 kabla ya Mei 25 kuvaana na KMC kisha kufunga dimba na JKT Tanzania Mei 28, mwaka huu.

The post Mgunda azipigia hesabu pointi 9 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/18/mgunda-azipigia-hesabu-pointi-9/feed/ 0
Mgunda aitolea macho nafasi ya pili https://www.greensports.co.tz/2024/05/17/mgunda-aitolea-macho-nafasi-ya-pili/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/17/mgunda-aitolea-macho-nafasi-ya-pili/#respond Fri, 17 May 2024 07:04:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10980 Na mwandishi wetuKaimu kocha mkuu Simba, Juma Mgunda amesema wanaihitaji nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu NBC kutokana na umuhimu wao wa kuwakilisha nchi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.Mgunda ameyazungumza hayo muda mchache kabla ya kuelekea Dodoma kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Dodoma Jiji utakaochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, […]

The post Mgunda aitolea macho nafasi ya pili first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kaimu kocha mkuu Simba, Juma Mgunda amesema wanaihitaji nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu NBC kutokana na umuhimu wao wa kuwakilisha nchi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
Mgunda ameyazungumza hayo muda mchache kabla ya kuelekea Dodoma kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Dodoma Jiji utakaochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Ijumaa hii kuanzia saa 10 jioni.
“Ukiwa unajua matokeo ya mpira yapo ya aina ngapi basi inakuwa haisumbui kidogo, tunajua kabisa tunakwenda kushindana na washindani wa mpira wenzetu.
“Basi yale yalikuwa matokeo ya mpira (1-1 dhidi ya Kagera Sugar), tumejifunza baada ya matokeo yale nini cha kwenda kufanya katika mchezo wetu wa Dodoma sababu matokeo ya Dodoma kwetu ni muhimu sana.
“Muhimu sababu moja ya malengo ya timu kwa kuwa bingwa ameshapatikana, nafasi ya pili ni muhimu kwa ajili ya uwakilishi wa nchi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa, kwa hiyo tunalijua hilo, tunalifahamu na tunalitambua.

“Kwa hiyo maandalizi yote ya kuendelea kushindana katika mechi hizi nne zilizobaki ni kuhakikisha tunafanya vizuri na mwisho wa yote kukipata tulichokusudia kukipata,” alifafanua Mgunda.


Simba ipo nafasi ya tatu kwa pointi 57 baada ya mechi 26 ikichuana na Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwa pointi 60 baada ya kushuka dimbani mara 27.
Yanga ikiwa tayari imetangaza ubingwa baada ya kufikisha pointi 71 ilizovuna kwenye mechi 27, ikisaliwa na michezo mitatu mkononi.
Simba ikimalizana na Dodoma, itamalizia mechi zake tatu ikiwa nyumbani dhidi ya Geita Gold, KMC na JKT Tanzania wakati Azam itapepetana na JKT Tanzania ugenini, kisha na Kagera ikiwa nyumbani kabla ya kwenda ugenini kufunga dimba na Geita Gold.

The post Mgunda aitolea macho nafasi ya pili first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/17/mgunda-aitolea-macho-nafasi-ya-pili/feed/ 0
Mgunda ataja kilichoikwaza Simba https://www.greensports.co.tz/2024/05/14/mgunda-ataja-kilichoikwaza-simba/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/14/mgunda-ataja-kilichoikwaza-simba/#respond Tue, 14 May 2024 05:06:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10947 Na mwandishi wetuKaimu kocha mkuu wa Simba, Juma Mgunda amesema miongoni mwa mambo yaliyowaangusha kwenye sare ya bao 1-1 dhidi ya Kagera Sugar ni kutotumia vyema nafasi nyingi za kufunga walizozitengeneza.Sare hiyo iliyopatikana Jumapili kwenye mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Kaitaba, inakuwa sare ya pili kwa Mgunda katika mechi alizoiongoza timu hiyo hadi sasa huku […]

The post Mgunda ataja kilichoikwaza Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kaimu kocha mkuu wa Simba, Juma Mgunda amesema miongoni mwa mambo yaliyowaangusha kwenye sare ya bao 1-1 dhidi ya Kagera Sugar ni kutotumia vyema nafasi nyingi za kufunga walizozitengeneza.
Sare hiyo iliyopatikana Jumapili kwenye mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Kaitaba, inakuwa sare ya pili kwa Mgunda katika mechi alizoiongoza timu hiyo hadi sasa huku akiwa ameshinda mechi tatu ambapo amesisitiza watapambana kuhakikisha makosa hayo ya kutotumia nafasi hayajirudii katika mechi zinazofuata.
“Matokeo ya sare hayamaanishi kwamba tumekwama ila haya ni mashindano, tumetengeneza nafasi nyingi lakini haikuwa riziki yetu, haikuwa bahati yetu, nafikiri ingekuwa habari nyingine kama ingekuwa ya kwetu leo lakini ndivyo mambo ya soka yalivyo.

“Iko wazi kuwa si kila nafasi mnayotengeneza mnaweza kufunga, tumetengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini huo ndio mpira na ni sehemu ya mapungufu tuliyoyaona kwa hiyo sasa ni nafasi yetu kwenda kuyafanyia kazi kwa ajili ya kuhakikisha kwenye mechi zinazokuja kwamba tukipata nafasi tuzitumie vizuri na zitupe matokeo mazuri,” alisema Mgunda.


Matokeo ya sare yameifanya Simba iendelee kusalia nafasi ya tatu kwa pointi 57 ikiendelea kuifukuzia Azam iliyo nafasi ya pili kwa pointi 60 baada ya kushinda kwa mabao 2-1 dhidi ya KMC Jumapili.

The post Mgunda ataja kilichoikwaza Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/14/mgunda-ataja-kilichoikwaza-simba/feed/ 0
Mgunda hajaukatia tamaa ubingwa https://www.greensports.co.tz/2024/05/04/mgunda-hajaukatia-tamaa-ubingwa/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/04/mgunda-hajaukatia-tamaa-ubingwa/#respond Sat, 04 May 2024 19:03:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10842 Na mwandishi wetuKaimu kocha mkuu wa Simba SC, Juma Mgunda ameweka wazi kuwa hajakata tamaa ya kuwania taji la Ligi Kuu NBC msimu huu kwa kuwa msimu bado haujamalizika na hakuna aliyejihakikishia ndoo hiyo mpaka sasa.Mgunda ameeleza hayo baada ya ushindi wa mabao 2-0 walioupata jana dhidi ya Mtibwa Sugar, ambapo Wekundu hao wameendelea kusalia […]

The post Mgunda hajaukatia tamaa ubingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kaimu kocha mkuu wa Simba SC, Juma Mgunda ameweka wazi kuwa hajakata tamaa ya kuwania taji la Ligi Kuu NBC msimu huu kwa kuwa msimu bado haujamalizika na hakuna aliyejihakikishia ndoo hiyo mpaka sasa.
Mgunda ameeleza hayo baada ya ushindi wa mabao 2-0 walioupata jana dhidi ya Mtibwa Sugar, ambapo Wekundu hao wameendelea kusalia nafasi ya tatu kwa pointi 50.
Simba wapo nyuma ya Azam wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 54 na vinara wa ligi hiyo Yanga wenye pointi 62, lakini Simba ikiwa na mchezo mmoja mkononi.
“Tunashukuru kwanza mchezo ulikuwa mzuri na wenye ushindani na haikuwa rahisi kama inavyofikiriwa, tumepata alama tatu, tunajipanga na mchezo mwingine.
“Na kuhusu ubingwa niseme ni kama marathon, huwa unapatikana pale mbio zinapoisha ila kwa sasa kuna anayeongoza, anayefuata nyuma, sasa yule atakayekata utepe mwisho ndio bingwa.

“Kwa hiyo bado tupo kwenye mbio, tunaangalia kilicho mbele yetu na michezo iliyo mbele yetu tunatazamia kufanya vizuri kwenye mechi zilizobaki kisha tutaangalia tumesimamia wapi, yaani maana yake ni kwamba haiishi mpaka iishe, mpaka ifike mwisho ndio tutaamini sasa imwekwisha,” alisema Mgunda kocha wa zamani wa Coastal Union.


Mgunda ambaye amerithi mikoba ya Abdelhak Benchikha ameeleza kuwa ameanza vizuri katika timu hiyo baada ya mechi iliyopita kupata sare ya mabao 2-2 na Namungo na hiyo inatokana na uwepo wa kocha msaidizi, Selemani Matola ambaye amewahi kufanya naye kazi Simba pia siku za nyuma, hivyo kazi yake inakuwa rahisi kwa kuwa wanajuana vizuri kikazi.

The post Mgunda hajaukatia tamaa ubingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/04/mgunda-hajaukatia-tamaa-ubingwa/feed/ 0
Mgunda: Sare ya Namungo inauma https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/mgunda-sare-ya-namungo-inauma/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/mgunda-sare-ya-namungo-inauma/#respond Wed, 01 May 2024 20:11:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10821 Na mwandishi wetuKaimu kocha mkuu wa Simba, Juma Mgunda amesema sare ya mabao 2-2 waliyoipata jana Jumanne dhidi ya Namungo imewagusa na kuwaumiza mno hasa kwa namna walivyopoteza pointi tatu dakika chache kabla ya kumalizika kwa mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC.Namungo walifuta ndoto za Simba kutoka na ushindi baada ya bao la kujifunga […]

The post Mgunda: Sare ya Namungo inauma first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kaimu kocha mkuu wa Simba, Juma Mgunda amesema sare ya mabao 2-2 waliyoipata jana Jumanne dhidi ya Namungo imewagusa na kuwaumiza mno hasa kwa namna walivyopoteza pointi tatu dakika chache kabla ya kumalizika kwa mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC.
Namungo walifuta ndoto za Simba kutoka na ushindi baada ya bao la kujifunga la Kennedy Juma dakika ya 90 katika harakati za kuokoa mpira uliochonganishwa langoni mwa Simba katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Majaliwa, Lindi.
“Niseme ndivyo mpira ulivyo, haiishi mpaka dakika 90 zikamilike maana ilibaki kama dakika mbili tu lakini goli linafungwa muda wowote, ni kweli inagusa, inauma na matokeo ya mpira ni katili lakini tumekubaliana nayo, tumejifunza, tunakwenda kukaa chini, kutafakari kujirekebisha ili kurejea kwenye matokeo mazuri na bora zaidi kwa timu,” alisema Mgunda.
Alisema pamoja na yote lakini walifahamu mchezo huo usingekuwa mwepesi kutokana na hali ilivyo kwenye msimamo wa ligi hasa ikizingatiwa kuwa ligi inaelekea ukiongoni kwa sasa na wao wanachukua matokeo hayo kama funzo.
Mgunda alisisitiza kuwa wanakwenda kujipanga zaidi kwenye uwanja wa mazoezi ili kutafuta matokeo yenye afya kwa timu hiyo katika mechi zilizosalia kabla ya kufungwa rasmi kwa pazia la ligi.
Naye kocha mkuu wa Namungo, Mwinyi Zahera alisema: “Sisi hatukuingia na pointi kwamba Simba imekuwa dhaifu au inashindwa kupambania ubingwa au vinginevyo. Tulijua dhidi ya Simba ni mechi ngumu sababu wametoka kuchukua Kombe la Muungano na walikuwa wanajiamini baada ya kuifunga Azam na kubeba lile kombe.
“Na kwenye ligi sababu Simba anapambania kupanda juu tukajua hawezi kuruhusu tena kupoteza pointi kwa hiyo hii mechi itakuwa ngumu, tukaiandaa timu kisaikolojia na kuwaambia wachezaji kwamba tupambane, tushikilie mbinu yetu.
“Na waiheshimu Simba kwa asilimia 80 na wakijitoa kweli, basi Mungu mwenyewe ataamua na hata tukifungwa tutajua tulifanya kile tulitaka, tukidroo tutajua kwamba tulijitolea tukafikia hapa, kwa hiyo kwangu nawapongeza wachezaji wangu, walijitoa sana.”
Kwa matokeo hayo, Simba imeendelea kusalia nafasi ya tatu kwa pointi zao 47 baada ya mechi 22 na Namumgo ambao katika mechi ya kwanza msimu huu walitoka sare ya bao 1-1 na Simba wameendelea kuganda nafasi ya tisa kwa pointi 27 baada ya mechi 24.

The post Mgunda: Sare ya Namungo inauma first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/mgunda-sare-ya-namungo-inauma/feed/ 0
Mgunda kaisoma, akaiua Yanga Princess https://www.greensports.co.tz/2024/04/26/mgunda-kaisoma-akaiua-yanga-princess/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/26/mgunda-kaisoma-akaiua-yanga-princess/#respond Fri, 26 Apr 2024 20:53:06 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10750 Na mwandishi wetuBaada ya ushindi wa mabao 3-1 jana Alhamisi dhidi ya Yanga Princess, kocha mkuu wa Simba Queens, Juma Mgunda amesema wamefanikiwa kupata ushindi kwa kuwa walitumia muda kuwasoma wapinzani wao wakati mechi inaendelea.Mgunda alisema alifahamu Yanga wangekuja na mbinu zaidi ya mechi ya awali ya Ligi Kuu ya Wanawake na ndicho kilichotokea, hivyo […]

The post Mgunda kaisoma, akaiua Yanga Princess first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Baada ya ushindi wa mabao 3-1 jana Alhamisi dhidi ya Yanga Princess, kocha mkuu wa Simba Queens, Juma Mgunda amesema wamefanikiwa kupata ushindi kwa kuwa walitumia muda kuwasoma wapinzani wao wakati mechi inaendelea.
Mgunda alisema alifahamu Yanga wangekuja na mbinu zaidi ya mechi ya awali ya Ligi Kuu ya Wanawake na ndicho kilichotokea, hivyo ili kuwadhibiti ilimbidi asubiri kipindi cha pili ndipo walipofanikiwa kufunga mabao yote matatu kipindi cha pili.
“Tulikuwa tunacheza na timu ambayo tulishacheza nayo kwa hiyo ilikuwa lazima wakija waje na mbinu nyingine tofauti.

“Na kweli waliingia tofauti kwa hiyo tukawa tunawaangalia uzuri wao na upungufu wao na baada ya kipindi cha kwanza tukaelezana cha kufanya mwisho tukashinda,” alisema Mgunda.


Mgunda pia alisema wanajua mechi iliyo mbele yao ni dhidi ya mabingwa watetezi, JKT Queens na ni mchezo mgumu kama ilivyo ligi yenyewe msimu huu.
Alifafanua kwamba kutokana na hilo wanakwenda kujipanga kuhakikisha wanafanya vizuri kiujumla hata kwenye michezo yao mingine iliyosalia msimu huu.
Naye kocha mkuu wa Yanga Princess, Charles Haalubono alisema: “Kwanza nianze kuwapongeza Simba, wamecheza vizuri wametufunga, kuhusu timu yetu naona mabadiliko makubwa ukilinganisha na mechi ya kwanza tulipocheza nao, nafikiri tunahitaji kurekebisha sehemu chache.
Akifafanua zaidi hoja hiyo alisema kwamba wapinzani wao walipata mabao mawili kwa makosa ya ulinzi ingawa ana furaha ya mabadiliko na maendeleo ya kikosi chake mbali na matokeo lakini timu anaiona ikianza kujengeka.

The post Mgunda kaisoma, akaiua Yanga Princess first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/26/mgunda-kaisoma-akaiua-yanga-princess/feed/ 0