Ibra Class - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 26 Oct 2023 20:03:16 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Ibra Class - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Ibra Class amtangazia kichapo Mchina https://www.greensports.co.tz/2023/10/26/ibra-class-amtangazia-kichapo-mchina/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/26/ibra-class-amtangazia-kichapo-mchina/#respond Thu, 26 Oct 2023 20:03:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8242 Na mwandishi wetu Bondia Ibrahim Mgenda maarufu Ibra Class amesema amejipanga vizuri kumvaa Xiao Su wa China katika pambano la kuwania mkanda wa TPBC litakalofanyika keshokutwa Jumamosi kwenye Ukumbi wa PTA, Dar es Salaam. Akizungumza leo Alhamisi jijini Dar es Salaam, Class alisema anajua ugumu wa mpinzani wake lakini hamhofii kwani amefanya maandalizi ya muda […]

The post Ibra Class amtangazia kichapo Mchina first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Ibra Class.

Na mwandishi wetu

Bondia Ibrahim Mgenda maarufu Ibra Class amesema amejipanga vizuri kumvaa Xiao Su wa China katika pambano la kuwania mkanda wa TPBC litakalofanyika keshokutwa Jumamosi kwenye Ukumbi wa PTA, Dar es Salaam. Akizungumza leo Alhamisi jijini Dar es Salaam, Class alisema anajua ugumu wa mpinzani wake lakini hamhofii kwani amefanya maandalizi ya muda mrefu na kipigo kitakuwa pale pale, tayari kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania. “Nimefanya maandalizi mazuri katika kambi niliyoiweka mkoani Tanga na niko tayari kuwasha moto, namwambia Mchina kuwa hatoki salama lazima aondoke na kovu nitakalompa,” alisema Class. Class hajapoteza pambano lolote hivi karibuni, kiwango chake kikionekana kupanda kadri siku zinavyokwenda. Ni bondia anayeshika nafasi ya kwanza Tanzania katika uzito wa ‘super featherweight’ akiwa na nyota mbili na nusu. Amecheza mapambano 36 akiwa ameshinda 30 na kupoteza sita. Kwa upande wa mpinzani wake kutoka China, bondia huyo amecheza mapambano 15 na kati ya hayo, ameshinda 12 na kupoteza matatu.

The post Ibra Class amtangazia kichapo Mchina first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/26/ibra-class-amtangazia-kichapo-mchina/feed/ 0
Chino sasa amtaka Ibra Class https://www.greensports.co.tz/2023/09/30/chino-sasa-amtaka-ibra-class/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/30/chino-sasa-amtaka-ibra-class/#respond Sat, 30 Sep 2023 20:54:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7901 Na mwandishi wetuBaada ya Said Chino kufanikiwa kuibuka na ushindi wa TKO dhidi ya Mmalawi, Yobe Kamnyonya, bondia huyo amedai kuwa sasa anamuhitaji Ibrahim Mgenda ‘Ibra Class’ ili alipe kisasi.Chino aliyasema hayo baada ya pambano hilo lililodumu kwa raundi tatu katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam jana Ijumaa huku Class aliyekuwepo ukumbini hapo […]

The post Chino sasa amtaka Ibra Class first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Baada ya Said Chino kufanikiwa kuibuka na ushindi wa TKO dhidi ya Mmalawi, Yobe Kamnyonya, bondia huyo amedai kuwa sasa anamuhitaji Ibrahim Mgenda ‘Ibra Class’ ili alipe kisasi.
Chino aliyasema hayo baada ya pambano hilo lililodumu kwa raundi tatu katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam jana Ijumaa huku Class aliyekuwepo ukumbini hapo naye akijibu mapigo kuwa Chino bado ana uwezo mdogo.
Wawili hao walipambana Mei, mwaka huu na Class kuibuka na ushindi wa pointi 98-91, 97-92, 97-92, hivyo Chino anahitaji pambano la marudiano ili mpinzani wake huyo athibitishe ubingwa wake.
Aidha, Chino alianza kwa kueleza kuwa ilibidi ashinde pambano lake dhidi ya Kamnyonya kwani alimzidi vitu vingi mpinzani wake huyo ikiwemo akili na nguvu, hivyo lilikuwa ni suala la muda tu.

“Kwa sasa nimeongezeka zaidi uzoefu na ninahitaji mabondia ambao mnawaona ni wakali, mfano Class ananikimbia kimbia sana, mara ya kwanza alishinda kwa pointi, nahitaji kukutana naye tena athibitishe ubingwa wake na akinipiga mara ya pili, mwenyewe nitakubali,” alisema Chino.


Class alisema: “Yaani Chino wa sasa namuona bado sana kwa kweli, nitampiga hata raundi ya tatu hatoboi na nina uhakika na hilo, mara ya kwanza nilimwonesha ngumi zinapigwa vipi akamaliza raundi lakini sasa hivi nasema ukweli hafiki raundi ya tatu.”

The post Chino sasa amtaka Ibra Class first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/30/chino-sasa-amtaka-ibra-class/feed/ 0