KVZ - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 28 Apr 2025 05:40:44 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg KVZ - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Yanga yaitoa KVZ Kombe la Muungano https://www.greensports.co.tz/2025/04/27/yanga-yaitoa-kvz-kombe-la-muungano/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/27/yanga-yaitoa-kvz-kombe-la-muungano/#respond Sun, 27 Apr 2025 10:24:57 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13317 Na mwandishi wetuYanga wameanza vyema mbio za kulisaka Kombe la Muungano baada ya kuilaza KVZ mabao 2-0 mechi iliyochezwa Jumamosi hii, Aprili 26, 2025 kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.Kwa ushindi huo Yanga ambao pia ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu NBC wanakuwa wamefuzu moja kwa moja hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo inayoendelea visiwani […]

The post Yanga yaitoa KVZ Kombe la Muungano first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga wameanza vyema mbio za kulisaka Kombe la Muungano baada ya kuilaza KVZ mabao 2-0 mechi iliyochezwa Jumamosi hii, Aprili 26, 2025 kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.
Kwa ushindi huo Yanga ambao pia ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu NBC wanakuwa wamefuzu moja kwa moja hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo inayoendelea visiwani Zanzibar.
Yanga walianza kulichachafya mapema lango na KVZ kabla ya kuandika bao la kwanza katika dakika ya 27 lililofungwa na Stephane Aziz Ki kwa pasi ya Dennis Nkane.
Baada ya kutoa pasi iliyozaa bao, nyota ya Nkane iling’ara kwa mara nyingine katika dakika ya 86 alipoifungia Yanga bao la pili na la ushindi.
Katika mechi ya nusu fainali Yanga itacheza Jumanne ijayo na JKU ambayo ilifanikiwa kuitoa Singida Black Stars katika mechi nyingine ya robo fainali.
Mechi nyingine ya nusu fainali itapigwa Jumatatu kati ya Azam FC na Zimamoto ambayo ilifuzu hatua hiyo kwa kuitoa Coastal Union kwa bao 1-0 wakati Azam nayo iliitoa KMKM pia kwa bao 1-0.

The post Yanga yaitoa KVZ Kombe la Muungano first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/27/yanga-yaitoa-kvz-kombe-la-muungano/feed/ 0
KVZ yaigomea Yanga https://www.greensports.co.tz/2024/01/04/kvz-yaigomea-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/04/kvz-yaigomea-yanga/#respond Thu, 04 Jan 2024 19:41:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9169 Na mwandishi wetuYanga leo Alhamisi imeshindwa kutamba katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na KVZ, mechi iliyopigwa kwenye dimba la Amaan Complex.Hayo ni matokeo ya kwanza mabaya kwa Yanga katika michuano hiyo msimu huu baada ya kuweka rekodi ya kuichapa Jamhuri mabao 5-0 na kuilaza Jamus 2-1 katika […]

The post KVZ yaigomea Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga leo Alhamisi imeshindwa kutamba katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na KVZ, mechi iliyopigwa kwenye dimba la Amaan Complex.
Hayo ni matokeo ya kwanza mabaya kwa Yanga katika michuano hiyo msimu huu baada ya kuweka rekodi ya kuichapa Jamhuri mabao 5-0 na kuilaza Jamus 2-1 katika mechi zake mbili za kwanza.
Ikitumia baadhi ya wachezaji wake wapya na wale wa kikosi cha pili, Yanga ilipata tabu kuipenya ngome ya KVZ na kwa kipindi cha kwanza haikuweza kuonesha kuwa tishio mbele ya timu hiyo.
Yanga ilikianza kipindi cha pili kwa kuongeza nguvu ikiwaingiza, Augustine Okrah, Jesus Moloko na Kibwana Shomari kuchukua nafasi ya Maulid Tamila, Issack Emmanuel na Dennis Nkane.
Mabadiliko hayo bado hayakuweza kuisumbua ngome ya KVZ iliyoongozwa vyema na mlinda mlango, Bashir Darwesh na mabeki, Salum Khamis Gado, Idd Mgeni na Salum Athuman.
Dakika ya 58, Yanga ilipata pigo baada ya Okrah kuumia wakati akiuwahi mpira wa juu na kutolewa nje ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Farid Mussa.
Bado mabadiliko hayo hayakuweza kuipatia Yanga bao ingawa timu hiyo iliongeza uhai ikilisakama lango la KVZ mara kwa mara lakini ukuta imara wa timu hiyo ya Zanzibar uliendelea kuwa kikwazo kwa washambuliaji wa Yanga.
Katika dakika 20 za mwisho KVZ walianza kuja juu wakilisalama lango la Yanga kwa mashambulizi yaliyomuweka katika wakati mgumu kipa wa Yanga, Awesu Kassim na kuibua hofu kwa mashabiki wa timu hiyo.
Katika dakika za 75, 77 na 80, KVZ walionesha uhai kwa kucheza pasi za uhakika na kufika ndani ya eneo la 18 la Yanga lakini washambuliaji wa timu hiyo walikosa umakini na hivyo kushindwa kubadili matokeo.

The post KVZ yaigomea Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/04/kvz-yaigomea-yanga/feed/ 0