Jurgen Klinsmann - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 16 Mar 2026 16:33:05 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Jurgen Klinsmann - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Klinsmann akataa kujitenga Spurs https://www.greensports.co.tz/2026/03/12/klinsmann-akataa-kujitenga-spurs/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/12/klinsmann-akataa-kujitenga-spurs/#respond Thu, 12 Mar 2026 15:07:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14420 London, EnglandMshambuliaji wa zamani wa Tottenham Hotspur, Jurgen Klinsmann (pichani) amekataa kujiweka kando na uwezekano wa kuwa kocha wa timu hiyo wakati huu kocha wa sasa, Igor Tudor akipitia kipindi kigumu.Tudor amekuwa kocha wa Spurs tangu mwezi uliopita lakini matokeo mabaya ya kufungwa mechi nne mfululizo yaliyoiacha timu hiyo ikipambana na janga la kushuka daraja […]

The post Klinsmann akataa kujitenga Spurs first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Hotspur, Jurgen Klinsmann (pichani) amekataa kujiweka kando na uwezekano wa kuwa kocha wa timu hiyo wakati huu kocha wa sasa, Igor Tudor akipitia kipindi kigumu.
Tudor amekuwa kocha wa Spurs tangu mwezi uliopita lakini matokeo mabaya ya kufungwa mechi nne mfululizo yaliyoiacha timu hiyo ikipambana na janga la kushuka daraja yanaweza kumfanya atimuliwe kama alivyokuwa mtangulizi wake, Thomas Frank.
Mechi tisa zilizobaki za Ligi Kuu England ndizo zitakazoamua kama Spurs itabaki katika ligi hiyo kubwa barani Ulaya au itashuka, mazingira ambayo yanatoa picha kwamba nafasi ya kocha wa timu hiyo ipo njia panda.
Klinsmann ambaye enzi zake za kucheza soka la ushindani pia alikuwa akiichezea timu ya taifa ya Ujerumani, bado hajafanya mazungumzo yoyote na mabosi wa Spurs ingawa kwa sasa jina la Sean Dyche nalo limekuwa likitajwa.
Akiwa Spurs enzi zake, Klinsmann aliichezea timu hiyo mechi 68 na kufunga mabao 37, alipoulizwa kuhusu kuinoa timu hiyo alisema kwamba hakuna anayekataa kazi hiyo.

“Nani atakayeikataa kazi hiyo, yeyote utakayemchagua utahitaji mtu atakayekuwa kiunganishi kwa kila hali, mtu anayeijua klabu, ana mtazamo wa klabu na mwenye fikra za watu,” alisema Klinsmann.


Alisema kwamba kwa vyovyote itakavyokuwa ili kuondoka katika hali mbaya waliyopo ni lazima kujenga hali ya upambanaji wa nguvu na hilo ni lazima liwe katika fikra za watu.
Katika mazingira kama hayo, Klinsmann anaamini si suala la kuanza kutengeneza mbinu tu na yanayohusiana na hayo badala yake kila mtu kuingia vitani kupambana na kuwa katika msimamo chanya kukimbia uwezekano wa kushuka daraja.

The post Klinsmann akataa kujitenga Spurs first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/12/klinsmann-akataa-kujitenga-spurs/feed/ 0
Klinsmann atimuliwa Korea Kusini https://www.greensports.co.tz/2024/02/16/klinsmann-atimuliwa-korea-kusini/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/16/klinsmann-atimuliwa-korea-kusini/#respond Fri, 16 Feb 2024 19:14:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9765 Seoul, Korea KusiniKocha Jurgen Klinsmann aliyekuwa akiinoa timu ya taifa ya Korea Kusini, ametimuliwa katika nafasi hiyo ikiwa imepita miezi 12 tangu akabidhiwe jukumu hilo.Uamuzi wa Korea Kusini kumtimua Klinsmann unahusishwa moja kwa moja na hatua ya timu hiyo kuishia nusu fainali ya Kombe la Asia baada ya kushindwa kutamba mbele ya Jordan.Klinsmann, 59, alikabidhiwa […]

The post Klinsmann atimuliwa Korea Kusini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Seoul, Korea Kusini
Kocha Jurgen Klinsmann aliyekuwa akiinoa timu ya taifa ya Korea Kusini, ametimuliwa katika nafasi hiyo ikiwa imepita miezi 12 tangu akabidhiwe jukumu hilo.
Uamuzi wa Korea Kusini kumtimua Klinsmann unahusishwa moja kwa moja na hatua ya timu hiyo kuishia nusu fainali ya Kombe la Asia baada ya kushindwa kutamba mbele ya Jordan.
Klinsmann, 59, alikabidhiwa majukumu ya kuinoa timu hiyo Februari mwaka jana kwa mkataba ambao ulitarajiwa kufikia mwisho mwaka 2026 baada ya fainali za Kombe la Dunia.
Korea Kusini ambayo inahaha kwa zaidi ya miaka 60 ikiwania kubeba Kombe la Asia ilichukua uamuzi huo na chama cha soka cha nchi hiyo kiliweka wazi kutoridhishwa na aina ya uongozi wa Klinsmann na kwamba mabadiliko lilikuwa jambo muhimu.
Mashabiki na baadhi ya wanasiasa wa Korea Kusini mara baada ya timu hiyo kutolewa kwenye Kombe la Asia wamekuwa wakitaka kocha huyo atimuliwe huku kukiwa na madai ya ugomvi baina ya wachezaji wa timu hiyo.
Habari za ndani zinadai kuwa nahodha wa timu ya Korea Kusini, Son Heung-min aliumia kidole baada ya kutokea ugomvi na mchezaji mwenzake wakati wa chakula cha jioni kabla ya timu hiyo kupoteza mechi yake na Jordan.
Inaaminika kuwa malalamiko hayo ndiyo yaliyokishawishi Chama cha Soka Korea Kusini (KFA) kutangaza kuachana na kocha huyo kutoka Ujerumani, kocha ambaye iliaminika angekwenda na timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026.
Klinsmann pia alikuwa akilalamikiwa kwa kitendo chake cha kutopenda kuishi Korea Kusini badala yake alikuwa akitumia muda mwingi katika makazi yake California nchini Marekani wakati makocha wengine wa kigeni waliishi mjini Seoul.

The post Klinsmann atimuliwa Korea Kusini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/16/klinsmann-atimuliwa-korea-kusini/feed/ 0