Luis Rubiales - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 05 Apr 2024 18:06:00 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Luis Rubiales - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Aliyembusu mchezaji adai tatizo ni kuwa mwanaume https://www.greensports.co.tz/2024/04/05/aliyembusu-mchezaji-adai-tatizo-ni-kuwa-mwanaume/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/05/aliyembusu-mchezaji-adai-tatizo-ni-kuwa-mwanaume/#respond Fri, 05 Apr 2024 18:05:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10526 Madrid, HispaniaRais wa zamani wa Shirikisho la Soka Hispania, (RFEF) Luis Rubiales amehoji hatua ya kumshitaki mahakamani kwa kumpiga busu mdomoni mchezaji wa timu ya taifa ya Hispania, Jenni Hermoso kwamba imekuja kwa sababu yeye ni mwanaume.Rubiales anajiandaa kupanda mahakamani kwa kosa la kumbusu mdomoni mshambuliaji huyo wa Hispania wakati wa hafla ya utoaji tuzo […]

The post Aliyembusu mchezaji adai tatizo ni kuwa mwanaume first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Hispania, (RFEF) Luis Rubiales amehoji hatua ya kumshitaki mahakamani kwa kumpiga busu mdomoni mchezaji wa timu ya taifa ya Hispania, Jenni Hermoso kwamba imekuja kwa sababu yeye ni mwanaume.
Rubiales anajiandaa kupanda mahakamani kwa kosa la kumbusu mdomoni mshambuliaji huyo wa Hispania wakati wa hafla ya utoaji tuzo baada ya Hispaia kuibwaga England, Agosti mwaka jana na kubeba Kombe la Dunia la Wanawake mjini Sydney, Australia.
Tukio hilo ambalo limeibua mjadala duniani kote lilisababisha Rubiales kujiuzulu nafasi yake ya urais wa RFEF baada ya kushinikizwa kufanya hivyo huku Jenni na wachezaji wenzake wakidai kwamba tukio hilo limewashushia heshima na halikufanyika kwa makubaliano.
Akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni nchini Hispania, Rubiales alikana kufanya kosa lolote na kuongeza kwamba haiwezekani kuumuliza Jenni kuhusu suala hilo badala yake anaulizwa yeye kwa sababu ni mwanaume.

“Mnaweza kuniuliza mimi hilo kwa sababu mimi ni mwanaume,, kwangu mimi hakuna kosa lolote dhidi ya Jenni, kwa yeyote aliyeona picha za tukio lile, siwezi kuelewa iwapo kuna mtu ataliona tukio lile kuwa ni la udhalilishaji kijinsia,” alisema Rubiales.


Rubiales apia alisema kuwa wahanga wa tukio hilo ambalo liligeuka mjadala katika nchi nyingi hasa za Ulaya ni familia yake pamoja na marafiki zake.
Waendesha mashitaka nchini Hispania wanataka Rubiales afungwa miaka miwili na nusu jela kwa makosa mawili anayotuhumiwa ya ubabe akidaiwa alimlazimisha Jenni kumpiga busu pamoja na udhalilishaji kijinsia.
Rubiales ambaye alikuwa beki enzi zake za soka la ushindani, alisema kwamba labda alitakiwa kuwa kimya bila kufurahia baada ya Hispania kushinda bao 1-0 dhidi ya Engla na kubeba Kombe la Dunia.


Ukiachana na sakala hilo, Rubiales pia alikamatwa juzi Jumatano akihusishwa na tuhuma za kupokea rushwa akidaiwa kupewa mgao usio rasmi wakati wa majadiliano ya kuandaa mechi ya Spanish Super Cup nchini Saudi Arabia.
Akizungumzia tuhuma hizo, Rubiales ambaye akaunti zake zimefungiwa alisema kwamba hajawahi kuchukua rushwa katika maisha yake na kuzitaja tuhuma anazohusishwa nazo kuwa ni uwongo.
“Wamefungi akaunti zangu, na kwa sasa siwezi hata kulipia kinywaji, kama kuna uchunguzi unaofanywa basi hapo kuna hisia kwamba sina kosa,” alisema Rubiales.

The post Aliyembusu mchezaji adai tatizo ni kuwa mwanaume first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/05/aliyembusu-mchezaji-adai-tatizo-ni-kuwa-mwanaume/feed/ 0
Aliyembusu mchezaji matatani kwa rushwa https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/aliyembusu-mchezaji-matatani-kwa-rushwa/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/aliyembusu-mchezaji-matatani-kwa-rushwa/#respond Thu, 04 Apr 2024 12:54:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10496 Madrid, HispaniaRais wa zamani wa Shirikisho la Soka Hispania (RFEF) Luis Rubiales anayekabiliwa na kashfa ya kumbusu mdomoni mchezaji wa timu ya taifa, amekamatwa kwa ajili ya uchunguzi unaomhusisha na kashfa ya kupokea rushwa.Rubiales alikamatwa jana Jumatano mara baada ya kuwasili jijini Madrid akitokea Jamhuri ya Dominica ingawa aliachiwa huru muda mfupi baadaye.Habari zinadai kwamba […]

The post Aliyembusu mchezaji matatani kwa rushwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Hispania (RFEF) Luis Rubiales anayekabiliwa na kashfa ya kumbusu mdomoni mchezaji wa timu ya taifa, amekamatwa kwa ajili ya uchunguzi unaomhusisha na kashfa ya kupokea rushwa.
Rubiales alikamatwa jana Jumatano mara baada ya kuwasili jijini Madrid akitokea Jamhuri ya Dominica ingawa aliachiwa huru muda mfupi baadaye.
Habari zinadai kwamba Rubiales alikamatwa kwa tuhuma za kupokea rushwa wakati akiufanyia kazi mpango wa kuandaa mechi ya Spanish Super Cup mjini Riyadh, Saudi Arabia na waendesha mashtaka wanataka afungwe jela miaka miwili na nusu.
Rubiales ambaye amekana kufanya kosa lolote, alikamatwa mara baada ya ndege aliyosafiria kutua Madrid na kupelekwa moja kwa moja polisi kwa gari jeusi akiwa chini ya ulinzi wa maofisa kadhaa.
Chanzo kimoja cha habari Hispania kilieleza kuwa Rubiales anatarajia kufikishwa mahakamani Alhamisi hii huku pia ikidaiwa kwamba wakati akiwa Dominica, polisi waliivamia nyumba yake na kufanya upekuzi.
Ukiachana na sakata hilo jipya la rushwa, Rubiales anakabiliwa na kashfa ya udhalilishaji kijinsia kwa kitendo alichofanya Agosti mwaka jana cha kumbusu mdomoni hadharani mchezaji wa timu ya taifa ya Hispania, Jenni Hermoso.

Rubiales akionekana mwenye furaha wakati wa hafla za kukabidhiwa tuzo za ushindi wa Kombe la Dunia la Wanawake mjini Sydney, Australia, alimkumbatia kwa nguvu na kumbusu mdomoni Jenni, tukio ambalo lilizua taharuki duniani kote.
Baada ya tukio hilo, Rubiales alijikuta akiandamwa kila kona na kushinikizwa kujiuzulu nafasi yake RFEF jambo ambalo awali alilikataa akidai kulikuwa na makubaliano baina yake na Jenni ingawa baadaye alitangaza kujiuzulu.

The post Aliyembusu mchezaji matatani kwa rushwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/aliyembusu-mchezaji-matatani-kwa-rushwa/feed/ 0
Hatimaye aliyembusu mchezaji ajiuzulu https://www.greensports.co.tz/2023/09/12/hatimaye-aliyembusu-mchezaji-ajiuzulu/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/12/hatimaye-aliyembusu-mchezaji-ajiuzulu/#respond Tue, 12 Sep 2023 16:36:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7734 Madrid, HispaniaRais wa Shirikisho la Soka Hispania (REEF), Luis Rubiales (pichani) hatimaye amejiuzulu nafasi yake baada ya kuandamwa na tukio la kumbusu mdomoni mshambuliaji wa timu ya wanawake ya Hispania, Jenni Hermoso.Rubiales aliyembusu Jenni Agosti 20 baada ya Hispania kuibwaga England bao 1-0 na kubeba taji la dunia, awali alitangaza kutokuwa tayari kujiuzulu akisisitiza hajafanya […]

The post Hatimaye aliyembusu mchezaji ajiuzulu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Rais wa Shirikisho la Soka Hispania (REEF), Luis Rubiales (pichani) hatimaye amejiuzulu nafasi yake baada ya kuandamwa na tukio la kumbusu mdomoni mshambuliaji wa timu ya wanawake ya Hispania, Jenni Hermoso.
Rubiales aliyembusu Jenni Agosti 20 baada ya Hispania kuibwaga England bao 1-0 na kubeba taji la dunia, awali alitangaza kutokuwa tayari kujiuzulu akisisitiza hajafanya jambo lolote baya, aliwasilisha barua ya kujiuzulu Jumatatu hii kwa rais wa muda wa REEF, Pedro Rocha.
Mbali na kujiuzulu REEF, Rubiales pia ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya makamu rais wa Umoja vya Vyama vya Soka Ulaya (Uefa)
Kujiuzulu kwa Rubiales huenda kukapunguza shutuma zilizokuwa zikielekezwa kwake kutoka makundi mbalimbali yaliyomtaka ajiuzulu wakiwamo wachezaji wa timu ya wanawake Hispania waliotangaza kutoichezea timu hiyo kama Rubiales angeendelea kukalia kiti cha REEF.
Wakati Rubiales akichukua uamuzi wa kujiuzulu, Jenni, 33, ameshalifikisha suala hilo kwenye vyombo vya sheria akisisitiza kwamba hakukuwa na makubaliano ya yeye kupigwa busu mdomoni.


Katika madai yake ya awali, Rubiales, 46, alisisitiza kwamba hawezi kujiuzulu na kwamba kulikuwa na makubaliano baina yake na Jenni ingawa Fifa walimsimamisha kwa siku 90 na kutangaza kuanza uchunguzi wa tukio hilo.
“Baada ya kusimamishwa haraka kulikofanywa na Fifa pamoja na kufunguliwa mashtaka dhidi yangu, ni dhahiri kwamba siwezi kurudi katika nafasi yangu,” alisema Rubiales.
“Kusisitiza kusubiri na kushikilia msimamo hakutachangia jambo lolote chanya kwa shirikisho la soka Hispania au soka la Hispania,” alisema Rubiales kuutetea uamuzi wake wa kujiuzulu.
“Nina imani katika ukweli na nitafanya kila liwezekanalo kwa uwezo wangu ukweli uwekwe wazi,” alisema Rubiales.
“Wanangu (wa kike) watu wa familia yangu na watu wanaonipenda wameumizwa na matokeo ya adhabu ninayopewa pamoja na kuwapo kwa uwongo mwingi lakini pia upo ukweli kwamba mitaani siku hadi siku ukweli umeendelea kujiweka wazi,” alisema Rubiales.

“Baba yangu, wanangu, hao nimezungumza nao, wanajua hapa si tena suala langu, na baadhi ya marafiki wa karibu wameniambia, Luis ni lazima uangalie hadhi yako na kuendelea na maisha yako kwa sababu tofauti na hivyo utawaumiza watu unaowapenda na mchezo unaoupenda,” alisema Rubiales.


“Hili si suala langu peke yangu, misimamo yangu inaweza kuwaumiza watu wengine ambao ni muhimu, ni jambo la busara kwa uamuzi niliouchukua,” alisema Rubiales.

The post Hatimaye aliyembusu mchezaji ajiuzulu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/12/hatimaye-aliyembusu-mchezaji-ajiuzulu/feed/ 0