Harry Kane - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 16 Feb 2026 14:39:31 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Harry Kane - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Kane afikisha mabao 500 https://www.greensports.co.tz/2026/02/15/kane-afikisha-mabao-500/ https://www.greensports.co.tz/2026/02/15/kane-afikisha-mabao-500/#respond Sun, 15 Feb 2026 11:12:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14344 Bremen, UjerumaniMshambuliaji wa Bayern Munich na timu ya taifa ya England, Harry Kane ameweka rekodi mpya ya mabao kwa kufikisha mabao 500 katika soka la ushindi, mabao 100 kati ya hayo akiyafunga kwa penalti.Kane amefikisha rekodi hiyo ya mabao baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 ambao Bayern imeupata Jumamosi Februari 14, 2026 […]

The post Kane afikisha mabao 500 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Bremen, Ujerumani
Mshambuliaji wa Bayern Munich na timu ya taifa ya England, Harry Kane ameweka rekodi mpya ya mabao kwa kufikisha mabao 500 katika soka la ushindi, mabao 100 kati ya hayo akiyafunga kwa penalti.
Kane amefikisha rekodi hiyo ya mabao baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 ambao Bayern imeupata Jumamosi Februari 14, 2026 katika mechi ya Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga dhidi ya Werder Bremen.
Katika mechi na Bremen, Kane alifunga bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 22 baada ya Senne Lynen kumchezea rafu Lennart Karl wa Bayern katika eneo la penalti.
Kane, 32, ambaye hilo ni bao lake la tisa analofunga kwa penalti msimu huu, aliongeza bao la pili dakika nne baadaye, bao lililomfanya afikishe mabao 500 katika mechi 743 za klabu na timu ya taifa.
Bao la tatu na la ushindi kwa Bayern lilifungwa na Leon Goretzka katika dakika ya 70 na kuihakikishia timu hiyo ushindi ambao umeifanya kushika usukani katika Bundesliga kwa tofauti ya pointi sita.
Kwa msimu huu pekee, Kane hadi sasa ameifungia Bayern mabao 41, kati ya hayo 26 ni ya kwenye ligi na mengine katika mashindano mengine ya Ujerumani na Ulaya.

The post Kane afikisha mabao 500 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/02/15/kane-afikisha-mabao-500/feed/ 0
Kane apiga hat trick ya tatu Bundesliga https://www.greensports.co.tz/2023/11/05/kane-apiga-hat-trick-ya-tatu-bundesliga/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/05/kane-apiga-hat-trick-ya-tatu-bundesliga/#respond Sun, 05 Nov 2023 20:05:23 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8371 Dortmund, UjerumaniMshambuliaji wa Bayern Munich, Harry Kane anazidi kuuwasha moto kwenye Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga baada ya kufunga mabao matatu (hat trick) Bayern ikiichapa Borussia Dortmund 4-0.Hiyo inakuwa hat trick ya tatu kwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Tottenham na hivyo kuiweka pazuri Bayern inayosaka taji la 12 mfululizo la Bundesliga ikiwa nafasi ya […]

The post Kane apiga hat trick ya tatu Bundesliga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Dortmund, Ujerumani
Mshambuliaji wa Bayern Munich, Harry Kane anazidi kuuwasha moto kwenye Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga baada ya kufunga mabao matatu (hat trick) Bayern ikiichapa Borussia Dortmund 4-0.
Hiyo inakuwa hat trick ya tatu kwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Tottenham na hivyo kuiweka pazuri Bayern inayosaka taji la 12 mfululizo la Bundesliga ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Kane pia anakuwa ameifungia Bayern mabao 15 katika ligi hiyo lakini pia anakuwa amefikisha jumla ya mabao 19 msimu huu kwa Bayern pamoja na timu yake ya taifa ya England.
Mabao hayo pia yanamfanya awe mchezaji wa kwanza kufunga mabao 15 katika mechi 10 za kwanza za Bundesliga na sasa ndiye anayeshika usukani kwa wafungaji wenye mabao mengi kwenye ligi hiyo.
Kwa Dortmund matokeo hayo ya jana Jumamosi yanakuwa yameivunja rasmi rekodi waliyokuwa wakijivunia ya kutopoteza mchezo wowote wa ligi hiyo tangu Aprili Mosi
Mabao ya washindi yalipatikana kuanzia dakika ya nne, la kwanza likifungwa na Dayot Upamecano kabla Kane hajaisambaratisha Dortmund kwa mabao ya dakika za 3, 72 na 90.
Bayern katika mechi hiyo ilipata pigo baada ya kocha wake Thomas Tuchel kulimwa kadi dakika ya 43 baada ya kuonekana akiwakoromea waamuzi.
Matokeo ya mechi za Bundesliga Jumamosi hii ni kama ifuatavyo…
B Dortmund 0-4 Bayern Munich
Köln 1-1 Augsburg
Union Berlin 0-3 Frankfurt
Mainz 2-0 RB Leipzig
Freiburg 3-3 B Mgladbach
Hoffenheim 2-3 B Leverkusen

The post Kane apiga hat trick ya tatu Bundesliga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/05/kane-apiga-hat-trick-ya-tatu-bundesliga/feed/ 0
Kane aanza vibaya Bayern https://www.greensports.co.tz/2023/08/13/kane-aanza-vibaya-bayern/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/13/kane-aanza-vibaya-bayern/#respond Sun, 13 Aug 2023 01:26:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7357 Munich, UjerumaniMshambuliaji wa zamani wa Tottenham Hotspur, Harry Kane (pichani) ameanza na mguu mbaya kwenye timu yake mpya ya Bayern Munich baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 3-0 na RB Leipztig katika mechi ya Super Cup UjerumaniIkiwa ni saa kadhaa baada ya Bayern kukamilisha usajili wa Kane ambaye pia ni nahodha wa timu ya England […]

The post Kane aanza vibaya Bayern first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Hotspur, Harry Kane (pichani) ameanza na mguu mbaya kwenye timu yake mpya ya Bayern Munich baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 3-0 na RB Leipztig katika mechi ya Super Cup Ujerumani
Ikiwa ni saa kadhaa baada ya Bayern kukamilisha usajili wa Kane ambaye pia ni nahodha wa timu ya England kwa ada ya Pauni 86 milioni, Jumamosi hii mchezaji huyo aliingia uwanjani dakika ya 64 akitokea benchi.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Alianz Arena, mashabiki wa Bayern walimpokea kwa furaha mpachika mabao huyo kwa kumshangilia lakini uwapo wake haukuizuia Leipzig kutamba.
Kane katika mehezo huo aligusa mpira mara tatu tu na hakuwa na mchango wowote wakati Dani Olmo alipoifungia Leipzig mabao matatu peke yake (hat trick) yaliyotosha kumnyima Kane taji la kwanza na klabu hiyo mpya.
Akizungumzia matokeo hayo, kocha wa Bayern, Thomas Tuchel alisema kwamba ni tatizo kubwa kwani ilikuwa kama vile hakuna chochote walichokifanya katika wiki nne zilizopita.

“Siwezi kuelezea, ni kwamba hatukuwa katika ubora wa kutosha kila eneo, sijui ni kwa nini, hakuna uhusiano kati ya hali tuliyokuwa nayo na mtazamo wetu katika mechi pamoja na kiwango chetu uwanjani,” alisema Tuchel.


Msimu uliopita katika mechi kama hiyo, Bayern iliifunga Leipzig mabao 5-3 na kubeba taji hilo ambalo safari hii Leipzig wamejibu mapigo.

The post Kane aanza vibaya Bayern first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/13/kane-aanza-vibaya-bayern/feed/ 0
Bayern yamkomalia Harry Kane https://www.greensports.co.tz/2023/07/04/bayern-yamkomalia-harry-kane/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/04/bayern-yamkomalia-harry-kane/#respond Tue, 04 Jul 2023 19:30:20 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6816 Munich, UjerumaniKlabu ya Bayern Munich imeendelea kukomaa katika mbio za kuisaka saini ya mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane baada ya kuwasilisha ofa nyingine kwa mara ya pili.Kane mwenye umri wa miaka 29 tayari amebainisha wazi kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo ili kusaka changamoto kwingineko na tayari timu nne zimeingia katika mbio za kumsaka […]

The post Bayern yamkomalia Harry Kane first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Klabu ya Bayern Munich imeendelea kukomaa katika mbio za kuisaka saini ya mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane baada ya kuwasilisha ofa nyingine kwa mara ya pili.
Kane mwenye umri wa miaka 29 tayari amebainisha wazi kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo ili kusaka changamoto kwingineko na tayari timu nne zimeingia katika mbio za kumsaka mshambuliaji huyo.
Man United ilikuwa ya kwanza ingawa baadaye ilitangaza kujitoa na kuziacha timu za PSG, Real Madrid na Bayern ambayo inaonekana kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inampata Kane.
Vigogo wa klabu ya Bayern wanadaiwa kutofurahishwa na mwenendo wa timu yao msimu wa 2022-23 ulioisha hivi karibuni na wanaamini ipo haja ya kuiimarisha safu ya ushambuliaji na Kane anaonekana kuwa mtu sahihi katika eneo hilo.
Tangu Robert Lewandowski aihame Bayern na kujiunga na Barcelona, vigogo wa klabu hiyo ya nchini Ujerumani wanaamini walipoteza mtu muhimu katika safu ya ushambuliaji na sasa akili yao ipo kwa Kane lakini Spurs wanadaiwa kuwa wagumu kumuachia kirahisi mshambuliaji huyo.
Klabu za PSG na Real Madrid nazo zinadaiwa kufuatilia taratibu mbio za Bayern kabla ya kuamua nini cha kufanya kwani tangu zihusishwe na mpango wa kumtaka mshambuliaji huyo hakuna iliyotangaza kujitoa katika mbio hizo zaidi ya Man United.

The post Bayern yamkomalia Harry Kane first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/04/bayern-yamkomalia-harry-kane/feed/ 0
Kane kumrithi Benzema Real Madrid https://www.greensports.co.tz/2023/06/05/kane-kumrithi-benzema-real-madrid/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/05/kane-kumrithi-benzema-real-madrid/#respond Mon, 05 Jun 2023 13:31:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6463 Madrid, HispaniaStraika wa Tottenham Hotspur, Harry Kane anaongoza orodha ya wachezaji wanaotakiwa Real Madrid ili kuziba pengo la Karim Benzema ambaye anatimkia Saudi Arabia na jana Jumapili aliagwa rasmi.Kane (pichani) ameifungia Spurs mabao 280 katika mechi 435, ana mwaka mmoja katika mkataba na Spurs lakini kwa siku za karibuni amekuwa akitajwa kuwa na nia ya […]

The post Kane kumrithi Benzema Real Madrid first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Straika wa Tottenham Hotspur, Harry Kane anaongoza orodha ya wachezaji wanaotakiwa Real Madrid ili kuziba pengo la Karim Benzema ambaye anatimkia Saudi Arabia na jana Jumapili aliagwa rasmi.
Kane (pichani) ameifungia Spurs mabao 280 katika mechi 435, ana mwaka mmoja katika mkataba na Spurs lakini kwa siku za karibuni amekuwa akitajwa kuwa na nia ya kutafuta changamoto mpya katika klabu nyingine.
Baadhi ya klabu ambazo amekuwa akihusishwa nazo Kane ukiacha Real Madrid ni Bayern Munich, PSG na Man United lakini tangu kuibuka habari za kuondoka kwa Benzema, Real Madrid inadaiwa kuongeza nguvu katika mbio za kumtaka mchezaji huyo.
Kane mwenye umri wa miaka 29 bado hajasema lolote kuhusu klabu anayotaka kujiunga nayo lakini kilicho wazi ni kwamba azma ya kuihama Spurs amekuwa nayo kwa muda mrefu na hapana shaka atapenda kuhamia Real Madrid.
Ukiacha Kane wachezaji wengine ambao Real Madrid inawawinda ni Victor Osimhen wa Napoli, Kai Havertz wa Chelsea, Dusan Vlahovic wa Juventus na Lautaro Martinez wa Inter Milan.
Kati ya wachezaji wote hao jina la Kane ndilo linaloongoza orodha hiyo na matumaini yaliyopo ni kwamba kuondoka kwa baadhi ya mastaa katika klabu hiyo kutasaidia kurahisisha usajili wa Kane ambaye pia ni nahodha na mshambuliaji tegemeo wa timu ya Taifa ya England.
Ukiacha Benzema, wachezaji wengine wanaoondoka Real Madrid ni pamoja na Marion Diaz, Eden Hazard na Marco Asensio.
Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy anapenda kumbakisha Kane katika klabu hiyo ya utotoni ingawa inaeleweka kwamba atapenda kufanya biashara na kutaka Pauni 100 milioni ambazo hapana shaka Real Madrid watajenga hoja ili wapunguziwe.
Wakati nguvu ikiwekwa katika usajili wa Kane, Real Madrid pia ipo katika mazungumzo yanayodaiwa kwenda vizuri ya kumsajili kiungo wa England na klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani, Jude Bellingham.

The post Kane kumrithi Benzema Real Madrid first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/05/kane-kumrithi-benzema-real-madrid/feed/ 0
Kane aisaka rekodi ya Shearer EPL https://www.greensports.co.tz/2023/05/07/kane-aisaka-rekodi-ya-shearer-epl/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/07/kane-aisaka-rekodi-ya-shearer-epl/#respond Sun, 07 May 2023 12:38:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6043 London, EnglandStraika wa Tottenham, Harry Kane amefikisha mabao 209 katika Ligi Kuu England (EPL) na kushika nafasi ya pili nyuma ya straika wa zamani wa Newcastle, Alan Shearer aliyefunga mabao 260.Kane ambaye alifunga bao lake la 209 jana Jumamosi katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Crystal Palace, amempiku nyota wa zamani wa Man United, Wayne […]

The post Kane aisaka rekodi ya Shearer EPL first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Straika wa Tottenham, Harry Kane amefikisha mabao 209 katika Ligi Kuu England (EPL) na kushika nafasi ya pili nyuma ya straika wa zamani wa Newcastle, Alan Shearer aliyefunga mabao 260.
Kane ambaye alifunga bao lake la 209 jana Jumamosi katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Crystal Palace, amempiku nyota wa zamani wa Man United, Wayne Rooney aliyekuwa akishikilia nafasi ya pili na mabao yake 208.
Kwa sasa Kane ana kazi ya kuifukizia rekodi ya Shearer ambaye aliwahi kunukuliwa akimtaka mchezaji huyo kupigania taji kwa kutafuta changamoto kwingineko badala ya kuwekeza nguvu katika kusaka rekodi pekee.
Rekodi ya Shearer ya mabao 260 ambayo aliiacha tangu astaafu soka la ushindani mwaka 2006 ni mlima ambao Kane ambaye pia ni nahodha wa timu ya Taifa ya England, ana nia ya kuupanda.
Jambo la kufurahisha kwa Kane ni kwamba amempiku Rooney akitumia mechi 317 kufikisha mabao 208, mechi ambazo ni pungufu ya mechi 174 alizotumia Rooney kufunga mabao hayo.
Akizungumzia mafanikio ya Kane ambaye kwa sasa ana miaka 29, kocha wa zamani wa England, Roy Hodgson alisema kwamba Shearer anahitaji kuguswa na jambo hilo.
“Ni bado kijana, bado ana mengi katika soka mbele yake, nina hakika Alan (Shearer) anahitaji kuguswa na rekodi yake ya mabao kwa sababu Kane atakuwa anamfukuzia kwa karibu,” alisema Hodgson.

The post Kane aisaka rekodi ya Shearer EPL first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/07/kane-aisaka-rekodi-ya-shearer-epl/feed/ 0
Kane ataka mabao 100 England https://www.greensports.co.tz/2023/03/28/kane-ataka-mabao-100-england/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/28/kane-ataka-mabao-100-england/#respond Tue, 28 Mar 2023 12:08:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5616 London, EnglandNahodha na mshambuliaji wa timu ya Taifa ya England, Harry Kane amesema anataka kuweka rekodi ya kuifungia timu hiyo mabao 100 jambo ambalo amekiri ni gumu lakini si kwamba haliwezekani.Kane ambaye pia anaichezea Tottenham Hotspur, Jumapili iliyopita alifikisha mabao 55 na timu hiyo alipofunga bao katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Ukraine katika mechi […]

The post Kane ataka mabao 100 England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Nahodha na mshambuliaji wa timu ya Taifa ya England, Harry Kane amesema anataka kuweka rekodi ya kuifungia timu hiyo mabao 100 jambo ambalo amekiri ni gumu lakini si kwamba haliwezekani.
Kane ambaye pia anaichezea Tottenham Hotspur, Jumapili iliyopita alifikisha mabao 55 na timu hiyo alipofunga bao katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Ukraine katika mechi ya kuwania kufuzu Euro 2024.
Kwa sasa Kane ndiye kinara wa mabao wa wakati wote wa England akiwa amempiku nyota wa zamani wa timu hiyo, Wayne Rooney aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo akiwa amefunga mabao 53.

“Kwa hakika kufunga mabao 100 litakuwa jambo gumu lakini mimi siwezi kuliondoa kabisa, bado kijana nina miaka 29, bado niko fiti na imara na nataka niichezee England kadri nitakavyoweza,” alisema Kane.


“Kila mechi nitakuwa najiweka tayari kwa ajili ya kucheza, tutakwenda hatua kwa hatua, kwa sasa hatua inayofuata ni kufikisha mabao 60,” aliongeza Kane.
“Siwezi kufuta suala la kufunga mabao 100, litakuwa jambo gumu hasa lakini tunatakiwa kuona miaka michache ijayo itakwendaje,” alisema Kane.
England itaumana na Malta na North Macedonia Juni mwaka huu katika mechi nyingine ya kuwania kufuzu Euro 2024.
Rooney aliifungia England mabao 53 katika mechi 120 kuanzia mwaka 2003 hadi 2018 alipostaafu rasmi kuichezea timu hiyo wakati Kane ameanza kuichezea England mwaka 2015 na hadi sasa ameichezea mechi 82.
Kinara mwingine wa mabao wa England ni Bobby Charlton ambaye anashika nafasi ya tatu akiwa ameifungia timu hiyo mabao 49 katika mechi 106 kuanzia mwaka 1958 hadi mwaka 1970.

The post Kane ataka mabao 100 England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/28/kane-ataka-mabao-100-england/feed/ 0
Kane aweka rekodi England https://www.greensports.co.tz/2023/03/24/kane-aweka-rekodi-england/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/24/kane-aweka-rekodi-england/#respond Fri, 24 Mar 2023 12:58:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5585 Naples, ItaliaEngland imeilaza Italia mabao 2-1 ikiwa ni ushindi wao wa kwanza ugenini dhidi ya timu hiyo tangu mwaka 1961 huku nahodha Harry Kane akiweka rekodi ya kuwa mfungaji wa timu hiyo mwenye mabao mengi.Katika mechi hiyo ya kuwania kufuzu Euro 2024 iliyopigwa jana Alhamisi mjini Naples, Kane aliweka rekodi hiyo katika dakika ya 44 […]

The post Kane aweka rekodi England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Naples, Italia
England imeilaza Italia mabao 2-1 ikiwa ni ushindi wao wa kwanza ugenini dhidi ya timu hiyo tangu mwaka 1961 huku nahodha Harry Kane akiweka rekodi ya kuwa mfungaji wa timu hiyo mwenye mabao mengi.
Katika mechi hiyo ya kuwania kufuzu Euro 2024 iliyopigwa jana Alhamisi mjini Naples, Kane aliweka rekodi hiyo katika dakika ya 44 kwa bao la penalti na kuwa bao lake la 54 kuifungia England.
Kwa bao hilo, Kane sasa anakuwa amempiku mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Wayne Rooney ambaye kwa muda mrefu alikuwa akishikilia rekodi ya kuifungia England mabao mengi.
Declan Rice ndiye aliyefunga bao la kwanza la England katika dakika ya 13 akimalizia shuti la Kane ambalo awali liliokolewa.
Bao pekee la Italia lilifungwa na Mateo Retegui katika dakika ya 56 akineemeka na makosa yaliyofanywa na beki wa England, Harry Maguire kuchelewa kuokoa mpira.
Zikiwa zimebaki dakika 10 mpira kumalizika, England ilipata pigo baada ya Luke Shaw kulimwa kadi ya pili ya njano na hivyo kuiacha timu hiyo na wachezaji 10 uwanjani lakini ilifanikiwa kulinda ushindi.
Shaw alipewa kadi ya kwanza ya njano dakika ya 78 kwa kuchelewa kurusha mpira wakati kadi ya pili iliyomfanya atoke uwanjani alipewa dakika mbili baadaye kwa kumchezea rafu mfungaji wa bao la Italia, Retegui.
Baada ya ushindi huo dhidi ya timu inayotajwa kuwa ngumu katika kundi lake, England sasa itakuwa na kazi ya kujiweka vizuri ili kuhakikisha inafuzu Euro 2024 keshokutwa Jumapili itakapoumana na Ukraine kwenye dimba la Wembley. Timu nyingine zilizo kundi moja na England ni Malta na North Macedonia.
Matokeo ya mechi nyingine za kufuzu Euro 2024 zilizochezwa jana Alhamisi ni kama ifuatavyo…
Portugal 4-0 Liechtenstein
Italia 1-2 England
San Marino 0-2 N. Ireland
Kazakhstan 1-2 Slovenia
Bos-Herze 3-0 Iceland
Slovakia 0-0 Luxembourg
North Macedonia 2-1 Malta
Denmark 3-1 Finland

The post Kane aweka rekodi England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/24/kane-aweka-rekodi-england/feed/ 0
Kane avunja rekodi Spurs https://www.greensports.co.tz/2023/02/06/kane-avunja-rekodi-ya-mabao-spurs/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/06/kane-avunja-rekodi-ya-mabao-spurs/#respond Mon, 06 Feb 2023 12:21:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5013 London, EnglandMshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane sasa ndiye mfungaji anayeongoza kwa kufunga mabao mengi katika historia ya klabu hiyo akifikisha mabao 267 na kumpiku, Jimmy Greaves mwenye mabao 266.Kane alifunga bao lake la 267 na klabu hiyo jana Jumapili katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Man City katika mechi ya Ligi Kuu England […]

The post Kane avunja rekodi Spurs first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane sasa ndiye mfungaji anayeongoza kwa kufunga mabao mengi katika historia ya klabu hiyo akifikisha mabao 267 na kumpiku, Jimmy Greaves mwenye mabao 266.
Kane alifunga bao lake la 267 na klabu hiyo jana Jumapili katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Man City katika mechi ya Ligi Kuu England au EPL na sasa anataka kumpiku Alan Shearer mwenye rekodi ya mabao 260 kwenye EPL.
Akizungumzia azma yake ya kumpiku Shearer baada ya kuwa tayari amempiku Greaves, Kane alisema, “Alan ameweka rekodi inayotakiwa kuvunjwa, tutaona kama nitaivunja.”
Katika EPL, Kane amefikisha jumla ya mabao 200 hadi sasa na hivyo ana kazi ya kuzifumania nyavu mara 60 ili kuifikia rekodi ya Shearer na baada ya hapo kujipanga kuivunja na kuweka rekodi mpya.

“Nina hakika Shearer atakuwa akiangalia lakini sina hakika kama atakuwa mwenye furaha au la, bado nina mabao mengi ya kufunga, najisikia vizuri,” alisema Kane.


Kwa kipindi kirefu, Greaves aliyeanzia kutamba Chelsea amekuwa akijivunia rekodi ya mabao 266 aliyoyafunga akiwa na Spurs katika mechi 379 kati ya mwaka 1961 hadi 1970 kabla ya Kane kuifikia rekodi hiyo mwezi uliopita kwa kufikisha mabao 266 na kuivunja rasmi Jumapili alipofikisha mabao 267.
Kane mwenye umri wa miaka 29 yeye alianza kuichezea Spurs mwaka 2011 na hadi sasa amecheza jumla ya mechi 416 akiwa na timu hiyo.
Katika timu ya Taifa, Kane pia anawania rekodi ya kuwa mfungaji mwenye mabao mengi kwani kwa sasa amefungana na mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Wayne Rooney kila mmoja akiwa na mabao 53 na hivyo anahitaji bao moja ili kumpiku Rooney.

The post Kane avunja rekodi Spurs first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/06/kane-avunja-rekodi-ya-mabao-spurs/feed/ 0