Harry Maguire - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 08 Dec 2023 22:04:05 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Harry Maguire - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Maguire, Ten Hag watwaa tuzo ya mwezi https://www.greensports.co.tz/2023/12/09/maguire-ten-hag-watwaa-tuzo-ya-mwezi/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/09/maguire-ten-hag-watwaa-tuzo-ya-mwezi/#respond Fri, 08 Dec 2023 22:04:04 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8794 London, EnglandBeki wa Man United, Harry Maguire na kocha wake Erik ten Hag wameshinda tuzo za mchezaji na kocha bora kwa mwezi Novemba, tuzo ambayo ina maana kubwa zaidi kwa Maguire aliyepitia kipindi kigumu.Man United imepoteza mechi nne kati ya saba za mwanzo za Ligi Kuu England (EPL) kabla ya kujitutumua na kupaa hadi nafasi […]

The post Maguire, Ten Hag watwaa tuzo ya mwezi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Beki wa Man United, Harry Maguire na kocha wake Erik ten Hag wameshinda tuzo za mchezaji na kocha bora kwa mwezi Novemba, tuzo ambayo ina maana kubwa zaidi kwa Maguire aliyepitia kipindi kigumu.
Man United imepoteza mechi nne kati ya saba za mwanzo za Ligi Kuu England (EPL) kabla ya kujitutumua na kupaa hadi nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Katika kipindi cha mwezi Novemba timu hiyo imeshinda mechi zake dhidi ya Fulham, Luton na Everton, mechi ambazo Maguire alicheza zote baada ya kupitia kipindi kirefu cha kusugua benchi kilichoandamana na lawama za kufanya makosa ya kizembe pale alipopata nafasi ya kucheza.
Kwa kushinda tuzo hiyo, Maguire anakuwa beki wa kwanza kufanya hivyo tangu Januari 2009 baada ya beki mwingine wa timu hiyo, Nemanja Vidic naye kushinda tuzo hiyo.
Hadi kuibuka kinara wa tuzo hiyo, Maguire aliwabwaga Anthony Gordon wa Newcastle, Jeremy Doku wa Man City, Raheem Sterling wa Chelsea, Marcus Tavenier wa Bournemouth na kipa wa Luton, Thomas Kaminski.

“Nisengeweza kushinda bila ya wachezaji wenzangu, maofisa wa timu na mashabiki, mapenzi yenu na sapoti vyote haviwezi kupita hivi hivi, nashukuru,” alisema Maguire.


Wakati akiwa katika kipindi kigumu Man United, Maguire alivuliwa unahodha na Ten Hag mwezi Julai na mipango ikaanza ya kumpiga bei lakini aliikataa ofa ya West Ham na kuamua kubaki United licha ya kusugua benchi.

The post Maguire, Ten Hag watwaa tuzo ya mwezi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/09/maguire-ten-hag-watwaa-tuzo-ya-mwezi/feed/ 0
Maguire achoka kusugua benchi https://www.greensports.co.tz/2023/03/01/maguire-achoka-kusugua-benchi/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/01/maguire-achoka-kusugua-benchi/#respond Wed, 01 Mar 2023 07:17:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5349 Seul, Korea KusiniNahodha na beki wa Man United, Harry Maguire amesema kwamba anaungwa mkono na kocha wake, Erik ten Hag lakini amekiri kuchoka kukaa benchi na anataka apewe nafasi ya kucheza.Tangu kuanza msimu huu, Maguire ameanza mechi tisa tu na aliingia dakika mbili za mwisho katika mechi ya fainali ya Carabao Jumapili iliyopita, mechi ambayo […]

The post Maguire achoka kusugua benchi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Seul, Korea Kusini
Nahodha na beki wa Man United, Harry Maguire amesema kwamba anaungwa mkono na kocha wake, Erik ten Hag lakini amekiri kuchoka kukaa benchi na anataka apewe nafasi ya kucheza.
Tangu kuanza msimu huu, Maguire ameanza mechi tisa tu na aliingia dakika mbili za mwisho katika mechi ya fainali ya Carabao Jumapili iliyopita, mechi ambayo United iliichapa Newcastle mabao 2-0 na kubeba taji hilo.
Katika beki ya kati Man United, Ten Hag anapenda kuwatumia, Raphael Varane na Lisandro Martinez na Maguire anakiri kiwango bora cha wachezaji hao kimemfanya awe na wakati mgumu kupenya kikosi cha kwanza.

“Mimi ni mchezaji ambaye nataka kucheza mechi tangu mwanzo, kuwaongoza vijana kutokea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo lakini pia naelewa hii ni sehemu ya soka, unapocheza katika soka la hadhi ya juu kunakuwa na ushindani mkubwa wa nafasi,” alisema Maguire.


“Jamaa wanaoanza, Rapha anacheza vizuri mno na tunaona mawazo yake, ni vile anavyotaka kocha, anacheza beki wa kati, anatumia mguu wa kushoto, kwa hiyo ushindani ni mkubwa,” alisema Maguire.
Ten Hag tangu atue Man United ameendelea kumuamini Maguire katika nafasi ya unahodha licha ya ya mchezaji huyo kutokuwa na uhakika wa moja kwa moja wa kupata nafasi kikosi cha kwanza tangu Agosti mwaka jana.
Kinachoonekana sasa ni kwamba mchezaji huyo anataka kuhama na huenda dirisha la usajili majira ya kiangazi akaondoka ingawa katika dirisha dogo la Januari alidaiwa kukataa ofa ya kusajiliwa West Hem.
“Nafikiri kocha (Ten Hag) amekuwa akiulizwa mara kadhaa kuhusu mimi na majukumu yangu na amekuwa wazi kuwa ananiamini lakini hili ni soka na hii ni Manchester United, tunataka kushinda mataji, mataji makubwa na ili kufanya hivyo unahitaji ushindani wa kuwania namba,” alisema Maguire.

The post Maguire achoka kusugua benchi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/01/maguire-achoka-kusugua-benchi/feed/ 0