Iran - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 15 Mar 2026 14:02:20 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Iran - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Iran ikikataa Kombe la Dunia, Trump awaita, atoa tahadhari https://www.greensports.co.tz/2026/03/15/iran-ikikataa-kombe-la-dunia-trump-awaita-atoa-tahadhari/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/15/iran-ikikataa-kombe-la-dunia-trump-awaita-atoa-tahadhari/#respond Sun, 15 Mar 2026 14:02:18 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14431 New York, MarekaniRais wa Marekani, Donald Trump amesema itakuwa sahihi kwa Iran kutoshiriki fainali za Kombe la Dunia 2026 kwa usalama wao na maisha yao wakati Iran wamedai kuwa sababu ya wao kutoshiriki fainali hizo ni Marekani.Katika andiko lake kupitia mitandao ya kijamii, Rais Trump alisema anaikaribisha Iran kwenye fainali hizo lakini hapo hapo akasema […]

The post Iran ikikataa Kombe la Dunia, Trump awaita, atoa tahadhari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Rais wa Marekani, Donald Trump amesema itakuwa sahihi kwa Iran kutoshiriki fainali za Kombe la Dunia 2026 kwa usalama wao na maisha yao wakati Iran wamedai kuwa sababu ya wao kutoshiriki fainali hizo ni Marekani.
Katika andiko lake kupitia mitandao ya kijamii, Rais Trump alisema anaikaribisha Iran kwenye fainali hizo lakini hapo hapo akasema kwamba anadhani hawapaswi kushiriki.
Kauli ya Trump imekuja baada ya Waziri wa Michezo na Vijana wa Iran, Ahmad Donyamali kusema kwamba nchi yake haiko katika nafasi ya kushiriki fainali hizo ambazo zitafanyika katika nchi za Marekani, Mexico na Canada kuanzia Juni 11 mwaka huu.
Katika fainali hizo Iran imepangwa kuanza mechi zake Juni 15 dhidi ya New Zealand na Juni 21 dhidi ya Ubelgiji zitakazopigwa mjini Los Angeles na kumalizia na mechi dhidi ya Misri itakayopigwa Juni 26 mjini Seattle.
Ushiriki wa timu ya Iran hata hivyo bado upo njia panda tangu Marekani na Israel waanze mashambulizi ya anga dhidi ya taifa hilo na kumuua kiongozi wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei.
Iran nayo ikajibu mapigo kwa kufanya mashambulizi kama hayo Israel na mengine katika nchi za Bahrain, Qatar, Kuwait na Umoja wa Falme za Kiarabu, nchi ambazo zina kambi za kijeshi za Marekani.

“Timu ya taifa ya soka ya Iran inakaribishwa kwenye Kombe la Dunia lakini kwa hakika siamini kama ni sahihi wao kuwa hapa, ni kwa usalama wao na maisha yao,” alisema Trump katika andiko lake.


Ujumbe wa Iran hata hivyo umekuwa tofauti kuhusu hoja hiyo ya Trump baada ya kudai kuwa waandaaji wa fainali za Kombe la Dunia ni Fifa (Shirikisho la Soka la Kimataifa) na si nchi yoyote.

“Timu ya taifa ya Iran pia imefuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia na hiyo ni baada ya kupata ushindi na kuwa moja ya timu za kwanza kufikia katika hatua hii muhimu,” ilieleza taarifa ya kutoka Iran.


Taarifa hiyo pia ilifafanua kwamba nchi ambayo inaweza kutolewa kwenye fainali za Kombe la Dunia ni ile ambayo imebeba hadhi ya kuwa nchi mwenyeji lakini haina uwezo wa kuzihakikishia usalama timu zinazoshiriki fainali hizo.
Awali Rais wa Fifa, Gianni Infantino alisema kwamba Rais Trump alimwambia kuwa Iran inakaribishwa kushiriki kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Wakati Infantino akitoa kauli hiyo, Waziri wa Michezo wa Iran alinukuliwa akisema kwa sababu serikali dhalimu imemuua kiongozi wao haoni kama wapo katika nafasi nzuri ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia.
Ikitokea Iran ikajitoa katika fainali hizo, kanuni za Fifa zinalipa shirikisho hilo nafasi ya kuchagua timu ya kushiriki badala ya Iran ingawa hadi sasa haijaweza kufahamika timu inayoweza kupewa nafasi hiyo.

The post Iran ikikataa Kombe la Dunia, Trump awaita, atoa tahadhari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/15/iran-ikikataa-kombe-la-dunia-trump-awaita-atoa-tahadhari/feed/ 0