Mayanga - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 02 Sep 2023 20:08:45 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Mayanga - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mayanga aitaka Mbeya City ligi kuu https://www.greensports.co.tz/2023/09/02/mayanga-aitaka-mbeya-city-ligi-kuu/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/02/mayanga-aitaka-mbeya-city-ligi-kuu/#respond Sat, 02 Sep 2023 20:08:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7650 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Mbeya City inayoshiriki Ligi ya Championship, Salum Mayanga amesema licha ya kuwa na kazi ngumu mbele yao lakini wamepania kuhakikisha wanairejesha timu hiyo Ligi Kuu NBC msimu ujao.Mayanga ameyasema hayo wakati kikosi chake kikiendelea na maandalizi ya kuivaa Green Warriors katika mchezo wa kwanza wa ligi hiyo itakayoanza Septemba 9, […]

The post Mayanga aitaka Mbeya City ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Mbeya City inayoshiriki Ligi ya Championship, Salum Mayanga amesema licha ya kuwa na kazi ngumu mbele yao lakini wamepania kuhakikisha wanairejesha timu hiyo Ligi Kuu NBC msimu ujao.
Mayanga ameyasema hayo wakati kikosi chake kikiendelea na maandalizi ya kuivaa Green Warriors katika mchezo wa kwanza wa ligi hiyo itakayoanza Septemba 9, mwaka huu.
“Tuko kwenye maandalizi mazuri, tumefanya usajili wa wachezaji vijana na wazoefu ukiwa ni mchanganyiko ambao tumekuwa nao mazoezini kwa takriban wiki mbili na umetupa picha nzuri kuelekea mechi ya kwanza na Green Warriors.

“Niseme kuna kazi ngumu ya kufanya mbele ya safari lakini ni lazima tuifanye na tuwe kwenye hali ya kupambana kuirejesha timu ligi kuu msimu ujao, hiyo ndio nia ya uongozi, mimi na wenzangu wa benchi la ufundi,” alisema Mayanga kocha wa zamani wa Mtibwa Sugar.


Kocha huyo pia alisema anaamini cha muhimu ni ushirikiano baina ya benchi la ufundi, mashabiki na wakazi wa Mbeya kwa ujumla kuhakikisha timu hiyo iliyodumu kwenye ligi kuu kwa misimu 10 mfululizo kabla ya kushuka mwishoni mwa msimu uliopita, inarejea kwa kishindo msimu ujao.

The post Mayanga aitaka Mbeya City ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/02/mayanga-aitaka-mbeya-city-ligi-kuu/feed/ 0
Mayanga kurekebisha mambo Mtibwa Sugar https://www.greensports.co.tz/2023/05/23/mayanga-kurekebisha-mambo-mtibwa-sugar/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/23/mayanga-kurekebisha-mambo-mtibwa-sugar/#respond Tue, 23 May 2023 13:29:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6261 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Salum Mayanga amesema anayatumia mapumziko ya Ligi Kuu NBC kukifanyia marekebisho kikosi chake ili kuhakikisha anakusanya pointi sita na kujiondoa chini ya msimamo wa ligi hiyo.Mtibwa inayoshika nafasi ya 14 baada ya michezo 28 na kujikusanyia pointi 29 inatarajiwa kuwakabili Kagera Sugar Juni 6, mwaka huu kwenye Uwanja […]

The post Mayanga kurekebisha mambo Mtibwa Sugar first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Salum Mayanga amesema anayatumia mapumziko ya Ligi Kuu NBC kukifanyia marekebisho kikosi chake ili kuhakikisha anakusanya pointi sita na kujiondoa chini ya msimamo wa ligi hiyo.
Mtibwa inayoshika nafasi ya 14 baada ya michezo 28 na kujikusanyia pointi 29 inatarajiwa kuwakabili Kagera Sugar Juni 6, mwaka huu kwenye Uwanja wa Manungu Complex, Morogoro.
Wakata Miwa hao wanatarajia kumaliza msimu huu wa 2022-23 Juni 9, kwa kuwaalika Geita Gold kwenye Uwanja wa Manungu Complex.
Mayanga (pichani juu) alisema baada ya ligi kusogezwa mbele anaendelea kuyafanyia kazi mapungufu ya kikosi na kuweka mikakati ya kuhakikisha wanakusanya pointi zote zilizosalia kabla ya kufungwa rasmi kwa ligi msimu huu.

“Bado hatuko kwenye eneo zuri kwenye msimamo, tunahitaji ushindi zaidi kwenye michezo ijayo tukianza na ule wa Kagera Sugar ambao naamini utakuwa mgumu maana tumetoka kupoteza mechi iliyopita.


“Lakini pia tutamaliza msimu kwa kucheza na Geita Gold, kwenye uwanja wetu wa nyumbani hivyo hatupaswi kufanya makosa katika mchezo huo pia,” alisema Mayanga.

The post Mayanga kurekebisha mambo Mtibwa Sugar first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/23/mayanga-kurekebisha-mambo-mtibwa-sugar/feed/ 0