Mamadou Doumbia - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 01 Apr 2023 15:08:39 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Mamadou Doumbia - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Doumbia kupigania namba Yanga https://www.greensports.co.tz/2023/04/01/doumbia-kupigania-namba-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/01/doumbia-kupigania-namba-yanga/#respond Sat, 01 Apr 2023 15:08:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5650 Na mwandishi wetuBeki mpya wa kati wa Yanga, Mamadou Doumbia ameahidi kupambana mazoezini ili kumshawishi kocha mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi ili ampe nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.Mchezaji huyo raia wa Mali, tangu ametua Yanga akitokea Stade Meliane ya Mali kwenye dirisha dogo la usajili msimu huu ametumika kwa dakika 45 kwenye michuano […]

The post Doumbia kupigania namba Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Beki mpya wa kati wa Yanga, Mamadou Doumbia ameahidi kupambana mazoezini ili kumshawishi kocha mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi ili ampe nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.
Mchezaji huyo raia wa Mali, tangu ametua Yanga akitokea Stade Meliane ya Mali kwenye dirisha dogo la usajili msimu huu ametumika kwa dakika 45 kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyofanyika Zanzibar.
Mchezaji huyo ameeleza kuwa kinachomfanya asipate nafasi tangu ajiunge na timu hiyo ni kufanyia kazi mifumo ya kiuchezaji ambayo wachezaji wenzake tayari wameshaizoea. “Bado kuna vitu havijawa sawa kwangu kama kufuata vizuri mbinu ambazo kocha anataka tucheze lakini vitu vingine vyote ikiwemo namna ya kushirikiana na wenzangu pamoja na kuanzisha mashambulizi nipo sawa,” alisema Doumbia.


Mchezaji huyo ameeleza kuwa pamoja na changamoto hizo lakini hajakata tamaa, ataendelea kupambana kupigania nafasi ya kucheza na anaamini siku chache zijazo ataanza kuitumikia timu hiyo.
Alisema mbali na kuyafanyia kazi maelekezo ya benchi la ufundi lakini pia amekuwa akijifunza kutoka kwa wachzaji wenzake namna ya kutimiza kile ambacho wanatakiwa kukifanya hivyo mashabiki watarajie kumuona uwanjani hivi karibuni.
Doumbia ambaye mashabiki wengi wamekuwa wakitamani kumuona akikipiga kwenye mechi za Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Afrika, anapokea ushindani mkubwa kutoka kwa mabeki wa nafasi hiyo aliowakuta, nahodha Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Ibrahim Bacca na wakati mwingine Yanick Bangala.

The post Doumbia kupigania namba Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/01/doumbia-kupigania-namba-yanga/feed/ 0
Nabi: Doumbia anahitaji muda https://www.greensports.co.tz/2023/02/16/nabi-doumbia-anahitaji-muda/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/16/nabi-doumbia-anahitaji-muda/#respond Thu, 16 Feb 2023 17:44:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5178 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema kuwa licha ya ubora aliokuwa nao beki wa kati wa timu hiyo, Mamadou Doumbia, bado anahitaji muda zaidi ili aweze kuzoea falsafa zake.Doumbia (pichani kulia) ambaye amejiunga na Yanga katika dirisha dogo la usajili akitokea Stade Malien ya Mali, amepata nafasi ya kucheza mchezo mmoja wa […]

The post Nabi: Doumbia anahitaji muda first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema kuwa licha ya ubora aliokuwa nao beki wa kati wa timu hiyo, Mamadou Doumbia, bado anahitaji muda zaidi ili aweze kuzoea falsafa zake.
Doumbia (pichani kulia) ambaye amejiunga na Yanga katika dirisha dogo la usajili akitokea Stade Malien ya Mali, amepata nafasi ya kucheza mchezo mmoja wa Kombe la FA (ASFC) dhidi ya Rhino Rangers ambapo aliingia akitokea benchi.
Safu ya ulinzi ya Yanga ambayo imeruhusu mabao 10 pekee kwenye Ligi Kuu NBC hadi sasa huku pacha ya Dickson Job na Yannick Bangala ikifanya kazi nzuri ya kuiweka salama ngome ya mabingwa hao watetezi.
Nabi alisema kuwa anajua kiu ya mashabiki ni kumuona beki huyo wa kati akianza kwenye michezo ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Afrika ili kuongeza uimara wa safu ya ulinzi ya timu.
“Doumbia ni mchezaji mzuri ambaye naamini anaenda kuongeza kitu kwenye kikosi changu sio rahisi kuona akianza kucheza haraka hivyo ndio maana anaendelea kupikwa taratibu kujua falsafa za timu.
“Nimeona watu wanaongelea sana kuhusu Mamadou (Doumbia), si kila mchezaji akiletwa basi ataanza kucheza kwa haraka, huyu ni beki wa kati hili ni eneo ambalo unahitaji utulivu kumuingiza mtu mpya.
“Tunafanya kazi kubwa sasa ya kumfanya Doumbia azoee, wakati wake ukifika atacheza tu akishafanikiwa kucheza kama tunavyotaka. Huyu si mshambuliaji ambaye anaweza kuja na ukampa nafasi,” alifafanua Nabi.

The post Nabi: Doumbia anahitaji muda first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/16/nabi-doumbia-anahitaji-muda/feed/ 0