Mason Greenwood - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 01 Mar 2024 08:12:00 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Mason Greenwood - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Greenwood atakiwa abaki Hispania https://www.greensports.co.tz/2024/03/01/greenwood-atakiwa-abaki-hispania/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/01/greenwood-atakiwa-abaki-hispania/#respond Fri, 01 Mar 2024 08:11:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9950 Madrid, HispaniaRais wa Ligi Kuu Hispania au La Liga, Javier Tebas amesema anatumaini mshambuliaji wa Man United, Mason Greenwood anayecheza kwa mkopo katika klabu ya Getafe atabaki Hispania hata baada ya muda wake wa mkopo kufikia mwisho.Greenwood alijiunga na Getafe, Septemba mwaka jana baada ya Man United kubadili uamuzi wa awali wa kumtaka abaki katika […]

The post Greenwood atakiwa abaki Hispania first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Rais wa Ligi Kuu Hispania au La Liga, Javier Tebas amesema anatumaini mshambuliaji wa Man United, Mason Greenwood anayecheza kwa mkopo katika klabu ya Getafe atabaki Hispania hata baada ya muda wake wa mkopo kufikia mwisho.
Greenwood alijiunga na Getafe, Septemba mwaka jana baada ya Man United kubadili uamuzi wa awali wa kumtaka abaki katika klabu hiyo licha ya kuandamwa na kashfa ya kumdhalilisha mwanamke.
Man United walitangaza kufanya uchunguzi wa ndani baada ya Greenwood kufutiwa kesi ya udhalilishaji na kukawa na dalili za mchezaji huyo kubaki katika klabu hiyo lakini jambo hilo lilikumbana na vikwazo kadhaa na hivyo ikaonekana bora kumuuza kwa mkopo.
Akizungumzia suala la Greenwood, Tebas alisema yeye kama mwanasheria hana sababu ya kuhoji mambo yaliyopita ya mchezaji huyo kuhusu mashtaka yaliyokuwa yakimkabili kufutwa badala yake anachofahamu ni kwamba amekutwa hana hatia

“Mimi ni mwanasheria, kama mtu anapitia mahakamani kisheria na kukutwa hana hatia, hapo hakuna zaidi la kuzungumza,” alisema Tebas.


Tebas alimsifia Greenwood akisema kwamba anafanya vizuri na anaamini ataendelea kucheza soka la Hispania kwani jambo hilo pia ni zuri kwao La Liga.
Alipobanwa zaidi kuhusu sakata la udhalilishaji linalomkabili mchezaji huyo, Tebas alisema kwamba kama mchezaji huyo hakuadhibiwa huko, si jukumu la La Liga kumchukulia hatua za kisheria.
“Ni lazima mheshimu mifumo ya kisheria, watu wanaweza kumshutumu kwenye vyombo vya habari lakini mna ulazima wa kuheshimu maamuzi wa kimahakama, hakuna la kuzungumza zaidi ya hilo,” alisema Tebas.

The post Greenwood atakiwa abaki Hispania first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/01/greenwood-atakiwa-abaki-hispania/feed/ 0
Sakata la Greenwood lamuibua Gary Neville https://www.greensports.co.tz/2023/08/22/sakata-la-greenwood-lamuibua-gary-neville/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/22/sakata-la-greenwood-lamuibua-gary-neville/#respond Tue, 22 Aug 2023 17:38:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7477 Manchester, EnglandBeki wa zamani wa Man United, Gary Neville amekerwa kwa jinsi klabu hiyo inavyochunguza sakata la mshambuliaji Mason Greenwood ambaye Februari mwaka huu alifutiwa mashtaka ya udhalilishaji kijinsia na jaribio la kubaka.Neville (pichani juu), beki wa zamani wa kulia na ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka amesema klabu hiyo imeliendesha suala hilo katika […]

The post Sakata la Greenwood lamuibua Gary Neville first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Beki wa zamani wa Man United, Gary Neville amekerwa kwa jinsi klabu hiyo inavyochunguza sakata la mshambuliaji Mason Greenwood ambaye Februari mwaka huu alifutiwa mashtaka ya udhalilishaji kijinsia na jaribio la kubaka.
Neville (pichani juu), beki wa zamani wa kulia na ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka amesema klabu hiyo imeliendesha suala hilo katika namna ya hovyo na kumekosekana uongozi imara katika kulisimamia jambo hilo.
Greenwood, 21, anatarajia kuondoka Man United kwa makubaliano ya pande mbili baada ya uchunguzi wa takriban miezi sita unaofanywa na klabu hiyo kukamilika.
“Ilikuwa wazi tangu siku ya kwanza kwamba asingeweza kuichezea tena Manchester United,” alisema Neville ambaye mbali na Man United pia alikuwa beki wa timu ya Taifa ya England.
“Tukio zima limeendeshwa hovyo, unapokuwa na mazingira kama haya kunahitajika uongozi imara na wenye maamuzi, na huo unatoka kwa viongozi wa juu, Manchester United hawana watu hao,” alisema Neville.
Greenwood (pichani chini) ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya Taifa ya England, alikamatwa Januari 2022 baada ya kuwapo tuhuma za udhalilishaji kijinsia ambazo pia zilichapishwa kwenye mitandao ya kijamii.
Katika taarifa yake, Greenwood alikubali kuwa alifanya makosa na anastahili kubeba lawama lakini hapo hapo alisema kwamba hakufanya makosa ambayo anatuhumiwa kuyafanya.
Man United katika taarifa yao walidai kuwa kwa kuzingatia ushahidi walio nao wamefikia hitimisho kwamba yaliyochapishwa kwenye mitandao hayatoi picha ya Greenwood kutohusika na makosa ambayo awali alishitakiwa akidaiwa kuyafanya.

Taarifa hiyo pia iliongeza kuwa watu wote waliohusishwa katika kuutafuta ukweli akiwamo Mason mwenyewe wamebaini ugumu wa mchezaji huyo kuendelea na maisha yake ya soka katika klabu ya Manchester United.
Awali ilielezwa kwamba hatma ya mchezaji huyo ingejulikana kabla ya Agosti 14 siku ambayo Man United ilicheza mechi yake ya kwanza ya msimu mpya wa Ligi Kuu England dhidi ya Wolves lakini haikuwa hivyo kwa kinachodhaniwa kuwa ni mjadala mkali baina ya vigogo wa klabu hiyo kuhusu uwezekano wa kumrudisha Greenwood Man United.
Makundi ya wanawake wa klabu ya Man United wanaongoza kampeni ya kupinga uwezekano wa mchezaji huyo kurudishwa na kuendelea na maisha ya soka katika klabu hiyo.

The post Sakata la Greenwood lamuibua Gary Neville first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/22/sakata-la-greenwood-lamuibua-gary-neville/feed/ 0
Wanawake washikilia hatma ya Greenwood Man United https://www.greensports.co.tz/2023/08/11/wanawake-wabeba-hatma-ya-greenwood-man-united/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/11/wanawake-wabeba-hatma-ya-greenwood-man-united/#respond Fri, 11 Aug 2023 19:29:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7346 Manchester, EnglandKlabu ya Manchester United itashauriana na timu yake ya wanawake kabla ya kuamua kumbakisha au kuachana na mshambuliaji wake, Mason Greenwood (pichani) aliyekuwa akikabiliwa na tuhuma za udhalilishaji kijinsia.Awali uamuzi wa klabu hiyo kuhusu Greenwood ilitarajiwa ungetangazwa kabla ya timu hiyo kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu England (EPL) msimu wa 2023-24, […]

The post Wanawake washikilia hatma ya Greenwood Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Klabu ya Manchester United itashauriana na timu yake ya wanawake kabla ya kuamua kumbakisha au kuachana na mshambuliaji wake, Mason Greenwood (pichani) aliyekuwa akikabiliwa na tuhuma za udhalilishaji kijinsia.
Awali uamuzi wa klabu hiyo kuhusu Greenwood ilitarajiwa ungetangazwa kabla ya timu hiyo kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu England (EPL) msimu wa 2023-24, Jumatatu hii dhidi ya Wolves lakini umechelewa.
Februari mwaka huu tuhuma zilizokuwa zikimkabili Greenwood za kusudio la kubaka na udhalilishaji kijinsia zilifutwa na mahakama baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha.
Mapema Ijumaa hii kundi la mashabiki wanawake wa Man United walitangaza nia yao ya kufanya maandamano juu ya uamuzi wowote wa kumpa nafasi Greenwood, maandamano ambayo yangefanywa nje ya Uwanja wa Old Trafford kabla ya mechi ya Jumatatu.
Hoja ya mashabiki hao ni katika kuitaka klabu hiyo kutovumilia aina yoyote ya unyanyasaji dhidi ya wanawake.
Man United sasa inataka kuwashirikisha wadau muhimu wakiwamo viongozi wa timu ya wanawake ambao baadhi yao wapo nchini New Zealand na Australia zinapofanyika fainali za Kombe la Dunia za Wanawake kabla ya kuamua lolote kuhusu Greenwood.
Hata hivyo haijaweza kufahamika mara moja sakata la mchezaji huyo litafikia tamati lini ingawa zipo habari kwamba mbali na timu ya wanawake kuhusishwa kumekuwa na mazungumzo yanayoendelea ambayo pia yanaihusisha familia ya mchezaji huyo.
Greenwood alikamatwa Januari mwaka jana baada ya kutuhumiwa kwa makosa ya kutaka kubaka na udhalilishaji wa kijinsia baada ya kuwapo habari kwamba picha zake zikiwamo za video zimewekwa kwenye mitandao ya kijamii.
Badaye hata hivyo mchezaji huyo alishitakiwa kwa tuhuma za kutaka kubaka na kuwa na tabia za kibabe dhidi ya wanawake.

The post Wanawake washikilia hatma ya Greenwood Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/11/wanawake-wabeba-hatma-ya-greenwood-man-united/feed/ 0
Greenwood wa Man Utd afutiwa kesi ya ubakaji https://www.greensports.co.tz/2023/02/03/greenwood-wa-man-utd-afutiwa-kesi-ya-ubakaji/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/03/greenwood-wa-man-utd-afutiwa-kesi-ya-ubakaji/#respond Fri, 03 Feb 2023 06:08:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4987 Manchester, EnglandKesi ya kupanga mikakati ya kubaka na shambulio la kimwili iliyokuwa ikimkabili mshambuliaji wa Man United, Mason Greenwood hatimaye imefutwa.Greenwood mwenye umri wa miaka 21 alikamatwa Januari mwaka jana akituhumiwa kwa kosa la kupanga mipango ya kubaka, tabia za kibabe na udhalilishaji mwili.Katika taarifa yake Greenwood ambaye Desemba, 2021 alikuwa akiwindwa na klabu za […]

The post Greenwood wa Man Utd afutiwa kesi ya ubakaji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kesi ya kupanga mikakati ya kubaka na shambulio la kimwili iliyokuwa ikimkabili mshambuliaji wa Man United, Mason Greenwood hatimaye imefutwa.
Greenwood mwenye umri wa miaka 21 alikamatwa Januari mwaka jana akituhumiwa kwa kosa la kupanga mipango ya kubaka, tabia za kibabe na udhalilishaji mwili.
Katika taarifa yake Greenwood ambaye Desemba, 2021 alikuwa akiwindwa na klabu za Barcelona na Arsenal, alisema kwamba anajisikia faraja na kuishukuru familia, marafiki na wapendwa wote ambao wamekuwa naye pamoja wakimpa ushirikiano katika kadhia iliyokuwa ikimkabili.
Taarifa ya kimahakama ilidai kuziarifu pande zote husika juu ya uamuzi huo na kwamba wakati wote ilishauriwa kwa mtu yeyote aliyekutwa na kadhia hiyo kujitokeza na kuripoti polisi na uchunguzi ungefanywa kadri ambavyo ingewezekana.
Tangu kuhusishwa na tuhuma hizo, Greenwood alisimamishwa kuichezea Man United lakini baada ya hukumu kutoka, mwakilishi wa klabu hiyo alisema kwamba wamepokea uamuzi wa waendesha mashtaka wa kufuta tuhuma zote zilizokuwa zikimkabili mchezaji huyo.
Kwa mujibu wa mwakilishi huyo hata hivyo, klabu itapitia taratibu zake za ndani kabla ya kuamua hatua zinazofuata, “kwa sasa hatutoweza kusema lolote zaidi ya hilo, ni hadi taratibu zetu zitakapokamilika.”

The post Greenwood wa Man Utd afutiwa kesi ya ubakaji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/03/greenwood-wa-man-utd-afutiwa-kesi-ya-ubakaji/feed/ 0