Mbappe - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 17 Apr 2025 09:54:55 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Mbappe - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mbappe alimwa red card, aomba radhi https://www.greensports.co.tz/2025/04/14/mbappe-alimwa-red-card-aomba-radhi/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/14/mbappe-alimwa-red-card-aomba-radhi/#respond Mon, 14 Apr 2025 06:58:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13246 Madrid, HispaniaMshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappe amelimwa kadi nyekundu (red card) Jumapili hii, Aprili 13, 2025 katika mechi ya La Liga dhidi ya Alaves ambayo Real Madrid imeshinda kwa bao 1-0.Ushindi huo umeifanya timu hiyo kuendelea kuwafukuzia mahasimu wao Barcelona wanaoshika usukani wa La Liga kwa tofauti ya pointi nne.Mbappe ambaye ataikosa mechi ya […]

The post Mbappe alimwa red card, aomba radhi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappe amelimwa kadi nyekundu (red card) Jumapili hii, Aprili 13, 2025 katika mechi ya La Liga dhidi ya Alaves ambayo Real Madrid imeshinda kwa bao 1-0.
Ushindi huo umeifanya timu hiyo kuendelea kuwafukuzia mahasimu wao Barcelona wanaoshika usukani wa La Liga kwa tofauti ya pointi nne.
Mbappe ambaye ataikosa mechi ya Jumapili ijayo dhidi ya Athletic Bilbao, awali alipewa kadi ya njano kwa kumkanyaga kwenye ugoko Antonio Blanco lakini baada ya VAR kutumika mwamuzi aliamua kumpa kadi nyekundu moja kwa moja.
Tukio la Mbappe lilitokea dakika ya 38 ikiwa ni dakika nne baada ya Real Madrid kupata bao hilo pekee lililofungwa na Eduardo Camavinga kwa shuti la mguu wa kushoto nje kidogo ya eneo la penalti.
Real Madrid iliyobaki na wachezaji 10 uwanjani ilikuwa na kazi nzito ya kujihami ambapo kipa Thibaut Courtois aliazimika kuokoa michomo sita iliyoelekezwa langoni mwake.
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti alianza mchezo huo bila ya wachezaji wake nyota, Vinicius Junior na Jude Bellingham walioanzia kwenye benchi ikiwa ni siku chache baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 3-0 na Arsenal katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ancelotti ambaye Mei 11 atakuwa na mechi ngumu dhidi ya Barcelona, hata hivyo baadaye aliwapa nafasi wachezaji hao lakini kuwapo kwao hakukuweza kubadili matokeo.
Mbappe aomba radhi
Baada ya mechi hiyo, Mbappe aliwaomba radhi wachezaji wenzake wa Real Madrid pamoja na Blanco huku akionekana kuchukizwa na tukio hilo.
Kwa upande wake Blanco alikiri kuombwa radhi na kukubaliana na tukio hilo ambalo alisema mambo kama hayo hutokea kwenye soka.
“Ni rafu mbaya, nimezungumza na Kylian, ameomba radhi, matukio ya aina hii huto9kea kwenye soka,” alisema Blancxo mbele ya waandishi wa habari.

The post Mbappe alimwa red card, aomba radhi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/14/mbappe-alimwa-red-card-aomba-radhi/feed/ 0
Mbappe asafishwa kesi ya kubaka https://www.greensports.co.tz/2024/12/12/mbappe-asafishwa-kesi-ya-kubaka/ https://www.greensports.co.tz/2024/12/12/mbappe-asafishwa-kesi-ya-kubaka/#respond Thu, 12 Dec 2024 18:39:09 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12399 Stockholm, SwedenWaendesha mashitaka wa Sweden leo Alhamisi wametangaza kufuta uchunguzi ulioanzishwa wa tuhuma za kubaka alizokuwa akihusishwa nazo mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappe.Kwa mujibu ya taarifa ya waendesha mashitaka hao, uamuzi wa kufuta uchunguzi huo umekuja baada ya kubaini kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuendelea na uchunguzi.Tuhuma hizo zilimhusisha Mbappe ambaye alidaiwa kufanya tukio […]

The post Mbappe asafishwa kesi ya kubaka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Stockholm, Sweden
Waendesha mashitaka wa Sweden leo Alhamisi wametangaza kufuta uchunguzi ulioanzishwa wa tuhuma za kubaka alizokuwa akihusishwa nazo mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappe.
Kwa mujibu ya taarifa ya waendesha mashitaka hao, uamuzi wa kufuta uchunguzi huo umekuja baada ya kubaini kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuendelea na uchunguzi.
Tuhuma hizo zilimhusisha Mbappe ambaye alidaiwa kufanya tukio hilo katika hoteli moja ya jijini Stockholm.
Katika tukio hilo ilielezwa kuwa kulikuwa na mtu alihusishwa na tukio la kubaka na wawili waliohusishwa na tukio la udhalilishwaji kijinsia lakini hakujawa na ushahidi wa kutosha kuendelea na uchunguzi wa tukio hilo na hivyo uchunguzi huo umefutwa.
Taarifa ya waendesha mashitaka hao haikumtaja mtuhumiwa wa kadhia hiyo lakini vyanzo kadhaa vya habari nchini Sweden vilimtaja mshambuliaji huyo wa Real Madrid ambaye alitembelea jiji la Stockholm wakati wa mapumziko mwezi Oktoba.
Chanzo kimoja cha habari kimeeleza kuwa awali wakili wa Mbappe alizipuuza tuhuma hizo akidai kuwa ni za uwongo ingawa baada ya uamuzi wa kufuta uchunguzi, wakili huyo hakutoa taarifa yoyote.
Mbappe ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Ufaransa, alijiunga na Real Madrid mwanzoni mwa msimu huu akitokea PSG ya Ufaransa.

The post Mbappe asafishwa kesi ya kubaka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/12/12/mbappe-asafishwa-kesi-ya-kubaka/feed/ 0
Mbappe akosa tena penalti https://www.greensports.co.tz/2024/12/05/mbappe-akosa-tena-penalti/ https://www.greensports.co.tz/2024/12/05/mbappe-akosa-tena-penalti/#respond Thu, 05 Dec 2024 09:42:26 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12338 Madrid, HispaniaBaada ya Kylian Mbappe kukosa penalti kwa mara ya pili, kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amedai bado ana imani mshambuliaji huyo ana uwezo wa kufanya vizuri na ataendelea kuwa mpigaji penalti.Mbappe alikosa penalti jana Jumatano katika mechi ya La Liga dhidi ya Athletic Bilbao na hivyo kushindwa kuiokoa timu yake ambayo mwishowe ililala […]

The post Mbappe akosa tena penalti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Madrid, Hispania
Baada ya Kylian Mbappe kukosa penalti kwa mara ya pili, kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amedai bado ana imani mshambuliaji huyo ana uwezo wa kufanya vizuri na ataendelea kuwa mpigaji penalti.
Mbappe alikosa penalti jana Jumatano katika mechi ya La Liga dhidi ya Athletic Bilbao na hivyo kushindwa kuiokoa timu yake ambayo mwishowe ililala kwa mabao 2-1.
Athletic ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 53 lililofungwa na Alex Berenguer na Mbappe akapata nafasi ya kusawazisha kupitia penalti lakini shuti alilopiga liliokolewa na kipa Julen Agirrezabala.
Mbappe hata hivyo juhudi zake zilizaa bao la kusawazisha lililofungwa na Jude Bellingham kufuatia shuti la Mbappe lililookolewa kabla ya kumkuta mfungaji.
Athletic hata hivyo walineemeka na makosa ya Federico Valverde katika dakika za lala salama baada ya kupata bao lililofungwa na Gorka Guruzeta.
Hii ni mara ya pili katika kipindi kisichozidi wiki moja kwa Mbappe kukosa penalti, awali alikosa penalti wiki iliyopita katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool, mechi ambayo Real Madrid ililala kwa mabao 2-0.

“Sijazungumza na Mbappe na siwezi katu kumfanyia tathmini mchezaji kupitia penalti, kuna wakati unafunga na kuna wakati unakosa, najua amehuzunika na kukatishwa tamaa lakini lazima tuangalie mbele,” alisema Ancelotti.


Ancelotti pia alisema kwamba hata Valverde ana huzuni na amekatishwa tamaa kama ilivyo kwa Mbappe lakin naye ni mchezaji mkubwa na watu hufanya makosa kwenye soka.
Mbappé hadi sasa ana mabao 10 katika mechi 20 za Real Madrid tangu ajiunge na timu hiyo msimu huu lakini amejikuta akishutumiwa mara kadhaa kwa kinachodaiwa kuwa hayuko katika kiwango bora.
Akizungumzia kukosa kwake penalti, Mbappe alisema kwamba anawajibika kwa kila kitu lakini akasisitiza kwamba ni wakati wa kubadilika na kuonesha yeye ni nani.
Ancelotti kwa upande mwingine alisema kwamba Mbappe ataendelea na majukumu ya upigaji wa penalti katika timu hiyo pamoja na Vinícius Júnior na Bellingham.

The post Mbappe akosa tena penalti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/12/05/mbappe-akosa-tena-penalti/feed/ 0
‘Huyu ndiye Mbappe tunayemtaka’ https://www.greensports.co.tz/2024/12/02/huyu-ndiye-mbappe-tunayemtaka/ https://www.greensports.co.tz/2024/12/02/huyu-ndiye-mbappe-tunayemtaka/#respond Mon, 02 Dec 2024 12:34:15 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12296 Madrid, HispaniaKocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amemsifia mshambuliaji wake Kylian Mbappe akimtaja kuwa ni hatari baada ya kufunga bao katika ushindi wa 2-0 walioupata jana Jumapili dhidi ya Getafe.Mbappe amekuwa akipitia kipindi kigumu cha lawama tangu ajiunge na timu hiyo msimu huu baada ya kuandamwa na ukame wa mabao huku baadhi ya wachambuzi wakidai […]

The post ‘Huyu ndiye Mbappe tunayemtaka’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Madrid, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amemsifia mshambuliaji wake Kylian Mbappe akimtaja kuwa ni hatari baada ya kufunga bao katika ushindi wa 2-0 walioupata jana Jumapili dhidi ya Getafe.
Mbappe amekuwa akipitia kipindi kigumu cha lawama tangu ajiunge na timu hiyo msimu huu baada ya kuandamwa na ukame wa mabao huku baadhi ya wachambuzi wakidai hayuko katika ubora uliozoeleka.
Baada ya kufunga bao hiyo jana Ancelotti alisema kwamba hicho ndicho wanachokihitaji kutoka kwa mshambuliaji huyo.
Katika mechi hiyo, Jude Bellingham ndiye aliyeifungia Real Madrid bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti dakika ya 30 kabla ya kutoa pasi iliyozaa bao la pili lililofungwa na Mbappe dakika nane baadaye.
Ushindi huo umeifanya Real Madrid kujiimarisha katika nafasi ya pili kwenye La Liga wakiwa wamezidiwa na vinara Barca kwa tofauti ya pointi moja ingawa Real Madrid wana mechi moja pungufu.

“Mbappe alikuwa hatari kama anavyokuwa siku zote, alifunga bao muhimu lililosaidia kutufanya tuutawale mchezo vizuri na akapata nafasi katika kipindi cha pili, alikuwa shapu na hicho ndicho tunachohitaji kutoka kwake,” alisema Ancelotti.


Mbappe amefunga mabao mawili tu katika mechi tisa na alikosa penalti katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool katikati ya wiki lakini sasa ni kama ameanza kurudi katika makali yaliyozoeleka.

The post ‘Huyu ndiye Mbappe tunayemtaka’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/12/02/huyu-ndiye-mbappe-tunayemtaka/feed/ 0
Mbappe aonja shubiri El-Clasico https://www.greensports.co.tz/2024/10/27/mbappe-aonja-shubiri-el-clasico/ https://www.greensports.co.tz/2024/10/27/mbappe-aonja-shubiri-el-clasico/#respond Sun, 27 Oct 2024 19:48:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12092 Barcelona, HispaniaShubiri inafahamika kwa uchungu na ndicho kilichomkuta mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappe, Jumamosi hii alipocheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Barcelona maarufu El Clasico na kujikuta pagumu baada ya timu yake kubugizwa mabao 4-0.Mbappe ambaye huu ni msimu wake wa kwanza Real Madrid tangu ajiunge na timu hiyo akitokea PSG, kwa mara […]

The post Mbappe aonja shubiri El-Clasico first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Barcelona, Hispania
Shubiri inafahamika kwa uchungu na ndicho kilichomkuta mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappe, Jumamosi hii alipocheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Barcelona maarufu El Clasico na kujikuta pagumu baada ya timu yake kubugizwa mabao 4-0.
Mbappe ambaye huu ni msimu wake wa kwanza Real Madrid tangu ajiunge na timu hiyo akitokea PSG, kwa mara ya kwanza alicheza mechi hiyo kubwa ya El Clasico lakini ukawa mwanzo mbaya.
Kwa Mbappe bila shaka aliingia katika mechi hiyo akikumbuka mabao matatu (hat trick) ambayo aliwafunga Barca, Februari 2021 na kuiwezesha PSG kutoka na ushindi wa 4-1 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mbappe hata hivyo alishindwa kufanya jambo linalofanana na hilo baada ya kuwa na wakati mgumu Jumamosi katika uwanja huo huo wa Nou Camp ambao mwaka 2021 alitoka kifua mbele na mabao matatu.
Kushindwa kwa Mbappe kutamba katika El Clasico kunatajwa kuwa ni mwendelezo wa mwanzo usio wa kuvutia kwa mshambuliaji huyo tishio duniani ambaye katika mechi zake tatu za awali za La Liga alitoka uwanjani bila bao.
Mbappe pia tangu aanze kuivaa jezi ya Real Madrid hadi sasa ana mabao sita tu katika La Liga jambo ambalo halikutarajiwa hasa kutokana na matarajio makubwa yaliyokuwapo kabla ya usajili wake haujakamilika.
Mchezaji mwingine wa Real Madrid anayepitia wakati mgumu ni Jude Bellingham ambaye msimu uliopita ambao pia ulikuwa wa kwanza kwake, alikuwa moto akitupia wavuni mabao 19 lakini kwa msimu huu hadi sasa hana bao hata moja.

The post Mbappe aonja shubiri El-Clasico first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/10/27/mbappe-aonja-shubiri-el-clasico/feed/ 0
Ronaldo amtaja Mbappe Ballon d’Or https://www.greensports.co.tz/2024/09/11/ronaldo-amtaja-mbappe-ballon-dor/ https://www.greensports.co.tz/2024/09/11/ronaldo-amtaja-mbappe-ballon-dor/#respond Wed, 11 Sep 2024 04:59:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11890 Porto, UrenoWinga wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo amemtaja mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappé kuwa ni mchezaji ambaye ana nafasi ya kubeba tuzo ya Ballon d’Or.Akizungumza kupitia chaneli ya You Tube, Ronaldo pia alisema kwamba Mbappe atapata mafaniko katika klabu ya Real Madrid ambayo alisema kwake itabaki kuwa ndiyo […]

The post Ronaldo amtaja Mbappe Ballon d’Or first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Porto, Ureno
Winga wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo amemtaja mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappé kuwa ni mchezaji ambaye ana nafasi ya kubeba tuzo ya Ballon d’Or.
Akizungumza kupitia chaneli ya You Tube, Ronaldo pia alisema kwamba Mbappe atapata mafaniko katika klabu ya Real Madrid ambayo alisema kwake itabaki kuwa ndiyo klabu bora.
Ronaldo alisema kwamba anafikiri Mbappe atafanya vizuri na kuutaja muundo wa klabu hiyo kuwa ni mzuri na upo sawa.
“Wana kocha bora, Carlo Ancelotti na raisi Florentino (Perez) ambaye yupo pale kwa miaka mingi, nafikiri haitokuwa tatizo kubwa kwa sababu Mbappe ana kipaji, atakuwa mshindi ajaye wa Ballon d’Or, yeye (Erling) Haaland, (Jude) Bellingham, Lamine (Yamal),” alisema Ronaldo.
Akiizungumzia zaidi Real Madrid, Ronaldo alisema ni aina ya timu ambayo haina presha, ingawa kuna wanaosema ina bahati kwenye Ligi ya Mabingwa, Ronaldo anakataa hilo badala yake anasema ni timu inayojiandaa kwa matukio ya aina hiyo na hata uwanja wao (Bernabéu) ipo kivingine kabisa.

“Kwa sasa huwezi kusema kama Real Madrid itakuwa timu bora au la, hatujui, Mbappe yupo pale kwa sasa, nafikiri itaendelea kuwa timu imara ingawa sijui kama itakuwa hivyo kuliko msimu uliopita, Mungu tu ndiye anayejua,” alisema Ronaldo.

Ancelotti aliwahi kumzungumzia Mbappe akisema wanaendelea kujizoeza maisha ya kuwa na nyota huyo ambaye ameonesha kila dalili za kuanza kuwa bora akiwa na mabao mawili dhidi ya Real Betis kabla ya kwenda kuitumikia timu ya taifa.
Real Madrid imeshinda mechi zake mbili na kutoka sare mbili katika mechi nne za msimu huu ikiwa nafasi ya pili kwenye La Liga nyuma ya mahasimu wao, Barcelona kwa tofauti ya pointi nne.

The post Ronaldo amtaja Mbappe Ballon d’Or first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/09/11/ronaldo-amtaja-mbappe-ballon-dor/feed/ 0
Ancelotti hana hofu na Mbappe https://www.greensports.co.tz/2024/08/25/ancelotti-hana-hofu-na-mbappe/ https://www.greensports.co.tz/2024/08/25/ancelotti-hana-hofu-na-mbappe/#respond Sun, 25 Aug 2024 20:18:03 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11815 Madrid, HispaniaKocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amesema kitendo cha mshambuliaji wake mpya, Kylian Mbappe kushindwa kuzifumania nyavu katika mechi mbili mfululizo za La Liga hakimsumbui.Mbappe amejiunga na Real Madrid kwa mkataba wa miaka mitano huu ukiwa msimu wake wa kwanza na ingawa mambo hayajawa mazuri kwenye La Liga, tayari ameifungia timu hiyo bao katika […]

The post Ancelotti hana hofu na Mbappe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amesema kitendo cha mshambuliaji wake mpya, Kylian Mbappe kushindwa kuzifumania nyavu katika mechi mbili mfululizo za La Liga hakimsumbui.
Mbappe amejiunga na Real Madrid kwa mkataba wa miaka mitano huu ukiwa msimu wake wa kwanza na ingawa mambo hayajawa mazuri kwenye La Liga, tayari ameifungia timu hiyo bao katika mechi ya Uefa Super Cup dhidi ya Atalanta mapema mwezi huu.
Usajili wa Mbappe Real Madrid ulikuwa gumzo duniani kote lakini bado hajaanza kutema cheche zake na Jumapili katika mechi na Real Valladolid licha ya Real Madrid kushinda kwa 3-0 lakini Mbappe alitupwa benchi dakika ya 86.
Akizungumza baada ya mechi hiyo, Ancelotti alipingana na hoja kwamba Mbappe anashindwa kufunga kwa sababu anacheza nafasi ya mshambuliaji wa kati badala ya pembeni.
“Hapana, sidhani kama kuna hilo tatizo hata kidogo, Mbappe ni mshambuliaji wa kipekee, ana kasi na anakwenda vizuri hata asipokuwa na mpira,” alisema Ancelotti.
Akifafanua zaidi kuhusu Mbappe katika mechi na Valladolid, Ancelotti alisema mshambuliaji huyo alipata nafasi tatu na anaamini katika nafasi hizo ataweza kufunga kama ambavyo amekuwa akifunga mara zote na hadhani kama ili kufunga ni lazima acheze kushoto au kulia.
Katika hatua nyingine, Ancelotti pia alimpongeza Endrick ambaye amesaini timu hiyo msimu huu mara baada ya kufikisha miaka 18.
Alisema kwamba mchezaji huyo ni hazina na akiwa kwenye lango ameonesha uwezo wake wote, anamiliki vizuri mpira na anapiga mashuti vizuri.

The post Ancelotti hana hofu na Mbappe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/08/25/ancelotti-hana-hofu-na-mbappe/feed/ 0
‘Mbappe hatobadili nafasi ya Bellingham Real Madrid’ https://www.greensports.co.tz/2024/08/05/mbappe-kutobadili-nafasi-ya-bellingham-real-madrid/ https://www.greensports.co.tz/2024/08/05/mbappe-kutobadili-nafasi-ya-bellingham-real-madrid/#respond Mon, 05 Aug 2024 11:53:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11715 Charlotte, MarekaniKocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amesema nafasi na majukumu ya Jude Bellingham katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid hayatobadilika licha ya klabu hiyo kumsajili, Kylian Mbappe.Bellingham, 21, ambaye pia ni kiungo wa timu ya taifa ya England katika msimu wake wa kwanza na Real Madrid wa 2023-24 amebeba vyema majukumu yake akifunga […]

The post ‘Mbappe hatobadili nafasi ya Bellingham Real Madrid’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Charlotte, Marekani
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amesema nafasi na majukumu ya Jude Bellingham katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid hayatobadilika licha ya klabu hiyo kumsajili, Kylian Mbappe.
Bellingham, 21, ambaye pia ni kiungo wa timu ya taifa ya England katika msimu wake wa kwanza na Real Madrid wa 2023-24 amebeba vyema majukumu yake akifunga mabao 23 katika mechi 42 na timu hiyo kubeba mataji ya La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika msimu mpya wa 2024-25, Real Madrid imemsajili Mbappe, 25, ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Ufaransa, usajili ambao inadhaniwa unaweza kumfanya Ancelotti ambadilishie Bellingham majukumu yake kwenye kikosi cha kwanza.
Ancelotti hata hivyo alikana kuwa na mpango wowote wa kumbadilishia majukumu Bellingham kwa kumsogeza mbele zaidi ili Mbappe aingie vyema katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Kocha huyo badala yake alisisitiza kwamba hakuna kitakachobadilika kwa mchezaji huyo ambaye pia aliwahi kunukuliwa akisema kwamba kucheza timu moja na Mbappe litakuwa jambo zuri.

“Msimu wa kwanza tu ameshangaza kweli kwa sababu ameonesha kiwango cha kipekee, amekuwa bora, msimu ujao hautokuwa tofauti, atakuwa mmoja wa wachezaji bora tulio nao, anaisaidia sana timu kwa kiwango chake,” alisema Ancelotti.

Ancelotti pia alimtetea Bellingham baada ya mchezaji huyo kushutumiwa kwa kiwango kisichovutia kwenye fainali za soka za Euro 2024 zilizomalizika hivi karibuni nchini Ujerumani ambapo England ilifikia hatua ya fainali lakini ilishindwa kutamba mbele ya Hispania waliobeba kombe.
“Hayo ni mawazo tu lakini Bellingham alicheza vizuri kwenye Euro, England pia ilicheza vizuri hasa hadi kufikia hatua ya fainali na ilikuwa bado kidogo wabebe kombe,” alisema Ancelotti.
Mbappe na Bellingham ambao wote walikuwa na timu zao za taifa kwenye fainali za Euro 2024 wanasubiriwa kwa hamu kuibeba Real Madrid katika msimu mpya wa 2024-25 unaotarajia kuanza kutimua vumbi baadaye mwezi huu.

The post ‘Mbappe hatobadili nafasi ya Bellingham Real Madrid’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/08/05/mbappe-kutobadili-nafasi-ya-bellingham-real-madrid/feed/ 0
Real Madrid hii yenye Mbappe, Vinicius Jr, Bellingham https://www.greensports.co.tz/2024/07/19/real-madrid-hii-yenye-mbappe-vinicius-jr-bellingham/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/19/real-madrid-hii-yenye-mbappe-vinicius-jr-bellingham/#respond Fri, 19 Jul 2024 11:21:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11637 Madrid, HispaniaJulai 16, 2024, Real Madrid inamtambulisha rasmi mshambuliaji wake mpya, Kylian Mbappe ambaye anaongeza nguvu mpya na ya kipekee katika kikosi cha timu hiyo kwenye safu ya ushambuliajiSafu ya ushambuliaji ya Real Madrid yenye Jude Bellingham na Vinicius Junior tayari imeonesha kiwango cha juu msimu uliopita wa 2023-24 hadi kubeba taji la La Liga […]

The post Real Madrid hii yenye Mbappe, Vinicius Jr, Bellingham first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Julai 16, 2024, Real Madrid inamtambulisha rasmi mshambuliaji wake mpya, Kylian Mbappe ambaye anaongeza nguvu mpya na ya kipekee katika kikosi cha timu hiyo kwenye safu ya ushambuliaji
Safu ya ushambuliaji ya Real Madrid yenye Jude Bellingham na Vinicius Junior tayari imeonesha kiwango cha juu msimu uliopita wa 2023-24 hadi kubeba taji la La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kwa sasa safu hiyo imeongezewa nguvu kwa usajili wa Mbappe, mshambuliaji tishio duniani ambaye amethibitisha hilo kwenye kikosi cha PSG na timu ya taifa ya Ufaransa.
Mbio za Real Madrid kuisaka saini ya Mbappe ni za muda mrefu ingawa bila Mbappe timu hiyo imeendelea kuwa tishio na hapo unaweza kujiuliza itakuwaje timu hiyo ikiwa na Mbappe.
Itakuwaje timu hiyo ikiwa na mshambuliaji anayeshika rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika klabu ya PSG na ambaye kukosekana kwake kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya Ufaransa kuliibua sintofahamu wakati wa fainali za Euro 2024.
Juhudi za kuinasa saini ya Mbappe ziliposhindwa kuzaa matunda kabla ya msimu wa 2023-24, kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti alisema kwamba timu yake ilikuwa imekamilika bila ya Mbappe.
Kwa Ancelloti kilichoonekana ni kwamba Mbappe hakuwa mchezaji wa kumsumbua kichwa na akalithibitisha hilo kwa kuiwezesha Real Madrid kubeba taji la La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kauli ya Ancelloti kutoonekana mwenye kusumbuliwa na usajili wa Mbappe pia ilitoa dalili kwamba huenda mchezaji huyo asingesajiliwa Real Madrid kwa kuwa kocha aliamini maisha bila ya mchezaji huyo yanawezekana.
Ukimuweka kando Mbappe, Real Madrid ina watu wengine hatari katika safu hiyo kuanzia kwa Vinicius, Bellingham lakini hapo hapo yupo mshambuliaji wa Kibrazil, Endrick anayesubiriwa kukamilisha usajili.


Orodha hiyo pia ina Arda Guller ambaye ameonesha umahiri wake akiwa na timu ya taifa ya Uturuki kwenye fainali za Euro 2024 naye huenda akapata nafasi ya ndani ya kikosi cha Real Madrid.
Hapo hapo ikumbukwe kwamba Rodrygo naye ni mchezaji mwingine ambaye tayari ameonesha uwezo na bila shaka ana nafasi yake zaidi kwenye kikosi cha timu hiyo katika msimu wa 2024-25 pengine kuliko ilivyokuwa katika msimu ulioisha wa 2023-24.
Kwa wanaojua utamaduni wa Real Madrid, ujio wa Mbappe na mastaa wengine hauwashangazi, ni mwendelezo wa mfumo wa klabu hiyo kusajili wachezaji mastaa wakubwa wa bei mbaya au madogo wenye vipaji vya juu.
Ilikuwa hivyo tangu zama za kina Zinedine Zidane, Luis Figo, David Beckham, Ronaldo de Lima, Roberto Carlos, Kaka, Cristiano Ronaldo, Gareth Bale na sasa Bellingham, Vinicius Jr na hatimaye Mbappe huku Erling Haaland naye akisubiriwa.
Kwa haraka haraka unaweza kusema kwamba Real Madrid hii yenye Mbappe, Bellingham, Vinicius Jr na wengineo itashinda kila taji lililo mbele yake lakini ukweli wa mchezo wa soka hauko hivyo.
Kutafuta mfumo wa kuwatumia wachezaji hao ni jambo la kwanza gumu ambalo linaweza kumpa tabu Ancelotti kwani kuna wachezaji ambao panga pangua ni lazima wapangwe kwenye kikosi cha kwanza, ikitokea hawajapangwa kunakuwa na tatizo la ndani na wakati mwingine hata nje ya uwanja.
Kazi ngumu nyingine ngumu kwa Ancelotti ni kuwaongoza mastaa hao wa bei mbaya na kutowapa nafasi ya kumpanda kichwani na wachezaji hao kumpa hadhi na nafasi yake ya ukocha, tofauti na hivyo atajikuta pagumu.
Kazi hii ya kuwasimamia mastaa wa bei mbaya ilimshinda Jose Antonio Camacho akiwa kocha wa Real Madrid yenye Zidane, Beckham, Roberto Carlos, Ronaldo de Lima na wengineo, aliamua kujiuzulu na kueleza wazi kuwa ameshindwa kuwaongoza mastaa hao wa bei mbaya.
Tusishangae katikati ya safari ya Real Madrid hii badala ya mataji likatokea jambo kama hilo kwa Ancelotti naye akajikuta akilazimika kujiuzulu.
Sambamba na hilo pia tushishangae katikati ya safari hii tukasikia, Florentino Perez, rais wa Real Madrid amechukua uamuzi mgumu wa kumfuta kazi Ancelotti baada ya kuona mambo yanakwenda kinyume na matarajio yake.

The post Real Madrid hii yenye Mbappe, Vinicius Jr, Bellingham first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/19/real-madrid-hii-yenye-mbappe-vinicius-jr-bellingham/feed/ 0
Mbappe kutambulishwa Madrid mbele ya mashabiki 81,000 https://www.greensports.co.tz/2024/07/12/mbappe-kutambulishwa-madrid-mbele-ya-mashabiki-81000/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/12/mbappe-kutambulishwa-madrid-mbele-ya-mashabiki-81000/#respond Fri, 12 Jul 2024 07:15:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11593 Madrid, HispaniaKlabu ya Real Madrid ya Hispania Julai 16 itamtangaza rasmi mbele ya mashabiki 81,000 mshambuliaji wake mpya, Kylian Mbappe ambaye pia wametangaza kumpa jezi namba 9.Mbappe amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitano akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na klabu ya PSG ya Ufaransa kufikia ukomo Juni mwaka huu.Utambulisho wa […]

The post Mbappe kutambulishwa Madrid mbele ya mashabiki 81,000 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Klabu ya Real Madrid ya Hispania Julai 16 itamtangaza rasmi mbele ya mashabiki 81,000 mshambuliaji wake mpya, Kylian Mbappe ambaye pia wametangaza kumpa jezi namba 9.
Mbappe amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitano akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na klabu ya PSG ya Ufaransa kufikia ukomo Juni mwaka huu.
Utambulisho wa Mbappe unatarajia kuweka historia mpya ya klabu hiyo kwa kushuhudiwa na mashabiki wengi tangu klabu hiyo imtambulishe Cristiano Ronaldo mwaka 2009.
Utambulisho wa Mbappe unakuwa umehitimisha mbio za muda mrefu za Real Madrid kuisaka saini ya mchezaji huyo baada ya kujaribu katika vipindi viwili tofauti lakini kwa wakati wote kulikuwa na ugumu.
Bado haijawekwa wazi kama Mbappe atakuwa na klabu hiyo katika ziara za kujiandaa na msimu mpya wa 2024-25 nchini Marekani ambazo zitaanza hivi katibuni kwa timu hiyo kucheza mechi za kirafiki dhidi ya AC Milan, Barcelona na baadaye Chelsea.
Baada ya mechi hiyo, Real Madrid itacheza mechi ya Uefa Super Cup dhidi ya Atalanta, mechi itakayopigwa Agosti 14 na baada ya hapo Agosti 18, timu hiyo itaanza rasmi mbio za kulitetea taji la La Liga kwa kuuumana na Mallorca.
Mbappe alianza kuwindwa na Real Madrid tangu akiwa Monaco kabla ya kujiunga na PSG mwaka 2017 na hadi sasa ameifungia PSG mabao 256 katika misimu saba.

The post Mbappe kutambulishwa Madrid mbele ya mashabiki 81,000 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/12/mbappe-kutambulishwa-madrid-mbele-ya-mashabiki-81000/feed/ 0