Kevin de Bruyne - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 06 Apr 2025 18:58:28 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Kevin de Bruyne - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 De Bruyne aaga Man City https://www.greensports.co.tz/2025/04/04/de-bruyne-aaga-man-city/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/04/de-bruyne-aaga-man-city/#respond Fri, 04 Apr 2025 18:46:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13208 Manchester, EnglandKiungo wa Man Ciy, Kevin De Bruyne, 33, ametangaza kuwa ataachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu wa 2024-25 baada ya kumalizika kwa mkataba wake na klabu hiyo.De Bruyne (pichani) amekuwa mchezaji muhimu wa Man City tangu ajiunge na timu hiyo mwaka 2015 akitokea Wolfsburg ya Ujerumani na hadi sasa amebeba mataji 16 […]

The post De Bruyne aaga Man City first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kiungo wa Man Ciy, Kevin De Bruyne, 33, ametangaza kuwa ataachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu wa 2024-25 baada ya kumalizika kwa mkataba wake na klabu hiyo.
De Bruyne (pichani) amekuwa mchezaji muhimu wa Man City tangu ajiunge na timu hiyo mwaka 2015 akitokea Wolfsburg ya Ujerumani na hadi sasa amebeba mataji 16 likiwamo la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2023.
Kocha wa Man City, Pep Guardiola alisema De Bruyne ni kati ya viungo bora waliowahi kucheza soka England na haingekuwa rahisi kwake kumwambia kwamba hatoendelea kuichezea Man City.
De Bruyne ambaye pia ni kiungo wa timu ya taifa ya Ubelgiji ameifungia Man City mabao 106 katika mechi 413 ingawa msimu huu kidogo haukuwa mzuri kwake kwani ameanza kipindi cha kwanza mechi 19 tu.
“Iwe tunataka au hatutaki, huu ni wakati wa kusema kwaheri,” alisema De Brunye kupitia mitandao ya kijamii.
De Bruyne alisema soka limemfikisha kwa watu wa Manchester na jiji la Manchester na hakuwa na la kufanya zaidi ya kuifukuzia ndoto yake bila kufahamu kwamba kipindi chote hicho kilikuwa cha kubadili maisha yake.

“Hawa watu wamenipa kila kitu, nami sikuwa na la kufanya zaidi ya kujitoa kwa kila kitu, nini kilitokea…Tulishinda kila kitu,” alisema De Bruyne.


Alisema yeye na familia yake Man City kutaendelea kuwa nyumbani kwao na hawezi kutoa shukrani za kutosha kwa jiji, klabu na maofisa wa klabu, wachezaji wenzake, marafiki na familia kwa safari ya kipindi cha miaka 10.

The post De Bruyne aaga Man City first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/04/de-bruyne-aaga-man-city/feed/ 0
Pep: Sina ugomvi na De Bruyne https://www.greensports.co.tz/2024/12/04/pep-sina-ugomvi-na-de-bruyne/ https://www.greensports.co.tz/2024/12/04/pep-sina-ugomvi-na-de-bruyne/#respond Wed, 04 Dec 2024 06:40:18 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12327 Manchester, EnglandKocha wa Man City, Pep Guardiola amepuuza habari kwamba ana ugomvi na kiungo, Kevin de Bruyne badala yake amesema ana shauku kubwa kumuona nyota huyo akirejea katika ubora wake.Kiungo huyo mahiri amekuwa akiandamwa na janga la kuwa majeruhi na amecheza kuanzia kipindi cha kwanza katika mechi nne tu za Ligi Kuu England (EPL).Kwa ujumla […]

The post Pep: Sina ugomvi na De Bruyne first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Manchester, England
Kocha wa Man City, Pep Guardiola amepuuza habari kwamba ana ugomvi na kiungo, Kevin de Bruyne badala yake amesema ana shauku kubwa kumuona nyota huyo akirejea katika ubora wake.
Kiungo huyo mahiri amekuwa akiandamwa na janga la kuwa majeruhi na amecheza kuanzia kipindi cha kwanza katika mechi nne tu za Ligi Kuu England (EPL).
Kwa ujumla De Bruyne amecheza dakika 72 zikiwamo mechi tano ambazo ameingizwa akitokea benchi tangu kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki nane kutokana na kuandamwa na majanga ya kuwa majeruhi.
Katika mechi ya Man City na Liverpool iliyopigwa Jumapili na City kulala kwa mabao 2-0, De Bruyne aliingia dakika 12 za mwisho na kufanikiwa kutengeneza nafasi ambayo bado kidogo iipatie City bao.
Wachambuzi wawili wa soka ambao pia ni wanasoka wa zamani Jamie Carragher na Gary Neville wote wamehoji namna Pep anavyompa nafasi De Bruyne na kujiaminisha kwamba kuna tatizo baina ya wawili hao.
Katika kilichoonekana kama kujibu hoja hizo bila kuwataja majina, Pep amesema kwamba hakuna jambo lolote baya kati yake na De Bruyne.

“Kuna wanaosema kuna tatizo kati yangu na Kevin, mnadhani sitaki kumchezesha, sitaki Kevin acheze? Mtu ambaye ana kipaji, sikihitaji hicho kipaji, eti nina tatizo binafsi naye baada ya miaka tisa?” Alihoji Pep.


Pep alifafanua kwamba mchezaji huyo amempa mafanikio makubwa kwenye klabu ya Man City na ana shauku kubwa ya kumuona akirudi katika ubora wake.
“Lakini huyu amekuwa nje kwa miezi mitano akiwa majeruhi, na akaumia tena na kuwa nje kwa miezi miwili, ana miaka 33, anahitaji muda arudi katika ubora wake,” alisema Pep.
Mkataba wa De Bruyne na Man City utafikia ukomo Juni mwakani na mchezaji huyo amethibitisha kuwa hakuna mazungumzo yaliyofanyika hadi sasa kuhusu kumuongezea mkataba ingawa kwa sasa anachokipigania ni kurudi katika kiwango chake bora.

The post Pep: Sina ugomvi na De Bruyne first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/12/04/pep-sina-ugomvi-na-de-bruyne/feed/ 0
De Bruyne awataka mashabiki waache hasira https://www.greensports.co.tz/2024/06/27/de-bruyne-awataka-mashabiki-waache-hasira/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/27/de-bruyne-awataka-mashabiki-waache-hasira/#respond Thu, 27 Jun 2024 08:48:41 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11446 Stuttgart, UjerumaniKiungo wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Kevin De Bruyne amewataka mashabiki wa timu hiyo wenye hasira kuipa sapoti timu hiyo baada ya kuwazomea wakichukizwa na sare ya 0-0 dhidi ya Ukraine jana Jumatano.Ubelgiji hata hivyo imefuzu hatua ya mtoano kwenye Euro 2024 na Jumapili itaikabili Ufaransa mjini Dusseldorf, mechi ambayo itaamua timu ipi […]

The post De Bruyne awataka mashabiki waache hasira first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Stuttgart, Ujerumani
Kiungo wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Kevin De Bruyne amewataka mashabiki wa timu hiyo wenye hasira kuipa sapoti timu hiyo baada ya kuwazomea wakichukizwa na sare ya 0-0 dhidi ya Ukraine jana Jumatano.
Ubelgiji hata hivyo imefuzu hatua ya mtoano kwenye Euro 2024 na Jumapili itaikabili Ufaransa mjini Dusseldorf, mechi ambayo itaamua timu ipi iende robo fainali na De Bruyne amewataka mashabiki kuwaunga mkono katika mechi hiyo.
Mashabiki wa Ubelgiji pamoja na kufahamu kwamba timu yao imefuzu hatua ya mtoano lakini waliwazomea wachezaji kwa kuwa walitaka timu hiyo ishinde ili iwe kinara Kundi E.
Awali De Bruyne alijaribu kukabiliana na mashabiki hao lakini baadaye akaachana nao na kuwataka wachezaji wenzake waondoke baada ya zomeazomea kuongezekana wakati mchezji huyo akitajwa kuwa nyota wa mchezo huo.
“Tulijaribu kushinda mechi, tulikuwa na nafasi za kufunga magoli lakini hatukuwa tayari kujiweka katika mazingira hatarishi hasa katika mipira ya kona kwa sababu tulijua tungeweza kufungwa,” alisema De Bruyne.
De Bruyne hata hivyo alikiri kwamba ni aibu kwao kutofunga magoli kwa kuwa walikuwa na nafasi za kufanya hivyo na hali inapokuwa hivyo wanachohitaji ni mashabiki kuwa nao pamoja.

“Hawa mashabiki tunawahitaji, tutawahitaji katika mechi dhidi ya Ufaransa, hilo ndilo jambo pekee ninaloweza kulisema,” alisema De Bruyne.


Alipoulizwa ni kwanini aliwaambia wachezaji wenzake waondoke uwanjani na si kuzungumza na mshabiki wa Ubelgiji, De Bruyne aliishia kusisitiza umuhimu wa mashabiki katika timu yao kwenye mechi dhidi ya Ufaransa.
Ratiba ya mechi za mtoano Euro 2024
Switzerland v Italia (Jumamosi Juni, 29)
Ujeruman v Denmark (Jumamosi Juni, 29)
England v Slovakia (Jumapili Juni, 30)
Hispania v Georgia (Jumapili Juni 30)
Ufaransa v Ubelgiji (Jumatatu Julai 1)
Portugal v Slovenia (Jumatatu Julai 1)
Romania v Uholanzi (Jumanne Julai 2)
Austria v Uturuki (Jumanne Julai 2)

The post De Bruyne awataka mashabiki waache hasira first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/27/de-bruyne-awataka-mashabiki-waache-hasira/feed/ 0
De Bruyne awekwa kando Ubelgiji https://www.greensports.co.tz/2024/03/15/de-bruyne-awekwa-kando-ubelgiji/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/15/de-bruyne-awekwa-kando-ubelgiji/#respond Fri, 15 Mar 2024 07:33:05 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10196 Manchster, EnglandKiungo wa Man City, Kevin De Bruyne ameachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ubelgiji kwa kinachodaiwa kuwa ni kusumbuliwa na matatizo ya misuli.De Bruyne alijikuta akiwekwa kando kwa miezi mitatu mwanzoni mwa msimu huu kutokana na mataizo ya misuli na alirudi kuiwakilisha Man City kwa mara ya kwanza Januari mwaka huu.Mchezaji huyo […]

The post De Bruyne awekwa kando Ubelgiji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchster, England
Kiungo wa Man City, Kevin De Bruyne ameachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ubelgiji kwa kinachodaiwa kuwa ni kusumbuliwa na matatizo ya misuli.
De Bruyne alijikuta akiwekwa kando kwa miezi mitatu mwanzoni mwa msimu huu kutokana na mataizo ya misuli na alirudi kuiwakilisha Man City kwa mara ya kwanza Januari mwaka huu.
Mchezaji huyo sasa atazikosa mechi za timu ya taifa ya Ubelgiji dhidi ya Jamhuri ya Ireland pamoja na England zitakazopigwa wiki hii.
“Sina hakika kama ni matatizo ya misuli, ni matatizo mengine ambayo yamekuwa yakimpa tabu katika mechi kadhaa za hivi karibuni,” alisema kocha wa Ubelgiji, Domenico Tedesco katika mkutano wake na waandishi wa habari jana Alhamisi.

“Jana nilizungumza na daktari pamoja na Kevin na tukaamua hali hatarishi ni kubwa, ni jukumu letu kwa mchezaji lakini pia kwa klabu yake,” alisema Tedesco.


Kocha huyo alisema kwamba ni bora kumpa nafasi ya kupona vizuri akiwa Man City ili baadaye kuwa naye akiwa fiti kwenye fainali za Kombe la Ulaya 2024 au Euro 2024 zitakazoanza Juni mwaka huu nchini Ujerumani.
Tedesco ambaye ameongezewa mkataba hadi Julai 2026, alikabidhiwa jukumu la kuinoa timu ya Ubelgiji baada ya fainali za Kombe la Dunia 2022 akichukua nafasi ya Roberto Martinez na tangu apewe jukumu hilo, Ubelgiji haijapoteza hata mechi moja kati ya 10 zilizopita.
Kocha huyo ambaye ameiwezesha Ubelgiji kufuzu Euro 2024 kwa kishindo hata hivyo amekuwa haivi chungu kimoja na kipa tegemeo wa timu hiyo, Thibaut Courtois ambaye hayumo katika kikosi chake.
Kikosi cha Ubelgiji kilichotangazwa na Tedesco ni kama ifuatavyo…
Makipa: Arnaud Bodart, Matz Sels, Koen Casteels, na Thomas Kaminski.
Mabeki: Koni De Winter, Timothy Castagne, Zeno Debast, Wout Faes, Jan Vertonghen, Thomas Meunier na Arthur Theate.
Viungo: Arthur Vermeeren, Olivier Deman, Jérémy Doku, Dodi Lukébakio, Orel Mangala, Amadou Onana, Youri Tielemans na Aster Vranckx
Washambuliaji: Johan Bakayoko, Leandro Trossard, Michy Batshuayi, Charles De Ketelaere, Romelu Lukaku na Loïs Openda.

The post De Bruyne awekwa kando Ubelgiji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/15/de-bruyne-awekwa-kando-ubelgiji/feed/ 0
De Bruyne nje miezi minne https://www.greensports.co.tz/2023/08/16/de-bruyne-nje-miezi-minne/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/16/de-bruyne-nje-miezi-minne/#respond Wed, 16 Aug 2023 05:23:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7401 Manchester, EnglandKiungo wa Man City, Kevin de Bruyne atakuwa nje ya uwanja kwa takriban miezi minne wakati klabu yake ikiangalia kama atahitaji kufanyiwa upasuaji wa matatizo ya misuli yanayomkabili.De Bruyne aliumia Ijumaa iliyopita na kutoka nje ya uwanja huku akichechemea katika dakika ya 23 wakati Man City ikiumana na Burnley katika mechi ya kwanza ya […]

The post De Bruyne nje miezi minne first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kiungo wa Man City, Kevin de Bruyne atakuwa nje ya uwanja kwa takriban miezi minne wakati klabu yake ikiangalia kama atahitaji kufanyiwa upasuaji wa matatizo ya misuli yanayomkabili.
De Bruyne aliumia Ijumaa iliyopita na kutoka nje ya uwanja huku akichechemea katika dakika ya 23 wakati Man City ikiumana na Burnley katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England (EPL) msimu wa 2023-24.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32, pia aliumia na kutoka nje ya uwanja Juni mwaka huu katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Inter Milan, mechi ambayo Man City iliibuka na ushindi na kubeba taji hilo.
De Bruyne ambaye pia ni kiungo wa timu ya Taifa ya Ubelgiji, alizikosa mechi zote za Man City za maandalizi ya msimu wa 2023-24 kabla ya kurudi uwanjani kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Arsenal ambayo aliingia kipindi cha pili, mechi ambayo Man City ilishindwa kutamba.
“Ni maumivu makubwa, tunawajibika kuamua kama atahitaji kufanyiwa upasuaji au la, lakini atakuwa nje ya uwanja kwa miezi michache,” alisema kocha wa Man City, Pep Guardiola.
Pep ambaye pia alifafanua kwamba mchezaji huyo anasumbuliwa na tatizo lile lile la misuli, uamuzi wa kumfanyia upasuaji utajulikana siku chache zijazo ingawa aliweka wazi kuwa kwa hali ilivyo sasa, De Bruyne atakosekana uwanjani kwa miezi mitatu au minne.
Katika hatua nyingine, Pep pia alisema kwamba De Bruyne aliwahi kuwaambia mapema mwezi huu kwamba katika miezi miwili iliyopita alikuwa akicheza huku akiwa mwenye maumivu ya misuli ingawa kabla ya mechi na Burnley walichukua tahadhari zote.

“Ninachoweza kusema ni kwamba kuumia kwa Kevin ni pigo kwetu, tumepoteza kitu kikubwa, Kevin ana kiwango cha kipekee ambacho unaweza kukikosa kwa mechi moja au mbili lakini si kwa kipindi kirefu, hakika ni jambo gumu kwetu, ingawa pia tunatakiwa kuangalia mbele, tuna suluhisho japo mbinu na uwezo wa Kevin ni mambo yasiyo na mbadala,” alisema Pep.


Katika msimu uliopita wa 2022-23, ambao Man City ilibeba mataji matatu ya FA, EPL na Ligi ya Mabingwa Ulaya, De Bruyne aliifungia timu hiyo mabao 10 na kutoa asisti 31.

The post De Bruyne nje miezi minne first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/16/de-bruyne-nje-miezi-minne/feed/ 0
De Bruyne, Salah haooo Saudi Arabia https://www.greensports.co.tz/2023/08/07/de-bruyne-salah-haooo-saudi-arabia/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/07/de-bruyne-salah-haooo-saudi-arabia/#respond Mon, 07 Aug 2023 19:15:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7272 Riyadh, Saudi ArabiaKlabu ya Al-Ittihad ya Saudi Arabia inajiandaa kuwasilisha ofa ya Pauni 51 milioni kwa mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah wakati huo huo kukiwa na habari kuwa kiungo wa Man City, Kevin de Bruyne (pichani) naye anatakiwa nchini humo.Salah mwenye umri wa miaka 31, klabu ya Al-Ittihad ambayo pia imemsajili mshambuliaji wa zamani wa […]

The post De Bruyne, Salah haooo Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Riyadh, Saudi Arabia
Klabu ya Al-Ittihad ya Saudi Arabia inajiandaa kuwasilisha ofa ya Pauni 51 milioni kwa mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah wakati huo huo kukiwa na habari kuwa kiungo wa Man City, Kevin de Bruyne (pichani) naye anatakiwa nchini humo.
Salah mwenye umri wa miaka 31, klabu ya Al-Ittihad ambayo pia imemsajili mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid, Karim Benzema, inadaiwa kumuandalia Salah mkataba wa miaka miwili na malipo yanayofikia Pauni 155 milioni katika kipindi hicho.
Kuhusu De Bruyne mwenye umri wa miaka 32 ofa yake haijawekwa wazi lakini yumo katika hesabu za klabu hiyo kuhakikisha naye anaiacha Ligi Kuu England (EPL) na kuhamia Ligi Kuu Saudi Arabia.
Ikitokea mpango wa Salah kwenda Saudi Arabia utafanikiwa, mchezaji huyo pia atakuwa anaungana na nyota mwenzake wa zamani wa Liverpool, Sadio Mane ambaye msimu uliopita ulikuwa mgumu kwake katika klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani.
Mane amejiunga na Al-Nassr akitokea Bayern iliyomsajili kutoka Liverpool kabla ya kuanza msimu wa 2022-23. Winga wa zamani wa Real Madrid na Man United, Cristiano Ronaldo naye anaichezea timu hiyo
Kwa Salah ambaye pia ni mshambuliaji nyota wa timu ya Taifa ya Misri, hii itakuwa ofa ya pili kumtaka atoke Liverpool kwani PSG ya Ufaransa nayo inamtaka ikisubiri pesa za mauzo ya Kylian Mbappe ili iwe na jeuri ya kumnunua Salah.
Mpango wa De Bruyne ambaye pia anaichezea timu ya taifa ya Ubelgiji, haujawekwa wazi zaidi ya kuwapo habari kuwa naye yumo kwenye hesabu za wachezaji wanaotakiwa kuinogesha ligi ya Saudi Arabia.

The post De Bruyne, Salah haooo Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/07/de-bruyne-salah-haooo-saudi-arabia/feed/ 0
De Bruyne aibeba City ugenini https://www.greensports.co.tz/2023/05/10/de-bruyne-aibeba-city-ugenini/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/10/de-bruyne-aibeba-city-ugenini/#respond Wed, 10 May 2023 06:41:26 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6086 Madrid, HispaniaBao la Kevin de Bruyne limeiwezesha Man City kutoka sare ya ugenini ya bao 1-1 mbele ya Real Madrid katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.Matokeo hayo yaliyopatikana jana Jumanne yanakuwa mwanzo mzuri kwa City ambao watajipanga kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani Jumatano ijayo ili kupata ushindi katika mechi […]

The post De Bruyne aibeba City ugenini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Bao la Kevin de Bruyne limeiwezesha Man City kutoka sare ya ugenini ya bao 1-1 mbele ya Real Madrid katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Matokeo hayo yaliyopatikana jana Jumanne yanakuwa mwanzo mzuri kwa City ambao watajipanga kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani Jumatano ijayo ili kupata ushindi katika mechi ya marudiano na kufuzu hatua ya fainali kwa mara ya pili.
Iwapo azma hiyo ya City itafanikiwa, timu hiyo itakuwa na kibarua cha mwisho katika fainali kwa kuumana na timu mojawapo mahasimu wa Italia kati ya Inter au AC Milan ambazo zitaanza kuisaka tiketi hiyo leo Jumatano.
City pia itakuwa imejiweka vizuri katika mbio za kubeba mataji matatu msimu huu ikiwa vizuri kwenye mbio za kulibeba taji la Ligi Kuu England na Juni 3 itaumana na Man United katika mechi ya fainali ya Kombe la FA
Man City iliutawala vyema mchezo kipindi cha kwanza lakini kipa wa Real Madrid, Thibaut Courtois alikuwa makini na kuwanyima Rodri, Erling Haaland na De Bruyne nafasi za kuipatia City mabao.
Zikiwa zimebakia dakika 10 timu kwenda mapumziko, Vinicius Jr aliwageuzia kibao City na kuwapa raha mashabiki wa Real Madrid kwa bao alililofunga kwa shuti la umbali wa mita 25.
Dakika ya 67, De Bruyne naye alimaliza kazi kwa kufunga bao la kusawazisha na kuamsha shangwe kwa mashabiki wa City waliosafiri hadi Madrid.
Nusu fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya leo, Jumatano, Mei 10…
AC Milan v Inter Milan

The post De Bruyne aibeba City ugenini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/10/de-bruyne-aibeba-city-ugenini/feed/ 0
FA wachunguza kadhia ya De Bruyne https://www.greensports.co.tz/2023/02/17/fa-wachunguza-kadhia-ya-de-bruyne/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/17/fa-wachunguza-kadhia-ya-de-bruyne/#respond Fri, 17 Feb 2023 09:45:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5188 London, EnglandChama cha Soka England (FA), kimeanzisha uchunguzi baada ya mchezaji wa Man City, Kevin de Bruyne kurushiwa vitu uwanjani katika mechi na Arsenal ambayo City ilishinda kwa mabao 3-1.De Bruyne alikumbana na kadhia hiyo wakati akitoka uwanjani na inaaminika mwamuzi wa mchezo huo uliochezwa juzi Jumatano, Anthony Taylor amelitaja tukio hilo katika ripoti yake.Arsenal […]

The post FA wachunguza kadhia ya De Bruyne first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Chama cha Soka England (FA), kimeanzisha uchunguzi baada ya mchezaji wa Man City, Kevin de Bruyne kurushiwa vitu uwanjani katika mechi na Arsenal ambayo City ilishinda kwa mabao 3-1.
De Bruyne alikumbana na kadhia hiyo wakati akitoka uwanjani na inaaminika mwamuzi wa mchezo huo uliochezwa juzi Jumatano, Anthony Taylor amelitaja tukio hilo katika ripoti yake.
Arsenal wanachunguza tukio hilo kupitia picha za CCTV na kuahidi kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kuhusika. “Hili jambo halikubaliki na halivumiliki,” alisema msemaji wa Arsenal.
De Bruyne katika mechi hiyo alifunga goli na kutoa pasi iliyozaa goli na kuipa City matokeo ambayo yameifanya iiengue Arsenal kileleni ingawa timu hizo zinalingana kwa pointi zote zikiwa na pointi 51 City ikineemeka na idadi ya mabao ya kufunga na City imecheza mechi moja kuizidi Arsenal.
Katika kinachoonekana kudhihaki tukio hilo, De Bruyne alitupia picha yake kwenye mtandao wa kijamii ikiwa na maneno, ‘asanteni’ na nyingine yenye ujumbe unaozungumzia unywaji wa bia.

The post FA wachunguza kadhia ya De Bruyne first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/17/fa-wachunguza-kadhia-ya-de-bruyne/feed/ 0