Klopp - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 12 Jul 2024 07:18:56 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Klopp - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Klopp atakiwa Ujerumani, Marekani https://www.greensports.co.tz/2024/07/12/klopp-atakiwa-ujerumani-marekani/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/12/klopp-atakiwa-ujerumani-marekani/#respond Fri, 12 Jul 2024 07:18:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11595 Berlin, UjerumaniTimu za taifa za Ujerumani na Marekani zinadaiwa kuanza mbio za kutaka kumuajiri kocha wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp.Ujerumani mwenyeji wa fainali za Euro 2024, tayari imetolewa katika fainali hizo na Klopp ambaye wamekuwa wakimuwinda kwa muda mrefu sasa ni wakati sahihi kwake kuchukua nafasi ya kocha Julian Nagelsmann.Klopp ambaye ni Mjerumani aliamua […]

The post Klopp atakiwa Ujerumani, Marekani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Berlin, Ujerumani
Timu za taifa za Ujerumani na Marekani zinadaiwa kuanza mbio za kutaka kumuajiri kocha wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp.
Ujerumani mwenyeji wa fainali za Euro 2024, tayari imetolewa katika fainali hizo na Klopp ambaye wamekuwa wakimuwinda kwa muda mrefu sasa ni wakati sahihi kwake kuchukua nafasi ya kocha Julian Nagelsmann.
Klopp ambaye ni Mjerumani aliamua kuachana na Liverpool mwishoni mwa msimu ulioisha hivi karibuni wa 2023-24, hadi sasa hajasema lolote kuhusu timu atakayojiunga nayo baada ya Liverpool.
Baada ya kuondoka Liverpool matarajio ya wengi ni kwamba kocha huyo alikuwa akielekea kujiunga na Bayern Munich ya Ujerumani kabla ya timu hiyo kumpa majukumu hayo Vincent Kompany.
Kwa upande wa Marekani, timu hiyo pia mambo yake si mazuri kwenye fainali za Copa America ambazo zinaendelea nchini humo na inaamini Klopp anafaa kuchukua nafasi ya Gregg Berhalter.

The post Klopp atakiwa Ujerumani, Marekani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/12/klopp-atakiwa-ujerumani-marekani/feed/ 0
Klopp awaaga mashabiki Liverpool https://www.greensports.co.tz/2024/05/20/klopp-awaaga-mashabiki-liverpool/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/20/klopp-awaaga-mashabiki-liverpool/#respond Mon, 20 May 2024 17:55:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11042 Liverpool, EnglandKocha wa Liverpool, Jurgen Klopp jana Jumapili aliwaaga mashabiki wa timu hiyo huku akiliimba jina la mrithi wake Arne Slot mbele ya mashabiki hao katika uwanja wa nyumbani wa Anfield.Klopp amekuwa na Liverpool kwa kipindi cha miaka minane na nusu, alihitimisha majukumu yake kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wolverhampton katika mechi ya […]

The post Klopp awaaga mashabiki Liverpool first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Liverpool, England
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp jana Jumapili aliwaaga mashabiki wa timu hiyo huku akiliimba jina la mrithi wake Arne Slot mbele ya mashabiki hao katika uwanja wa nyumbani wa Anfield.
Klopp amekuwa na Liverpool kwa kipindi cha miaka minane na nusu, alihitimisha majukumu yake kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wolverhampton katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu England (EPL) msimu wa 2023-24.
Mabao hayo yaliyofungwa katika kipindi cha kwanza na Alexis Mac Allister na Jarell Quansah pia yalihitimisha ushindi wa 305 kwa kocha huyo katika mechi 491 alizoiongoza Liverpool hadi sasa.
Slot aliyekuwa kocha wa timu ya Feyenoord ya Uholanzi alithibitishwa Ijumaa iliyopita kuwa ndiye atakayebeba mikoba ya Klopp ambaye alitangaza mapema kuwa hatoendelea na timu hiyo baada ya msimu huu.
“Kocha mpya, nataka muliimbe jina lake,” Klopp alisema kuwaambia mashabiki kabla ya kuendelea, kuwaimbisha kwa wimbo wenye ujumbe wa kumtaka Slot abebe majukumu akiwa kamili msimu mpya utakapoanza huku akimtaka ajiamini na asiache kufanya hivyo.

“Naona watu wengi wanalia, na mimi pia lakini mabadiliko ni jambo zuri, kama unakwenda na hulka sahihi na kila kitu kitakuwa sawa,” alisema Klopp.


Klopp alisema kuna wakati alikuwa katika kipindi kibaya lakini anashukuru Mungu si leo (Jumapili) badala yake anashukuru kwa yote yaliyotokea kwa kuwa unapokuwa vizuri unasahau hata yale yaliyobora na kuona ni ya kawaida.
Chini ya Klopp, Liverpool imefanikiwa kubeba mataji yote makubwa isipokuwa taji la Europa Ligi, na katika msimu wa 2019-20 walibeba taji la EPL na kufuta ukame wa miaka 30 tangu wabebe taji hilo mara ya mwisho.

The post Klopp awaaga mashabiki Liverpool first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/20/klopp-awaaga-mashabiki-liverpool/feed/ 0
Klopp, Salah wamaliza utata https://www.greensports.co.tz/2024/05/04/klopp-salah-wamaliza-utata/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/04/klopp-salah-wamaliza-utata/#respond Sat, 04 May 2024 18:57:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10839 Liverpool, EnglandKocha wa Liverpool, Jürgen Klopp amesema kwamba mzozo ulioibuka kati yake na mshambuliaji wake, Mohamed Salah mwishoni mwa wiki iliyopita katika mechi yao na West Ham haupo tena.Klopp na Salah walionekana katika picha za televisheni wakitoleana kauli zilizoashiria kuwapo mzozo baina yao wakati wa mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya mabao 2-2.Baada ya mechi […]

The post Klopp, Salah wamaliza utata first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Liverpool, England
Kocha wa Liverpool, Jürgen Klopp amesema kwamba mzozo ulioibuka kati yake na mshambuliaji wake, Mohamed Salah mwishoni mwa wiki iliyopita katika mechi yao na West Ham haupo tena.
Klopp na Salah walionekana katika picha za televisheni wakitoleana kauli zilizoashiria kuwapo mzozo baina yao wakati wa mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya mabao 2-2.
Baada ya mechi hiyo, Salah ambaye alizozana na kocha wake wakati akiingia uwanjani kutokea benchi, alisema kwamba ‘moto ungeweza kuwaka’ iwapo angeamua kuzungumza kilichojiri.
Katika mkutano na waandishi wa habari jana Ijumaa, Klopp hakutaka kuelezea kwa nini waliingia katika mzozo yeye na mchezaji wake badala yake alisisitiza kwamba jambo hilo limepita na kwa sasa wanaangalia mbele.

“Yote yamemalizwa, hakuna tatizo, kama tungekuwa hatujuani kwa muda mrefu sina hakika kama tungeweza kulifanyia kazi suala hilo, lakini tunajuana kwa muda mrefu na vile vile tunaheshimiana,” alisema Klopp.


Klopp alisisitiza kwamba hakuna tatizo na mambo ya aina hiyo wanaweza kuyamaliza wao wenyewe bila ya kuwapo matarajio ya kuingiliwa na watu wengine wa nje.
Sare dhidi ya West Ham imezidi kufifisha matumaini ya Liverpool kubeba taji la Ligi Kuu England (EPL) kwani kwa sasa inashika nafasi ya tatu ikiwa imeachwa na vinara Arsenal kwa tofauti ya pointi tano zikiwa zimebaki mechi tatu kabla ya kumalizika kwa ligi hiyo.

The post Klopp, Salah wamaliza utata first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/04/klopp-salah-wamaliza-utata/feed/ 0
Klopp, Salah hali si shwari https://www.greensports.co.tz/2024/04/28/klopp-salah-hali-si-shwari/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/28/klopp-salah-hali-si-shwari/#respond Sun, 28 Apr 2024 09:46:36 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10769 Liverpool, EnglandKocha wa Liverpool, Jurgen Klopp na mshambuliaji wake, Mohamed Salah inaonekana hawana uhusiano mzuri baada ya kuzozana jana Jumamosi katika mechi ya Ligi Kuu England (EPL) dhidi ya West Ham.Katika mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya mabao 2-2, Salah alionekana kama kutoleana maneno yasiyo mazuri na Klopp wakati akijiandaa kuingia uwanjani akitokea benchi katika […]

The post Klopp, Salah hali si shwari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Liverpool, England
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp na mshambuliaji wake, Mohamed Salah inaonekana hawana uhusiano mzuri baada ya kuzozana jana Jumamosi katika mechi ya Ligi Kuu England (EPL) dhidi ya West Ham.
Katika mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya mabao 2-2, Salah alionekana kama kutoleana maneno yasiyo mazuri na Klopp wakati akijiandaa kuingia uwanjani akitokea benchi katika dakika ya 79.
Klopp baadaye alisema kwamba hawezi kuweka wazi mzozo ulioibuka baina yake na mchezaji huyo ingawa kilicho wazi ni kwamba hali haikuwa shwari baina ya wawili hao.
Akizungumzia tukio hilo, mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Peter Crouch alisema kwamba halikuwa jambo zuri kwa timu hiyo.
“Salah ni mchezaji ambaye katika mechi nyingi za Liverpool amekuwa akianza tangu kipindi cha kwanza na atakuwa mwenye hasira kwa kuanzia benchi,” alisema Crouch na kuongeza kuwa hakuna mtu anayependa kuona jambo kama hilo kwa kocha na mchezaji wake muhimu.
Kilichoonekana kwa Salah ni kama vile alichukizwa na jambo aliloambiwa na Klopp wakati akijiandaa kuingia uwanjani na alitaka kuendeleza mzozo huo lakini wachezaji wenzake, Darwin Nunez na Joe Gomez waliingilia kati na kumlazimisha aondoke.

Salah baada ya mechi alisema kama angeamua kuzungumza ‘moto ungewaka’ wakati Klopp alisema kwamba suala hilo lilizungumzwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na limekwisha.
Sare hiyo ya mabao 2-2 iliyoipata Liverpool inazidi kuiweka timu hiyo pagumu kwenye mbio za kulisaka taji la EPL kwani inabaki katika nafasi yake ya tatu na inachoomba sasa ni Man City na Arsenal ziharibikiwe katika mechi zao.

The post Klopp, Salah hali si shwari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/28/klopp-salah-hali-si-shwari/feed/ 0
Klopp adai Liverpool imenyimwa penalti https://www.greensports.co.tz/2024/03/11/klopp-adai-liverpool-imenyimwa-penalti-2/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/11/klopp-adai-liverpool-imenyimwa-penalti-2/#respond Mon, 11 Mar 2024 05:49:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10129 Liverpool, EnglandKocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema timu yake imenyimwa penalti ya wazi kwa asilimia 100 katika mechi yao na Man City iliyoisha kwa sare ya bao 1-1 na kuhoji chakula alichokula mchana msimamizi wa VAR.Klopp ametoa kauli hiyo kuhusu mechi hiyo iliyopigwa jana Jumapili akihusisha rafu ya dakika za nyongeza aliyochezewa Alexis Mac Allister […]

The post Klopp adai Liverpool imenyimwa penalti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Liverpool, England
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema timu yake imenyimwa penalti ya wazi kwa asilimia 100 katika mechi yao na Man City iliyoisha kwa sare ya bao 1-1 na kuhoji chakula alichokula mchana msimamizi wa VAR.
Klopp ametoa kauli hiyo kuhusu mechi hiyo iliyopigwa jana Jumapili akihusisha rafu ya dakika za nyongeza aliyochezewa Alexis Mac Allister na Jeremy Doku wa Man City.
Man City ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kipindi cha kwanza mfungaji akiwa John Stones lakini Liverpool ilisawazisha kupitia kwa Mac Allister kwa penalti iliyotolewa baada ya kipa wa Man City kumchezea rafu Darwin Nunez.
Tukio ambalo Klopp amelilalamikia la kuinyima timu yake penalti lilipitiwa kwa kutumia VAR lakini hakuna penalti iliyotolewa kwa timu hiyo na mwamuzi wa kati hakupewa nafasi ya kulifanyia mapitio.
“Kwa nini jamaa wa chumba ch VAR anafikiri kwamba ile haikuwa penalti ya wazi na isiyo na shaka, nini hasa alichokuwa mchana,” alihoji Klopp.

“Ile ilikuwa penalti asilimia 100, wao (maofisa) watakuwa na ufafanuzi, ilikuwa faulo kwa asilimia 100 katika maeneo yote ya uwanja na pengine ingetolewa kadi ya njano, kuna mtu atalazimika kuniambia ni vipi haikuwa penalti,” alisema Klopp.


Alifafanua kuwa huenda Howard (Webb bosi wa waamuzi) atanipigia kesho na kuniambia samahani, kwa kuwa anaamini kuna mambo mawili yatakayotokea na yote hayawezi kubadili matokeo ya mchezo.
Klopp pia alisema kwamba pamoja na tukio hilo lakini jambo la kujivunia ni kwamba watu wataendelea kushuhudia soka la kuvutia ambalo tayari limeoneshwa na wachezaji wa timu yake.

The post Klopp adai Liverpool imenyimwa penalti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/11/klopp-adai-liverpool-imenyimwa-penalti-2/feed/ 0
Klopp ampamba Xabi Alonso https://www.greensports.co.tz/2024/02/17/klopp-ampamba-xabi-alonso/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/17/klopp-ampamba-xabi-alonso/#respond Sat, 17 Feb 2024 18:53:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9785 London, EnglandKocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amempongeza kocha wa Bayer Leverkusen ya Ujerumani, Xabi Alonso (pichani) akidai kuwa ni kocha wa kizazi kipya.Mwezi uliopita, Klopp alitangaza atang’atuka kuinoa Liverpool mwishoni mwa msimu huu na Alonso, kiungo wa zamani wa Liverpool aliyeichezea timu hiyo kati ya mwaka 2004 na 2009, jina lake linatajwa kuwa ni kocha […]

The post Klopp ampamba Xabi Alonso first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amempongeza kocha wa Bayer Leverkusen ya Ujerumani, Xabi Alonso (pichani) akidai kuwa ni kocha wa kizazi kipya.
Mwezi uliopita, Klopp alitangaza atang’atuka kuinoa Liverpool mwishoni mwa msimu huu na Alonso, kiungo wa zamani wa Liverpool aliyeichezea timu hiyo kati ya mwaka 2004 na 2009, jina lake linatajwa kuwa ni kocha anayefaa kumrithi Klopp.
Alonso, 42 ambaye pia ni kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania kwa sasa anainoa Leverkusen ambayo inashika usukani katika Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga ikiwa mbele ya vigogo Bayern Munich inayoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi tano.
Zaidi ya mafanikio hayo yanayoonekana kwenye Bundesliga, Alonso pia ameweka rekodi ya kucheza mechi 31 za mashindano yote bila kupoteza hata moja na hivyo amebakisha mechi moja kuweka rekodi iliyowahi kuwekwa na Bayern ya mechi 32 bila kupoteza.

“Xabi anafanya kazi nzuri, hili ni langu binafsi (halimhusishi na Liverpool) ni mchezaji wa zamani wa hadhi ya juu duniani na anayetokea katika familia ya ukocha jambo ambalo pia linasaidia, ni kama vile tayari alishakuwa kocha wakati akicheza soka,” alisema Klopp.


Alonso hata hivyo alipoulizwa juu ya uwezekano wa kumrithi Klopp katika klabu ya Liverpool, aliamua kujiweka kando na hoja hiyo akisema kwamba kwa sasa anaifikiria Leverkusen tu.
Akiwa mchezaji wa Liverpool, Alonso alibeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na FA na kazi ya ukocha katika kiwango cha juu aliianza Oktoba, 2022 katika klabu ya Leverkusen ambayo ameendelea kuwa nayo hadi sasa.

The post Klopp ampamba Xabi Alonso first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/17/klopp-ampamba-xabi-alonso/feed/ 0
Arteta, Klopp watajwa Barca https://www.greensports.co.tz/2024/01/30/arteta-klopp-watajwa-barca/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/30/arteta-klopp-watajwa-barca/#respond Tue, 30 Jan 2024 05:22:57 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9500 Barcelona, HispaniaKocha wa Arsenal, Mikel Ateta ni miongoni mwa makocha watatu wanaotajwa kuchukua nafasi ya Xavi wa Barca pamoja na Jurgen Klopp wa Liverpool na Julian Nagelsman wa timu ya taifa ya Ujerumani.Xavi ametangaza hivi karibuni kwamba ataachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu wa 2023-24 uamuzi ambao umeacha maswali ya nani atarithi mikoba […]

The post Arteta, Klopp watajwa Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Kocha wa Arsenal, Mikel Ateta ni miongoni mwa makocha watatu wanaotajwa kuchukua nafasi ya Xavi wa Barca pamoja na Jurgen Klopp wa Liverpool na Julian Nagelsman wa timu ya taifa ya Ujerumani.
Xavi ametangaza hivi karibuni kwamba ataachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu wa 2023-24 uamuzi ambao umeacha maswali ya nani atarithi mikoba ya kocha huyo.
Vyanzo mbalimbali vya habari vimemtaja Arteta kwamba huenda akaachana na Arsenal licha ya ukweli kwamba kuna ugumu kwani inaelezwa kuwa kocha huyo amepania kuipaisha Arsenal na haoneshi dalili zozote za kuwa tayari kuondoka katika timu hiyo.
Kwa upande wa Klopp ambaye naye ametangaza kuachana na Liverpool baada ya msimu huu haitoshangaza akienda Barca kwani amenukuliwa akisema kwamba hatoinoa timu nyingine yoyote ya England baada ya kuondoka Liverpool hivyo suala la kwenda Barca si la kulifuta moja kwa moja.


Klopp hata hivyo zipo habari kwamba anasubiriwa kwa hamu kwenye timu ya taifa ya Ujerumani ambako inaaminika mashabiki wengi wanaamini ana uwezo wa kuirejeshea heshima timu hiyo ambayo imekuwa ikipitia kipindi kigumu katika miaka ya karibuni.
Kuhusu Nagelsmann kilicho wazi ni kwamba mara baada ya fainali za Kombe la Ulaya 2024 au Euro 24 zitakazofanyika nchini Ujerumani kuanzia mwezi Juni mwaka huu, kocha huyo ataachana na timu hiyo na hivyo kuwa huru kujiunga na timu nyingine yoyote ikiwamo Barca..

The post Arteta, Klopp watajwa Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/30/arteta-klopp-watajwa-barca/feed/ 0
Klopp asubiriwa timu ya taifa Ujerumani https://www.greensports.co.tz/2024/01/28/klopp-asubiriwa-timu-ya-taifa-ujerumani/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/28/klopp-asubiriwa-timu-ya-taifa-ujerumani/#respond Sun, 28 Jan 2024 09:19:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9475 Berlin, UjerumaniUamuzi wa kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp kutangaza kuachana na timu hiyo baada ya msimu huu umepokewa vizuri na baadhi ya mashabiki wa soka Ujerumani wakiamini ndiye mtu sahihi kukabidhiwa timu yao ya taifa.Mtazamo huo unabebwa na mwenendo usio mzuri wa timu ya taifa ya Ujerumani kuanzia kwenye fainali za Kombe la Dunia za […]

The post Klopp asubiriwa timu ya taifa Ujerumani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Berlin, Ujerumani
Uamuzi wa kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp kutangaza kuachana na timu hiyo baada ya msimu huu umepokewa vizuri na baadhi ya mashabiki wa soka Ujerumani wakiamini ndiye mtu sahihi kukabidhiwa timu yao ya taifa.
Mtazamo huo unabebwa na mwenendo usio mzuri wa timu ya taifa ya Ujerumani kuanzia kwenye fainali za Kombe la Dunia za Qatar 2022 ambapo timu hiyo yenye heshima yake katika soka duniani iliaga fainali hizo mapema.
Uamuzi wa Klopp umeshangaza kwani umekuja wakati Liverpool ikionekana kuwa imara zaidi katika mbio za kulisaka taji la Ligi Kuu England (EPL) ikiwa ndiyo timu inayoshika usukani.
Hiyo ni baada ya kupitia kipindi cha msukosuko wa matokeo yasiyoridhisha lakini alivumilia na ajabu mambo yameanza kunyooka lakini kocha huyo ameamua kuja na uamuzi huo mgumu na ulioshangaza wengi.
Kiujumla Klopp ni kocha ambaye ameipa mafanikio makubwa Liverpool kuanzia kuipa taji la EPL, kuifikisha fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na safari hii ilitarajiwa angefikia hatua hiyo au hata kubeba mataji hayo mawili makubwa.
Mafanikio ya Liverpool chini ya Klopp ni mambo ambayo Wajerumani wamekuwa wakiyakosa kwenye timu yao ya taifa na katika hali ya kawaida kwa makocha wengi Wajerumani, jina la Klopp linaweza kuwa namba moja kati ya majina yanayofaa kukabidhwa kikosi cha Ujerumani.
Mashabiki Ujerumani wanadhani ni wakati sahihi kwa kocha huyo wa zamani wa Borussia Dortmund kuyahamishia mafanikio yaliyoonekana Liverpool kwenye timu ya taifa lake.
Hadithi ya Klopp kuhusishwa na timu ya taifa ya Ujerumani haijaanza sasa, ilikuwa hivyo Septemba mwaka jana baada ya Hansi Flick kutimuliwa kuinoa timu ya taifa.
Chama cha Soka Ujerumani (DFB) kiliamua kumkabidhi timu hiyo, Julian Nagelsmann, kocha wa zamani wa klabu za Bayern Munich na RB Leipzig ambaye pia baadhi ya mashabiki hawakuridhishwa na uteuzi wake.
Nagelsmann ambaye pia mwenendo wake na timu hiyo si wa kuridhisha, amesaini mkataba ambao utafikia ukomo baada ya fainali za Kombe la Ulaya 2024 (Euro 24) ambazo zitafanyika nchini Ujerumani kuanzia Juni mwaka huu.
Klopp ameshasema kwamba hatofundisha timu yoyote ya England zaidi ya Liverpool, na hapo ndipo swali linapokuja je atakwenda timu gani baada ya kuachana na Liverpool kama si timu yake ya taifa?

The post Klopp asubiriwa timu ya taifa Ujerumani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/28/klopp-asubiriwa-timu-ya-taifa-ujerumani/feed/ 0
Klopp atangaza kuondoka Liverpool https://www.greensports.co.tz/2024/01/26/klopp-atangaza-kuondoka-liverpool/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/26/klopp-atangaza-kuondoka-liverpool/#respond Fri, 26 Jan 2024 12:24:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9453 Liverpool, EnglandKocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ametangaza kuachana na timu hiyo mara baada ya msimu huu kwa kile alichosema kwamba ‘amechoka’.Klopp alijiunga na Liverpool Oktoba mwaka jana akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani na mkataba wake wa sasa na timu hiyo unafikia mwisho mwaka 2026 lakini ameamua kuachana na timu hiyo kabla ya mkataba kufikia mwisho.Akiwa […]

The post Klopp atangaza kuondoka Liverpool first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Liverpool, England
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ametangaza kuachana na timu hiyo mara baada ya msimu huu kwa kile alichosema kwamba ‘amechoka’.
Klopp alijiunga na Liverpool Oktoba mwaka jana akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani na mkataba wake wa sasa na timu hiyo unafikia mwisho mwaka 2026 lakini ameamua kuachana na timu hiyo kabla ya mkataba kufikia mwisho.
Akiwa na Liverpool, Klopp ameiwezesha timu hiyo kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2019 na taji la Ligi Kuu England (EPL) msimu wa 2019-20 ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kubeba taji hilo baada ya miaka 30.
Klopp mwenye umri wa miaka 56 na ambaye timu yake kwa sasa inashika usukani EPL, alisema alishauarifu uongozi wa klabu hiyo tangu Novemba mwaka jana na anaelewa kwamba uamuzi huo utawashtua wengi.
“Naelewa ni uamuzi unaoshitua watu wengi kwa wakati huu, pale unaposikia kwa mara ya kwanza lakini naweza kuelewa hilo au walau kujaribu kutoa ufafanuzi,” alisema Klopp.
“Napenda karibu kila kitu katika klabu hii, napenda kila kitu kuhusu jiji hili, napenda kila kitu kwa mashabiki wetu, naipenda timu, nawapenda maofisa, napenda kila kitu lakini bado nimeamua kuchukua uamuzi, hiyo ni kuwaonesha kwamba ni mimi mwenyewe ndiye niliyelazimika kuchukua uamuzi huu,” alisema Klopp.
“Hivyo ndivyo nilivyoamua, nawezaje kulisema hilo la kuishiwa nguvu, sina tatizo nilifahamu tangu awali kwamba kuna wakati nitalazimika kutangaza, lakini kwa sasa niko sawa,” alisema.

“Baada ya kuwa pamoja kwa miaka mingi na baada ya kushirikiana kwa muda mrefu na yale yote tuliyopitia pamoja, nimejenga heshima kwenu, mapenzi kwenu yamekuwa, huo ndio ukweli,” alisema Klopp.


Liverpool chini ya Klopp imefanikiwa kubeba karibu mataji yote makubwa kuanzia Ligi ya Mabingwa Ulaya, EPL, Uefa Super Cup na Kombe la Dunia la Fifa.

The post Klopp atangaza kuondoka Liverpool first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/26/klopp-atangaza-kuondoka-liverpool/feed/ 0
Klopp adai Liverpool imenyimwa penalti https://www.greensports.co.tz/2023/12/24/klopp-adai-liverpool-imenyimwa-penalti/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/24/klopp-adai-liverpool-imenyimwa-penalti/#respond Sun, 24 Dec 2023 12:45:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9003 London, EnglandKocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amemshutumu msimamizi wa VAR, David Coote kwa alichodai kuwa ni timu yake imenyimwa penalti katika mechi ya Ligi Kuu England (EPL) dhidi ya Arsenal iliyoisha kwa sare ya bao 1-1.Klopp ambaye timu yake kwa sasa inapambana vikali na Arsenal kuwania kushika usukani EPL, alisema walitakiwa kupewa penalti baada ya […]

The post Klopp adai Liverpool imenyimwa penalti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amemshutumu msimamizi wa VAR, David Coote kwa alichodai kuwa ni timu yake imenyimwa penalti katika mechi ya Ligi Kuu England (EPL) dhidi ya Arsenal iliyoisha kwa sare ya bao 1-1.
Klopp ambaye timu yake kwa sasa inapambana vikali na Arsenal kuwania kushika usukani EPL, alisema walitakiwa kupewa penalti baada ya Martin Odegaard kuunawa mpira katika mechi hiyo iliyopigwa jana Jumamosi.
Sare hiyo iliyopatikana kwa mabao ya Gabriel mapema dakika ya nne na kabla ya Mohamed Salah kuisawazishia Liverpool, yanaifanya Arsenal kula Krismasi ikiwa kileleni mwa msimamo wa EPL ikiidizi Liverpool kwa pointi moja.
Akizungumzia tukio hilo la dakika ya 19, Klopp alisema kwamba Odegaard alionekana akitumia mkono kuzuia mpira uliopigwa na Salah kwa kuunawa ndani ya eneo la 18.
Mwamuzi, Chris Kavanagh aliruhusu mpira kuendelea na hakukuwa na tukio la kusimamisha mpira ili kuangalia VAR huku Coote akidai kwamba Odegaard aliunawa mpira wakati akianguka.
“Ndio nimeona, nina hakika kabisa kwamba kuna mtu atakuja kunielezea ni kwa nini haikuwa mtu kuunawa mpira lakini sijui ni kwa namna ipi,” alisema Klopp.

“Siwezi kusema kwamba mwamuzi anaweza kuona kwa sababu sijui alikuwa wapi wakati wa tukio lile, lakini inawezekanaje mtu aliyekuwa ofisini aone kwa namna ile na asije na hitimisho labda kwa mwamuzi kuangalia kwa mara nyingine,” alisema Klopp.


Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, kocha wa Arsenal, Mikel Arteta alisema kwamba kulikuwa na maamuzi makubwa mawili ambayo hakuyaangalia kwa mara nyingine, matukio ambayo aliulizwa kabla lakini yote hakuyaangalia kwa mara nyingine.
Matokeo ya mechi za EPL jana Jumamosi…
West Ham 2-0 Man Utd
Fulham 0-2 Burnley
Luton 1-0 Newcastle
Nottm Forest 2-3 Bournemouth
Tottenham 2-1 Everton
Liverpool 1-1 Arsenal

The post Klopp adai Liverpool imenyimwa penalti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/24/klopp-adai-liverpool-imenyimwa-penalti/feed/ 0