Mangungu. - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 30 Jan 2023 09:56:09 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Mangungu. - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mangungu ashinda uenyekiti Simba https://www.greensports.co.tz/2023/01/30/mangungu-ashinda-uenyekiti-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/01/30/mangungu-ashinda-uenyekiti-simba/#respond Mon, 30 Jan 2023 09:55:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4913 Na mwandishi wetuMurtaza Mangungu ameitetea nafasi ya uenyekiti wa klabu ya Simba baada ya kupata kura 1,311 katika uchaguzi uliofanyika Jumapili hii usiku akimbwaga wakili Moses Kaluwa aliyepata kura 1,045.Mbali na Mangungu, katika nafasi ya wajumbe washindi na idadi ya kura walizopata zikiwa kwenye mabano ni Dr Seif Muba (1,636), Asha Baraka (1,564), Issa Masoud […]

The post Mangungu ashinda uenyekiti Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Murtaza Mangungu ameitetea nafasi ya uenyekiti wa klabu ya Simba baada ya kupata kura 1,311 katika uchaguzi uliofanyika Jumapili hii usiku akimbwaga wakili Moses Kaluwa aliyepata kura 1,045.
Mbali na Mangungu, katika nafasi ya wajumbe washindi na idadi ya kura walizopata zikiwa kwenye mabano ni Dr Seif Muba (1,636), Asha Baraka (1,564), Issa Masoud Idd (1,285), Rodney Chiduo (1,267) na Seleman Harubu (1,250).
Wakati akijinadi katika kampeni zake, Mangungu pamoja na mambo mengine aliahidi kufuta uteja kwa mahasimu wao Yanga na kuhakikisha Simba inafanya vizuri katika mashindano mbalimbali.
Uchaguzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, ulitanguliwa na mkutano mkuu ambapo watendaji wa klabu hiyo walipata fursa ya kuanika mipango na mikakati ya timu ya Simba.
Katika mkutano huo, wanachama walielezwa kuwa bajeti ya klabu hiyo kwa mwaka 2021-22 ilikuwa ni Sh 11.94 bilioni wakati makusanyo kwa kipindi hicho hicho yalikuwa ni Sh 12.73 bilioni.
Katika matumizi, wanachama walielezwa kuwa yalihusisha malipo ya mishahara ya wachezaji na benchi la ufundi (Sh 4.3 bilioni) kambi ndani na nje ya nchi (Sh 2.2 bilioni) kambi timu ya wanawake (Sh 100 milioni) usajili (Sh 1.2 bilioni) katika fedha hizo Mohammed Dewji au Mo aliongeza Sh 2 bilioni pamoja na malipo mengineyo ikiwamo mishahara ya watendaji.


Mkutano huo pia ulipambwa na washiriki kutoka nje ya nchi akiwamo kocha wa Al Hilal ya Sudan, Florent Ibenge ambaye aliwapongeza wanachama na viongozi wa Simba akidai amefurahishwa na mualiko huo.
Mgeni mwingine kutoka nje aliyehudhuria mkutano huo ni mchezaji wa zamani wa Vipers ya Uganda ambaye pia alikuwa akicheza soka la kulipwa nchini China, Cesar Manzoki ambaye aliwafurahisha wanachama wa Simba kwa kudai kwamba hawezi kuichezea timu yenye rangi ya nyoka.
Kauli hiyo ilitafsiriwa na wanachama wengi katika mkutano huo kuwa mchezaji huyo alikuwa akiwananga mahasimu wa Simba, Yanga ambao wanatumia jezi za kijani na njano.
Mchezaji huyo amekuwa akihusishwa na mipango ya kujiunga na Simba na hapana shaka kwa kitendo chake cha kushiriki mkutano huo, haitoshangaza akivaa jezi nyekundu na nyeupe wakati wowote kuanzia sasa.
Mangungu aliingia madarakani Febuari 7, 2021 katika uchaguzi mdogo uliofanyika kuziba nafasi ya mwenyekiti iliyoachwa wazi na Swedi Nkwabi aliyejiuzulu miezi 10 baada ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo kwenye uchaguzi uliofanyika Novemba 5, 2018.

The post Mangungu ashinda uenyekiti Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/01/30/mangungu-ashinda-uenyekiti-simba/feed/ 0