Luis Diaz - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 17 Nov 2023 13:28:30 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Luis Diaz - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Luis Diaz aitungua Brazil, baba amwaga chozi https://www.greensports.co.tz/2023/11/17/luis-diaz-aitungua-brazil-baba-amwaga-chozi/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/17/luis-diaz-aitungua-brazil-baba-amwaga-chozi/#respond Fri, 17 Nov 2023 13:28:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8491 Bogota, ColombiaSiku chache baada ya Manuel Diaz kuachiwa na watekaji, hatimye amemshuhudia mwanaye Luis Diaz akifunga mabao mawili na kuiwezesha Colombia kuichapa Brazil 2-1, tukio lililomtoa machozi mzee huyo akiwa jukwaani.Mechi hiyo ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 imekuwa ya kipekee kwa mzee huyo aliyetekwa Oktoba 28 na kujikuta akitokwa machozi ya […]

The post Luis Diaz aitungua Brazil, baba amwaga chozi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Bogota, Colombia
Siku chache baada ya Manuel Diaz kuachiwa na watekaji, hatimye amemshuhudia mwanaye Luis Diaz akifunga mabao mawili na kuiwezesha Colombia kuichapa Brazil 2-1, tukio lililomtoa machozi mzee huyo akiwa jukwaani.
Mechi hiyo ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 imekuwa ya kipekee kwa mzee huyo aliyetekwa Oktoba 28 na kujikuta akitokwa machozi ya furaha kama vile kutoamini kilichotokea.
Mzee huyo alijiangusha mbele ya watu waliokuwa karibu yake katika jukwaa moja la Uwanja wa Metropolitan na kuanza kushangilia pembeni ya mkewe Cilenis Marulanda huku akitokwa na machozi.
Tukio la kutekwa mzee huyo lilitokea kwenye kituo kimoja cha mafuta baada ya wanaume wawili waliokuwa kwenye pikipiki kumteka na mkewe na kukaa na mzee huyo kwa siku 12 ingawa mkewe aliachiwa muda mfupi baadaye.

Mzee huyo aliungana na familia yake kwa mara ya kwanza Jumanne iliyopita na mtoto wake Luis Diaz ambaye ni mchezaji wa Liverpool, akiwa Colombia kwa maandalizi ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia alipata nafasi ya kukutana na baba yake kwa mara ya kwanza tangu kutekwa kwa mzee huyo.

“Namshuruku Mungu, amefanya lililowezekana, kwa wakati wote tumeishi katika kipindi kigumu lakini maisha yanakufanya kuwa imara na jasiri, ni hivyo, ni soka ni maisha, tulikuwa na haki ya kupata ushindi,” alisema Luis Diaz mara baada ya mechi hiyo.


Katika mechi hiyo iliyopigwa jana Alhamisi, Díaz alifunga mabao yote kwa kichwa katika dakika za 75 na 79 na kuipa timu ya Colombia ushindi wa kwanza dhidi ya Brazil katika mechi 15 za kufuzu Kombe la Dunia.

The post Luis Diaz aitungua Brazil, baba amwaga chozi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/17/luis-diaz-aitungua-brazil-baba-amwaga-chozi/feed/ 0
Hatimaye Luis Díaz, baba yake wakutana https://www.greensports.co.tz/2023/11/14/hatimaye-luis-diaz-baba-yake-wakutana/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/14/hatimaye-luis-diaz-baba-yake-wakutana/#respond Tue, 14 Nov 2023 19:09:06 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8462 Bogota, ColombiaWinga wa Liverpool na timu ya taifa ya Colombia, Luis Diaz hatimaye ameungana kwa mara ya kwanza na baba yake ambaye alitekwa na kundi la waasi nchini humo.Shirikisho la Soka Colombia limethibitisha leo Jumanne kuhusu kukutana kwa Luis na baba yake Manuel Diaz ambaye alitekwa na waasi wa kundi la ELN akiwa na mkewe […]

The post Hatimaye Luis Díaz, baba yake wakutana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Bogota, Colombia
Winga wa Liverpool na timu ya taifa ya Colombia, Luis Diaz hatimaye ameungana kwa mara ya kwanza na baba yake ambaye alitekwa na kundi la waasi nchini humo.
Shirikisho la Soka Colombia limethibitisha leo Jumanne kuhusu kukutana kwa Luis na baba yake Manuel Diaz ambaye alitekwa na waasi wa kundi la ELN akiwa na mkewe ingawa mkewe alipatikana saa kadhaa baada ya tukio hilo.
Utekaji huo ulifanywa Oktoba 28 na watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki katika kituo kimoja cha mafuta kwenye mji wa Barrancas jimbo la La Guajira ambako mzee huyo mwenye umri wa miaka 58 anaishi na mkewe.
Baada ya tukio hilo, Luis aliendelea kuiwakilisha Liverpool na Jumapili alikuwapo katika mechi dhidi ya Brentford kabla ya kurudi Colombia akijiandaa kuiwakilisha timu yake ya taifa ambayo keshokutwa Alhamisi itacheza na Brazil katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026.
Luis katika mechi ya Liverpool alionekana akiwa amevaa fulana yenye maandishi ya kuwasihi waasi wamuachie huru baba yake huku klabu yake nayo ikiwa sambamba naye katika kilio hicho ambacho hatimaye waasi wamekisikia kwa kumuachia huru mzee huyo.
Shirikisho la Soka Colombia lilitoa picha ya baba huyo akiwa na mwanaye katika mitandao ya kijamii, picha hiyo ikiwa na kichwa cha habari kilichosema, ‘we are family’.

The post Hatimaye Luis Díaz, baba yake wakutana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/14/hatimaye-luis-diaz-baba-yake-wakutana/feed/ 0
Luis Diaz afunga bao, amlilia baba yake aliyetekwa https://www.greensports.co.tz/2023/11/06/luis-diaz-afunga-bao-amlilia-baba-yake-aliyetekwa/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/06/luis-diaz-afunga-bao-amlilia-baba-yake-aliyetekwa/#respond Mon, 06 Nov 2023 19:00:17 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8386 London, EnglandMchezaji wa Liverpool, Luis Diaz ambaye baba yake Manuel Diaz ametekwa na waasi wa Colombia ameifungia bao timu yake na baada ya bao hilo akaonesha fulana yenye maandishi ya kuwataka waasi wamuachie huru baba yake.Diaz, 26, alifunga bao hilo jana Jumapili katika mechi ya Ligi Kuu England (EPL) dhidi ya Luton na kuiwezesha Liverpool […]

The post Luis Diaz afunga bao, amlilia baba yake aliyetekwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Mchezaji wa Liverpool, Luis Diaz ambaye baba yake Manuel Diaz ametekwa na waasi wa Colombia ameifungia bao timu yake na baada ya bao hilo akaonesha fulana yenye maandishi ya kuwataka waasi wamuachie huru baba yake.
Diaz, 26, alifunga bao hilo jana Jumapili katika mechi ya Ligi Kuu England (EPL) dhidi ya Luton na kuiwezesha Liverpool kutoka sare ya bao 1-1.
Fulana ya ndani aliyovaa Diaz ilionesha maandishi yaliyosomeka ‘freedom for papa’ akihimiza kuachiwa huru kwa baba yake ambaye ametekwa na kundi la waasi nchini Colombia la ELN tangu Oktoba 28 mwaka huu.

“Mama yangu, kaka zangu na mimi tuna shauku kubwa, tuna mawazo na hatuna neno la kuelezea hisia zetu, maumivu yataisha pale tu tutakapokuwa naye pamoja nyumbani,” alisema Luis Diaz.


“Nawaomba wamuachie haraka, waheshimu utu wake na kuyamaliza maumivu haya ya kusubiri, tunawaomba wafikirie mara mbili matendo yake na kumuacha awe pamoja nasi,” alisema Luis Diaz.
Serikali ya Colombia imeendelea na msako unaohusisha wanajeshi na polisi kwa lengo la kumtafuta baba wa Luis Diaz na kutangaza donge nono kwa atakayefanikisha upatikanaji wa mzee huyo.
Baba wa Luis alitekwa na waasi waliokuwa kwenye pikipiki wakiwa na silaha wakati akiwa na mkewe kwenye kituo kimoja cha mafuta ingawa baadaye mkewe alipatikana.

The post Luis Diaz afunga bao, amlilia baba yake aliyetekwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/06/luis-diaz-afunga-bao-amlilia-baba-yake-aliyetekwa/feed/ 0
‘Baba wa Luis Diaz ametekwa na waasi’ https://www.greensports.co.tz/2023/11/03/baba-wa-luis-diaz-ametekwa-na-waasi/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/03/baba-wa-luis-diaz-ametekwa-na-waasi/#respond Fri, 03 Nov 2023 16:20:18 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8351 Barrancas, ColombiaSerikali ya Colombia imesema kuwa Manuel Díaz ambaye ni baba wa mchezaji wa Liverpool, Luis Diaz (pichani) ametekwa na waasi wa Chama cha National Liberation Army (ELN).Utekwaji wa Manuel Diaz ulifanyika Jumamosi ambapo waasi hao wakiwa na silaha walimteka akiwa na mkewe, Cilenis Marulanda ambaye aliachwa kwenye gari na waasi hao kutokomea na mumewe.Wanajeshi […]

The post ‘Baba wa Luis Diaz ametekwa na waasi’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barrancas, Colombia
Serikali ya Colombia imesema kuwa Manuel Díaz ambaye ni baba wa mchezaji wa Liverpool, Luis Diaz (pichani) ametekwa na waasi wa Chama cha National Liberation Army (ELN).
Utekwaji wa Manuel Diaz ulifanyika Jumamosi ambapo waasi hao wakiwa na silaha walimteka akiwa na mkewe, Cilenis Marulanda ambaye aliachwa kwenye gari na waasi hao kutokomea na mumewe.
Wanajeshi zaidi ya 120 pamoja na polisi walianzisha msako siku moja baada ya tukio hilo na mamlaka nchini Colombia zimeahidi kutoa Pauni 40,000 kwa mtu atakayewezesha kupatikana kwa baba wa Luis Diaz.
Awali taarifa ya polisi ilihusisha tukio hilo na makundi ya wahalifu lakini jana Alhamisi, serikali ambayo imekuwa katika mazungumzo ya amani na waasi wa ELN, ilidai kuwa ina taarifa za kundi hilo la waasi kuhusika na utekaji huo.
ELN ni kundi la waasi nchini Colombia ambalo limekuwa likijiendesha tangu mwaka 1964 na limekuwa vitani na serikali likidaiwa kuwa na wafuasi wapatao 2,500 na lina nguvu zaidi katika mji wa mpakani na Venezuela.
Manuel Diaz na mkewe walitekwa na watu waliokuwa na silaha katika mji wa La Guajira baada ya kusimama kwenye kituo cha mafuta na kamera za CCTV ziliwaonesha watekaji wakiwa kwenye pikipiki ambao walikuwa wakilifuatilia gari alilokuwa Manuel Diaz na mkewe.
Watekaji hao baadaye walilitelekeza gari likiwa na mama yake Luis Diaz wakati polisi wakiwakaribia lakini walitokomea na Manuel Diaz.
Msako dhidi ya watekaji unaendeshwa zaidi katika maeneo ya mpakani na Venezuela na tayari pikipiki mbili zimekamatwa pamoja na gari moja ambalo polisi wanadhani vilitumika katika utekaji ingawa bado hawajaweza kumpata baba wa Luis Diaz.
Jumanne iliyopita mamia ya watu waliandamana wakiwa na Cilenis Marulanda wakitaka Manuel Diaz aachiwe huru na waasi wakati Liverpool, klabu anayoichezea Luis Diaz ilitangaza kuwa ushindi wao wa mabao 3-0 dhidi ya Nottingham wanautoa kama heshima kwa Luis Diaz.

The post ‘Baba wa Luis Diaz ametekwa na waasi’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/03/baba-wa-luis-diaz-ametekwa-na-waasi/feed/ 0
Wanajeshi 120 Colombia wamsaka baba wa Luis Diaz https://www.greensports.co.tz/2023/10/30/wanajeshi-120-colombia-wamsaka-baba-wa-luis-diaz/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/30/wanajeshi-120-colombia-wamsaka-baba-wa-luis-diaz/#respond Mon, 30 Oct 2023 09:25:00 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8287 Barrancas, ColombiaWanajeshi zaidi ya 120 nchini Colombia wanaendesha operesheni kumsaka Luis Manuel Diaz ambaye ni baba wa mshambuliaji wa Liverpol, Luis Diaz (pchani) na tayari mamlaka zimetangaza kutoa Pauni 40,000 kwa atakayesaidia kupatikana kwa mzee huyo.Wanajeshi hao pamoja na polisi wameanza kufanya msako huo Kaskazini mwa Colombia kuanzia jana Jumapili wakimsaka baba wa mchezaji huyo […]

The post Wanajeshi 120 Colombia wamsaka baba wa Luis Diaz first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barrancas, Colombia
Wanajeshi zaidi ya 120 nchini Colombia wanaendesha operesheni kumsaka Luis Manuel Diaz ambaye ni baba wa mshambuliaji wa Liverpol, Luis Diaz (pchani) na tayari mamlaka zimetangaza kutoa Pauni 40,000 kwa atakayesaidia kupatikana kwa mzee huyo.
Wanajeshi hao pamoja na polisi wameanza kufanya msako huo Kaskazini mwa Colombia kuanzia jana Jumapili wakimsaka baba wa mchezaji huyo ambaye awali alitekwa yeye na mkewe aitwaye Cilenis Marulanda.
Baadaye Jumapili hiyo hiyo Cilenis ambaye ndiye mama wa Luis Diaz taarifa za kupatikana kwake zilitolewa ikidaiwa kwamba mama huyo alipatikana Jumamosi akiwa Barrancas.
Kutokana na tukio la kutekwa kwa wazazi wake, Luis Diaz, 26, aliikosa mechi ya Jumapili ambayo Liverpool ilicheza na Nottingham Forest na kutoka na ushindi wa mabao 3-0.
Taarifa ya jeshi ilieleza kuwa katika mpango wa kumsaka mzee huyo wameweka vizuizi barabarani huku wakitumia helikopta, ndege pamoja na rada katika zoezi hilo.
Mamlaka za kiserikali nchini Colombia hazijaweka wazi kwa undani kuhusu utekaji huo lakini vyombo vya habari nchini humo vilidai kwamba baba na mama wa Luis Diaz walitekwa wakiwa katika kituo kimoja cha mafuta mjini Barrancas.
Mwanasheria mkuu wa serikali nchini Colombia, Francisco Barbosa aliwasiliana na Luis Diaz mara mbili na kumpa taarifa za uchunguzi wa kutekwa kwa mzazi wake.
Barbosa alimwambia mchezaji huyo kuwa taarifa walizonazo ni kwamba kuna uwezekano baba yake yuko nchini Venezuela na hivyo watahitaji ushirikiano na mamlaka za nchini humo.
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp alisema kwamba ushindi wa mabao 3-0 walioupata katika mechi ya Ligi Kuu England (EPL) dhidi ya Nottingham Forest unakuwa heshima kwa Diaz.
Klabu ya Liverpool ilieleza kufahamu tukio hilo na katika mechi na Forest, mchezaji wa Liverpool, Diogo Jota akiwa amezungukwa na wachezaji wenzake aliinua juu jezi yenye namba 7 kama kuonesha mshikamano wao kwa Luis Diaz.

The post Wanajeshi 120 Colombia wamsaka baba wa Luis Diaz first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/30/wanajeshi-120-colombia-wamsaka-baba-wa-luis-diaz/feed/ 0