Inzaghi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 11 Jun 2023 20:52:09 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Inzaghi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Inzaghi ajivunia Inter Milan https://www.greensports.co.tz/2023/06/11/inzaghi-ajivunia-inter-milan/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/11/inzaghi-ajivunia-inter-milan/#respond Sun, 11 Jun 2023 20:30:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6551 Istanbul, UturukiKocha wa Inter Milan, Simone Inzaghi amesema anajivunia mafanikio ya timu yake licha ya kushindwa kutamba mbele ya Man City katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jana Jumamosi.Inter Milan jana ililala kwa bao pekee la Man City lililofungwa na Rodri dakika ya 68 na kuifanya City ambayo pia ni kinara wa […]

The post Inzaghi ajivunia Inter Milan first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Istanbul, Uturuki
Kocha wa Inter Milan, Simone Inzaghi amesema anajivunia mafanikio ya timu yake licha ya kushindwa kutamba mbele ya Man City katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jana Jumamosi.
Inter Milan jana ililala kwa bao pekee la Man City lililofungwa na Rodri dakika ya 68 na kuifanya City ambayo pia ni kinara wa Ligi Kuu England (EPL) ibebe kwa mara ya kwanza taji la Ligi ya Mabingwa.
Inzaghi (pichani juu) hata hivyo hajakata tamaa na matokeo hayo akidai ameiongoza timu katika msimu mgumu uliojaa presha na hatimaye akaiwezesha kushika nafasi ya tatu katika Serie A na kubeba mataji ya Super Cup na Italia Cup.
“Usiku kama huu (Jumamosi) siwezi kuwataja wachezaji japo mmoja ambaye amecheza chini ya kiwango, nilisema jana (Ijumaa) sitoweza kumbadili mchezaji kwa yeyote na leo dunia nzima imeona ni kwa nini nilisema hivyo,” alisema Inzaghi.
“Wameoionyesha duniani yote ni kwa kiasi gani walivyoweza kuizuia Manchester City, kikosi ambacho kila mtu anajua kina wachezaji wa viwango vya juu,” alisema Inzaghi.
“Niliwakumbatia wachezaji wangu mmoja baada ya mwingine, kwani walikuwa wa kipekee ni kama jinsi mashabiki wetu walivyokuwa na walikuwa na haki ya kupata matokeo tofauti lakini ni matumaini yangu kwamba walikuwa na furaha kwa namna timu yetu ilivyocheza,” alisema Inzaghi.
“Mimi na wachezaji wangu tulikumbana na lawama na nikiri kwamba kuna mechi tulizopoteza ambazo hatukutakiwa kupoteza lakini nafikiri tulipata somo zuri katika mechi tulizopoteza,” alisema na kuongeza kuwa timu yake imeshinda mataji manne katika kipindi cha miaka miwili.

“Kwa ari, mshikamano na matumaini tuliyonayo, nafikiri tutakuwa katika hatua hii kwa mara nyingine siku zijazo,” aliongeza Inzaghi.


The post Inzaghi ajivunia Inter Milan first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/11/inzaghi-ajivunia-inter-milan/feed/ 0
Inzaghi azihofia Man City, Real Madrid https://www.greensports.co.tz/2023/05/17/inzaghi-azihofia-man-city-real-madrid/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/17/inzaghi-azihofia-man-city-real-madrid/#respond Wed, 17 May 2023 09:55:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6189 Milan, ItaliaBaada ya kufuzu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010, kocha wa Inter Milan, Simone Inzaghi sasa anamhofia mpinzani atakayekutana naye kwenye fainali kati ya Man City au Real Madrid.Inter jana Jumanne ilifuzu hatua ya fainali baada ya kuwalaza mahasimu wake AC Milan kwa bao 1-0 jana Jumanne […]

The post Inzaghi azihofia Man City, Real Madrid first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Milan, Italia
Baada ya kufuzu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010, kocha wa Inter Milan, Simone Inzaghi sasa anamhofia mpinzani atakayekutana naye kwenye fainali kati ya Man City au Real Madrid.
Inter jana Jumanne ilifuzu hatua ya fainali baada ya kuwalaza mahasimu wake AC Milan kwa bao 1-0 jana Jumanne na hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-0 baada ya ushindi wa mabao 2-0 katika mechi ya kwanza.
Timu hiyo sasa inasubiri kucheza fainali na mshindi wa mechi ya leo usiku kati ya Real Madrid au Man City itakayopigwa kwenye dimba la Ittihad baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya kwanza iliyopigwa kwenye dimba la Santiago Bernabeu.
Baada ya ushindi dhidi ya Inter Inzaghi (pichani juu) aliulizwa atapenda kukutana na timu ipi kati ya Man City na Real Madrid katika mechi ya fainali itakayopigwa Juni 10 mwaka huu kwenye dimba la Ataturk Olympic mjini Istanbul, Uturuki.
Kocha huyo hata hivyo hakutaka kuitaja kwa jina ni timu ipi ambayo itakuwa rahisi kwake badala yake alisema kwamba unapocheza na moja ya timu hizo wewe unaanza ukiwa timu ndogo.
“Ni jambo la kawaida unapoumana na City au Real kwanza unakuwa timu ndogo, lakini soka ni mchezo wa wazi, tulikutana na Real Madrid mwaka jana tukapoteza mechi mbili lakini tulicheza vizuri, Manchester City huhitaji kuwazungumzia, tutaona itakavyokuwa, yeyote atakayekuja ndio amekuja,” alisema Inzaghi.

“Yeyote tutakayekutana naye kwetu halitokuwa jambo zuri kwa sababu hizi ni timu mbili kubwa na zenye viwango vya kipekee, tutawaangalia hapo kesho (leo Jumatano), nitawaangalia kama vile naangalia mechi ya kwanza, ni dhahiri kwamba tutaifuatilia mechi yao kwa karibu,” aliongeza Inzaghi.


Man City inatarajia kutangazwa bingwa wa Ligi Kuu England (EPL) wikiendi hii iwapo Arsenal itapoteza mechi yake ya Jumamosi au City itashinda mechi yake ya Jumapili. Kwa upande wa Real Madrid imeshapoteza taji la La Liga ambalo limechukuliwa na mahasimu wao Barca.

The post Inzaghi azihofia Man City, Real Madrid first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/17/inzaghi-azihofia-man-city-real-madrid/feed/ 0