Kaze - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 14 Jun 2023 15:00:32 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Kaze - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mikataba ya Nabi, Kaze kujadiliwa https://www.greensports.co.tz/2023/06/14/mikataba-ya-nabi-kaze-kujadiliwa/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/14/mikataba-ya-nabi-kaze-kujadiliwa/#respond Wed, 14 Jun 2023 15:00:19 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6594 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi na msaidizi wake Cedric Kaze kesho Alhamisi wanatarajia kukutana na uongozi wa timu hiyo kuendeleza mazungumzo ya kusaini mkataba mpya wa kukinoa kikosi hicho msimu ujao.Mikataba ya makocha hao na wengine wa benchi la ufundi imemalizika baada ya mchezo wa fainali wa Kombe la FA (ASFC) juzi […]

The post Mikataba ya Nabi, Kaze kujadiliwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi na msaidizi wake Cedric Kaze kesho Alhamisi wanatarajia kukutana na uongozi wa timu hiyo kuendeleza mazungumzo ya kusaini mkataba mpya wa kukinoa kikosi hicho msimu ujao.
Mikataba ya makocha hao na wengine wa benchi la ufundi imemalizika baada ya mchezo wa fainali wa Kombe la FA (ASFC) juzi mkoani Tanga ambapo Yanga ilibeba taji hilo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC.
Makamu Rais wa Yanga, Arafat Haji alieleza kuwa dhamira yao kubwa ni kuhakikisha wanawabakisha makocha hao kwa kuwaboreshea maslahi yao ili kuendeleza mafanikio ambayo wameyapata msimu huu.

“Tutakuwa viongozi wa ajabu kama tutawaacha makocha hawa waliotupa mafanikio kuondoka, tumeandaa ofa nono kwa ajili yao ikiwemo kuwapa mikataba mirefu ili tuendeleze mazuri waliyotupa msimu huu,” alisema Arafat.


Kiongozi huyo alieleza kuwa kabla ya msimu kuisha tayari walishaanza kuzungumza na makocha hao kuhusu kuongeza mkataba na mazungumzo yao yalifikia sehemu nzuri hivyo anaamini baada ya kikao cha kesho, mustakabali wa benchi la ufundi utajulikana.
Haji pia alisema kwamba katika kikao hicho wanatarajia kupokea ripoti nzima ya msimu uliopita pamoja na maboresho ya kikosi chao cha msimu unaokuja wa 2023/24.
Alifafanua kuwa dhamira yao ni kuhakikisha wanawabakisha kundini nyota wote pia walioisaidia timu yao kupata mafanikio waliyokuwa nayo na kusajili wachezaji wachache kwa ajili ya kuimarisha sehemu zilizokuwa na udhaifu.
Baadhi ya wachezaji ambao wanatajwa kusajiliwa na Yanga kwenye dirisha kubwa ni mshambuliaji Ranga Chivaviro kutoka Marumo Gallants ya Afrika Kusini na winga wa TP Mazembe ya DR Congo, Philipe Kinzumbi.

The post Mikataba ya Nabi, Kaze kujadiliwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/14/mikataba-ya-nabi-kaze-kujadiliwa/feed/ 0
Wachezaji Yanga washushwa presha https://www.greensports.co.tz/2023/05/26/wachezaji-yanga-washushwa-presha/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/26/wachezaji-yanga-washushwa-presha/#respond Fri, 26 May 2023 19:35:19 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6304 Na mwandishi wetuKocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema kwa sasa wanafanya kazi ya kupunguza presha ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa wachezaji wao ili watulize akili siku hiyo na kucheza kwa mipango waliyonayo. Kaze amesema kila kitu kinakwenda sawa na wachezaji wako vizuri isipokuwa wameamua kushughulika na presha hiyo ili kuhakikisha wanapata […]

The post Wachezaji Yanga washushwa presha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema kwa sasa wanafanya kazi ya kupunguza presha ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa wachezaji wao ili watulize akili siku hiyo na kucheza kwa mipango waliyonayo.


Kaze amesema kila kitu kinakwenda sawa na wachezaji wako vizuri isipokuwa wameamua kushughulika na presha hiyo ili kuhakikisha wanapata matokeo stahiki kwenye mechi ya kwanza ya fainali hiyo.
Yanga itaumana na USM Alger ya Algeria katika fainali ya kwanza kihistoria kwa Yanga ya michuano hiyo keshokutwa Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kabla ya mechi ya marudiano Juni 3, mwaka huu kwenye Uwanja wa Julai 5, 1962, Algiers.


“Tunaendelea vizuri, wachezaji wote wako vizuri, kitu kizuri ni fainali ya Kombe la Afrika, ni mara ya kwanza kwenye historia kila mtu amehamasika, haina haja ya hamasa zaidi kwa wachezaji, wanafahamu ni pakubwa hapa tulipofika.

“Lakini nafikiri kilichopo sasa ni kushusha kidogo kwanza presha kwa wachezaji, wasiipeleke hiyo presha uwanjani, tunapaswa kujiandaa kwa mchezo, tucheze vile tunavyocheza huku tukifahamu tunatakiwa kufanya vizuri na kuongeza kitu kwa ajili ya mechi ya marudiano na tunaamini kila kitu kitakwenda sawa hiyo Jumapili,” alisema Kaze.


Kocha huyo pia aliwataka mashabiki wa soka na Watanzania kwa ujumla kwenda uwanjani kwa wingi ili kuitumia faida ya uwanja wa nyumbani ipasavyo kwa kuwapa sapoti wachezaji wa Yanga kwa dakika zote 90 huku wakiwabughudhi wapinzani kwa shangilia yao.


Naye kocha wa USMA, Abdelhak Benchikha ambaye ametua na kikosi chake usiku wa kuamkia jana amesema wamekuja kulitetea taifa la Algeria huku akitaka kuweka heshima kwa makocha wazawa kwa kutwaa kombe hilo.


“Tumekuja si kama klabu tu bali pia kama taifa la Algeria lakini pia kuwapa heshima makocha wazawa kama mimi baada ya kuifikisha timu hapa ilipo. Tunaifahamu Yanga, tunafahamu wametupeleleza nasi pia tumewapeleleza lakini dakika 90 uwanjani ndio zitaamua,” alisema Benchikha raia wa Algeria.

The post Wachezaji Yanga washushwa presha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/26/wachezaji-yanga-washushwa-presha/feed/ 0
Kaze ataja walipoizidi Singida Big https://www.greensports.co.tz/2023/05/05/kaze-ataja-walipoizidi-singida-big/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/05/kaze-ataja-walipoizidi-singida-big/#respond Fri, 05 May 2023 12:41:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6027 Na mwandishi wetuKocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema siri ya ushindi wao dhidi ya Singida Big Stars ni wachezaji kucheza kwa kujitoa bila kujali uchovu waliokuwa nao kwa kucheza mechi mfululizo.Yanga juzi Jumatano ilikuwa ugenini Uwanja wa Liti, Singida na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Big Stars matokeo ambayo yamewafanya […]

The post Kaze ataja walipoizidi Singida Big first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema siri ya ushindi wao dhidi ya Singida Big Stars ni wachezaji kucheza kwa kujitoa bila kujali uchovu waliokuwa nao kwa kucheza mechi mfululizo.
Yanga juzi Jumatano ilikuwa ugenini Uwanja wa Liti, Singida na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Big Stars matokeo ambayo yamewafanya kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu NBC na sasa wanahitaji pointi tatu ili kutetea ubingwa ligi hiyo.
Kaze ameeleza kuwa mbali na wachezaji wao kucheza kwa kujituma lakini mbinu waliyotumia ya kupeleka mashambulizi ya kasi kwenye lango la wapinzani wao, imesaidia kumaliza mchezo huo mapema.

“Lengo letu lilikuwa ni kupata mabao ya haraka na mbinu tuliyoingia nayo ni kupiga mipira kwenye nafasi na wachezaji wetu wa pembeni kukimbia, hicho kiliwachanganya Singida na kufanikiwa kupata mabao hayo ambayo kwetu ni furaha sababu tumetimiza lengo,” alisema Kaze.


Kocha Mkuu wa Singida BS, Hans Pluijm kwa upande wake amekiri kuwa kipigo hicho kimetokana na kuzidiwa kimbinu na wapinzani wao, kitu ambacho kilisababisha waruhusu mabao mawili ya haraka.
“Hatukucheza kwenye kiwango kile ambacho tulitarajia, hata tulivyorudi kipindi cha pili tulijaribu kupambana kutafuta mabao ya kusawazisha lakini bado hatukuweza kucheza kwenye kiwango kile ambacho tulikitarajia,” alisema Pluijm.
Pluijm alisema wanayakubali matokeo hayo na wanarudi kujpanga ili kuhakikisha wanalipa kisasi kwa kushinda mchezo wa nusu fainali wa michuano ya Kombe la FA (ASFC) dhidi ya Yanga ambao utachezwa kwenye uwanja huo huo wa Liti.

The post Kaze ataja walipoizidi Singida Big first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/05/kaze-ataja-walipoizidi-singida-big/feed/ 0
Kaze: Mabao matano yametufanya tujiamini https://www.greensports.co.tz/2023/04/12/kaze-mabao-matano-yametufanya-tujiamini/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/12/kaze-mabao-matano-yametufanya-tujiamini/#respond Wed, 12 Apr 2023 19:25:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5788 Na mwandishi wetuKocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu NBC jana Jumanne umewapa nafasi ya kujiamini kuelekea mchezo wao na Simba utakaochezwa Jumapili hii.Kaze alisema katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, wachezaji walionesha kiwango cha juu na […]

The post Kaze: Mabao matano yametufanya tujiamini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu NBC jana Jumanne umewapa nafasi ya kujiamini kuelekea mchezo wao na Simba utakaochezwa Jumapili hii.
Kaze alisema katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, wachezaji walionesha kiwango cha juu na kila mmoja alikuwa vizuri kuhakikisha wanapata matokeo bora.
“Uwezo wa wachezaji kutaka mafanikio katika mchezo huo ulikuwa wa juu, kila mtu alikuwa anakimbia, anafanya kazi yake na kuonesha mahusiano mazuri baina ya mmoja kwenda mwingine, hii kwetu ni faida kuelekea mechi ijayo,” alisema.
Alisema kushinda mechi kuelekea mchezo dhidi ya mtani wao ni vizuri kwa sababu watafanya maandalizi kwa kujiamini wakitambua umuhimu wa mchezo huo ambao iwapo watashinda itawahakikishia nafasi ya kutetea taji la Ligi Kuu NBC.
Ingawa alisema mechi dhidi ya mtani mara nyingi haitabiriki kwa sababu unaweza kuwa bora ukafungwa hata kama mwenzako anashika nafasi ya saba au ya mwisho.


“Derby haitabiriki hata kama uko bora, ni mechi tofauti na nyingine. Ni muhimu kwetu kurudi kujipanga kwa ajili ya mchezo tukijua hautakuwa rahisi,” alisema Kaze.


Kwa upande wake, kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime aliwapongeza wapinzani wake Yanga akisema walistahili kushinda kwas ababu walicheza vizuri kuliko wao.
“Mpinzani alikuwa juu, tulizidiwa, tulitegewa mtego tukanasa tutarudi kujiandaa kuangalia mechi zilizobaki na kujipanga kufanya vizuri zaidi,” alisema.

The post Kaze: Mabao matano yametufanya tujiamini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/12/kaze-mabao-matano-yametufanya-tujiamini/feed/ 0
Kaze: Ratiba nzuri kwa Yanga https://www.greensports.co.tz/2022/08/04/kaze-ratiba-nzuri-kwa-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/04/kaze-ratiba-nzuri-kwa-yanga/#respond Thu, 04 Aug 2022 15:07:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2162 Na mwandishi wetuBenchi la Ufundi Yanga limeeleza kufurahishwa kwake na ratiba ya Ligi Kuu ya NBC iliyotolewa jana na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) kwa madai kuwa imekaa katika mkakati wao waliojiwekea kuelekea msimu ujao.Kocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema kwamba ratiba hiyo imekuwa kama ni faida kwao kwa kuwa wanaanza na timu ambazo […]

The post Kaze: Ratiba nzuri kwa Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Benchi la Ufundi Yanga limeeleza kufurahishwa kwake na ratiba ya Ligi Kuu ya NBC iliyotolewa jana na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) kwa madai kuwa imekaa katika mkakati wao waliojiwekea kuelekea msimu ujao.
Kocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema kwamba ratiba hiyo imekuwa kama ni faida kwao kwa kuwa wanaanza na timu ambazo zimekuwa zikiwasumbua hivyo ni vyema wakamalizana nazo mapema.
Katika ratiba hiyo, Yanga itaanza kampeni ya kutetea taji hilo kwa kucheza na Polisi Tanzania Uwanja
wa Ushirika, Moshi na baada ya hapo itacheza na Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kisha itarejea Dar es Salaam kuumana na Azam FC.
“Mechi hizo tatu ni kama fainali na dira kuelekea mbio za kutetea taji letu la Ligi Kuu, msimu uliopita timu zote tatu tulizifunga kwenye mechi zote mbili za ligi na Coastal tulicheza nao mara tatu zaidi ikiwemo mchezo wa fainali ya Kombe la FA, ni wazi hawatokubali kuendelea kupoteza dhidi yetu,” alisema Kaze.
Kocha huyo ameeleza kuwa pamoja na yote wamekiandaa kikosi chao kikamilifu kuhakikisha kinakabiliana na changamoto yoyote itakayojitokeza kwenye ligi sababu bado wana malengo ya kuendelea kutawala soka la Tanzania.
Kaze alisema wanachojivunia ni usajili mzuri ambao wameufanya kwenye dirisha kubwa na idadi kubwa ya wachezaji wao kukaa pamoja kwa muda mrefu, kitu ambacho hakijapoteza muunganiko wa timu yao.

The post Kaze: Ratiba nzuri kwa Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/04/kaze-ratiba-nzuri-kwa-yanga/feed/ 0