Manunited - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 09 May 2022 08:02:21 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Manunited - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Beckham ambakisha Ronaldo Man United https://www.greensports.co.tz/2022/05/09/beckham-ambakisha-ronaldo-man-united/ https://www.greensports.co.tz/2022/05/09/beckham-ambakisha-ronaldo-man-united/#respond Mon, 09 May 2022 08:01:04 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=677 London, EnglandKiungo na nahodha wa zamani wa England, David Beckham ameshauri staawa Man United, Cristiano Ronaldo aendelee kuichezea timu hiyo.Beckham ambaye pia amewahi kuichezea Man United pamoja na Real Madridya Hispania kama ilivyo kwa Ronaldo, ametoa kauli hiyo wakati huukukiwa na mjadala kuhusu majaliwa ya mchezaji huyo kama aendelee kuwahapo au aondoke.Akitetea Ronaldo kuendelea kubaki […]

The post Beckham ambakisha Ronaldo Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kiungo na nahodha wa zamani wa England, David Beckham ameshauri staa
wa Man United, Cristiano Ronaldo aendelee kuichezea timu hiyo.
Beckham ambaye pia amewahi kuichezea Man United pamoja na Real Madrid
ya Hispania kama ilivyo kwa Ronaldo, ametoa kauli hiyo wakati huu
kukiwa na mjadala kuhusu majaliwa ya mchezaji huyo kama aendelee kuwa
hapo au aondoke.
Akitetea Ronaldo kuendelea kubaki hapo, Beckham kupitia akaunti yake
ya Twitter alisema, “Bado anafanya yale anayofanya kwa ubora, anafunga
mabao na kutengeneza mabao, hicho ndicho anachokifanya Cristiano.
Beckham aliongeza kuwa, “kwa umri wake kitu anachokifanya ni cha
kipekee, natumaini ataendelea kukifanya na natumaini atabaki kwa mwaka
mwingine mmoja au miwili.


Pamoja na sifa anazopewa Ronaldo, Man United ina wakati mgumu kwenye
Ligi Kuu England ikiwa nafasi ya sita na pointi 58 na hivyo upo
uwezekano mkubwa wa kukosa nafasi katika michuano ya Ulaya msimu ujao.
Na ingawa kwa Man United hali si nzuri lakini Ronaldo mwenye umri wa
miaka 37 amekuwa akifanya juhudi kubwa na hadi sasa ameifungia timu
hiyo mabao 24, rekodi ambayo kwa hali ya kawaida si mbaya kwa mchezaji
mwenye umri huo..
Ronaldo alitua, United mwaka jana akitokea Juventus ya Italia ikiwa ni
takriban miaka 12 tangu aondoke katika klabu hiyo na kutua Real
Madrid.

The post Beckham ambakisha Ronaldo Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/05/09/beckham-ambakisha-ronaldo-man-united/feed/ 0
Rangnick: Pogba akitaka aondoke https://www.greensports.co.tz/2021/12/11/rangnick-pogba-akitaka-aondoke/ https://www.greensports.co.tz/2021/12/11/rangnick-pogba-akitaka-aondoke/#respond Sat, 11 Dec 2021 13:21:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=551 London, EnglandPamoja na ubora wa kiungo wa Man United, Paul Pogba, kocha wa muda wa timu hiyo, Ralf Rangnick amesema hatomshawishi mchezaji huyo abaki katika klabu hiyo kama ana mawazo ya kuondoka.Mkataba wa sasa wa Pogba na Man United unafikia ukomo mwakani majira ya kiangazi na hadi Januari mwakani atakuwa huru kuanza mazungumzo na klabu […]

The post Rangnick: Pogba akitaka aondoke first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Pamoja na ubora wa kiungo wa Man United, Paul Pogba, kocha wa muda wa timu hiyo, Ralf Rangnick amesema hatomshawishi mchezaji huyo abaki katika klabu hiyo kama ana mawazo ya kuondoka.
Mkataba wa sasa wa Pogba na Man United unafikia ukomo mwakani majira ya kiangazi na hadi Januari mwakani atakuwa huru kuanza mazungumzo na klabu nyingine kama ataona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.
Akifafanua kuhusu uamuzi wake kwa mchezaji huyo Rangnick alisema, “Siwezi kusema hana sifa za kuendelea kubaki hapa lakini wachezaji wanatakiwa wawe wanataka kubaki na kuichezea klabu.”
Rangnick alisema kama mchezaji hataki kuichezea klabu kubwa yenye mashabiki wengi ya Man United hata kwa mkataba mrefu hadhani kama kuna maana kumshawishi ili abadili mawazo yake.
Pogba ambaye mwaka 2018 alikuwamo katika kikosi cha Ufaransa kilichotwaa taji la dunia inadaiwa kuwa huduma yake inahitajika katika klabu kadhaa kubwa barani Ulaya.

The post Rangnick: Pogba akitaka aondoke first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2021/12/11/rangnick-pogba-akitaka-aondoke/feed/ 0