Hersi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 24 Jun 2024 18:42:04 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Hersi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Hersi ampokea Hakimi Tanzania https://www.greensports.co.tz/2024/06/24/hersi-ampokea-hakimi-tanzania/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/24/hersi-ampokea-hakimi-tanzania/#respond Mon, 24 Jun 2024 18:42:00 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11412 Na mwandishi wetuRais wa Klabu ya Yanga, Hersi Said amempokea mgeni wake beki wa klabu ya PSG na timu ya Taifa ya Morocco, Achraf Hakimi leo Jumatatu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).Hakimi ambaye ni mchezaji bora wa PSG msimu wa 2023-24, ameelezwa kwamba atadumu Tanzania kwa muda wa wiki moja kwa […]

The post Hersi ampokea Hakimi Tanzania first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Klabu ya Yanga, Hersi Said amempokea mgeni wake beki wa klabu ya PSG na timu ya Taifa ya Morocco, Achraf Hakimi leo Jumatatu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Hakimi ambaye ni mchezaji bora wa PSG msimu wa 2023-24, ameelezwa kwamba atadumu Tanzania kwa muda wa wiki moja kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii.
Awali, Hersi alikutana na Hakimi nchini Ufaransa, Januari 3, mwaka huu baada ya kupata mwaliko maalumu kutoka kwa Rais wa Klabu ya PSG l, Nasser Al-Khelaifi.
Imefafanuliwa kuwa baada ya kukutana na Hakimi, Hersi alitumia nafasi hiyo kumshawishi mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid, Inter Milan na Borussia Dortmund kutembelea vivutio mbalimbali vya Tanzania.
Na sasa ushawishi huo umelipa, Hakimi ametua nchini akiwa na rafiki zake saba kwa ajili ya kufanya utalii huo.

The post Hersi ampokea Hakimi Tanzania first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/24/hersi-ampokea-hakimi-tanzania/feed/ 0
Hersi aweka mikakati ya robo fainali Afrika https://www.greensports.co.tz/2024/02/26/hersi-aweka-mikakati-ya-robo-fainali-afrika/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/26/hersi-aweka-mikakati-ya-robo-fainali-afrika/#respond Mon, 26 Feb 2024 18:42:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9889 Na mwandishi wetuRais wa Klabu ya Yanga, Hersi Saidi amesema mikakati yao kuelekea mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni kuongeza hamasa kwa wachezaji na benchi lao la ufundi kuzidi kufanya vizuri kwenye hatua hiyo.Yanga juzi Jumamosi ilikata tiketi ya kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa […]

The post Hersi aweka mikakati ya robo fainali Afrika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Klabu ya Yanga, Hersi Saidi amesema mikakati yao kuelekea mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni kuongeza hamasa kwa wachezaji na benchi lao la ufundi kuzidi kufanya vizuri kwenye hatua hiyo.
Yanga juzi Jumamosi ilikata tiketi ya kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria.
“Lengo letu ni kuwaongezea ari ya upambanaji wachezaji wetu. Awali lengo letu lilikuwa kufika makundi na wamefanya hivyo, na katika hatua hii, baada ya kuwajua wapinzani wetu tukasema tucheze na tutakubali matokeo yoyote, nafurahi kuona tumetinga robo fainali.
“Sasa baada ya kufika robo fainali, lengo letu ni kuongeza hamasa kwa wachezaji wetu na benchi la ufundi ili tushinde na hilo likitokea tutaongeza bonasi nyingine zaidi ya ilivyokuwa hatua zilizopita na ikishindikana hatuwezi kuwadai sababu hapa tulipofika tumevuka malengo tuliyokuwa tumejiwekea,” alisema.
Wakati Hersi akizungumza hayo, kocha mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi alisema kiu yake ni kuiona Yanga inafika mbali zaidi ya hapo na anaamini hilo linawezekana kutokana na ubora wa kikosi chake lakini pia ugumu waliokutana nao kwenye mechi za makundi.
“Tuna kikosi bora sana ambacho kama tukiongeza umakini tunaweza kufanya makubwa zaidi ya haya ingawa baadhi ya watu walitubeza baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Belouizdad kwao, najivunia sana ubora wa wachezaji wangu na sapoti ya mashabiki, miaka 25 kukaa bila kufika hapa si jambo dogo,” alisema Gamondi.
Yanga ambayo msimu uliopita ilitinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika imevuna kitita cha Dola za Marekani 900,000 ambazo ni sawa na Sh bilioni 2.4 baada ya kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.

The post Hersi aweka mikakati ya robo fainali Afrika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/26/hersi-aweka-mikakati-ya-robo-fainali-afrika/feed/ 0
Karimjee Group wamwaga milioni 300 Yanga https://www.greensports.co.tz/2024/02/23/yanga-yasaini-mkataba-wa-milioni-300/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/23/yanga-yasaini-mkataba-wa-milioni-300/#respond Fri, 23 Feb 2024 06:02:04 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9853 Na mwandishi wetuKlabu ya Yanga imesaini mkataba wa miezi 18 wenye thamani ya Sh milioni 300 na Kampuni ya Usafirishaji ya Karimjee Group, inayotengeneza pikipiki za Hero.Akizungumza Alhamisi hii kwenye hafla ya kutiliana saini mkataba huo iliyofanyika Makao Makuu ya klabu hiyo, Kariakoo, Dar es Salaam, Rais wa Yanga, Hersi Saidi alisema makubaliano hayo yanawapa […]

The post Karimjee Group wamwaga milioni 300 Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya Yanga imesaini mkataba wa miezi 18 wenye thamani ya Sh milioni 300 na Kampuni ya Usafirishaji ya Karimjee Group, inayotengeneza pikipiki za Hero.
Akizungumza Alhamisi hii kwenye hafla ya kutiliana saini mkataba huo iliyofanyika Makao Makuu ya klabu hiyo, Kariakoo, Dar es Salaam, Rais wa Yanga, Hersi Saidi alisema makubaliano hayo yanawapa fursa kutangaza bidhaa hiyo ndani na nje ya Tanzania.
Hersi alisema kwamba klabu ya Yanga inanufaika mara mbili katika mkataba huo, moja ni kiasi hicho cha fedha na mbili kupata kamisheni katika kila pikipiki itakayouzwa kupitia kwao.
“Nitoe wito kwa wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga, sasa hivi chapa yetu ya pikipiki kuanzia sasa ni Hero, ukiwa Mwanayanga pikipiki ya kupanda ni Hero, ukiwa dereva wa bodaboda pikipiki sahihi itakayoleta maslahi kwenye klabu yako ni Hero.

“Lakini pia ni bidhaa bora kabisa kutoka kwa kampuni kubwa ulimwenguni ya Hero, pikipiki hiyo pia itakwenda kukufanya wewe Mwanayanga uwe sehemu ya kuchangia maendeleo ya klabu yako lakini pia kuchangia tawi lako,” alisema Hersi.


Alisema watatengeneza kituo maalumu ambacho kitakuwa kinapokea oda za uuzaji wa pikipiki hizo na kitakuwa kinapokea mahitaji ya wanachama kupitia matawi na baada ya kupokea mahitaji hayo, tawi linatakiwa litaje jina la mteja anayetaka kununua na baada ya hapo tawi hilo litakuwa limeorodheshwa kupata kamisheni itakayowanufaisha.
Kwa upande wake, mkuu wa masoko kutoka Karimjee Group, Nada Vievi alisema pikipiki hizo zitakuja na bima kwa mteja pamoja na kofia mbili zenye nembo za Yanga.

The post Karimjee Group wamwaga milioni 300 Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/23/yanga-yasaini-mkataba-wa-milioni-300/feed/ 0
Hersi alipongeza benchi la ufundi https://www.greensports.co.tz/2024/02/15/hersi-alipongeza-benchi-la-ufundi/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/15/hersi-alipongeza-benchi-la-ufundi/#respond Thu, 15 Feb 2024 05:22:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9731 Na mwandishi wetuRais wa Klabu ya Yanga, Hersi Saidi amelipongeza benchi la ufundi pamoja na wachezaji wa timu hiyo kwa kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu NBC wakiwa vinara.Mabingwa hao watetezi wa ligi wamekamilisha mzunguko wa kwanza kwa kukusanya pointi 40 walizozipata katika michezo 15 ambapo kati ya hiyo wameshinda mechi 13, sare mechi […]

The post Hersi alipongeza benchi la ufundi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Klabu ya Yanga, Hersi Saidi amelipongeza benchi la ufundi pamoja na wachezaji wa timu hiyo kwa kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu NBC wakiwa vinara.
Mabingwa hao watetezi wa ligi wamekamilisha mzunguko wa kwanza kwa kukusanya pointi 40 walizozipata katika michezo 15 ambapo kati ya hiyo wameshinda mechi 13, sare mechi mmoja na kufungwa mara moja.
Akizungumza Dar es Salaam Jumatano hii, Hersi alisema matokeo hayo yametokana na uwekezaji mkubwa walioufanya kwenye kikosi chao ikiwemo kusajili wachezaji wenye ubora na viwango vya kimataifa.

“Mimi na viongozi wenzangu tunalipongeza benchi la ufundi chini ya kocha kuu Miguel Gamondi na wasaidizi wake lakini siwezi kuwasahau wachezaji ambao ndio watendaji wakuu, ukweli tunaona kazi yao na sisi kama uongozi tutaendelea kuwatengenezea mazingira mazuri ili watimize malengo,” alisema Hersi.


Kiongozi huyo alisema wamekuwa karibu na timu yao lengo likiwa ni kuendeleza mafanikio waliyoyapata kwenye misimu miwili iliyopita walipobeba mataji yote ya ndani na kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Alisema mikakati yao ni kuongeza kasi ya kupata matokeo mazuri kwenye mzunguko wa pili na kubeba taji hilo kwa mara ya tatu na kwa mwendo walionao anaamini hilo linaweza kutimia pasipo na shaka yoyote.
Kutokana na msimamo wa ligi ulivyo hivi sasa, Yanga inahitaji kushinda idadi kama hiyo ya mechi kwenye mzunguko wa pili ili kutetea taji hilo kwa msimu wa tatu mfululizo.

The post Hersi alipongeza benchi la ufundi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/15/hersi-alipongeza-benchi-la-ufundi/feed/ 0
Hersi ateta na rais wa PSG https://www.greensports.co.tz/2024/01/04/hersi-ateta-na-rais-wa-psg/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/04/hersi-ateta-na-rais-wa-psg/#respond Thu, 04 Jan 2024 17:46:40 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9163 Na mwandishi wetuRais wa Klabu ya Yanga na Mwenyekiti wa Vilabu Afrika, Hersi Said jana Jumatano, alikutana na Rais wa Klabu ya PSG ya Ufaransa, Nasser Al-Khelaifi na kujadili mambo kadhaa kuhusu uhusiano wao wa soka.Al-Khelaifi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vilabu Ulaya alikutana na Hersi baada ya kumpa mwaliko maalum ikiwamo kuhudhuria mechi ya […]

The post Hersi ateta na rais wa PSG first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Klabu ya Yanga na Mwenyekiti wa Vilabu Afrika, Hersi Said jana Jumatano, alikutana na Rais wa Klabu ya PSG ya Ufaransa, Nasser Al-Khelaifi na kujadili mambo kadhaa kuhusu uhusiano wao wa soka.
Al-Khelaifi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vilabu Ulaya alikutana na Hersi baada ya kumpa mwaliko maalum ikiwamo kuhudhuria mechi ya fainali ya Trophée des Champions iliyochezwa Uwanja wa Parc de Princes, ambapo PSG ilibeba ubingwa ikiichapa Toulouse mabao 2-0.
Pia, baada ya mchezo huo, Hersi alipata fursa ya kukutana na baadhi ya wachezaji nyota wa timu hiyo wakiwemo Marquinhos, Kylian Mbappe na Achraf Hakimi.
Taarifa ya mtandao wa Yanga imeripoti kuwa viongozi hao walipata wakati wa kujadiliana baadhi ya mambo ya soka kama vile jinsi vyama hivyo vikubwa vinavyoweza kujenga uhusiano mzuri wa kusaidia maendeleo ya klabu wanachama wa mabara ya Ulaya na Afrika.

“Hersi alipewa mualiko maalum kutoka Kwa ndugu Nasser Bin Ghanim Al-Khelaifi kwa lengo la kujadili jinsi vyama hivyo vikubwa vinavyoweza kujenga uhusiano mzuri utakaosaidia maendeleo ya vilabu wanachama,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo iliyowekwa leo Alhamisi kwenye vyanzo vya habari vya klabu ya Yanga.

The post Hersi ateta na rais wa PSG first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/04/hersi-ateta-na-rais-wa-psg/feed/ 0
CAF yampa ujumbe Hersi https://www.greensports.co.tz/2023/12/17/caf-yampa-ujumbe-hersi/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/17/caf-yampa-ujumbe-hersi/#respond Sun, 17 Dec 2023 17:05:31 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8910 Na mwandishi wetuShirikisho la Soka Afrika (CAF), limemteua Mwenyekiti wa Shirikisho cha Klabu Afrika (ACA) na Rais wa Yanga, Hersi Saidi kuwa mjumbe wa Kamati ya Maandalizi za Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) na Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan).Hayo yameelezwa Jumamosi hii na Rais wa TFF, Wallace Karia katika […]

The post CAF yampa ujumbe Hersi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limemteua Mwenyekiti wa Shirikisho cha Klabu Afrika (ACA) na Rais wa Yanga, Hersi Saidi kuwa mjumbe wa Kamati ya Maandalizi za Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) na Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan).
Hayo yameelezwa Jumamosi hii na Rais wa TFF, Wallace Karia katika mkutano mkuu wa mwaka wa shirikisho hilo unaofanyika mjini Iringa.
Karia alisema kuwa Hersi ameteuliwa kuingia katika kamati hiyo kwa vile ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF, nafasi aliyoipata baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa ACA takribani wiki mbili zilizopita.

“Kwa nafasi ya kuwa rais wa klabu Afrika, Hersi Saidi ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF na hivyo ameingia kwenye Kamati ya Maandalizi ya Chan na Afcon,” alisema Karia.


Hersi aliingia madarakani Yanga akirithi mikoba ya Dk Mshindo Msolla, ambapo katika uongozi wake amefanikiwa kuibadilisha timu hiyo kucheza soka la kisasa na ushindani wa hali ya juu huku ikiendelea kusajili wachezaji wenye viwango vya juu Afrika.

The post CAF yampa ujumbe Hersi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/17/caf-yampa-ujumbe-hersi/feed/ 0
Rage ampongeza Injinia Hersi https://www.greensports.co.tz/2023/12/02/rage-ampongeza-injinia-hersi/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/02/rage-ampongeza-injinia-hersi/#respond Sat, 02 Dec 2023 18:39:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8715 Na mwandishi wetuMwenyekiti wa zamani wa Simba SC, Aden Rage amempongeza Rais wa Yanga, Hersi Said kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Chama cha Klabu za Afrika (ACA).Rage baada ya pongezi hizo pia alisema kwamba klabu za Tanzania sasa zitafaidika mno na wadhifa wake huo mpya.Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumamosi, Rage alisema kwa namna […]

The post Rage ampongeza Injinia Hersi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mwenyekiti wa zamani wa Simba SC, Aden Rage amempongeza Rais wa Yanga, Hersi Said kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Chama cha Klabu za Afrika (ACA).
Rage baada ya pongezi hizo pia alisema kwamba klabu za Tanzania sasa zitafaidika mno na wadhifa wake huo mpya.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumamosi, Rage alisema kwa namna anavyomfahamu Hersi ni imani yake kwamba klabu za Tanzania bila kujali upinzani uliopo, zote zitafaidika na uwepo wa Hersi kwenye Shirikisho la Soka Afrika (Caf).
“Kwanza nimpongeze Injinia Hersi kwa kuchaguliwa kwa kishindo sababu kura zilikuwa 15, yeye akapata tisa kwa hiyo ni ushindi wa kujivunia na ni rekodi katika historia ya Tanzania.

“Bahati mbaya Watanzania wengi tunashindwa kufahamu kwamba unapopata Mtanzania anayeingia kwenye hizi taasisi za kimataifa kama Caf na Fifa unatakiwa ushukuru kwa kuwa ni bahati kwetu, nina imani ninavyomjua Hersi bila Yanga, Simba, Azam au klabu nyingine yoyote tutafaidika sana na uwepo wake mule,” alisema Rage.


Rage alisema kwa kuwa wadhifa huo unamfanya Hersi kuingia katika Kamati ya Utendaji ya Caf basi itakuwa rahisi kuwakilisha pia matatizo ya timu za ndani ya nchi yake na klabu zote Afrika zitafaidika kwa uwepo wa ACA.
Hersi alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho juzi katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa Marriot Mena House mjini Cairo, Misri pamoja na manaibu wake wawili; Jessica Mataung wa Kaizer Chiefs na Paul Basset wa Akwa United.

The post Rage ampongeza Injinia Hersi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/02/rage-ampongeza-injinia-hersi/feed/ 0
Wachezaji Yanga waahidiwa milioni 200 https://www.greensports.co.tz/2023/08/13/wachezaji-yanga-waahidiwa-milioni-200/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/13/wachezaji-yanga-waahidiwa-milioni-200/#respond Sun, 13 Aug 2023 00:25:21 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7350 Na mwandishi wetuRais wa Klabu ya Yanga, Hersi Said ameahidi kutoa Sh milioni 200, kwa wachezaji na benchi la ufundi endapo watashinda mchezo wa fainali wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani zao Simba SC.Mchezo huo wa fainali unatarajia kuchezwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kuanzia saa moja jioni na hiyo ni baada […]

The post Wachezaji Yanga waahidiwa milioni 200 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Klabu ya Yanga, Hersi Said ameahidi kutoa Sh milioni 200, kwa wachezaji na benchi la ufundi endapo watashinda mchezo wa fainali wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani zao Simba SC.
Mchezo huo wa fainali unatarajia kuchezwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kuanzia saa moja jioni na hiyo ni baada ya timu hizo kuibuka washindi katika mechi za nusu fainali.
Yanga iliifunga Azam mabao 2-0 wakati Simba iliiondosha Singida Fountain Gate kwa penalti 4-2 baada ya matokeo ya suluhu kwenye dakika 90 za awali.
Akizungumza na mtandao wa timu hiyo, Hersi alisema ameamua kutoa ofa hiyo kama hamasa kwa wachezaji wake ili wazidi kujituma na kulitetea taji hilo ambalo wanalishikilia kwa mara ya pili mfululizo.

“Uongozi kwa pamoja tumekubaliana kutoa ofa hiyo kwa wachezaji wetu nadhani hiyo itawaongezea hamasa hata wachezaji wageni na kuzidi kujituma kwa ajili ya kuipigania timu na maslahi yao kwa ujumla,” alisema Hersi.


Kiongozi huyo alisema mpaka sasa wanafurahishwa na mwanzo mzuri wa benchi lao jipya la ufundi chini ya kocha Miguel Gamondi na wasaidizi wake na imani yao ni kwamba ubora wanaouonesha kwenye mechi hizo za Ngao ya Jamii hautoishia hapo.
Alisema wao kama viongozi watahakikisha wanakuwa karibu na timu yao na kutimiza vyema majukumu yao ili kuhakikisha malengo yao ya kutetea mataji yote ya ndani wanayatimiza na kufika angalau hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

The post Wachezaji Yanga waahidiwa milioni 200 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/13/wachezaji-yanga-waahidiwa-milioni-200/feed/ 0
Fei Toto amgeuzia kibao Rais Yanga https://www.greensports.co.tz/2023/06/01/fei-toto-amgeuzia-kibao-rais-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/01/fei-toto-amgeuzia-kibao-rais-yanga/#respond Thu, 01 Jun 2023 19:17:30 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6423 Na mwandishi wetuKiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema manyanyaso ni kikwazo kikuu cha yeye kuondoka kwenye klabu hiyo lakini akasema endapo Rais wa Yanga, Hersi Said akiachia ngazi basi muda huohuo atarejea kuendelea na klabu hiyo.Kauli hiyo pamoja na mengine aliyofunguka ameitoa leo Alhamisi kwenye mahojiano na kipindi cha Power Breakfast cha redio […]

The post Fei Toto amgeuzia kibao Rais Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema manyanyaso ni kikwazo kikuu cha yeye kuondoka kwenye klabu hiyo lakini akasema endapo Rais wa Yanga, Hersi Said akiachia ngazi basi muda huohuo atarejea kuendelea na klabu hiyo.
Kauli hiyo pamoja na mengine aliyofunguka ameitoa leo Alhamisi kwenye mahojiano na kipindi cha Power Breakfast cha redio Clouds.
“Mashabiki wa Yanga nawapenda na nimechezea timu kwa jasho na kujitoa lakini hawajui kilichonitoa Yanga maana wanaaminishwa sivyo na mimi niliondoka kwa sababu ya manyanyaso na imefikia hatua nikasema bora niondoke niwape stahiki zao niondoke,” alisema.
Alisema Yanga ni taasisi kubwa na yeye ana mapenzi nayo ila hana ugomvi na Yanga bali tatizo lake kubwa ni Hersi ambaye anadai aliwahi kuzungumza naye kwa masaa sita lakini hakukuwa na mwafaka.

“Niliambiwa nauza mechi na baadhi ya viongozi na kuna mtu ndani ya viongozi alikuwa ananiambia lakini nikimpigia simu hapokei wala jumbe zangu hazijibu lakini baadaye wanakuja wanamdhalilisha mama yangu ambaye ni pepo yangu na kumtukana, hivi ingekuwa wewe mama yako anatukanwa ungejisikiaje?,” alihoji Fei.


Anasema mama yake ndiyo alimsihi kuvumilia kipindi anakaa miezi mitatu hadi minne bila mshahara na yeye akawa anampa pesa za matumizi na kumwambia avumilie maana mama yake ni shabiki wa Yanga.
Alisema hata kauli aliyosikika akiisema mama yake ya kuhusu kula ugali na sukari ni mapito ambayo aliyapitia kabla ya udhamini wa sasa wa GSM.
Kuhusu mkataba wa sasa, Fei alisema walizungumza kuongeza mkataba na walizungumzia mkataba wa miaka miwili lakini anashangaa amekuja kusaini mkataba wenye lugha ya Kiingereza wa miaka mitatu.
Pia alifafanua kwamba si kweli pesa ya Sh milioni 100 ya ada ya usajili aliipata kwa kipindi kifupi, kwani ilimchukua muda zaidi ya mwaka kukamilishiwa pesa hizo.


Hersi alipokuwa kwenye mahojiano na kituo hicho wiki iliyopita alieleza kuwa wao hawana tatizo na Fei, akimsifia ni kijana mwenye nidhamu na zaidi wamempa maamuzi matatu ya kurudi kutumikia mkataba wake au warejee mezani kuboresha maslahi yake au klabu inayomtaka Fei iende mezani kuzungumza na Yanga na wao wako tayari kujadili dili hilo.
Fei na Yanga wameingia kwenye mgogoro tangu Desemba, mwaka jana mchezaji huyo aliporejesha kiasi cha Sh milioni 112 ikiwa ni ada ya usajili na mishahara ya miezi mitatu akifafanua amefanya hivyo kama moja ya vipengele vyake vya kuvunja mkataba Yanga na kubaki huru.

The post Fei Toto amgeuzia kibao Rais Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/01/fei-toto-amgeuzia-kibao-rais-yanga/feed/ 0
Hersi: Hatuna tatizo na Fei Toto https://www.greensports.co.tz/2023/05/24/hersi-hatuna-tatizo-na-fei-toto/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/24/hersi-hatuna-tatizo-na-fei-toto/#respond Wed, 24 May 2023 16:08:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6273 Na mwandishi wetuRais wa Yanga, Hersi Said amesema hawana tatizo na kiungo wao, Feisal Salum ‘Fei Toto’ akifafanua wamekuwa wakitimiza anayoyahitaji kwa kutambua ni miongoni mwa wachezaji bora walionao.Hersi ameeleza hayo leo Jumatano alipokuwa kwenye kipindi cha Power Breakfast cha redio Clouds ambapo ilifika wakati walikwenda kinyume kwa kumpa pesa ya ada yote ya usajili […]

The post Hersi: Hatuna tatizo na Fei Toto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Yanga, Hersi Said amesema hawana tatizo na kiungo wao, Feisal Salum ‘Fei Toto’ akifafanua wamekuwa wakitimiza anayoyahitaji kwa kutambua ni miongoni mwa wachezaji bora walionao.
Hersi ameeleza hayo leo Jumatano alipokuwa kwenye kipindi cha Power Breakfast cha redio Clouds ambapo ilifika wakati walikwenda kinyume kwa kumpa pesa ya ada yote ya usajili kiasi cha Shilingi milioni 100 kwa mkupuo mmoja wakati ilipaswa alipwe kwa vipindi vinne.
“Wakati GSM inaingia Yanga, tulimwita Fei tukaona ana maslahi madogo na yalikuwa stahiki kwa wakati ule mwaka 2020 ila tukaboresha, tukampa mkataba mpya akawa anapokea mashara wa Sh milioni 4 kutoka milioni 1.5 na ada ya usajili ya Sh milioni 100.

“Fei alileta ombi kuwa ana jambo anataka kufanya na anahitaji pesa hiyo yote. Tukafanya uungwana kwa kumpa pesa yote badala ya milioni 25 kwa kila mwaka, tazama huu uungwana,” alisema Hersi.


Hersi alimsifu Fei kuwa hajawahi kuwa na utovu wa nidhamu, ni mchezaji mzuri na wangependa kuendelea naye, wanatamani kumwona akifika mbali kisoka na Yanga ni sehemu kubwa ya kulifanikisha hilo akitolea mfano sasa wapo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Alisisitiza kuwa wapo tayari kumpokea Fei na kama tatizo ni maslahi, wapo tayari kuzunguma naye au kama kuna timu inamuhitaji ifike izungumze na uongozi wa Yanga, wabariki uhamisho huo.
Alisema tangu Fei aibue sekeseke la kuvunja mkataba Desemba, mwaka jana, wamekuwa wakimlipa mshahara wake kama kawaida isipokuwa kuanzia Februari, mwaka huu akaunti ya mchezaji huyo imekuwa na tatizo.
Hersi hata hivyo alisema kwamba tayari wamemwandikia barua wakihitaji akaunti mpya ya kumwekea mishara yake ila Fei amekuwa kimya katika hilo.
Hivi karibuni mwanasheria wa Yanga, Simon Patrick alinukuliwa na GreenSports akisema kwamba klabu hiyo inatambua Fei Toto ni mchezaji wao halali hivyo watampa medali za ubingwa kama wachezaji wengine.
Yanga tayari imeshatangazwa bingwa wa Ligi Kuu NBC msimu huu wa 2022-23 na sasa inapigania makombe mawili ikiwa katika hatua ya fainali ya Kombe la FA (ASFC) pamoja na Kombe la Shirikisho Afrika.

The post Hersi: Hatuna tatizo na Fei Toto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/24/hersi-hatuna-tatizo-na-fei-toto/feed/ 0