Manara - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 07 Aug 2022 14:00:14 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Manara - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Manara, Hersi wafikishwa Kamati ya Maadili https://www.greensports.co.tz/2022/08/07/manara-hersi-wafikishwa-kamati-ya-maadili/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/07/manara-hersi-wafikishwa-kamati-ya-maadili/#respond Sun, 07 Aug 2022 13:59:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2257 Na mwandishi wetuSekretarieti ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imewafungulia mashitaka ya kimaadili, Rais wa Yanga, Hersi Said na msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara ambaye kwa sasa anatumikia adhabu ya kufungiwa kwa miaka miwili.Kamati ya Maadili ya TFF hivi karibuni ilimfungia Manara kujihusisha na shughuli za soka ndani na nje ya nchi kwa miaka […]

The post Manara, Hersi wafikishwa Kamati ya Maadili first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Sekretarieti ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imewafungulia mashitaka ya kimaadili, Rais wa Yanga, Hersi Said na msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara ambaye kwa sasa anatumikia adhabu ya kufungiwa kwa miaka miwili.
Kamati ya Maadili ya TFF hivi karibuni ilimfungia Manara kujihusisha na shughuli za soka ndani na nje ya nchi kwa miaka miwili pamoja na kumtoza faini ya Sh 20 milioni ambapo TFF wanadai Manara ameshindwa kutekeleza adhabu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF iliyopatikana leo na kusainiwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa shirikisho hilo, Clifford Ndimbo, ilieleza kuwa Hersi anadaiwa kwenda kinyume na Ibara ya 16 ya Katiba ya TFF pamoja na Ibara ya 1 ya Katiba ya Yanga.
Ndimbo katika taarifa yake alifafanua kwamba baada ya Manara kuadhibiwa, TFF ilimuandikia barua Hersi akiwa ndiye kiongozi wa Yanga ili kuhakikisha klabu yake inaheshimu uamuzi huo wa Kamati ya Maadili dhidi ya Manara.
Tayari TFF imepeleka mashitaka hayo kwa mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ili walalamikiwa waelezwe mashitaka yao na hatimaye kuitwa wakati wowote kamati hiyo itakapopanga tarehe ya kusikiliza mashitaka hayo.
Taarifa ya TFF ingawa haikueleza ni vipi Manara ameshindwa kutekeleza adhabu aliyopewa lakini inadhaniwa kwamba kitendo chake cha kuwapo kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi jana Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam huenda kimetafsiriwa kuwa ni kujihusisha na masuala ya soka.
Manara hata hivyo akiwa katika sherehe hizo alishiriki kutambulisha wachezaji ambapo alisema kwamba ameshiriki kama MC wa shughuli kutoka Kigogo, Sambusa jijini Dar es Salaam.
Manara alifungiwa na kamati hiyo ya TFF baada ya mzozo kutokea baina yake na Rais wa TFF, Walace Karia, mzozo uliotokea Julai 2 mwaka huu kwenye Jukwaa Kuu la Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha wakati wa mechi ya fainali ya Kombe la FA kati ya Yanga na Costala Union.
Katika tukio hilo Manara anadaiwa alimshambulia Karia kwa kumwambia: “Wewe unanifuatafuata sana na hii ni mara ya tatu, sikuogopi kwa lolote nina uwezo wa kukufanya lolote na huna uwezo wa kunifanya lolote.”
Manara hata hivyo baadaye aliomba radhi kwa tukio hilo ingawa Kamati ya Maadili ya TFF iliendelea kusikiliza shauri hilo na hatimaye kumchukulia hatua.

The post Manara, Hersi wafikishwa Kamati ya Maadili first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/07/manara-hersi-wafikishwa-kamati-ya-maadili/feed/ 0
Manara amuomba radhi Waziri https://www.greensports.co.tz/2022/08/02/manara-amwomba-radhi-waziri-mchengerwa/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/02/manara-amwomba-radhi-waziri-mchengerwa/#respond Tue, 02 Aug 2022 14:29:00 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2095 Na mwandishi wetuMsemaji wa Yanga aliyefungiwa, Haji Manara amemuomba radhi Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa kwa kauli alizozitoa dhidi yake katika siku za karibuni.Manara aliomba radhi hiyo akifafanua kuwa alifanya makosa kuikosoa kauli ya waziri huyo juu ya maadili na nidhamu aliyoitoa wakati wa hafla ya tuzo za Ligi Kuu Bara 2021/22 […]

The post Manara amuomba radhi Waziri first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Msemaji wa Yanga aliyefungiwa, Haji Manara amemuomba radhi Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa kwa kauli alizozitoa dhidi yake katika siku za karibuni.
Manara aliomba radhi hiyo akifafanua kuwa alifanya makosa kuikosoa kauli ya waziri huyo juu ya maadili na nidhamu aliyoitoa wakati wa hafla ya tuzo za Ligi Kuu Bara 2021/22 mnamo Julai 7, mwaka huu akihisi analengwa na kukosolewa yeye.
Manara alikosoa kauli za Mchengerwa wakati akieleza kutokubali kufungiwa na TFF kutojihusisha na soka ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miaka miwili pamoja na faini ya Sh milioni 20 kwa kosa la kumtolea maneno yasiyofaa Rais wa TFF, Wallace Karia kwenye mechi ya fainali ya Kombe la FA iliyopigwa jijini Arusha.
“Kutokuelewa na ilichukuliwa hivyo na kwamba Waziri amemshukia Manara lakini na mimi vile vile kwa bahati mabaya niliingia kichwa kichwa, ilikuwa ndiyo wiki ile ile na hata katika ‘press’ yangu na wazee na baadhi ya viongozi waliingia hivyo pia kutokana na ile presha maana tukio lilitokea wiki ile ile tu.
“Na mimi katika maelezo yangu nikajikosea mimi, Serikali na waziri mwenyewe kuonyesha waziri alitoa malekezo kwa kiasi fulani, lakini baadaye nikafuatilia na kuzungumza na baadhi ya maofisa wa wizara wakanihakikishia kwamba hiyo ni ‘standard’ ameiweka waziri amekuwa anazungumzia maadili na nidhamu.
“Lilikuwa jambo jema analifanya waziri, yawezekana labda hawakuelewa tafsiri yangu ya lugha niliyotumia, kwa utashi wa kimaadili kama unasema jambo ambalo wenzio hawakuliona liko sahihi hakuna neno la kusema zaidi ya samahani, niseme samahani Waziri wangu, wizara na serikali yangu,” alisema Manara.
Manara pia alisema tayari wameshapokea barua ya hukumu na baada ya kupeleka malalamiko yao kwa mamlaka husika kuhusu kutosajiliwa kwa kanuni zilizotumika kumhukumu kupitia Kamati ya Maadili, sasa wiki hii yeye na mawakili wake wanajipanga kukata rufaa ya hukumu hiyo pia.

The post Manara amuomba radhi Waziri first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/02/manara-amwomba-radhi-waziri-mchengerwa/feed/ 0