Lamine Yamal - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 19 Jul 2025 12:54:22 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Lamine Yamal - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Lamine abebeshwa zigo la Messi https://www.greensports.co.tz/2025/07/17/lamine-abebeshwa-zigo-la-messi/ https://www.greensports.co.tz/2025/07/17/lamine-abebeshwa-zigo-la-messi/#respond Thu, 17 Jul 2025 09:15:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13748 Barcelona, HispaniaWinga wa Barcelona, Lamine Yamal amewahi kukataa kufananishwa kwa vyovyote na Lionel Messi lakini sasa amelazimika kubebeshwa hadhi hiyo baada ya kukabidhiwa rasmi jezi namba 10 iliyokuwa ikivaliwa na mchezaji huyo.Klabu ya Barcelona au Barca imethibitisha hilo Jumatano hii, Julai 16, 2025 ikiwa ni siku tatu zimepita baada ya winga huyo kusherehekee miaka 18 […]

The post Lamine abebeshwa zigo la Messi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Winga wa Barcelona, Lamine Yamal amewahi kukataa kufananishwa kwa vyovyote na Lionel Messi lakini sasa amelazimika kubebeshwa hadhi hiyo baada ya kukabidhiwa rasmi jezi namba 10 iliyokuwa ikivaliwa na mchezaji huyo.
Klabu ya Barcelona au Barca imethibitisha hilo Jumatano hii, Julai 16, 2025 ikiwa ni siku tatu zimepita baada ya winga huyo kusherehekee miaka 18 tangu kuzaliwa kwake.
Yamal ataanza rasmi kuvaa jezi namba 10 mwanzoni mwa msimu mpya wa 2025-26 na kabla yake jezi hiyo ilikuwa ikivaliwa na Ansu Fati ambaye mapema mwezi huu alikamilisha taratibu za kujiunga na Monaco kwa mkopo.
Fati alikabidhiwa jezi namba 10 mwaka 2021 kutoka kwa Messi lakini tangu wakati huo amekuwa akiandamwa na janga la kuwa majeruhi na kushindwa kuwa na namba ya uhakika kwenye kikosi cha kwanza.
Tukio la kumkabidhi Yamal jezi namba 10 lilishuhudiwa na familia yake na kuunganishwa na hafla ya mchezaji huyo kupewa mkataba mpya ambao unafikia ukomo mwaka 2031.

“Nilipokuwa mtoto ndoto yangu ilikuwa kucheza kwa mara ya kwanza Barca, kukua na kucheza nikiwa na jezi namba 10, kila mtoto aliyezaliwa Barcelona ana ndoto hiyo, Messi amefanya yake, nami nitafanya yangu,” alisema Yamal.


Kabla ya hapo, Yamal alikuwa akivaa jezi namba 19 na kitendo cha kumkabidhi jezi yenye namba ya Messi kinamuacha mchezaji huyo katika mtihani wa kusaka mafanikio kama ya Messi.

Messi alianza kuivaa jezi namba 10 akiwa na Barca mwaka 2008 na hadi anaondoka mwaka 2021 na kujiunga na PSG, amefanikiwa kuacha alama ya kipekee ya mafanikio.
Miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na kubeba mataji manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, 10 ya La Liga, tuzo mbalimbali binafsi na rekodi ya kuwa mfungaji bora kinara wa wakati wote wa klabu hiyo.

The post Lamine abebeshwa zigo la Messi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/07/17/lamine-abebeshwa-zigo-la-messi/feed/ 0
Rashford atamani kucheza timu moja na Lamine Yamal https://www.greensports.co.tz/2025/06/23/rashford-atamani-kucheza-timu-moja-na-lamine-yamal/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/23/rashford-atamani-kucheza-timu-moja-na-lamine-yamal/#respond Mon, 23 Jun 2025 09:24:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13649 Manchestern, EnglandMshambuliaji wa Man United, Marcus Rashford ameelezea shauku yake ya kutaka siku moja acheze kwenye timu moja na mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lamine Yamal (pichani).Rashford, 27, amekuwa nje ya kikosi cha Man United kuanzia nusu ya msimu uliopita wa 2024-25 baada ya kuuzwa kwa mkopo katika klabu ya Aston Villa.Man United iliamua kumtoa Rashford […]

The post Rashford atamani kucheza timu moja na Lamine Yamal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Manchestern, England
Mshambuliaji wa Man United, Marcus Rashford ameelezea shauku yake ya kutaka siku moja acheze kwenye timu moja na mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lamine Yamal (pichani).
Rashford, 27, amekuwa nje ya kikosi cha Man United kuanzia nusu ya msimu uliopita wa 2024-25 baada ya kuuzwa kwa mkopo katika klabu ya Aston Villa.
Man United iliamua kumtoa Rashford baada ya mshambuliaji huyo kutokuwa na namba ya uhakika kikosi cha kwanza na zipo habari kwamba klabu hiyo sasa inasikilizia ofa kwa timu yoyote itakayomtaka wakati wowote kuanzia sasa.
Zimewahi kuwapo habari kwamba mchezaji huyo anatakiwa na klabu za Inter Milan, PSG, Barcelona, Juventus na hata Bayern Munich.
Akizungumza hivi karibuni kuhusu uwezekano wa kucheza kikosi kimoja na Yamal, Rashford alisema ndio na kufafanua kuwa kila mtu duniani anapenda kucheza na aliye bora.
Yamal licha ya kuwa na umri mdogo wa miaka 17 lakini ametokea kuwa mmoja wa wachezaji mahiri duniani na mchango wake umeonekana kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Hispania iliyobeba taji la Ulaya (Euro 2024) pamoja na Barcelona iliyobeba taji la La Liga msimu ulioisha hivi karibuni wa 2024-25.

“Ni vigumu kuzungumza kwa maneno kuhusu kile anachokifanya, hakutakiwa kufanya hicho wakati akiwa na miaka 16 na 17,” alisema Rashford.


Kwa sasa Rashford anasubiri kurudi Man United na kuanza rasmi mazoezi kujiandaa na msimu mpya wa 2025-26 kama mipango ya kuhama itagonga mwamba lakini akiwa Villa ameifungia timu hiyo mabao manne katika mechi 17 na tayari amerudishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya England na kocha Thomas Tuchel.

The post Rashford atamani kucheza timu moja na Lamine Yamal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/23/rashford-atamani-kucheza-timu-moja-na-lamine-yamal/feed/ 0
Xavi ampa nafasi kinda wa miaka 15 https://www.greensports.co.tz/2023/04/23/xavi-ampa-nafasi-kinda-wa-miaka-15/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/23/xavi-ampa-nafasi-kinda-wa-miaka-15/#respond Sun, 23 Apr 2023 13:39:30 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5918 Barcelona, HispaniaKocha wa Barca, Xavi Hernandez amesema winga wake nyota mwenye miaka 15, Lamine Yamal (pichani) hana woga na amemjumuisha kwenye kikosi kitakachocheza na Atletico Madrid leo Jumapili.Yamal ambaye ni zao la akademi ya La Masia inayomilikiwa na Barca, Julai mwaka huu atafikisha miaka 16, anatarajiwa kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi […]

The post Xavi ampa nafasi kinda wa miaka 15 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Kocha wa Barca, Xavi Hernandez amesema winga wake nyota mwenye miaka 15, Lamine Yamal (pichani) hana woga na amemjumuisha kwenye kikosi kitakachocheza na Atletico Madrid leo Jumapili.
Yamal ambaye ni zao la akademi ya La Masia inayomilikiwa na Barca, Julai mwaka huu atafikisha miaka 16, anatarajiwa kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuichezea timu kubwa ya Barca katika mechi rasmi.
“Ni mchezaji ambaye anaweza kutusaidia kwa sababu ana kipaji,” alisema Xavi akimzungumzia Yamal ambaye ana asili ya Morocco.
“Ana mambo mengi binafsi, ana kipaji, anaweza kuutumia vizuri mpira wa mwisho, anaongoza wachezaji, ana nguvu, tunamzungumzia mchezaji ambaye anaweza kuweka alama katika zama fulani kwenye klabu,” alisema Xavi.
Yamal, ambaye baba yake ana asili ya Morocco na mama yake anatokea Equatorial Guinea, alizaliwa Julai 13 mwaka 2007 na amekuwa kwenye kikosi cha akademi ya Barca tangu akiwa na miaka mitano.
Kama atacheza mechi ya leo dhidi ya Atletico, Yamal ataweka rekodi ya kucheza mechi hiyo rasmi akiwa na miaka 15 na siku 285.
Kwa sasa rekodi ya mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kucheza mechi rasmi katika klabu hiyo inashikiliwa na Armand Martinez Sagi ambaye alicheza mechi dhidi ya Real Gijon Aprili 2, 1922 akiwa na miaka 15, miezi 11 na siku tano.
Xavi ambaye pia ni zao la akademi ya Barca alisema kwamba ni vigumu kumlinganisha Yamal na wachezaji wengine.

“Ana kipaji cha pekee, ni kizazi kipya, tofauti iliyopo na zama zangu ni kwamba kwa sasa hawana uwoga, Yamal yuko tofauti, ana vitu vya wachezaji mbalimbali, sijaona ulingano wa moja kwa moja na yeyote,” aliongeza Xavi.


Barca inashika usukani La Liga kwa tofauti ya pointi nane dhidi ya Real Madrid iliyo nafasi ya pili ingawa hivi karibuni imekuwa na matokeo yasiyo ya kuridhidhisha ya mechi mbili mfululizo dhidi ya
Getafe na Girona zilizoisha kwa sare ya bila kufungana.

The post Xavi ampa nafasi kinda wa miaka 15 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/23/xavi-ampa-nafasi-kinda-wa-miaka-15/feed/ 0