Maxime - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 18 May 2024 17:11:33 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Maxime - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Maxime ajivunia ubora Ihefu akiivaa Yanga https://www.greensports.co.tz/2024/05/18/maxime-ajivunia-ubora-ihefu-akiivaa-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/18/maxime-ajivunia-ubora-ihefu-akiivaa-yanga/#respond Sat, 18 May 2024 17:11:30 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11013 Na mwandishi wetuKocha mkuu wa Ihefu FC, Mecky Maxime amesema anatambua wapinzani wao katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho CRDB, Yanga wana wachezaji hatari lakini hata wao pia wana wachezaji wenye ubora mkubwa wa kuamua matokeo.Maxime ameyasema hayo leo Jumamosi kuelekea mechi hiyo itakayopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha ambapo amesisitiza […]

The post Maxime ajivunia ubora Ihefu akiivaa Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Ihefu FC, Mecky Maxime amesema anatambua wapinzani wao katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho CRDB, Yanga wana wachezaji hatari lakini hata wao pia wana wachezaji wenye ubora mkubwa wa kuamua matokeo.
Maxime ameyasema hayo leo Jumamosi kuelekea mechi hiyo itakayopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha ambapo amesisitiza kuwa anafahamu ushindi wao utatokana na umoja wakishirikiana kudhibiti, kukaba na kushambulia kwa pamoja kama timu.
“Kikubwa kwanza kwenye timu kuwa kitimu kimpira na sio walinzi peke yao ndio wafanye kazi ya kuzuia, yaani mnazuia kama timu na hiyo inakuwa pale mpira mnaponyang’anywa ndipo mara moja mnapoanza kufanya ulinzi.
“Japo tunafahamu Yanga ina wachezaji wazuri kama alivyosema mwalimu wao (Miguel Gamondi), wachezaji hatari ambao nafasi moja mbili wanakumaliza.
“Sasa Ihefu pia ina wachezaji bora na sasa hivi tupo kwenye muunganiko mzuri toafuti na mwanzo, sasa hivi timu imeshasimama kwa hiyo na sisi pia tunao watu ambao wanaweza kumaliza mechi.
“Kikubwa Yanga wanakimbia sana, sasa ili kwenda nao sawa lazima na wewe ubora wa kazi yako uwe mkubwa sana, kitu ambacho naamini tutakwenda kukifanya hiyo kesho,” alisema Maxime.

The post Maxime ajivunia ubora Ihefu akiivaa Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/18/maxime-ajivunia-ubora-ihefu-akiivaa-yanga/feed/ 0
Maxime ataka vipaji vitumike Ihefu https://www.greensports.co.tz/2024/01/17/maxime-ataka-vipaji-vitumike-ihefu/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/17/maxime-ataka-vipaji-vitumike-ihefu/#respond Wed, 17 Jan 2024 19:32:57 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9328 Na mwandishi wetuKocha wa Ihefu FC, Mecky Maxime amewataka wachezaji wake kutumia vipaji vyao kikamilifu kwa faida yao na kuipa matokeo mazuri timu hiyo.Akizungumza na GreenSports, Maxime alisema nafasi waliyopo kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC haiendani na ukubwa wa majina na umaarufu waliokuwa nao katika ligi hiyo.“Ligi ya msimu huu ni ngumu, inahitaji wachezaji […]

The post Maxime ataka vipaji vitumike Ihefu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha wa Ihefu FC, Mecky Maxime amewataka wachezaji wake kutumia vipaji vyao kikamilifu kwa faida yao na kuipa matokeo mazuri timu hiyo.
Akizungumza na GreenSports, Maxime alisema nafasi waliyopo kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC haiendani na ukubwa wa majina na umaarufu waliokuwa nao katika ligi hiyo.
“Ligi ya msimu huu ni ngumu, inahitaji wachezaji wanaopambana na siyo umaarufu au ukubwa wa majina. Mimi na vijana wangu tunapaswa kupambana na kila mmoja kutimiza majukumu yake ili kuiondoa timu kwenye nafasi mbaya iliyopo hivi sasa,” alisema Maxime.
Alisema kuwa na wachezaji wazuri si kitu muhimu, kama wachezaji hao hawajitumi, hivyo atahakikisha anaandaa mpango mkakati utakaomwezesha kila mchezaji kuchangia mafanikio wanayakusudia.
Ihefu ipo nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi ikikusanya pointi 13, imefanya usajili wa wachezaji; Elvis Rupia, Duke Abuya na Bruno Gomes wote kutoka Singida Fountain Gate kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao kuelekea duru la pili la ligi hiyo.

The post Maxime ataka vipaji vitumike Ihefu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/17/maxime-ataka-vipaji-vitumike-ihefu/feed/ 0
Maxime aahidi makubwa Ihefu https://www.greensports.co.tz/2024/01/03/maxime-aahidi-makubwa-ihefu/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/03/maxime-aahidi-makubwa-ihefu/#respond Wed, 03 Jan 2024 17:42:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9140 Na mwandishi wetuKocha mkuu wa Ihefu, Mecky Maxime amewataka mabosi wa timu hiyo watarajie mambo makubwa kutokana na mifumo ya kisasa anayoipandikiza kwa wachezaji wake.Akizungumza leo Jumatano, kocha huyo alisema timu hiyo ina wachezaji wazuri isipokuwa kilichokuwa kinawasumbua kutopata matokeo mazuri ni mfululizo wa vipigo. “Kufungwa mfululizo kumevuruga saikolojia ya wachezaji, baada ya kukabidhiwa timu […]

The post Maxime aahidi makubwa Ihefu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Ihefu, Mecky Maxime amewataka mabosi wa timu hiyo watarajie mambo makubwa kutokana na mifumo ya kisasa anayoipandikiza kwa wachezaji wake.
Akizungumza leo Jumatano, kocha huyo alisema timu hiyo ina wachezaji wazuri isipokuwa kilichokuwa kinawasumbua kutopata matokeo mazuri ni mfululizo wa vipigo.

“Kufungwa mfululizo kumevuruga saikolojia ya wachezaji, baada ya kukabidhiwa timu kitu cha kwanza nilichoanza nacho ni kujenga saikolojia zao na kupandisha ari ya upambanaji ili waweze kufanya vizuri,” alisema Maxime.


Kocha huyo alisema mipango yake ni kuiondoa Ihefu nafasi ya 13 hivi sasa kwenye Ligi Kuu NBC na kuipandisha nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 16.
Alisema anatambua ugumu uliopo kwenye ligi ya msimu huu lakini anajivunia uwezo wa wachezaji wake pamoja na wasaidizi wake hakuna kitu kitashindikana.
Ihefu ambayo hadi sasa imeshatimua makocha wawili ambao ni Zuberi Katwila na Moses Basena, ipo nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi ikikusanya pointi 13 katika michezo 14.

The post Maxime aahidi makubwa Ihefu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/03/maxime-aahidi-makubwa-ihefu/feed/ 0
Maxime kocha mpya Ihefu https://www.greensports.co.tz/2023/12/28/maxime-kocha-mpya-ihefu/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/28/maxime-kocha-mpya-ihefu/#respond Thu, 28 Dec 2023 14:27:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9050 Na mwandishi wetuIhefu FC imemtangaza Mecky Maxime kuwa kocha wao mkuu mpya kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho chenye makazi yake Mbarali mkoani Mbeya.Maxime ametangazwa na klabu hiyo leo Alhamisi ikiwa ni siku tano zimepita tangu aachane na Kagera Sugar kwa makubaliano ya pande zote mbili baada ya matokeo ya timu hiyo kuzidi kudorora.Kwa mujibu […]

The post Maxime kocha mpya Ihefu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Ihefu FC imemtangaza Mecky Maxime kuwa kocha wao mkuu mpya kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho chenye makazi yake Mbarali mkoani Mbeya.
Maxime ametangazwa na klabu hiyo leo Alhamisi ikiwa ni siku tano zimepita tangu aachane na Kagera Sugar kwa makubaliano ya pande zote mbili baada ya matokeo ya timu hiyo kuzidi kudorora.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ihefu iliyowekwa kwenye mtandao wake, wanaamini Maxime ni kocha mzuri na mkubwa katika nchi hii, hivyo atawasaidia kufikia malengo waliyokusudia msimu huu.

“Maxime ni kocha mkubwa ndani ya nchi yetu na ni mzoefu kisoka kwa ngazi ya klabu na timu za taifa kwa ujumla, kuanzia sasa ataliongoza benchi letu la ufundi la Mbogo Maji kama kocha mkuu katika ligi na mashindano mengine,” ilieleza taarifa hiyo.


Maxime, mchezaji wa zamani wa Taifa Stars na timu ya Mtibwa Sugar, anatua Ihefu kuchukua mikoba ya kocha kutoka Uganda, Moses Basena aliyeoneshwa mlango wa kutokea mwanzoni mwa mwezi huu.
Kocha huyo mpya ana kazi kubwa ya kufanya kuiondosha timu hiyo kwenye nafasi za chini ambapo sasa inashika nafasi ya 13 ikiwa na pointi 13 baada ya michezo 14.

The post Maxime kocha mpya Ihefu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/28/maxime-kocha-mpya-ihefu/feed/ 0
Maxime atamba kuifunga Simba https://www.greensports.co.tz/2023/12/11/maxime-atamba-kuifunga-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/11/maxime-atamba-kuifunga-simba/#respond Mon, 11 Dec 2023 18:27:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8821 Na mwandishi wetuKocha mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime ametamba kuifunga Simba katika mchezo wa Ligi Kuu NBC utakaochezwa Desemba 15, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.Kocha huyo alisema kinachompa matumaini ya kushinda mchezo huo ni wakati mgumu wanaopitia wapinzani wao Simba, kwenye michuano ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika. […]

The post Maxime atamba kuifunga Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime ametamba kuifunga Simba katika mchezo wa Ligi Kuu NBC utakaochezwa Desemba 15, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kocha huyo alisema kinachompa matumaini ya kushinda mchezo huo ni wakati mgumu wanaopitia wapinzani wao Simba, kwenye michuano ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Simba ni timu yenye wachezaji wazuri hilo hatulipingi lakini kuhusu uzoefu hata Kagera Sugar tuna uzoefu wa kutosha, cha msingi tumejipanga kupata pointi tatu katika mchezo huo bila kujali tunacheza wapi na timu gani,” alisema Maxime.


Alisema hawapo tayari kupoteza mechi mbili mfululizo baada ya wiki iliyopita kufungwa na Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Kagera Sugar inashika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 13 baada ya michezo 11 huku Simba ikishikilia nafasi ya tatu kwa pointi 19 baada ya mechi nane.

The post Maxime atamba kuifunga Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/11/maxime-atamba-kuifunga-simba/feed/ 0
Maxime: Stars inahitaji pongezi https://www.greensports.co.tz/2023/03/30/maxime-stars-inahitaji-pongezi/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/30/maxime-stars-inahitaji-pongezi/#respond Thu, 30 Mar 2023 12:37:06 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5635 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema licha ya timu ya taifa, Taifa Stars kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Uganda lakini wachezaji wanapaswa kupongezwa kwa kazi waliyoifanya.Maxime ameeleza hayo akisisitiza kuwa mbali na matokeo hayo lakini vijana walijitahidi kupambana na kwamba haikuwa riziki yao na ushindi ukatua kwa Uganda.Alisema kuwa wanapaswa […]

The post Maxime: Stars inahitaji pongezi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema licha ya timu ya taifa, Taifa Stars kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Uganda lakini wachezaji wanapaswa kupongezwa kwa kazi waliyoifanya.
Maxime ameeleza hayo akisisitiza kuwa mbali na matokeo hayo lakini vijana walijitahidi kupambana na kwamba haikuwa riziki yao na ushindi ukatua kwa Uganda.
Alisema kuwa wanapaswa kupongezwa na si kukatishwa tamaa kwani bado kuna nafasi ya mechi mbili za kufanya vizuri kufuzu kushiriki fainali za Mataifa Afrika (Afcon) 2023 zitakazofanyika Ivory Coast.

“Inabidi tuwapongeze, wamepambana kwa kiasi chao lakini yote kwa yote haikuwa riziki yetu, wao (Uganda) wamepata matokeo lakini kikubwa ni kuwapongeza wachezaji maana bado wana nafasi, tuna mechi mbili tusikate tamaa,” alisema Maxime nahodha wa zamani wa Stars.


Alisema kiufundi timu hiyo ilipoteza mchezo huo uliopigwa juzi Jumanne, Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam baada ya kutoka kwa viungo Mzamiru Yassin na Himid Mao ambao kwa kiasi kikubwa walifanikiwa kuidhibiti Uganda eneo la katikati ambalo walikuwa hatari zaidi.
Katika Kundi F, Stars inashikilia nafasi ya pili kwa pointi nne sawa na Uganda inayoshika nafasi ya tatu. Algeria imeshafuzu kwa pointi zake 12 ikiwa kileleni huku Niger ikiburuza mkia kwa pointi mbili.

The post Maxime: Stars inahitaji pongezi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/30/maxime-stars-inahitaji-pongezi/feed/ 0
Maxime aipigia hesabu Uganda Cranes https://www.greensports.co.tz/2022/08/30/maxime-aipigia-hesabu-uganda-cranes/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/30/maxime-aipigia-hesabu-uganda-cranes/#respond Tue, 30 Aug 2022 19:03:00 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2619 Na mwandishi wetuKocha msaidizi wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mecky Maxime ameanza kuipigia hesabu mechi yao na timu ya Taifa ya Uganda au Uganda Cranes akisema kwamba ingawa soka ni mchezo usiotabirika lakini watajitahidi kuanza kazi yao vizuri kwa kupata matokeo.Maxime nahodha wa zamani wa Stars na timu ya Mtibwa Sugar, mbali na kuizungumzia […]

The post Maxime aipigia hesabu Uganda Cranes first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha msaidizi wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mecky Maxime ameanza kuipigia hesabu mechi yao na timu ya Taifa ya Uganda au Uganda Cranes akisema kwamba ingawa soka ni mchezo usiotabirika lakini watajitahidi kuanza kazi yao vizuri kwa kupata matokeo.
Maxime nahodha wa zamani wa Stars na timu ya Mtibwa Sugar, mbali na kuizungumzia mechi hiyo ya marudiano na Uganda Cranes pia ameshukurun kwa kupewa nafasi hiyo kulipigania taifa lake huku akisisitiza ushirikiano kwa Watanzania wote katika kuipeleka nchi ya ahadi timu hiyo.
“Hakuna asiyetamani kupata nafasi hii maana hii ni timu yetu wote Watanzania kwa hiyo kikubwa ni kushirikiana. Mchezo wa soka ukiwa kama kocha ni kama unacheza kamari wakati mwingine, ni kama unafanya ‘sub’ ya mchezaji na huwezi kujua kama ataenda kuleta unachotaka au atakosea,” alisema kocha huyo mpya wa Stars.
“Kwa hiyo siwezi kusema maneno mengi sana kikubwa ni kufanya kazi, mpira ni mchezo wa wazi kila mtu anauona kwa hiyo kazi yetu itaonekana kutokana na matokeo yatakayopatikana,” alieleza Maxime.
Kuhusu mchezo huo wa marudiano ambao ni wa kuwania kufuzu michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani au CHAN utakaopigwa Septemba 3, mwaka huu nchini Uganda, kocha huyo alisema inawezekana kupata matokeo dhidi ya Uganda ingawa itawabidi kupambana.
Katika mechi ya kwanza iliyopigwa juzi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, Stars ililala kwa bao 1-0 na kupelekea kuondolewa kwa kocha Kim Poulsen na mikoba yake kupewa Mzambia, Hanour Janza akisaidiwa na Maxime na kocha wa makipa, Juma Kaseja.
“Huu ni mchezo wa mpira tusidanganyane, kikubwa tumepewa nafasi acha tufanye kile tunachoweza kwa mechi hii lakini nafikiri mbele huko yatakuwepo makubwa zaidi, kwa hiyo mechi hii acha tukapambane tutafute matokeo na inawezekana sio kama haiwezekani, inawezekana vizuri tu.
“Kama nilivyosema tushirikiane, tunaweza kufanya kazi lakini kwanza kuombeana uzima na wao pia mashabiki wana mchango mkubwa, warudi tuipende timu yetu, hilo ndiyo muhimu zaidi kuliko mimi kuja hapa. Watanzania tuje uwanjani wachezaji nao wapate moyo, tuipende timu yetu tuwatie moyo wachezaji wetu,” alisisitiza Maxime.

The post Maxime aipigia hesabu Uganda Cranes first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/30/maxime-aipigia-hesabu-uganda-cranes/feed/ 0