Luis Enrique - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 04 Apr 2024 08:53:01 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Luis Enrique - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Kocha PSG akana, Mbappe hajamtukana https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/kocha-psg-akana-mbappe-hajamtukana/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/kocha-psg-akana-mbappe-hajamtukana/#respond Thu, 04 Apr 2024 08:52:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10494 Paris, UfaransaKocha wa PSG, Luis Enrique amekana na kuziita uwongo habari zinazodai kwamba alitukanwa na mshambuliaji wake, Kylian Mbappe baada ya kocha huyo kumtupa benchi katika mechi dhidi ya Marseille.Mbappe alionekana mwenye sura ya hasira wakati akielekea kwenye benchi na kuonekana kama akitoa kauli ambayo baadhi ya mitandao ya kijamii iliitafsiri kuwa ni kauli za […]

The post Kocha PSG akana, Mbappe hajamtukana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Paris, Ufaransa
Kocha wa PSG, Luis Enrique amekana na kuziita uwongo habari zinazodai kwamba alitukanwa na mshambuliaji wake, Kylian Mbappe baada ya kocha huyo kumtupa benchi katika mechi dhidi ya Marseille.
Mbappe alionekana mwenye sura ya hasira wakati akielekea kwenye benchi na kuonekana kama akitoa kauli ambayo baadhi ya mitandao ya kijamii iliitafsiri kuwa ni kauli za kumtukana Enrique.
Katika mechi baina ya timu hizo mahasimu iliyopigwa Jumapili iliyopita, PSG ilitoka na ushindi wa mabao 2-0 ingawa baada ya hapo tukio la Mbappe kutupwa benchi liligeuka mjadala.
“Jambo la msingi ni kwamba kila kitu kinachotengenezwa kutokana na uwongo ni katika yale mambo yanayotokea kwenye dunia ya soka, kuna mmoja ametengeneza mtu kutukanwa na uvumi wa kila aina ulioibuka,” alisema Enriqque.
Katika mechi saba zilizopita za PSG kwenye Ligi 1, Mbappe amecheza moja tu kwa dakika zote 90 ambapo Enrique amekuwa akimuweka benchi kwa kumuingiza kipindi cha pili au kumtoa wakati mechi ikiendelea.
Enrique amechukua uamuzi huo tangu Mbappe atangaze Februari mwaka huu uamuzi wake wa kuihama timu hiyo baada ya msimu huu huku habari zikidai kwamba mazungumzo kati yake na klabu ya Real Madrid yanaendelea.
Katika siku za karibuni, Enrique alisema kwamba anaamini mchezaji huyo atabadili maamuzi na kubaki PSG ingawa kabla ya hapo alisema kwamba ni lazima wajiandae na maisha bila ya Mbappe na hapo hapo akaanza utaratibu wa kumtupa benchi.
Kocha huyo pia alimsifia mchezaji huyo kwa ubora wake pamoja na wachezaji wote wa PSG mara baada ya mechi na Marseille na kuongeza kuwa Mbappe alikuwa na tabia njema.

The post Kocha PSG akana, Mbappe hajamtukana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/kocha-psg-akana-mbappe-hajamtukana/feed/ 0
Swali kuhusu Mbape lamtibua kocha PSG https://www.greensports.co.tz/2024/04/02/swali-kuhusu-mbape-lamtibua-kocha-psg/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/02/swali-kuhusu-mbape-lamtibua-kocha-psg/#respond Tue, 02 Apr 2024 14:10:03 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10477 Paris, UfaransaKocha wa PSG, Luis Enrique (pichani) amewalaumu waandishi wa habari kwa kumuuliza kila wakati swali kuhusu maamuzi anayoyafanya kwa Kylian Mbappe akidai kwamba swali hilo linamkera.Katika siku za hivi karibuni waandishi wa habari wamekuwa wakihoji nafasi ya Mbappe na muda anaocheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo ya jijini Paris.Maswali hayo yamekuwa yakiibuka […]

The post Swali kuhusu Mbape lamtibua kocha PSG first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Paris, Ufaransa
Kocha wa PSG, Luis Enrique (pichani) amewalaumu waandishi wa habari kwa kumuuliza kila wakati swali kuhusu maamuzi anayoyafanya kwa Kylian Mbappe akidai kwamba swali hilo linamkera.
Katika siku za hivi karibuni waandishi wa habari wamekuwa wakihoji nafasi ya Mbappe na muda anaocheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo ya jijini Paris.
Maswali hayo yamekuwa yakiibuka baada ya Enrique kuanza kumuweka benchi kwa baadhi ya mechi ambazo amekuwa ama akiingia kipindi cha pili au akitolewa kabla ya dakika 90 kwisha.
Jumapili PSG ilitoka na ushindi muhimu wa mabao 2-0 dhidi ya mahasimu wao, Marseille licha ya kucheza wakiwa 10 kwa takriban dakika 50 lakini mazingira yote hayo na matokeo mazuri havikutosha kuwa sababu ya swali kuhusu Mbappe kutoulizwa.
Enrique aliulizwa kuhusu hatua yake ya kumtoa Mbappe katika dakika ya 65 ya mchezo huo na nafasi yake kuingia Goncalo Ramos, swali ambalo kocha huyo hakulifurahia.

“Ni mziki huo huo wiki baada ya wiki, inanikera, mimi ni kocha na nafanya maamuzi kila siku, kila wiki, nitakuwa nikifanya hivyo hivyo hadi siku yangu ya mwisho hapa Paris, wakati wote huwa natafuta suluhisho bora kwa timu yangu, labda nakosea lakini nadhani niko sahihi,” alisema Enrique.


Enrique ameendelea kumtoa au kutomuanzisha Mbappe kikosi cha kwanza tangu mshambuliaji huyo atangaze hadharani kwamba ataihama klabu hiyo baada ya msimu huu huku mazungumzo baina yake na klabu ya Real Madrid yakidaiwa kuendelea.
Kocha huyo hata hivyo Jumamosi alinukuliwa akisema anaamini Mbappe atabaki na kuendelea kuichezea timu hiyo na hadi sasa amekuwa na mchango mzuri ikiwamo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo timu hiyo ipo hatua ya robo fainali ikisubiri kuumana na Barcelona.

The post Swali kuhusu Mbape lamtibua kocha PSG first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/02/swali-kuhusu-mbape-lamtibua-kocha-psg/feed/ 0