Kaluwa - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 01 Feb 2023 07:14:55 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Kaluwa - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Kaluwa: Nataka kuweka mambo sawa Simba https://www.greensports.co.tz/2023/02/01/kaluwa-nataka-kuweka-mambo-sawa-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/01/kaluwa-nataka-kuweka-mambo-sawa-simba/#respond Wed, 01 Feb 2023 07:10:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4936 Na mwandishi wetuAliyekuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Moses Kaluwa amefunguka kuwa hana mpango wa kuivuruga Simba kwa sababu ya kutoshinda kwenye uchaguzi.Badala yake Kaluwa amesema kwamba anachotaka ni kuweka sawa baadhi ya vitu kwa faida ya klabu hiyo kongwe Tanzania na hata Afrika.Kaluwa alishindwa na Murtaza Mangungu anayeendelea kuwa mwenyekiti […]

The post Kaluwa: Nataka kuweka mambo sawa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Moses Kaluwa amefunguka kuwa hana mpango wa kuivuruga Simba kwa sababu ya kutoshinda kwenye uchaguzi.
Badala yake Kaluwa amesema kwamba anachotaka ni kuweka sawa baadhi ya vitu kwa faida ya klabu hiyo kongwe Tanzania na hata Afrika.
Kaluwa alishindwa na Murtaza Mangungu anayeendelea kuwa mwenyekiti katika uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita jijini Dar es Salaam ambapo Mangungu alipata kura 1,311 dhidi ya 1,045 za Kaluwa.
Kaluwa ambaye hakusaini karatasi za matokeo ya uchaguzi huo alisema hakufanya hivyo si kwamba anataka kuleta migongano ndani ya Simba bali angependa kuona baadhi ya mambo yananyooka kwenye chaguzi zijazo za klabu hiyo.
“Siwezi kusema sijakubaliana na matokeo maana itakuwa ni suala la ugomvi na utengamano, ninachoamini ni kwenye Simba imara, hiyo ndiyo kitu namba moja kwamba inapaswa kuwa na Simba imara kuliko haya tunayosema.

“Haya yanarekebishika sababu niliyofanyiwa mimi sikuyapenda, yasijirudie na kwa kuwa sikuyapenda siyo lazima sasa niseme sikuyapenda lakini mwisho wa siku kutopenda kwangu sitaki kuwe na athari ya kudumu,” alisema Kaluwa.


Pia aliongeza kwamba alijaribu kuwashauri kamati ya uchaguzi kuhusu kutumia wino kwa wapiga kura ili kulinda haki za wapiga na wapigiwaji kura lakini ukatumika utaratibu wa kufunga karatasi mikononi ambao anadai haukufanya kazi zaidi ya kuvuruga uchaguzi huo kwa wengine kurudia kupiga kura.
Kaluwa pia alisema anaamini idadi iliyotangazwa kwa wapiga kura ilikuwa kubwa kuliko uhalisia wenyewe ingawa aliwapongeza Wanasimba kwa mwamko waliokuwa nao kujitokeza kutimiza haki yao ya msingi siku hiyo kwa kuwa wao ndiyo wenye maamuzi.
“Kulikuwa na mapungufu mengi, inabidi hii itushtue kwamba tunapokwenda tufanye maboresho. Sikusaini kuonesha sikuridhishwa na zile hatua na sitaki kuwa sehemu ya vurugu, nazungumza tu ukweli ili tujirekebishe kuwe na uchaguzi wa kweli kwa wapiga kura,” alisema Kaluwa.
Katika uchaguzi huo, Mangungu alishinda nafasi hiyo pamoja na wajumbe watano wa Bodi ya Wakurugenzi ambao ni Seif Muba, Asha Baraka, Issa Iddi, Rodney Chiduo na Seleman Harubu.

The post Kaluwa: Nataka kuweka mambo sawa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/01/kaluwa-nataka-kuweka-mambo-sawa-simba/feed/ 0