Majogoro - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 18 Oct 2023 05:18:37 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Majogoro - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Majogoro afurahia ndoto kutimia https://www.greensports.co.tz/2023/10/18/majogoro-afurahia-ndoto-kutimia/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/18/majogoro-afurahia-ndoto-kutimia/#respond Wed, 18 Oct 2023 05:18:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8131 Na mwandishi wetuKiungo wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Baraka Majogoro amesema anashukuru Mungu kutimia kwa ndoto yake ya kucheza nje ya nchi huku akiamini sasa ni njia sahihi ya kutimiza malengo yake katika soka.Mchezaji huyo anayekipiga Chippa United ya Ligi Kuu Afrika Kusini aliyojiunga nayo msimu huu akitokea KMC, amekuwa mchezaji tegemeo […]

The post Majogoro afurahia ndoto kutimia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Baraka Majogoro amesema anashukuru Mungu kutimia kwa ndoto yake ya kucheza nje ya nchi huku akiamini sasa ni njia sahihi ya kutimiza malengo yake katika soka.
Mchezaji huyo anayekipiga Chippa United ya Ligi Kuu Afrika Kusini aliyojiunga nayo msimu huu akitokea KMC, amekuwa mchezaji tegemeo katika kikosi cha Chippa inayoshika nafasi ya saba ikiwa na pointi 13 katika mechi tisa.

“Ilikuwa ndoto na malengo yangu kwamba siku moja nicheze nje ya Tanzania, nashukuru Mungu amenijaalia ndoto imetimia na zaidi naomba anijaalie nitimize malengo yangu zaidi ya hapo,” alisema Majogoro aliyewahi kukipiga Mtibwa Sugar.


Awali, Majogoro alipojiunga na Chippa hakucheza katika mechi nne za awali za ligi ambazo walifungwa mbili na sare mbili lakini alipopangwa kwenye mechi iliyofuata timu hiyo ilipata ushindi wa kwanza wa bao 1-0 dhidi ya Cape Town Spurs na tangu hapo amekuwa na namba ya kudumu katika kikosi hicho.
Kiungo huyo pia ameeleza kuhusu michuano ya Afcon ambapo Tanzania imepangwa Kundi F dhidi ya Morocco, DR Congo na Zambia akifafanua kufahamu ubora na ubabe wa timu hizo lakini kama wakijiandaa vya kutosha kwa uzito wa michuano hiyo, anaamini wapinzani hao hawawezi kuwazuia kutimiza ndoto zao.

The post Majogoro afurahia ndoto kutimia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/18/majogoro-afurahia-ndoto-kutimia/feed/ 0
Majogoro ang’ara Afrika Kusini https://www.greensports.co.tz/2023/09/27/majogoro-angara-afrika-kusini/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/27/majogoro-angara-afrika-kusini/#respond Wed, 27 Sep 2023 19:31:26 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7870 Na mwandishi wetuKiungo wa timu ya taifa, Taifa Stars, Baraka Majogoro (pichani) anayechezea Chippa United ya Afrika Kusini amepewa tuzo ya mchezaji bora wa mechi yao na Super Sport United katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini.Katika mchezo huo wa juzi Chippa United ilishinda kwa bao 1-0 na kukwea hadi nafasi ya nne ikifikisha pointi 12 […]

The post Majogoro ang’ara Afrika Kusini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo wa timu ya taifa, Taifa Stars, Baraka Majogoro (pichani) anayechezea Chippa United ya Afrika Kusini amepewa tuzo ya mchezaji bora wa mechi yao na Super Sport United katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Katika mchezo huo wa juzi Chippa United ilishinda kwa bao 1-0 na kukwea hadi nafasi ya nne ikifikisha pointi 12 katika msimamo wa ligi hiyo wakiongozwa na Mamelodi Sundown, Golden Arrow FC na Super Sport ipo nafasi ya tatu.
Akihojiwa baada ya mchezo huo Majogoro alisema mechi ilikuwa ngumu na yenye ushindani lakini wanashukuru kwa kupata matokeo mazuri.

“Nashukuru kwa tuzo niliyopata pia, mchezo haukuwa rahisi lakini tumepambana na kupata ushindi, halikuwa jambo jepesi kulingana na ushindi uliokuwepo muda wote uwanjani,” alisema.


Majogoro anayejumuishwa mara kwa mara kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania au Taifa Stars amekuwa na kiwango bora tangu kujiunga na timu hiyo akitokea KMC aliyokuwa akiitumikia msimu uliopita.

The post Majogoro ang’ara Afrika Kusini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/27/majogoro-angara-afrika-kusini/feed/ 0
Majogoro awaahidi furaha Chippa Utd https://www.greensports.co.tz/2023/08/05/majogoro-awaahidi-furaha-chippa-utd/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/05/majogoro-awaahidi-furaha-chippa-utd/#respond Sat, 05 Aug 2023 18:53:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7250 Na mwandishi wetuKiungo mpya wa timu ya Chippa United ya Afrika Kusini, Baraka Majogoro (pichani) ameeleza furaha yake ya kutua katika timu hiyo, akiahidi sasa ni wakati wa kuwapa furaha mashabiki na wadau wa timu hiyo.Majogoro ameyasema hayo baada ya jana kutambulishwa rasmi na klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini.“Kwangu ni changamoto mpya […]

The post Majogoro awaahidi furaha Chippa Utd first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo mpya wa timu ya Chippa United ya Afrika Kusini, Baraka Majogoro (pichani) ameeleza furaha yake ya kutua katika timu hiyo, akiahidi sasa ni wakati wa kuwapa furaha mashabiki na wadau wa timu hiyo.
Majogoro ameyasema hayo baada ya jana kutambulishwa rasmi na klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
“Kwangu ni changamoto mpya katika maisha yangu ya mpira, lakini namshukuru Mungu kwa yote haya na sasa ninaangazia zaidi namna ya kuwapa furaha wapenzi wa soka na wadau na mashabiki wa Chippa United,” alisema Majogoro.
Majogoro aliyejiunga na Chippa akitokea KMC ya Dar es Salaam anapishana na beki wa kati Mtanzania, Abdi Banda aliyeitumikia timu hiyo msimu uliopita kabla ya hivi karibuni kutimkia timu ya Richards Bay.
Kiungo huyo aliyewahi kuzitumikia Polisi Tanzania na Mtibwa Sugar ametua katika timu hiyo kuongeza nguvu kulingana na ushindani uliopo sasa katika Ligi Kuu uliopelekea Chippa kumaliza nafasi ya 14 na kuponea chupuchupu kushuka daraja.
Wachezaji wengine waliotambulishwa pamoja na Majogoro kwenye timu hiyo juzi ni Andile Fakude, Thabang Maloa, Senzo Nkwanyana na Lukhanyo July.

The post Majogoro awaahidi furaha Chippa Utd first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/05/majogoro-awaahidi-furaha-chippa-utd/feed/ 0