Hans Pluijm - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 29 Mar 2024 15:00:35 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Hans Pluijm - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Pluijm aitahadharisha Mamelodi https://www.greensports.co.tz/2024/03/29/pluijm-aitahadharisha-mamelodi/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/29/pluijm-aitahadharisha-mamelodi/#respond Fri, 29 Mar 2024 15:00:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10437 Na mwandishi wetuKocha wa zamani wa Yanga, Hans van der Pluijm ameitahadharisha Mamelodi Sundowns kuwa inakwenda kukutana na miongoni mwa timu bora Afrika kwa sasa itakapovaana na Yanga.Yanga na Mamelodi zitaumana kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam katika mechi ya kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.Pluijm aliyewahi kuipa Yanga […]

The post Pluijm aitahadharisha Mamelodi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha wa zamani wa Yanga, Hans van der Pluijm ameitahadharisha Mamelodi Sundowns kuwa inakwenda kukutana na miongoni mwa timu bora Afrika kwa sasa itakapovaana na Yanga.
Yanga na Mamelodi zitaumana kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam katika mechi ya kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Pluijm aliyewahi kuipa Yanga mataji mawili mfululizo ya ligi kuu msimu wa 2014-15 na 2015-16 huku akisifika kwa soka safi lililopewa jina la ‘Kampa, kampa tena’ alisema hapingi ubora wa Mamelodi na nafasi ya ushindi wanayopewa.
Kocha huyo hata hivyo alisema anaamini lolote linaweza kutokea katika mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa 3.00 usiku.
“Mpira una matokeo ya ajabu, msimu uliopita hakuna aliyeipa nafasi Yanga hata ya kufika makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini wakacheza fainali na kuwashangaza wengi.

“Binafsi naamini kwenye mipango ya kocha Miguel Gamondi, analijua vizuri soka la Afrika lakini kizuri zaidi anaifahamu Mamelodi na utamaduni wake na ana baadhi ya watu kutoka Afrika Kusini kwenye benchi lake, hivyo naamini atafanya vizuri kwenye mchezo huu,” alisema Pluijm.


Pluijm aliwataka pia wachezaji wa Yanga kuwaheshimu Mamelodi kwa kucheza kwa tahadhari kubwa wakitambua ubora na uimara wa wapinzani wao na kutumia kila nafasi watakayoipata ili kuhakikisha wanaumaliza mchezo nyumbani kabla ya mechi ya marudiano Ijumaa ijayo kwenye Uwanja wa Loftus Versfeld mjini Pretoria, Afrika Kusini.

The post Pluijm aitahadharisha Mamelodi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/29/pluijm-aitahadharisha-mamelodi/feed/ 0
Pluijm aitahadharisha Yanga kwa Madeama https://www.greensports.co.tz/2023/12/06/pluijm-aitahadharisha-yanga-kwa-madeama/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/06/pluijm-aitahadharisha-yanga-kwa-madeama/#respond Wed, 06 Dec 2023 18:17:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8769 Na mwandishi wetuKocha wa zamani wa Yanga SC, Hans Pluijm ameitahadharisha timu hiyo kutowadharau Madeama watakaokutana nao Ijumaa hii kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.Pluijm ambaye kwa sasa yuko nyumbani kwake Ghana kunakopigwa mechi hiyo, alisema mchezo huo hautokuwa rahisi kwani wanakutana na timu imara yenye wachezaji wenye ari ya […]

The post Pluijm aitahadharisha Yanga kwa Madeama first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha wa zamani wa Yanga SC, Hans Pluijm ameitahadharisha timu hiyo kutowadharau Madeama watakaokutana nao Ijumaa hii kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Pluijm ambaye kwa sasa yuko nyumbani kwake Ghana kunakopigwa mechi hiyo, alisema mchezo huo hautokuwa rahisi kwani wanakutana na timu imara yenye wachezaji wenye ari ya kupambana muda wote wa mchezo, hivyo wanapaswa kupambana ili kushinda.

“Ni mchezo mgumu kwa timu zote mbili hasa Yanga ambao lazima washinde kama wanataka kwenda hatua inayofuata ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa Afrika,” alisema Pluijm.


Kocha huyo alisema ameshuhudia mechi mbili za hatua hiyo walizocheza Yanga, walicheza vizuri na kuongoza katika maeneo mengi licha ya kutopata ushindi wakiwa na makosa madogo ambapo anaamini kocha wao, Miguel Gamondi atakuwa ameyabaini na kuyafanyia kazi.
Alisema miamba hiyo ya Tanzania kwa sasa imekamilika kwa kila kitu katika benchi lake la ufundi akiwemo mchambuzi wa picha za video za wapinzani na taarifa zote kuhusu wapinzani wao Medeama, hivyo anaamini wanayo nafasi ya kushinda mechi hiyo.
Kocha huyo raia wa Uholanzi alisema kitendo cha Yanga kwenda mapema Ghana kitawasaidia kuzoea hali ya hewa ya joto na unyevunyevu ambayo inahitaji wachezaji waizoee ili kumudu mapambano ndani ya dakika 90 za mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Baba Yara, Kumasi.
Hiyo ni mara ya pili kwa timu hizo kukutana kwenye michuano ya Caf, mara ya kwanza ilikuwa 2016 katika Kombe la Shirikisho Afrika. Mechi ya kwanza iliyofanyika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam iliisha kwa sare ya bao 1-1 na mchezo wa marudiano Yanga ikafungwa mabao 3-1.

The post Pluijm aitahadharisha Yanga kwa Madeama first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/06/pluijm-aitahadharisha-yanga-kwa-madeama/feed/ 0
Pluijm aanza kuichunguza JKU https://www.greensports.co.tz/2023/07/26/pluijm-aanza-kuichunguza-jku/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/26/pluijm-aanza-kuichunguza-jku/#respond Wed, 26 Jul 2023 19:22:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7134 Na mwandishi wetuSiku moja baada ya kupangwa ratiba ya mechi za Kombe la Shirikisho Afrika, Kocha Mkuu wa Singida Fountain Gate, Hans Pluijm amesema kuwa tayari ameanza kuwachunguza wapinzani wake, JKU ya Zanzibar.Jana Shirikisho la Soka Afrika (Caf) lilipanga droo iliyoonesha kuwa Singida itaanza hatua ya awali kwa kuumana na JKU na timu itakayopita hapo […]

The post Pluijm aanza kuichunguza JKU first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Siku moja baada ya kupangwa ratiba ya mechi za Kombe la Shirikisho Afrika, Kocha Mkuu wa Singida Fountain Gate, Hans Pluijm amesema kuwa tayari ameanza kuwachunguza wapinzani wake, JKU ya Zanzibar.
Jana Shirikisho la Soka Afrika (Caf) lilipanga droo iliyoonesha kuwa Singida itaanza hatua ya awali kwa kuumana na JKU na timu itakayopita hapo itapepetana na Future FC ya Misri katika raundi ya kwanza ya michuano hiyo.
Pluijm ameiambia GreenSports leo Jumatano kuwa kwake haijalishi kama mpinzani anatoka karibu au mbali cha msingi ni kumfahamu vyema mpinzani unayekutana naye na kupambana naye kwa nidhamu.
“Kila mechi ni ya ushindani na tunapaswa kucheza bila ya kujali ni timu kutoka Zanzibar au wapi, sifahamu mengi kuhusu wao na sasa nimeanza kuifuatilia kufahamu ubora wao, udhaifu wao na mengine kama hayo.

“Nafikiri wepesi pekee tulionao hapo ni ukaribu wa mechi hizi mbili za hatua ya awali kwamba tutakuwa hapahapa Tanzania, hilo ndilo lenye faraja kwa sasa lakini mengine ni ushindani na tunajipanga pia dhidi ya JKU,” alisema Pluijm.


The post Pluijm aanza kuichunguza JKU first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/26/pluijm-aanza-kuichunguza-jku/feed/ 0
Pluijm apania kuivua Yanga taji la FA https://www.greensports.co.tz/2023/04/14/pluijm-apania-kuivua-yanga-taji-la-fa/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/14/pluijm-apania-kuivua-yanga-taji-la-fa/#respond Fri, 14 Apr 2023 12:18:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5806 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Singida Big Stars, Hans Pluijm amesema kuwa wapo kwenye mikakati mizito ya kuivua Yanga ubingwa wa Kombe la FA (ASFC).Singida itacheza na Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa taji hilo katika mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Liti, Singida hivi karibuni.Pluijm ameeleza kuwa anajua […]

The post Pluijm apania kuivua Yanga taji la FA first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Singida Big Stars, Hans Pluijm amesema kuwa wapo kwenye mikakati mizito ya kuivua Yanga ubingwa wa Kombe la FA (ASFC).
Singida itacheza na Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa taji hilo katika mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Liti, Singida hivi karibuni.
Pluijm ameeleza kuwa anajua ubora waliokuwa nao wapinzani wao lakini amepanga kuutumia mchezo wa ‘derby’ dhidi ya Simba ili kujua namna ya kuwakabili wapinzani wao.

“Lazima nikiri Yanga ni timu bora kwa sasa Tanzania unapokutana nayo lazima uwe na mbinu zaidi ya moja ili kupata unachokitaka ndio maana pamoja na mikakati tuliyokuwa nayo lakini mchezo wao wa derby dhidi ya Simba utatuongezea mbinu za kuwakabili,” alisema Pluijm.


Kocha huyo aliyewahi kuinoa Yanga, alisema anajua haitokuwa kazi rahisi kutokana na uwezo waliokuwa nao wachezaji wa timu hiyo lakini watawabana kuhakikisha wanatimiza malengo yao hasa ukizingatia mchezo huo utachezwa kwao Singida.
Pluijm amewataka wachezaji wake kutumia mchezo huo kuthibitisha ubora waliokuwa nao na kupigania malengo ya timu ili msimu ujao iweze kuliwakilisha taifa kwenye michuano ya klabu Afrika.

The post Pluijm apania kuivua Yanga taji la FA first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/14/pluijm-apania-kuivua-yanga-taji-la-fa/feed/ 0
Pluijm akomaa na tatu bora https://www.greensports.co.tz/2023/02/21/pluijm-akomaa-na-tatu-bora/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/21/pluijm-akomaa-na-tatu-bora/#respond Tue, 21 Feb 2023 15:03:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5237 Na mwandishi wetuUbora wa kikosi cha timu ya Singida Big Stars unampa matumaini kocha mkuu wa timu hiyo, Hans Pluijm (pichani) kumaliza msimu huu wa Ligi Kuu NBC kwenye nafasi tatu za juu.Timu hiyo kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 44 nyuma ya Azam walio nafasi ya nne […]

The post Pluijm akomaa na tatu bora first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Ubora wa kikosi cha timu ya Singida Big Stars unampa matumaini kocha mkuu wa timu hiyo, Hans Pluijm (pichani) kumaliza msimu huu wa Ligi Kuu NBC kwenye nafasi tatu za juu.
Timu hiyo kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 44 nyuma ya Azam walio nafasi ya nne wakiwa na pointi 43 lakini huenda ikaishusha Singida kwenye nafasi hiyo ya tatu kama itashinda au kupata sare mchezo wake wa leo Jumanne jioni dhidi ya Simba.
Pluijm, raia wa Uholanzi ameeleza kuwa mikakati yao ni kuhakikisha wanashinda mechi zao zote zilizobaki ili kutimiza lengo lao ambalo ni kumaliza nafasi ya pili au ya tatu.

“Sizungumzii ubingwa sababu kuna tofauti kubwa ya pointi kati yetu na Yanga, lakini uwezo wa kupambana na timu za Azam na Simba tunao ndio maana tunapambana kuhakikisha tunamaliza kwenye nafasi hizo mbili nyuma ya kinara,” alisema Pluijm.


Kocha huyo ameeleza kuwa mapumziko ya wiki mbili ameyatumia kuimarisha kikosi chake ikiwemo kurekebisha baadhi ya mapungufu aliyoyaona kwenye mechi zilizopita ikiwemo ile dhidi ya Simba, ambayo walifungwa mabao 3-1.
Alisema pamoja na ushindani uliopo lakini kwa ubora wa kikosi chake haoni sababu ya kutomaliza katika nafasi hizo sababu hata wachezaji wake wameonesha utayari wa kuipigania timu hiyo kumaliza msimu ndani ya tatu bora.
Februari 27, mwaka huu Singida itakuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Liti ikipapatuana na Mtibwa Sugar ambapo Pluijm ametamba kuchukua pointi zote tatu na kulipa kisasi baada ya kupoteza mchezo wao wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Mtibwa uliopigwa kwenye dimba la Manungu Complex.

The post Pluijm akomaa na tatu bora first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/21/pluijm-akomaa-na-tatu-bora/feed/ 0
Kwa Pluijm 3 bora inawezekana https://www.greensports.co.tz/2023/01/18/kwa-pluijm-3-bora-inawezekana/ https://www.greensports.co.tz/2023/01/18/kwa-pluijm-3-bora-inawezekana/#respond Wed, 18 Jan 2023 20:25:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4796 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Singida Big Star, Hans Pluijm amesema ushindi walioupata jana dhidi ya Kagera Sugar umewaongezea ari ya kufanya vizuri kwenye mechi zijazo na kumaliza msimu wa Ligi Kuu NBC kwenye nafasi tatu za juu.Ushindi huo wa bao 1-0 umeifanya Singida kufikisha pointi 40, na kukaa nafasi ya nne kwenye msimamo wa […]

The post Kwa Pluijm 3 bora inawezekana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Singida Big Star, Hans Pluijm amesema ushindi walioupata jana dhidi ya Kagera Sugar umewaongezea ari ya kufanya vizuri kwenye mechi zijazo na kumaliza msimu wa Ligi Kuu NBC kwenye nafasi tatu za juu.
Ushindi huo wa bao 1-0 umeifanya Singida kufikisha pointi 40, na kukaa nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi hiyo huku Azam inayoshikilia nafasi ya tatu ikiwa na pointi 43, Simba 44 na kinara Yanga pointi 53.
Pluijm raia wa Uholanzi alikiri kuwa mchezo ulikuwa mgumu na wapinzani wao Kagera Sugar walicheza vizuri hasa kipindi cha kwanza lakini walishindwa kutumia vizuri nafasi walizotengeneza.

“Nawapongeza wachezaji wangu kwa kujituma na kupata ushindi, unajua haukuwa mchezo mwepesi ukizingatia tumetoka kupoteza mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Mlandege kule Zanzibar kwa hiyo wachezaji walikuwa na uchovu lakini nafurahi kupata pointi hizi tatu,” alisema Pluijm.


Kocha huyo ameeleza kuwa mikakati yao kwa sasa ni kuendelea kupambana ili kumaliza ligi kwenye nafasi ya tatu au nne msimu huu ambayo kwao itakuwa ni mafanikio makubwa sababu ndio msimu wao wa kwanza kwenye ligi.
Naye kocha mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa makosa madogo yaliyofanywa na mabeki wake ndiyo yamesababisha wakapoteza mchezo huo lakini amefuraishwa na kiwango ambacho kimeoneshwa na vijana wake.
“Mchezo ulikuwa mzuri, tulicheza kwa nidhamu na kutengeneza nafasi nyingi lakini hatukufanikiwa kuzitumia, ndio mpira tunakubali matokeo na pia nawapongeza Singida kwa ushindi tunarudi kujipanga kwa mechi zijazo,” alisema Maxime.
Kipigo hicho kimeiacha Kagera katika nafasi ya nane kwenye msimamo wakiwa na pointi zao 24 baada ya michezo 20.

The post Kwa Pluijm 3 bora inawezekana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/01/18/kwa-pluijm-3-bora-inawezekana/feed/ 0
Pluijm aahidi ushindani Ligi Kuu https://www.greensports.co.tz/2022/08/05/pluijm-aahidi-ushindani-ligi-kuu/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/05/pluijm-aahidi-ushindani-ligi-kuu/#respond Fri, 05 Aug 2022 11:11:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2176 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Singida Big Stars, Hans van Der Pluijm ametahadharisha mapema kuwa atahakikisha anapambana na timu kubwa za Ligi Kuu ya NBC ili kuonesha ushindani na ubora wao msimu ujao.Pluijm raia wa Uholanzi amefunguka hayo baada ya kuridhishwa na kiwango cha timu yake ilipoumana na Zanaco ya Zambia jana na kushinda kwa […]

The post Pluijm aahidi ushindani Ligi Kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Singida Big Stars, Hans van Der Pluijm ametahadharisha mapema kuwa atahakikisha anapambana na timu kubwa za Ligi Kuu ya NBC ili kuonesha ushindani na ubora wao msimu ujao.
Pluijm raia wa Uholanzi amefunguka hayo baada ya kuridhishwa na kiwango cha timu yake ilipoumana na Zanaco ya Zambia jana na kushinda kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Liti (zamani Namfua), Singida.
Kocha huyo aliyewahi kuzinoa Yanga na Azam amesema kwamba kiufundi bado anahitaji kurekebisha kikosi hicho sehemu kadhaa ili kuwa tishio zaidi na kuwaletea changamoto ya ushindani vigogo wanaoshika nafasi za juu kila msimu ambao ni Simba, Yanga na Azam ili kufanya vyema msimu ujao.
“Mchezo wetu na Zanaco ulikuwa mgumu na fursa nzuri ya kujifunza zaidi, tumeona kuna baadhi ya idara inabidi kuziweka sawa na kurekebisha suala la mawasiliano uwanjani ambalo ni muhimu sana.
“Unajua mpira hautabiriki lakini tunataka kuleta changamoto ya ushindani kwa timu kubwa, natumani tutafanya hivyo, pia tunatakiwa kushinda mechi hizi nyingine si tu kushinda kubwa, suala ambalo litategemea nguvu kazi na utayari wa wachezaji na kiubora nafikiri tuna asilimia 67, tunatafuta 30 za kukaa sawa kabisa,” alisema Pluijm.
Singida iliyokuwa ikiitwa DTB iliyopanda daraja kushiriki Ligi Kuu ya NBC msimu ujao wa 2022/23 imekuwa gumzo kutokana na usajili wa wachezaji wenye majina wanaoendelea kuufanya na kutabiriwa kuleta changmoto kubwa msimu ujao.
Baadhi ya wachezaji waliotambulishwa na Singida mpaka sasa ni Deus Kaseke, Paul Godfrey, Yassin Mustapha kutoka Yanga, Meddie Kegere, Pascal Wawa, Said Ndemla waliokuwa Simba, Kelvin Sabato aliyekuwa Mtibwa Sugar, kipa Metacha Mnata aliyetoka Polisi Tanzania na wengine wengi.

The post Pluijm aahidi ushindani Ligi Kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/05/pluijm-aahidi-ushindani-ligi-kuu/feed/ 0