Makabi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 26 May 2023 05:49:40 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Makabi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Azam yamtaka straika wa Al Hilal https://www.greensports.co.tz/2023/05/26/azam-yamtaka-straika-wa-al-hilal/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/26/azam-yamtaka-straika-wa-al-hilal/#respond Fri, 26 May 2023 05:49:26 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6285 Na mwandishi wetuAzam FC inahusishwa kuwa kwenye mipango ya kumsajili straika wa Al Hilal ya Sudan, Makabi Lilepo (pichani juu) kwenye dirisha kubwa.Habari hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tangu uongozi wa Azam FC utangaze nia yake ya kutaka kusajili wachezaji watatu wakiwemo washambuliaji wawili wa kigeni ili kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la […]

The post Azam yamtaka straika wa Al Hilal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Azam FC inahusishwa kuwa kwenye mipango ya kumsajili straika wa Al Hilal ya Sudan, Makabi Lilepo (pichani juu) kwenye dirisha kubwa.
Habari hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tangu uongozi wa Azam FC utangaze nia yake ya kutaka kusajili wachezaji watatu wakiwemo washambuliaji wawili wa kigeni ili kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Straika huyo ameelezwa kuwa bado ana mkataba wa kuitumikia Al Hilal lakini kwa sasa anataka kuondoka kutokana na nchi hiyo kuwa na vita na tayari amewaeleza suala hilo watu wake wa karibu wanaomsimamia.
Ofisa Habari wa Azam, Hashim Ibwe alikiri kuwa na mpango wa kusajili washambuliaji wawili kutoka nje ya Tanzania lakini alisema kwa sasa hawezi kutaja majina yao sababu bado wana mikataba na timu wanazozitumikia.

“Makabi ni mchezaji mzuri kila klabu ingependa kuwa naye lakini sisi Azam tunaheshimu sheria na kanuni za usajili sababu bado ana mkataba na timu yake, ni vyema tukasubiri kuona itakavyokuwa mpaka dirisha la usajili litakapofunguliwa,” alisema Ibwe akimzungumzia mchezaji huyo ambaye pia amewahi kuhusishwa na klabu ya Simba.


Ibwe alisema kutokana na malengo waliyokuwa nayo msimu ujao ana imani idara yao inayohusika na suala la usajili itatimiza vyema majukumu yake kwa kusajili wachezaji wenye ubora utakaoipa mafanikio timu yao.
Azam FC ni miongoni mwa timu nne zitakazopeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kutokana na kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na kumaliza ligi ndani ya nafasi nne za juu.

The post Azam yamtaka straika wa Al Hilal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/26/azam-yamtaka-straika-wa-al-hilal/feed/ 0