Mashujaa FC - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 05 May 2025 20:34:09 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Mashujaa FC - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Simba yailaza Mashujaa 2-1 kwa mbinde https://www.greensports.co.tz/2025/05/03/simba-yailaza-mashujaa-2-1-kwa-mbinde/ https://www.greensports.co.tz/2025/05/03/simba-yailaza-mashujaa-2-1-kwa-mbinde/#respond Fri, 02 May 2025 21:11:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13377 Na mwandishi wetuSimba imepambana na Mashujaa FC kwa mbinde hadi kupata ushindi wa mabao 2-1 baada ya kuwa nyuma kwa bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa leo Ijumaa, Mei 2, 2025 kwenye Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.Mashujaa walipata bao la mapema katika dakika ta sita ya mchezo huo lililopachikwa wavuni na […]

The post Simba yailaza Mashujaa 2-1 kwa mbinde first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Simba imepambana na Mashujaa FC kwa mbinde hadi kupata ushindi wa mabao 2-1 baada ya kuwa nyuma kwa bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa leo Ijumaa, Mei 2, 2025 kwenye Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.
Mashujaa walipata bao la mapema katika dakika ta sita ya mchezo huo lililopachikwa wavuni na Jaffar Salum na kuiweka Simba katika wakati mgumu.
Simba ilianza kupambana kusaka bao la kusawazisha lakini juhudi zao hazikuweza kuzaa matunda kwa dakika zote 45 za mchezo huo licha ya kulisogelea mara kwa mara lango la Mashujaa.
Simba ilifanikiwa kupata bao la kusawazisha katika dakika ya 65 lililofungwa na Leonel Ateba kwa mkwaju wa penalti kabla ya Ateba tena kufunga bao la pili kwa penalti katika dakika za nyongeza baada ya dakika 90 (90+14) za kawaida kumalizika.
Bao la pili la Simba lilipatikana wakati wapinzani wao Mashujaa wakiwa pungufu baada ya kipa wao, Patrick Mumthali kutolewa kwa kadi nyekundu katika dakika ya 77.
Kwa kuwa Mashujaa walikuwa wamemaliza idadi ya wachezaji wa kufanyiwa mabadiliko, kiungo Abdulnasir Mohamed alilazimika kwenda kukaa golini na kufanikiwa kuwadhiti Simba kabla ya kuzamishwa na mkwaju wa penalti ya Ateba.
Simba ambao wamecheza mechi 23 hadi sasa wanaendelea kushika nafasi ya pili wakiwa na pointi 60 na hivyo kuzidiwa pointi 10 na mahasimu wao Yanga wanaoshika usukani wa ligi hiyo wakiwa wamecheza mechi 26.
Kwa upande wa Mashujaa wao wanabaki na pointi zao 30 katika mechi 27 walizocheza hadi sasa huku wakiendelea kushika nafasi yao ya 10.

The post Simba yailaza Mashujaa 2-1 kwa mbinde first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/05/03/simba-yailaza-mashujaa-2-1-kwa-mbinde/feed/ 0
Yanga yaipiga mkono Mashujaa https://www.greensports.co.tz/2025/02/23/yanga-yaipiga-mkono-mashujaa/ https://www.greensports.co.tz/2025/02/23/yanga-yaipiga-mkono-mashujaa/#respond Sun, 23 Feb 2025 18:51:21 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13040 Na mwandishi wetuYanga imeendeleza makali katika Ligi Kuu NBC ikijiimarisha kileleni kwa kuipiga Mashujaa FC mabao 5-0 au mkono, mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, leo Jumapili, Februari 23, 2025.Katika mechi hiyo wenyeji Mashujaa walionesha uhai kuanzia kipindi cha kwanza kwa kuwadhibiti Yanga kabla ya mambo kuwaharibikia dakika ya 33 baada ya Duke Abuya […]

The post Yanga yaipiga mkono Mashujaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga imeendeleza makali katika Ligi Kuu NBC ikijiimarisha kileleni kwa kuipiga Mashujaa FC mabao 5-0 au mkono, mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, leo Jumapili, Februari 23, 2025.
Katika mechi hiyo wenyeji Mashujaa walionesha uhai kuanzia kipindi cha kwanza kwa kuwadhibiti Yanga kabla ya mambo kuwaharibikia dakika ya 33 baada ya Duke Abuya kuifungia Yanga bao la kwanza.
Bao hilo lilidumu kipindi chote cha kwanza kabla ya Yanga kuandika bao la pili dakika tatu baada ya kuanza kipindi cha pili, bao lililofungwa kwa kichwa na Prince Dube akiitumia pasi ya Pacome Zouzoua.
Bao hilo limempaisha Dube na kuungana na wachezaji wengine wawili wenye mabao 10 katika ligi hiyo ambao ni mshambuliaji mwenzake wa Yanga, Clement Mzize na kiungo wa Simba Jean Ahoua.
Yanga waliandika bao la tatu dakika ya 55 lililofungwa na Khalid Aucho ambaye kama ilivyokuwa kwa Dube naye alineemeka na pasi ya Pacome ambaye pia aliibuka mchezaji bora wa mechi hiyo.
Mabao mengine ya Yanga yalifungwa na Clatous Chama aliyeingia uwanjani dakika ya 68 akichukua nafasi ya Stephane Aziz Ki, Chama alifunga mabao hayo dakika za 74 na 83.
Kwa ushindi huo Yanga imefikisha pointi 55 katika michezo 21 ikifuatiwa na mahasimu wao Simba wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 19.

The post Yanga yaipiga mkono Mashujaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/02/23/yanga-yaipiga-mkono-mashujaa/feed/ 0
Dube atupia matatu Yanga ikiwaliza Mashujaa https://www.greensports.co.tz/2024/12/19/dube-atupia-matatu-yanga-ikiwaliza-mashujaa/ https://www.greensports.co.tz/2024/12/19/dube-atupia-matatu-yanga-ikiwaliza-mashujaa/#respond Thu, 19 Dec 2024 17:00:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12448 Na mwandishi wetuHatimaye nyota imeanza kung’aa kwa mshambuliaji wa Yanga, Prince Dube baada ya kufunga mabao matatu wakati timu yake ikiilaza Mashujaa FC mabao 3-2 katika Ligi Kuu NBC.Mabao hayo matatu au hat trick aliyoyafunga kwenye dimba la KMC leo Alhamisi ni ya kwanza kwa Dube katika ligi msimu huu na hivyo anakuwa kama anafungua […]

The post Dube atupia matatu Yanga ikiwaliza Mashujaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Hatimaye nyota imeanza kung’aa kwa mshambuliaji wa Yanga, Prince Dube baada ya kufunga mabao matatu wakati timu yake ikiilaza Mashujaa FC mabao 3-2 katika Ligi Kuu NBC.
Mabao hayo matatu au hat trick aliyoyafunga kwenye dimba la KMC leo Alhamisi ni ya kwanza kwa Dube katika ligi msimu huu na hivyo anakuwa kama anafungua akaunti ya mabao.
Dube amekuwa akiandamwa na ukame wa mabao msimu huu hali ambayo iliibua malalamiko kwa baadhi ya mashabiki hadi kuibuka hoja kwamba Yanga ilikosea kumsajili kutoka Azam FC.
Ushindi huo umeifanya Yanga kufikisha pointi 30 kwenye ligi wakati Dube anakuwa amefunga mabao matatu ya ligi hiyo na kukabidhiwa mpira lakini pia ametajwa kuwa nyota wa mchezo huo.
Dube alianza kuandika bao la kwanza mapema dakika ya saba kwa shuti la chinichini akiunganisha mpira ulioanzia kwa Stephane Aziz Ki aliyempasia Pacome Zouzoua kabla ya mpira kumkuta mfungaji.
Mashujaa hata hivyo walionekana kupambana kutaka kusawazisha bao hilo na katika dakika ya 33 walifanya shambulizi kali ambapo ushirikiano wa Ismail Mgunda na David Uromi nusura uipe timu hiyo bao.
Dube aliwakatisha tamaa Mashujaa dakika ya 21 alipounganisha kwa kichwa krosi iliyoanzia kwa Pacome na mpira kumbabatiza Clement Mzize na beki wa Mashujaa waliokuwa wakipambana kabla ya kumkuta mfungaji.
Juhudi za Mashujaa zilizaa matunda dakika ya 45 baada ya Uromi kuufumania mpira na kufumua shuti la chinichini na mpira kumshinda kipa Aboubakar Khomein ambaye alijichanganya wakati akitaka kuudaka.
Kipindi cha pili timu zote ziliingia kwa kasi lakini walikuwa ni Yanga waliopata bao la tatu dakika ya 52 mfungaji akiwa Dube safari hii akifunga tena kwa kichwa.
Dakika takriban 10 baada ya kuingia kwa bao hilo, Mashujaa walijibu mapigo kwa kuandika bao la pili lililofungwa na Idris Stambuli kwa shuti lililomshinda Khomein.
Mashujaa waliendelea na dhamira yao ya kutaka bao la kusawazisha na kuonesha wakati wote dhamira yao katika jambo hilo licha ya Yanga kufanya mabadiliko kadhaa ikiwamo kumtoa Mzize na kumuingiza Mudathir Yahya na baadaye Duke Abuya na nafasi yake kuingia Salum Aboubakar ‘Sure Boy’.
Kwa upande wa Mashujaa nao waliwatoa Balama na kumuingiza Josephat, baadaye Mginda na kumuingiza Nushi na Uromi ambaye nafasi yake aliingia Mundhir.
Mabadiliko hayo kwa ujumla wake hayakuwayumbisha Mashujaa badala yake waliendelea kuwa wapambanaji kwa muda wote wa mchezo ingawa mwisho wa mchezo matokeo hayakuwa mazuri kwao.

The post Dube atupia matatu Yanga ikiwaliza Mashujaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/12/19/dube-atupia-matatu-yanga-ikiwaliza-mashujaa/feed/ 0
Bao la jioni laiokoa Simba https://www.greensports.co.tz/2024/11/02/bao-la-jioni-laiokoa-simba/ https://www.greensports.co.tz/2024/11/02/bao-la-jioni-laiokoa-simba/#respond Sat, 02 Nov 2024 10:16:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12221 Na mwandishi wetuSimba imenyakua pointi tatu muhimu ikineemeka na bao pekee la jioni dhidi ya Mashujaa katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa leo Ijumaa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.Bao hilo pekee lilipatikana dakika ya sita katika dakika za nyongeza baada ya dakika 90 za kawaida kumalizika mfungaji akiwa Lionel Ateba kwa kichwa kufuatia […]

The post Bao la jioni laiokoa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Simba imenyakua pointi tatu muhimu ikineemeka na bao pekee la jioni dhidi ya Mashujaa katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa leo Ijumaa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
Bao hilo pekee lilipatikana dakika ya sita katika dakika za nyongeza baada ya dakika 90 za kawaida kumalizika mfungaji akiwa Lionel Ateba kwa kichwa kufuatia kona iliyochongwa na Awesu Awesu.
Muda mfupi baada ya kuingia bao hilo mwamuzi alipuliza filimbi ya kumaliza mchezo na hapo hapo akajikuta akizongwa na wachezaji wa Mashujaa waliokuwa wakimlalamikia kwa kuchelewa kumaliza mchezo.
Simba sasa imechupa hadi nafasi ya pili ikiwa imefikisha jumla ya pointi 22 ikiwa imefungana pointi na Singida BS lakini zikidiana wastani wa mabao wakati Yanga wakiwa kileleni na pointi zao 24.
Katika mechi yao ya leo, Simba ndio waliokuwa wa kwanza kulisakama lango la Mashujaa katika dakika ya kwanza tu ya mchezo huo baada ya Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ kupanda na mpira mbele.
Zimbwe Jr mara baada ya kupanda mpira huo alimuunganishia Lionel Ateba ambaye hata hivyo shuti lake lilipaa juu ya lango.
Dakika ya 41 Simba walifanya shambulizi jingine safari hii Ateba alimuunganishia pasi Kibu Denis ambaye akiwa katika eneo zuri aliumiki mpira vibaya na kuwahiwa na kipa wa Mashujaa, Eric Johola.
Mashujaa nao mara kadhaa walionekana kulisakama lango la Simba hususan mshambuliaji wake Ismail Mgunda akishirikiana na Seif Abdallah Karie ambao juhudi zao zilikwamishwa na ukuta wa Simba ukiongozwa na kipa Musa Camara.
Ligi hiyo itaendelea Jumamosi kwa mechi kati ya Yanga na Azam kwenye Uwanja wa Azam Complex wakati Singida BS itaumana na Coastal Union kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.

The post Bao la jioni laiokoa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/11/02/bao-la-jioni-laiokoa-simba/feed/ 0
Yanga yawapiga Mashujaa 1-0 https://www.greensports.co.tz/2024/05/06/yanga-yawapiga-mashujaa-1-0/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/06/yanga-yawapiga-mashujaa-1-0/#respond Mon, 06 May 2024 06:14:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10853 Na mwandishi wetuYanga imeendelea kuimarisha mbio zake za kulitetea taji la Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Mashujaa FC bao 1-0 katika mechi ya ligi hiyo iliyopigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi 65 na hivyo kuiacha Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi […]

The post Yanga yawapiga Mashujaa 1-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga imeendelea kuimarisha mbio zake za kulitetea taji la Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Mashujaa FC bao 1-0 katika mechi ya ligi hiyo iliyopigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi 65 na hivyo kuiacha Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi 11 na mahasimu wao Simba walio nafasi ya tatu kwa tofauti ya pointi 15.
Bao pekee lililoitoa kimasomaso Yanga lilipatikana dakika nne kabla ya mapumziko mfungaji akiwa ni Joseph Guede aliyeitumia vizuri pasi ya Mudathir Yahya kuifungia timu yake bao hilo.
Guede mshambuliaji mpya wa Yanga aliyejiunga na timu hiyo katikati ya msimu huu, katika mechi za hivi karibuni ameanza kuonesha ubora wa kuzifumania nyavu akiwa hadi sasa amefikisha mabao matano.
Yanga sasa inahitaji pointi nane ili iweze kufikisha pointi 73 ambazo kimsingi haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwenye ligi hiyo inayoshirikisha timu 16 na ambayo inaelekea ukingoni kila timu ikiwa imebakiza wastani wa mechi kati ya tano hadi sita.
Kwa upande wa Mashujaa, matokeo hayo yanawafanya wabaki na pointi zao 23 katika mechi 25 wakiwa nafasi ya 14 na kama wakishindwa kuzitumia vizuri mechi tano zilizobaki wanaweza kushuka daraja na kucheza Ligi ya Championship msimu ujao.

The post Yanga yawapiga Mashujaa 1-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/06/yanga-yawapiga-mashujaa-1-0/feed/ 0
Baresi aahidi ushindi, soka safi dhidi ya Yanga https://www.greensports.co.tz/2024/05/04/baresi-aahidi-ushindi-soka-safi-dhidi-ya-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/04/baresi-aahidi-ushindi-soka-safi-dhidi-ya-yanga/#respond Sat, 04 May 2024 18:47:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10835 Na mwandishi wetuKocha mkuu wa Mashujaa FC, Mohamed Abdallah ‘Baresi’ amesema timu yake imepania kuonesha soka safi la kuwaburudisha wananchi wa Kigoma na kuwapa matokeo ya ushindi kesho Jumapili katika mechi ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Yanga.Baresi ameeleza hayo leo Jumamosi alipokuwa akihojiwa na GreenSports kuelekea mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, […]

The post Baresi aahidi ushindi, soka safi dhidi ya Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Mashujaa FC, Mohamed Abdallah ‘Baresi’ amesema timu yake imepania kuonesha soka safi la kuwaburudisha wananchi wa Kigoma na kuwapa matokeo ya ushindi kesho Jumapili katika mechi ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Yanga.
Baresi ameeleza hayo leo Jumamosi alipokuwa akihojiwa na GreenSports kuelekea mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma nyumbani kwa Mashujaa kuanzia saa 10 jioni.
Akifafanua kuhusu maandalizi yao alisema pamoja na kujiandaa vyema lakini pia wamewaeleza wachezaji wao nini cha kufanya kutokana na wachezaji wanaokutana nao.
Alisema kwamba wengi wao ni wajanja wa kuhukumu yanapopatikana makosa hivyo wamewaeleza wachezaji nini cha kufanya kuepuka hayo na hatimaye kuvuna pointi tatu.
“Tunatambua wana mchezaji mmoja mmoja ambao muda mwingi unapofanya makosa wanaweza kukuhukumu na kuamua matokeo, kwa hiyo katika hilo wachezaji wetu tushawafundisha na tumewahimiza sana tuwe na hali ya tahadhari ya kucheza na wachezaji wa namna hiyo.
“Kwa hiyo kwa kifupi niseme wazi kwamba litakuwa pambano la kuheshimisha mkoa wa Kigoma na wananchi wake ambao wanahitaji kuona timu yao inabaki ligi kuu haishuki, sasa inabaki kwa staili gani?

“Ni kupata pointi tatu kwenye kila mchezo tunaocheza na sio Yanga tu, kila mchezo utakaofuata na kesho tunataka alama tatu kuhakikisha tunakaa vizuri, ikishindkana hivyo basi tusipoteze huu mchezo,” alisema Baresi.

The post Baresi aahidi ushindi, soka safi dhidi ya Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/04/baresi-aahidi-ushindi-soka-safi-dhidi-ya-yanga/feed/ 0
Mashujaa: Hatushuki daraja https://www.greensports.co.tz/2024/04/23/mashujaa-hatushuki-daraja/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/23/mashujaa-hatushuki-daraja/#respond Tue, 23 Apr 2024 07:18:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10707 Na mwandishi wetuLicha ya Mashujaa FC kuwa na hali mbaya kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC, lakini wamewaahidi mashabiki wao kuwa hawatashuka daraja na katika kudhihirisha hilo wataanza na ushindi kwenye mechi yao ijayo dhidi ya Yanga SC.Hayo yameelezwa Jumatatu hii na kocha msaidizi wa Mashujaa, Makata Maulidi baada ya matokeo ya suluhu dhidi ya […]

The post Mashujaa: Hatushuki daraja first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Licha ya Mashujaa FC kuwa na hali mbaya kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC, lakini wamewaahidi mashabiki wao kuwa hawatashuka daraja na katika kudhihirisha hilo wataanza na ushindi kwenye mechi yao ijayo dhidi ya Yanga SC.
Hayo yameelezwa Jumatatu hii na kocha msaidizi wa Mashujaa, Makata Maulidi baada ya matokeo ya suluhu dhidi ya Singida FG kwenye mchezo uliopigwa jana Jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na kufanya wasogee mpaka nafasi ya 13 kwa pointi 23 baada ya mechi 24.
“Mechi ilikuwa ngumu sababu mechi yoyote ya ugenini, mwenyeji anaamini atapata pointi tatu lakini Singida walitufunga mchezo wa kwanza (3-1) kwa hiyo tukaweka mpango wa namna ya kucheza nao na kujaribu kupambana lakini haikuwa riziki yetu, tumepata sare.
“Lakini hayo yamepita na sasa tunatazamia zaidi mechi ya Yanga inayofuata kule Kigoma, tunajua hatupo katika nafasi nzuri, tunataka kuona namna ya kutoka tulipo kwa hiyo yeyote ambaye yupo mbele yetu, tukicheza naye lazima tupate matokeo kwake.

“Tuwaambie na kuwahamasisha mashabiki wasikate tamaa, timu yetu haiwezi kushuka daraja, tutapambana kubaki ligi kuu kuhakikisha tunawapa burudani zaidi msimu ujao,” alisema Maulid.


Mashujaa iliyopanda kushiriki Ligi Kuu NBC msimu huu, imebakiza mechi sita kufunga pazia la ligi ambapo ikishaumana na Yanga Mei 8, itavaana na KMC, Tabora United, Tanzania Prisons, Mtibwa Sugar kisha itamalizana na Dodoma Jiji.

The post Mashujaa: Hatushuki daraja first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/23/mashujaa-hatushuki-daraja/feed/ 0
Baresi aiwaza tano bora ligi kuu https://www.greensports.co.tz/2024/03/19/baresi-aiwaza-tano-bora-ligi-kuu/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/19/baresi-aiwaza-tano-bora-ligi-kuu/#respond Tue, 19 Mar 2024 05:41:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10245 Na mwandishi wetuKocha mkuu wa Mashujaa FC, Mohamed Abdallah ‘Baresi’ amesema baada ya kutoka nafasi za chini kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC malengo yao kwa sasa ni kumaliza katika nafasi tano za juu.Akizungumza na GreenSports, Baresi alisema uwezo wa kufikia hivyo wanao na hiyo ni kutokana na maboresho waliyofanya kwenye dirisha dogo la usajili.“Ukweli […]

The post Baresi aiwaza tano bora ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Mashujaa FC, Mohamed Abdallah ‘Baresi’ amesema baada ya kutoka nafasi za chini kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC malengo yao kwa sasa ni kumaliza katika nafasi tano za juu.
Akizungumza na GreenSports, Baresi alisema uwezo wa kufikia hivyo wanao na hiyo ni kutokana na maboresho waliyofanya kwenye dirisha dogo la usajili.
“Ukweli naridhika na kiwango cha timu yangu hasa kwenye mzunguko huu wa pili, tumekuwa bora sana ndio maana tumeondoka nafasi za chini na sasa tupo sehemu salama.

“Lakini kama kocha na kwa ubora wa timu yangu nitafurahi kama tutamaliza msimu ndani ya tano bora,” alisema Baresi’.


Kocha huyo alisema wamekuwa wakiimarika siku baada ya siku na anachojivunia ni wachezaji wageni kuzoeana mapema na wale waliokuwepo tangu mzunguko wa kwanza msimu huu.
Mashujaa yenye maskani yake Kigoma iliyopanda kushiriki Ligi Kuu NBC msimu huu, kwa sasa ipo nafasi ya 12 kwenye msimamo ikikusanya pointi 21 katika michezo 21 iliyocheza hadi sasa.

The post Baresi aiwaza tano bora ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/19/baresi-aiwaza-tano-bora-ligi-kuu/feed/ 0
Simba yaipiga Mashujaa 2-0 https://www.greensports.co.tz/2024/03/16/simba-yaipiga-mashujaa-2-0/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/16/simba-yaipiga-mashujaa-2-0/#respond Sat, 16 Mar 2024 08:56:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10218 Na mwandishi wetuSimba imefanikiwa kuiengua Azam FC katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Mashujaa FC mabao 2-0 katika mechi iliyopigwa Ijumaa hii kwenye dimba la Azam Complex, Dar es Salaam.Ikionekana imetimia, Simba ilipata tabu kuipenya safu ya ulinzi ya Mashujaa na hadi dakika 45 zinakamilika timu hizo zilikwenda […]

The post Simba yaipiga Mashujaa 2-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba imefanikiwa kuiengua Azam FC katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Mashujaa FC mabao 2-0 katika mechi iliyopigwa Ijumaa hii kwenye dimba la Azam Complex, Dar es Salaam.
Ikionekana imetimia, Simba ilipata tabu kuipenya safu ya ulinzi ya Mashujaa na hadi dakika 45 zinakamilika timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa hazijafungana bao hata moja licha ya kushambuliana mara kadhaa.
Kipindi cha pili, Mashujaa waliendelea kukomaa na kuibua hali ya wasiwasi kwamba huenda wangeifanyia Simba kile walichoifanyia mwaka 2021 kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho Azam (FA) walipoichapa mabao 3-1 na kuitoa katika mashindano hayo.
Matarajio hayo hata hivyo yalianza kufutika katika dakika ya 57 baada ya Clatous Chota Chama kwa mara nyingine kudhihirisha ubora wake kwa kuifungia Simba bao la kwanza na kumalizia la pili dakika ya 73.
Ushindi huo umeifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 45 katika mechi 19 na kuishusha Azam hadi nafasi ya tatu ikiwa na ponti 44 katika mechi 20.
Azam hata hivyo inaweza kurudi katika nafasi ya pili kama itaweza kutoka na ushindi katika mechi yao ngumu ya Jumapili dhidi ya Yanga itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

The post Simba yaipiga Mashujaa 2-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/16/simba-yaipiga-mashujaa-2-0/feed/ 0