Marumo - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 17 May 2023 18:44:40 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Marumo - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Yanga hiyooo, fainali Shirikisho https://www.greensports.co.tz/2023/05/17/yanga-hiyooo-fainali-shirikisho/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/17/yanga-hiyooo-fainali-shirikisho/#respond Wed, 17 May 2023 18:44:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6192 Na mwandishi wetuHatimaye Yanga imefuzu hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza baada ya kuilaza Marumo Gallant ya Afrika Kusini mabao 2-1 katika mechi iliyopigwa leo Jumatano kwenye Uwanja wa Royal Bafokeng, Afrika Kusini.Yanga inakuwa imefuzu hatua hiyo kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-1 baada ya ushindi wa mabao […]

The post Yanga hiyooo, fainali Shirikisho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Hatimaye Yanga imefuzu hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza baada ya kuilaza Marumo Gallant ya Afrika Kusini mabao 2-1 katika mechi iliyopigwa leo Jumatano kwenye Uwanja wa Royal Bafokeng, Afrika Kusini.
Yanga inakuwa imefuzu hatua hiyo kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-1 baada ya ushindi wa mabao 2-0 iliyoupata katika mechi ya nusu fainali ya kwanza iliyopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.
Timu hiyo sasa inasubiri kuumana na mshindi wa mechi nyingine ya nusu fainali iliyozikutanisha Asec Mimosa na USM Alger ambazo katika nusu fainali ya kwanza iliyopigwa mjini Abidjan timu hizo zilitoka sare.
Yanga iliandika bao la kwanza dakika moja kabla ya mapumziko mfungaji akiwa Fiston Mayele ambaye anakuwa amefikisha mabao sita katika michuano hiyo na kujiweka pazuri katika kuwania tuzo ya mfungaji bora.
Mayele ambaye baadaye alitolewa na kuingia Farid Mussa, alifunga bao hilo kwa pasi ya Musonda, kwanza alifumua shuti ambalo liliokolewa na kipa Washington Arubi wa Marumo kabla ya kumkuta mfungaji aliyemalizia kwa kuujaza wavuni.
Marumo ambao waliutawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa, walijikuta wakifungwa bao la pili katika dakika ya 68 lililofungwa na Kennedy Musonda ambaye aliitumia vizuri pasi ya Mayele.
Mayele kabla ya kutoa pasi iliyozaa bao aliambaa na mpira na kumzidi mbio beki wa Marumo kabla ya kumuunganishia Musonda aliyeujaza wavuni akifumua shuti karibu na eneo la 18.
Marumo ambao kwa muda wote huo walikuwa wakimiliki vyema mipira na kufika mara kwa mara langoni mwa Yanga walichanganywa na bao hilo kwani lilikuja wakati wameonyesha uhai katika kutafuta bao la kusawazisha.
Bao pekee la Marumo lilipatikana katika dakika nne za nyongeza mfungaji akiwa ni Ranga Chivaviro ambaye sasa anakuwa amefungana na Mayele kwa idadi ya mabao kila mmoja akiwa n mabao sita.

The post Yanga hiyooo, fainali Shirikisho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/17/yanga-hiyooo-fainali-shirikisho/feed/ 0
Kiwango Yanga hakijamridhisha Nabi https://www.greensports.co.tz/2023/05/11/kiwango-yanga-hakijamridhisha-nabi/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/11/kiwango-yanga-hakijamridhisha-nabi/#respond Thu, 11 May 2023 13:09:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6117 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema licha ya timu yake kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini, hajaridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake katika mchezo huo.Mchezo huo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ulichezwa jana Jumatano jioni kwenye […]

The post Kiwango Yanga hakijamridhisha Nabi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema licha ya timu yake kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini, hajaridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake katika mchezo huo.
Mchezo huo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ulichezwa jana Jumatano jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Nabi alisema anasikitika kwa kuwa walitengeneza nafasi nyingi kipindi cha kwanza cha mchezo huo lakini walishindwa kuzitumia ipasavyo tofauti na alivyotarajia.

“Mechi ilikuwa ngumu, kipindi cha kwanza tulitengeneza nafasi nyingi hatukupata magoli. Ninachosikitika hatukutumia nafasi kama nilivyowafundisha wachezaji wangu kwenye mazoezi, walicheza tofauti kabisa,”alisema Nabi.


Kuhusu Marumo, Nabi alisema: “Siwezi kusema ni timu dhaifu, tofauti kidogo ipo kwenye safu yao ya ulinzi ila ni wazuri wana timu nzuri, timu yangu ndio iliyokuwa na matatizo kwa sababu wachezaji wangu hawakucheza vizuri.”
Alisema katika mchezo wa marudiano utakaopigwa Mei 17, mwaka huu Afrika Kusini kila mchezaji anatakiwa kufahamu wajibu wake kwa kufanya kazi kama alivyoelekezwa kwani kazi bado haijaisha.
Kwa upande wa Kocha wa Marumo, Dylan Kerr alisema anasikitika kwa timu yake kushindwa kuzitumia nafasi nne walizotengeneza kipindi cha kwanza licha ya kumiliki mpira.
“Tulipata nafasi nne za kufunga, tulimiliki mpira lakini umaliziaji wetu haukuwa bora, tunapaswa kwenda kurekebisha makosa yetu na kujipanga kwa mchezo wa pili,” alisema.

The post Kiwango Yanga hakijamridhisha Nabi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/11/kiwango-yanga-hakijamridhisha-nabi/feed/ 0
Nabi: Tutaikabili Marumo kwa tahadhari https://www.greensports.co.tz/2023/05/09/nabi-tutaikabili-marumo-kwa-tahadhari/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/09/nabi-tutaikabili-marumo-kwa-tahadhari/#respond Tue, 09 May 2023 17:15:04 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6070 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kipo kamili, kina ari na watacheza kwa tahadhari mechi ya kesho Jumatano ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini.Nabi amezungumza hayo leo Jumanne jijini Dar es Salaam akisema pia wanaingia kwenye mechi hiyo wakifahamu ubora wa […]

The post Nabi: Tutaikabili Marumo kwa tahadhari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kipo kamili, kina ari na watacheza kwa tahadhari mechi ya kesho Jumatano ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini.
Nabi amezungumza hayo leo Jumanne jijini Dar es Salaam akisema pia wanaingia kwenye mechi hiyo wakifahamu ubora wa Marumo mpaka wanafika nusu fainali bila ya kutazama hali mbaya waliyonayo kwenye Ligi ya Afrika Kusini.
Alisema kuelekea mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.00 jioni, amewasoma wapinzani wao hivyo wanaingia na tahadhari zote katika mtanange huo.
“Wachezaji wote wana utimamu wa mechi ya kesho, maandalizi yamekwenda kama tulivyopanga, wachezaji wamejiandaa kikamilifu, tumeisoma timu pinzani, wachezaji wako tayari kupambana na wana ari ya kucheza na Marumo.

“Niwapongeze Marumo ni timu nzuri japo kwenye ligi yao hawafanyi vizuri lakini kwenye michuano hii wanafanya vizuri, kila mechi wamepata bao na wameitoa Pyramids, hivyo hiyo si timu ya kubeza, tutacheza kwa umakini mkubwa kulingana na wapinzani tunaokutana nao ukizingatia ni mechi za mikondo miwili, nyumbani na ugenini,” alisema Nabi.


Nabi raia wa Tunisia pia aliwashukuru mashabiki wa Yanga kwa ushirikiano waliowapa mpaka sasa, akiwataka kuongeza nguvu hiyo kesho kwa kushangilia na kuwapa nguvu wachezaji hata inapotokea Yanga haina mpira kwa wakati huo.
Naye Raymond Mdaka, kocha msadizi wa Marumo alisema hawawezi kuzungumzia maandalizi yao kwa undani kwa sababu ni sehemu yao ya kazi ya kila siku kutokana na mechi za michuano hiyo na za ligi walizonazo kila wakati ingawa wamewasoma Yanga kuelekea mechi hiyo.
“Tumekuwa tukifanya maandalizi kila baada ya mechi moja kuelekea nyingine, tunachojua timu zina utofauti na huwezi kubadili kucheza kila mechi iliyo mbele lakini kuna vitu tumeangalia kama ugumu wao, namna wanavyocheza hivyo hakukuwa na maandalizi makubwa japo tupo tayari kwa kila mchezo ulio mbele yetu,” alisema Mdaka.
Timu hizo zinashuka dimbani zikiwa na uwiano tofauti kwenye ligi zao ambapo Yanga ni kinara wa Ligi Kuu NBC kwa pointi 71 wakati Marumo ipo nafasi ya 14 kwa pointi 29.
Marumo ambayo imeifunga Pyramids ya Misri jumla ya mabao 2-1 kwenye robo fainali ya Kombe la Shirikisho, kwenye michezo yao mitano ya mwisho ya ligi wameshinda mmoja, wakidroo mitatu na kufungwa mmoja.
Yanga wao ambao wamefungwa mechi moja kwenye mechi tano za ligi zilizopita na kushinda nne, iliiondosha Rivers United ya Nigeria kwa jumla ya mabao 2-0 na kutinga nusu fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza kama ilivyo Marumo.

The post Nabi: Tutaikabili Marumo kwa tahadhari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/09/nabi-tutaikabili-marumo-kwa-tahadhari/feed/ 0