Manula - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 15 Feb 2024 05:28:25 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Manula - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Manula: Niko fiti kuipigania Simba https://www.greensports.co.tz/2024/02/15/manula-niko-fiti-kuipigania-simba/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/15/manula-niko-fiti-kuipigania-simba/#respond Thu, 15 Feb 2024 05:28:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9735 Na mwandishi wetuKipa namba moja wa Simba, Aishi Manula amesema kwa sasa amepona kabisa maumivu ya goti na yupo tayari kuipigania timu yake katika michuano yote inayoshiriki.Kipa huyo alisema Jumatano hii kuwa kwa sasa anafanya mazoezi mara mbili kwa siku kwa lengo la kurejea kwenye kiwango chake ili kuipigania timu yake.“Kwa sasa nimepona, sihisi tena […]

The post Manula: Niko fiti kuipigania Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula amesema kwa sasa amepona kabisa maumivu ya goti na yupo tayari kuipigania timu yake katika michuano yote inayoshiriki.
Kipa huyo alisema Jumatano hii kuwa kwa sasa anafanya mazoezi mara mbili kwa siku kwa lengo la kurejea kwenye kiwango chake ili kuipigania timu yake.
“Kwa sasa nimepona, sihisi tena yale maumivu ambayo nilikuwa nikihisi wakati naanza mazoezi mepesi lakini hata madaktari wamenipa ruhusa, kitu cha msingi kwa sasa ni kupigania nafasi yangu kufikia malengo tuliyokusudia kuyafikia msimu huu,” alisema Manula.
Alisema pamoja na kukaa nje muda mrefu bila kucheza lakini anajivunia uzoefu alionao, kitu ambacho kilimsaidia kucheza mechi zote tatu akiwa na timu ya taifa, Taifa Stars kwenye michuano ya Afcon iliyomalizika majuzi nchini Ivory Coast.
Manula alikaa nje kwa kipindi cha miezi sita akiuguza goti alilofanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini baada ya kuumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu NBC msimu uliopita dhidi ya Ihefu.
Kipa huyo alirejea uwanjani Novemba 5, mwaka jana na kukumbana na kipigo cha mabao 5-1 kutoka kwa watani zao wa jadi, Yanga katika mechi ya Ligi Kuu NBC.

The post Manula: Niko fiti kuipigania Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/15/manula-niko-fiti-kuipigania-simba/feed/ 0
Manula apiga hatua muhimu https://www.greensports.co.tz/2023/09/02/manula-apiga-hatua-muhimu/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/02/manula-apiga-hatua-muhimu/#respond Sat, 02 Sep 2023 20:20:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7655 Na mwandishi wetuHatimaye kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula amepiga hatua muhimu kwa kuanza rasmi mazoezi ya uwanjani baada ya kuuguza jeraha la nyama za paja alilofanyiwa upasuaji takriban miezi mitatu iliyopita.Manula ameanza mazoezi hayo kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena, Dar es Salaam chini ya usimamizi wa timu ya wataalamu wa viungo na […]

The post Manula apiga hatua muhimu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Hatimaye kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula amepiga hatua muhimu kwa kuanza rasmi mazoezi ya uwanjani baada ya kuuguza jeraha la nyama za paja alilofanyiwa upasuaji takriban miezi mitatu iliyopita.
Manula ameanza mazoezi hayo kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena, Dar es Salaam chini ya usimamizi wa timu ya wataalamu wa viungo na tiba ya timu hiyo, ikielezwa kuwa kipa huyo amefikisha zaidi ya asilimia 80 ya kuwa fiti kama awali.
Daktari wa Simba, Edwin Kagabo alitoa ufafanuzi kuwa baada ya Manula kumaliza awamu ya kwanza ya upasuaji, ya pili ya mazoezi tiba, sasa wako hatua ya tatu ya kumpa mazoezi ya sehemu ya nyama aliyoumia ili akae sawa kabisa na maendeleo yamekuwa mazuri.

“Maendeleo ni mazuri na yanaridhisha kwa kiwango kikubwa, anaridhisha sasa kurudi uwanjani, lengo kubwa la awamu ya tatu ni kufanya mazoezi katika ile nyama iliyopata jeraha na kwa maendeleo tuko asilimia 80 kuelekea 90 ya kupona kabisa,” alisema Kagabo.


Manula alipata majeraha hayo Aprili 7 kwenye mechi ya robo fainali ya Kombe la FA (ASFC) dhidi ya Ihefu na kufanyiwa upasuaji Juni 2, mwaka huu.
Kurejea kwa Manula kutaifanya Simba iwe na makipa watano baada ya Ally Salim, Ayoub Lakred aliyesajiliwa kutoka FAR Rabat ya Morocco, Ahmed Feruz aliyepandishwa kutoka kikosi cha vijana na Hussein Abel aliyetua kutoka KMC.

The post Manula apiga hatua muhimu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/02/manula-apiga-hatua-muhimu/feed/ 0
Manula amfurahia kipa mpya Simba https://www.greensports.co.tz/2023/08/15/manula-amfurahia-kipa-mpya-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/15/manula-amfurahia-kipa-mpya-simba/#respond Tue, 15 Aug 2023 19:47:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7399 Na mwandishi wetuKipa wa Simba, Aishi Manula ameeleza kufurahishwa na uongozi wa timu hiyo kwa kusajili kipa mpya kutoka nje ya Tanzania akisema hiyo itamuongezea ushindani maradufu wa kuwania namba.Uongozi wa Simba wiki iliyopita ulimtambulisha Ayoub Lakred kuwa kipa mpya wa timu hiyo akitokea FAR Rabat ya Morocco ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia […]

The post Manula amfurahia kipa mpya Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kipa wa Simba, Aishi Manula ameeleza kufurahishwa na uongozi wa timu hiyo kwa kusajili kipa mpya kutoka nje ya Tanzania akisema hiyo itamuongezea ushindani maradufu wa kuwania namba.
Uongozi wa Simba wiki iliyopita ulimtambulisha Ayoub Lakred kuwa kipa mpya wa timu hiyo akitokea FAR Rabat ya Morocco ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo.
Kipa huyo ambaye ndiye kipa tegemezi wa Simba, alisema ujio wa kipa huyo utamuongezea ari ya kupambana ili kudumu kwenye nafasi yake pindi atakaporudi uwanjani baada ya kupona majeraha ya goti.

“Sijamfuatilia sana lakini naamini ni kipa mzuri ambaye atatupa ushindani mimi na wenzangu, Ally Salim na Hussein Abel sababu tunaamini ana uzoefu mkubwa kutokana na klabu aliyotoka lakini yeye ni kipa wa kigeni lazima atakuwa na kitu cha ziada ili kucheza kikosi cha kwanza,” alisema Manula.


Manula pia alisema uzoefu alionao kipa huyo anaamini atawasaidia katika michuano ya kimataifa pia wanayotarajia kushiriki hivi karibuni na hiyo ni kutokana na uzoefu aliokuwa nao kwenye michuano hiyo ambayo inatarajiwa kuanza mwezi ujao.
Alisema kwa upande wake tayari ameanza mazoezi mapesi huku akifuata maelekezo ya madaktari wa timu na atafanya hivyo kwa kipindi cha miezi miwili kabla ya kurudi uwanjani.
Kwa mujibu wa ripoti ya madaktari wa Simba, Manula anatarajiwa kurudi uwanjani mwishoni mwa Oktoba, mwaka huu kwa ajili ya kuendelea na majukumu ya kuipigania timu yake katika mashindano ya ndani na Ligi ya Mabingwa Afrika.

The post Manula amfurahia kipa mpya Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/15/manula-amfurahia-kipa-mpya-simba/feed/ 0
Manula aanza mazoezi mepesi https://www.greensports.co.tz/2023/07/22/manula-aanza-mazoezi-mepesi/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/22/manula-aanza-mazoezi-mepesi/#respond Sat, 22 Jul 2023 14:09:19 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7076 Na mwandishi wetuKipa namba moja wa Simba, Aishi Manula ambaye atakuwa nje ya uwanja kwa miezi minne ameanza kujifua kwa mazoezi mepesi akiwa gym.Manula ambaye amefanyiwa upasuaji wa nyama za paja, ameanza mazoezi hayo juzi akionekana kuchechemea kwa kujivuta akitumia mpira maalum wa kujifunga miguuni na kujaribu kupiga nao hatua.Kipa huyo ambaye pia anaichezea timu […]

The post Manula aanza mazoezi mepesi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula ambaye atakuwa nje ya uwanja kwa miezi minne ameanza kujifua kwa mazoezi mepesi akiwa gym.
Manula ambaye amefanyiwa upasuaji wa nyama za paja, ameanza mazoezi hayo juzi akionekana kuchechemea kwa kujivuta akitumia mpira maalum wa kujifunga miguuni na kujaribu kupiga nao hatua.
Kipa huyo ambaye pia anaichezea timu ya taifa, Taifa Stars, pia akiwa mazoezini hapo alisema kwa kifupi tayari ameanza kupiga hatua kurejea kazini akimaanisha kurejea kuitumikia Simba.
Manula alipata majeraha hayo Aprili 7 katika mechi ya robo fainali ya Kombe la FA (ASFC) dhidi ya Ihefu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam na kisha kufanyiwa upasuaji Mei 30, mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Kuelekea msimu ujao, Simba ambayo pia imeondokewa na kipa wake namba mbili, Beno Kakolanya, inaendelea na mipango ya kumnasa kipa Mcameroon, Medjo Omossola kutoka Saint-Eloi Lupopo ya DR Congo.

The post Manula aanza mazoezi mepesi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/22/manula-aanza-mazoezi-mepesi/feed/ 0
Kipa wa Lupopo kufunga usajili Simba https://www.greensports.co.tz/2023/07/18/kipa-wa-lupopo-kufunga-usajili-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/18/kipa-wa-lupopo-kufunga-usajili-simba/#respond Tue, 18 Jul 2023 19:02:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7000 Na mwandishi wetuKlabu ya Simba inatarajia kufunga zoezi la usajili kwa kumsajili kipa, Medjo Simon Loti Omossola (pichani) kutoka timu ya Saint-Eloi Lupopo ya DR Congo.Simba inasaka kipa atakayeziba pengo la Aishi Manula ambaye kwa sasa anauguza majeraha ya goti baada ya kufanyiwa upasuaji wiki nne zilizopita na atakuwa nje hadi mwishoni mwa Oktoba, mwaka […]

The post Kipa wa Lupopo kufunga usajili Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya Simba inatarajia kufunga zoezi la usajili kwa kumsajili kipa, Medjo Simon Loti Omossola (pichani) kutoka timu ya Saint-Eloi Lupopo ya DR Congo.
Simba inasaka kipa atakayeziba pengo la Aishi Manula ambaye kwa sasa anauguza majeraha ya goti baada ya kufanyiwa upasuaji wiki nne zilizopita na atakuwa nje hadi mwishoni mwa Oktoba, mwaka huu.
Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema wapo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa kipa huyo ambaye wanaamini atakuwa mbadala sahihi wa Manula hasa kutokana na uzoefu wake kwenye mashindano ya kimataifa.
“Simon ni nyanda wa viwango kwelikweli na hiyo ni kutokana na uzoefu aliokuwa nao baada ya kupita klabu mbalimbali ambazo ni kubwa na zimekuwa na desturi ya kushiriki michuano ya kimataifa mara kwa mara, huyu ndio tutafunga naye usajili wetu katika dirisha hili kubwa,” alisema Ally.
Ally alisema usajili wao wa msimu huu umezingatia vitu vingi ikiwemo ubora wa mchezaji husika na mchango wake kwenye timu anayotokea na kipa huyo amekidhi vigezo ndio maana wameamua kumchukua ili kuongeza thamani kwenye kikosi chao cha msimu ujao.
Alisema kupata saini ya Simon ambaye ni raia wa Cameroon kunaifanya safu yao ya ulinzi kuwa salama kama ilivyokuwa wakati wa Manula kabla hajapata majeraha yanayomweka nje kwa muda mrefu.
Awali Simba ilipanga kumsajili kipa Caique da Santos raia wa Brazil ambaye lilikuwa pendekezo la kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ lakini ilibadili mawazo na kuachana naye.
Sababu kubwa ya kuachana na kipa huyo ikielezwa ni kutokana na kuzungumza ya Kireno pekee, kitu ambacho kingemsumbua katika kuwasiliana na wachezaji wenzake.

The post Kipa wa Lupopo kufunga usajili Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/18/kipa-wa-lupopo-kufunga-usajili-simba/feed/ 0
Manula ashikilia hatma ya kipa mpya Simba https://www.greensports.co.tz/2023/05/31/manula-ashikilia-hatma-ya-kipa-mpya-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/31/manula-ashikilia-hatma-ya-kipa-mpya-simba/#respond Wed, 31 May 2023 18:11:04 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6403 Na mwandishi wetuSimba imeeleza kuwa suala la usajili wa kipa mpya wa timu hiyo kuelekea msimu ujao litategemea na ripoti ya madaktari itakayoonesha kipa wao majeruhi, Aishi Manula atakaa nje kwa muda gani.Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amefafanua kuwa upasuaji wa Manula utakaofanyika wiki hii mjini Johannesburg, Afrika Kusini ndio utakaotoa mwelekeo wa uamuzi […]

The post Manula ashikilia hatma ya kipa mpya Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba imeeleza kuwa suala la usajili wa kipa mpya wa timu hiyo kuelekea msimu ujao litategemea na ripoti ya madaktari itakayoonesha kipa wao majeruhi, Aishi Manula atakaa nje kwa muda gani.
Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amefafanua kuwa upasuaji wa Manula utakaofanyika wiki hii mjini Johannesburg, Afrika Kusini ndio utakaotoa mwelekeo wa uamuzi wa kusajili kipa mpya au la.
“Kwa kuwa Manula atafanyiwa matibabu ndani ya wiki hii maana yake ni kwamba ripoti yake ya kukaa nje itafahamika wiki hii, kwa hiyo ikitoka ripoti kwamba atakaa nje muda mrefu basi hatuna budi kuingia sokoni kutafuta makipa wengine wakati huo tukimsubiri Aishi aendelee kupona,” aisema Ally.
Manula (pichani juu) ametua juzi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya upasuaji wa nyama za paja, jeraha alilolipata Aprili 7, mwaka huu kwenye mechi ya robo fainali ya Kombe la FA (ASFC) iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Tangu hapo Simba imekuwa ikimtumia kipa namba tatu, Ally Salim huku fununu zikieleza kuwa kipa namba mbili wa Wekundu hao, Beno Kakolanya anatarajia kutimkia Singida Big Stars msimu ujao.
Na Simba ambayo inatarajia kucheza michuano ya Super League itakayoanza Agosti, mwaka huu imekuwa ikitajwa kumuwania kipa Alfred Mudekereza anayeidakia Vipers ya Uganda alikotokea kocha wa Simba wa sasa, Robert Oliveira ‘Robertinho’.

The post Manula ashikilia hatma ya kipa mpya Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/31/manula-ashikilia-hatma-ya-kipa-mpya-simba/feed/ 0
Manula, Inonga wapo fiti https://www.greensports.co.tz/2023/04/11/manula-inonga-wapo-fiti/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/11/manula-inonga-wapo-fiti/#respond Tue, 11 Apr 2023 12:21:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5756 Na mwandishi wetuRipoti ya matibabu ya wachezaji wa Simba, kipa Aishi Manula (pichani) na beki Henock Inonga imeondoa hofu kuhusu kuumia kwa wachezaji hao ikieleza kuwa wanaendelea vizuri, watajiunga na wenzao mazoezini.Wachezaji hao walishindwa kumaliza dakika 90 katika mechi ya robo fainali Kombe la FA (ASFC) dhidi ya Ihefu ambapo Simba ilishinda kwa mabao 5-1 […]

The post Manula, Inonga wapo fiti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Ripoti ya matibabu ya wachezaji wa Simba, kipa Aishi Manula (pichani) na beki Henock Inonga imeondoa hofu kuhusu kuumia kwa wachezaji hao ikieleza kuwa wanaendelea vizuri, watajiunga na wenzao mazoezini.
Wachezaji hao walishindwa kumaliza dakika 90 katika mechi ya robo fainali Kombe la FA (ASFC) dhidi ya Ihefu ambapo Simba ilishinda kwa mabao 5-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Daktari mkuu wa Simba, Edwin Kagoba alisema kuwa wachezaji hao waliumia lakini baada ya kuwapeleka hospitali na kuwafanyia vipimo wamebaini maumivu waliyopata ni ya kawaida.

“Siku ya pili baada ya mchezo tuliwapeleka Hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya vipimo zaidi na majibu yalipotoka juzi, yamebaini wana maumivu ya kawaida, tumewapa mapumziko ya siku tatu, timu itakaporudi kutoka Mbeya wataungana na wenzao kuendelea na mazoezi,” alisema Kagoba.


Taarifa hiyo imerudisha furaha na tabasamu kwa benchi la ufundi pamoja na mashabiki wa timu hiyo hasa ukizingatia mchango wa wachezaji hao kwenye kikosi cha Simba na ugumu wa mashindano yanayowakabili kwa sasa.
Simba ipo hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, imepangwa kucheza dhidi ya mabingwa watetezi Wydad Casablanca.
Kwenye Ligi Kuu NBC inaendelea kupambana, ipo nafasi ya pili ikipambana kurudisha taji hilo ambalo walilibeba kwa misimu minne mfulululizo kabla ya msimu uliopita kuporwa na mahasimu wao Yanga.
Simba pia wapo hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA wakitarajia kuumana na Azam FC ambayo iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye robo fainali iliyopigwa Azam Complex.

The post Manula, Inonga wapo fiti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/11/manula-inonga-wapo-fiti/feed/ 0