Hemed Morocco - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 23 Sep 2025 19:47:44 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Hemed Morocco - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Morocco apewa majukumu Simba https://www.greensports.co.tz/2025/09/23/morocco-apewa-majukumu-simba/ https://www.greensports.co.tz/2025/09/23/morocco-apewa-majukumu-simba/#respond Tue, 23 Sep 2025 19:46:18 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13942 Na mwandishi wetuKlabu ya soka ya Simba imemtangaza kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Hemed Suleiman ‘Morocco’ kuwa kocha wao wa muda akichukua nafasi ya Fadlu Davids aliyeachana na timu hiyo.Taarifa ya klabu ya Simba imeeleza kuwa kocha Morocco ambaye tayari ameanza majukumu hayo mapya, ataiongoza timu hiyo kwenye mechi za kimataifa kwa kuwa […]

The post Morocco apewa majukumu Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya soka ya Simba imemtangaza kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Hemed Suleiman ‘Morocco’ kuwa kocha wao wa muda akichukua nafasi ya Fadlu Davids aliyeachana na timu hiyo.
Taarifa ya klabu ya Simba imeeleza kuwa kocha Morocco ambaye tayari ameanza majukumu hayo mapya, ataiongoza timu hiyo kwenye mechi za kimataifa kwa kuwa kocha wao msaidizi, Suleiman Matola ana kadi nyekundu.
Uongozi wa Simba katika taarifa yao walilishuruku Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kumruhusu Morocco kuiongoza timu hiyo licha ya kuwa na majukumu mengine kwenye timu ya taifa.
Simba wamefafanua kuwa Morocco ataifanya kazi hiyo wakati huu klabu hiyo ikiendelea na mchakato wa kumsaka kocha mpya wa kudumu ambaye atakabidhiwa timu.
Kwa mantiki hiyo, Morocco ataanza kuliongoza benchi la timu hiyo kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United, mechi ambayo itachezwa Septemba 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Katika mechi ya kwanza ambayo Simba ilikuwa ugenini Botswana, timu hiyo ilitoka na ushindi wa bao 1-0 na hiyo ilikuwa mechi ya mwisho kwa Fadlu kuingoza Simba.
Fadlu, kocha kutoka Afrika Kusini ameachana na Simba baada ya kuitumikia kwa mwaka mmoja na kuiwezesha kufikia hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kushika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu NBC.

The post Morocco apewa majukumu Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/09/23/morocco-apewa-majukumu-simba/feed/ 0
Morocco aiona Tanzania ikifika mbali https://www.greensports.co.tz/2024/03/28/morocco-aiona-tanzania-ikifika-mbali/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/28/morocco-aiona-tanzania-ikifika-mbali/#respond Thu, 28 Mar 2024 19:11:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10413 Na mwandishi wetuKaimu kocha mkuu wa Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’ amesema anaiona Tanzania ikifika mbali katika soka kutokana na jitihada zinazofanywa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).Kocha huyo alisema kitendo cha kushiriki mashindano mbalimbali ikiwemo kushiriki michuano ya FIFA Series 2024 ni jitihada za wazi ambazo zinaonesha soka la Tanzania linapiga hatua.“Nimeridhishwa na jitihada […]

The post Morocco aiona Tanzania ikifika mbali first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kaimu kocha mkuu wa Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’ amesema anaiona Tanzania ikifika mbali katika soka kutokana na jitihada zinazofanywa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Kocha huyo alisema kitendo cha kushiriki mashindano mbalimbali ikiwemo kushiriki michuano ya FIFA Series 2024 ni jitihada za wazi ambazo zinaonesha soka la Tanzania linapiga hatua.
“Nimeridhishwa na jitihada zinazofanywa na TFF, chini ya Rais Wallace Karia, ukweli naiona mbali Tanzania, kitendo cha kucheza mechi nyingi za kirafiki na mataifa makubwa kama Bulgaria kunawapa wachezaji uzoefu na kufanya wasiwe wageni katika ulimwengu wa mpira,” alisema Morocco.
Kocha huyo alisema jitihada hizo kama zitaendelea anaamini Tanzania itaishangaza Afrika kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika 2027 ambayo itafanyika Tanzania kwa kushirikiana na mataifa ya Kenya na Uganda.
Alisema kingine kinachomvutia ni namna TFF inavyopambana kuwatafuta wachezaji wenye asili ya Tanzania kuitumikia timu yao ya taifa.
Alisema jambo hilo litaongeza ushindani dhidi ya wachezaji wanaocheza soka ligi ya ndani kitu ambacho kitaifanya timu hiyo kuwa bora kama yalivyo baadhi ya mataifa ya Afrika.
Morocco pia amewaomba wadau mbalimbali kuunga mkono jitihada zinazofanywa na TFF, ili Tanzania iwe miongoni mwa taifa linaloogopewa na kuheshimiwa katika mchezo wa soka kwani uwezo wa kufanya hivyo upo.

The post Morocco aiona Tanzania ikifika mbali first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/28/morocco-aiona-tanzania-ikifika-mbali/feed/ 0
Morocco: Tuko tayari kuivaa Bulgaria https://www.greensports.co.tz/2024/03/21/morocco-tuko-tayari-kuivaa-bulgaria/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/21/morocco-tuko-tayari-kuivaa-bulgaria/#respond Thu, 21 Mar 2024 19:18:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10297 Na mwandishi wetuKaimu kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’, amesema maandalizi yanaendelea vizuri na wapo tayari kuikabili Bulgaria kesho Ijumaa.Stars itatupa karata yake ya kwanza katika michuano ya Fifa Series 2024 katika mchezo huo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Olimpiki wa Baku, Azerbaijan.Morocco alisema mchezo huo ni kipimo kizuri […]

The post Morocco: Tuko tayari kuivaa Bulgaria first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kaimu kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’, amesema maandalizi yanaendelea vizuri na wapo tayari kuikabili Bulgaria kesho Ijumaa.
Stars itatupa karata yake ya kwanza katika michuano ya Fifa Series 2024 katika mchezo huo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Olimpiki wa Baku, Azerbaijan.
Morocco alisema mchezo huo ni kipimo kizuri kwa wachezaji wake ambao wengi wanaandaliwa kwa ajili ya kikosi cha baadaye na wametilia mkazo kuhakikisha wanapata ushindi.
Naye kipa wa Stars, Abutwalib Mshery amesema wamejiandaa vizuri na kwamba mchezo huo ni fursa kwao kwa sababu unaandaliwa kwa ajili ya timu ya baadaye itakayocheza Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2027) ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji pamoja na Kenya na Uganda.
Naye beki Novatus Miroshi alisema: “Kucheza na timu zinazotoka nje ya Afrika ni mara ya kwanza au chache, ila ni fursa kwa wachezaji wengi kwani itawajenga kuelekea mashindano ya kufuzu Afcon na ni kipimo kizuri kwetu. Benchi la ufundi watakuwa wameshajua tunatakiwa tufanye nini kizuri na kipi tunatakiwa kuongeza hivyo naamini utakuwa mchezo mzuri ambao utatujenga,”.
Baada ya mchezo huo nyota wa Stars wanaotoka klabu za Simba na Yanga watarejea nchini kuungana na timu zao ambazo zinajiandaa na mechi za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

The post Morocco: Tuko tayari kuivaa Bulgaria first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/21/morocco-tuko-tayari-kuivaa-bulgaria/feed/ 0
Stars yamtoa Morocco Geita Gold https://www.greensports.co.tz/2023/12/20/stars-yamtoa-morocco-geita-gold/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/20/stars-yamtoa-morocco-geita-gold/#respond Wed, 20 Dec 2023 08:47:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8951 Na mwandishi wetuKocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Hemed Morocco amesema kilichomuondoa katika kikosi cha Geita Gold ni majukumu ya kwenye timu ya taifa kuelekea michuano ya Afcon 2023.Morocco alisema kwamba ameshatoa taarifa rasmi ya barua kwa uongozi wa Geita Gold na tayari wamempa ruhusa ya kuendelea na majumu yake kwenye […]

The post Stars yamtoa Morocco Geita Gold first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Hemed Morocco amesema kilichomuondoa katika kikosi cha Geita Gold ni majukumu ya kwenye timu ya taifa kuelekea michuano ya Afcon 2023.
Morocco alisema kwamba ameshatoa taarifa rasmi ya barua kwa uongozi wa Geita Gold na tayari wamempa ruhusa ya kuendelea na majumu yake kwenye timu ya taifa kama alivyotaka kupitia barua yake.
“Nimeuandikia barua uongozi nikitaka kukaa pembeni kutokana na majukumu ya timu ya taifa sababu Afcon inaanza muda si mrefu na nitakuwa na timu kwa takribani miezi miwili ndio maana nikaamua kuwaeleza kilichopo na wamenikubalia,” alisema Morocco.
Akifafanua zaidi, Morocco alisema kwamba kwa mujibu wa mkataba wake na Geita, haikuwa ngumu kwake kuondoka katika timu hiyo kwa kuwa suala hilo lipo wazi.
Alisema kwamba kwa sasa tayari yupo kwenye majukumu ya Taifa Stars na wanaendelea na utaratibu wa kuchagua wachezaji ambao watakwenda kwenye michuano ya Afcon ambayo itaanza kutimua vumbi Januari 13 hadi Februari 11, mwakani nchini Ivory Coast.
Morocco amekuwa na Geita Gold tangu mwanzoni mwa msimu huu na ameiongoza katika mechi 12 na kwa sasa inashika nafasi ya tatu ikiwa na rekodi ya ushindi wa mechi tatu, sare nne na kufungwa mechi tano.
Katika mechi yake ya mwisho ya Ligi Kuu NBC akiwa na Geita, Morocco aliishuhudia timu hiyo ikikutana na kichapo cha mabao 3-1 mbele ya Coastal Union.
Baada ya kuondoka kwa Morocco, zipo habari kwamba Geita imekuwa katika mazungumzo na aliyekuwa kocha wa Namungo, Denis Kitambi ili ainoe timu hiyo.

The post Stars yamtoa Morocco Geita Gold first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/20/stars-yamtoa-morocco-geita-gold/feed/ 0
Morocco amfurahia kipa Geita https://www.greensports.co.tz/2023/08/05/morocco-amfurahia-kipa-geita/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/05/morocco-amfurahia-kipa-geita/#respond Sat, 05 Aug 2023 14:10:15 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7243 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Geita Gold, Hemed Morocco (pichani) amesema kwa sasa lango lake liko salama kwa asilimia 100 baada ya kutua kwa kipa Eric Johora katika kikosi hicho akitokea Yanga SC.Morocco ameiambia GreenSports kuwa mbali na ubora aliokuwa nao kipa huyo aliyetambulishwa na timu hiyo lakini pia mafanikio na ujuzi alioupata akiwa Yanga […]

The post Morocco amfurahia kipa Geita first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Geita Gold, Hemed Morocco (pichani) amesema kwa sasa lango lake liko salama kwa asilimia 100 baada ya kutua kwa kipa Eric Johora katika kikosi hicho akitokea Yanga SC.
Morocco ameiambia GreenSports kuwa mbali na ubora aliokuwa nao kipa huyo aliyetambulishwa na timu hiyo lakini pia mafanikio na ujuzi alioupata akiwa Yanga ni jambo muhimu kwao.
“Ni kipa anayekuja kuongeza upinzani na kuliweka lango salama zaidi kutokana na ujuzi alionao, anatokea Yanga ambayo imekuwa ikishiriki michuano mingi na kufika mbali hivyo ujuzi wake pia ni jambo zuri zaidi kabla ya kugusa kipaji kikubwa alichonacho,” alisema Morocco.
Kocha huyo wa zamani wa Taifa Stars alieleza kutua kwa Johora sasa ni wazi wako hatua za mwisho kukamilisha usajili kuelekea msimu ujao, wakitarajia kuhitimisha kwa kuongeza beki mmoja pekee.
Wachezaji wengine waliosajiliwa na Geita mpaka sasa ni Carlos Protas, Tariq Seif, Samuel Onditi, Valentino Kusengama, Yusuf Dunia, Mwaite Gereza na Abeid Athuman.

The post Morocco amfurahia kipa Geita first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/05/morocco-amfurahia-kipa-geita/feed/ 0