Kapombe - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 14 Mar 2023 05:58:39 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Kapombe - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Kapombe, Zimbwe Junior waachwa Stars https://www.greensports.co.tz/2023/03/13/kapombe-zimbwe-junior-waachwa-stars/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/13/kapombe-zimbwe-junior-waachwa-stars/#respond Mon, 13 Mar 2023 17:47:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5479 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche (pichani) ametangaza kikosi cha wachezaji 31 wa timu hiyo akiwaacha mabeki tegemeo wa Simba, Shomary Kapombe na Mohammed Hussein ‘Zimbwe Junior’.Kuachwa kwa mabeki hao ambao wamekuwa mhimili wa klabu ya Simba hadi kufikia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kumeacha maswali kwa mashabiki wengi […]

The post Kapombe, Zimbwe Junior waachwa Stars first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche (pichani) ametangaza kikosi cha wachezaji 31 wa timu hiyo akiwaacha mabeki tegemeo wa Simba, Shomary Kapombe na Mohammed Hussein ‘Zimbwe Junior’.
Kuachwa kwa mabeki hao ambao wamekuwa mhimili wa klabu ya Simba hadi kufikia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kumeacha maswali kwa mashabiki wengi wa soka.
Zimbwe mbali ya kuwa nahodha wa Simba pia amekuwa beki wa kushoto mwenye namba ya uhakika katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kama ilivyo kwa Kapombe anayecheza nafasi ya beki wa kulia.
Katika kikosi hicho pia yumo kiungo wa Yanga ambaye ana mgogoro na timu hiyo, Feisal Salum au Fei Toto ambaye hajaonekana kwenye mechi za ushindani kwa zaidi ya miezi miwili sasa akitaka kuvunja mkataba na timu hiyo.
Kwenye mitandao ya kijamii mashabiki walio wengi wanahoji kuachwa kwa Shomari na Zimbwe ambao mafanikio yao yamechangia kwa kiasi kikubwa hatua ambayo Simba imefikia hadi sasa kwenye Ligi ya Mabingwa.
Baadhi ya mashabiki mitandaoni pia wamehoji kama kikosi hicho ni chaguo la kocha mpya Amrouche aliyewahi pia kuinoa Harambee Stars ya Kenya kabla ya kuteuliwa hivi karibuni kuinoa Taifa Stars akimrithi Kim Paulsen aliyetimuliwa.
Stars inatarajia kucheza mechi mbili dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda au Uganda Cranes kuwania kufuzu Afcon 2023.
Kikosi kamili cha wachezaji wa timu hiyo na timu wanazotoka kwenye mabano ni kama ifuatavyo…
Aishi Manula (Simba), Beno Kakolanya (Simba) na Metacha Mnata (Yanga)
Wengine ni Kibwana Shomari (Yanga), Datius Peter (Kagera Sugar), Yahya Mbegu (Ihefu), David Luhende (Kagera Sugar), Dickson Job (Yanga), Bakari Mwamnyeto (Yanga) na Abdallah Mfuko (Kagera Sugar).
Pia wamo Ibrahim Baka (Yanga), Mudathir Yahya (Yanga), Sospeter Bajana (Azam), Muzamiru Yassin (Simba), Yusuph Kagoma (Singida BS), Ramadhan Makame (Bodrumspor-Uturuki) na Abdul Suleiman (Azam).
Wachezaji wengine ni Edmund John (Geita Gold), Feisal Salum (Yanga), Khalid Habibu (KMKM)
Anwar Jabir (Kagera Sugar), Simon Msuva (Al-Qadsiah-Saudi Arabia), Mbwana Samatta (KRC Genk-Ubelgiji), Novatus Dismas (Zulte Waragem-Ubelgiji) na Alphonce Mabula (FC Spartak Subotica-Ubelgiji).
Wengine ni Kelvin John (KRC Genk-Ubelgiji), Ben Starkie (Basford United-Uingereza), Haji Mnoga (Aldershot Town-Uingereza), Ally Msengi (Shallows-Afrika Kusini), Himid Mao (Ghazi El Mahala-Misri) na Said Hamis (Al Furjairah-UAE)

The post Kapombe, Zimbwe Junior waachwa Stars first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/13/kapombe-zimbwe-junior-waachwa-stars/feed/ 0