Graham Potter - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 25 Oct 2025 17:26:02 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Graham Potter - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Graham Potter kocha mkuu Sweden https://www.greensports.co.tz/2025/10/21/graham-potter-kocha-mkuu-sweden/ https://www.greensports.co.tz/2025/10/21/graham-potter-kocha-mkuu-sweden/#respond Tue, 21 Oct 2025 15:10:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14018 Stockholm, SwedenAliyekuwa kocha wa West Ham United, Graham Potter (50) ametangazwa kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya Sweden akiwa na jukumu la kuimarisha mbio za timu hiyo kusaka tiketi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026.Sweden imekuwa ikisaka kocha mpya tangu wamtimue Jon Dahl Tomasson baada ya timu hiyo kuchapwa bao […]

The post Graham Potter kocha mkuu Sweden first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Stockholm, Sweden
Aliyekuwa kocha wa West Ham United, Graham Potter (50) ametangazwa kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya Sweden akiwa na jukumu la kuimarisha mbio za timu hiyo kusaka tiketi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026.
Sweden imekuwa ikisaka kocha mpya tangu wamtimue Jon Dahl Tomasson baada ya timu hiyo kuchapwa bao 1-0 na Kosovo, mechi iliyochezwa Oktoba 13, matokeo yaliyoifanya timu hiyo iwe katika mazingira magumu ya kufuzu moja kwa moja Kombe la Dunia.
Mechi dhidi ya Kosovo ingawa matokeo yake yameiweka pagumu Sweden, timu hiyo bado inaweza kufuzu fainali hizo kupitia, play-offs hata kama haitomaliza katika nafasi mbili za juu za Kundi B na hiyo ni kutokana na mafanikio yao kwenye Nations Ligi walipomaliza kinara katika kundi lao
Kwa upande wake Potter amekubali jukumu la kuinoa timu hiyo kwa mkataba wa muda mfupi lengo likiwa ni moja tu, kuhakikisha anaibua matumaini na kuiwezesha Sweden kufuzu Kombe la Dunia.
Potter pia alisema kwamba ameipokea vizuri kazi ya kuinoa Sweden lakini pia amevutiwa na kazi hiyo akiamini kuwa Sweden ni timu yenye wachezaji wazuri ambao wanafanya vizuri katika ligi bora duniani kila wiki.

‘”Kazi yangu itakuwa ni kutengeneza mazingira ili timu iwe yenye kupata matokeo katika kiwango cha juu na kuipeleka Sweden kwenye Kombe la Dunia mwakani katika majira ya kiangazi,” alisema Potter.


Septemba mwaka huu Potter alitimuliwa West Ham baada ya kuwa na mwanzo mgumu katika msimu wa 2025-26 akiwa amepoteza mechi tano kati ya sita kabla ya hapo aliwahi kuzinoa timu za Brighton, Swansea City kabla ya kujiunga na Chelsea mwaka 2022 ingawa alitimuliwa baada ya kudumu kwa miezi saba.

The post Graham Potter kocha mkuu Sweden first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/10/21/graham-potter-kocha-mkuu-sweden/feed/ 0
Graham Potter atimuliwa Chelsea https://www.greensports.co.tz/2023/04/03/graham-potter-atimuliwa-chelsea/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/03/graham-potter-atimuliwa-chelsea/#respond Mon, 03 Apr 2023 08:34:36 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5672 London, EnglandKlabu ya Chelsea imemtimua kocha Graham Potter baada ya timu hiyo kufungwa na Aston Villa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu England juzi Jumamosi.Uamuzi wa kumtimua Potter umechukuliwa jana Jumapili ikiwa ni saa chache baada ya Leicester City nayo kumtimua kocha Brendan Rodgers baada ya timu hiyo kufungwa mabao 2-1 na Craystal Palace.Chelsea […]

The post Graham Potter atimuliwa Chelsea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Klabu ya Chelsea imemtimua kocha Graham Potter baada ya timu hiyo kufungwa na Aston Villa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu England juzi Jumamosi.
Uamuzi wa kumtimua Potter umechukuliwa jana Jumapili ikiwa ni saa chache baada ya Leicester City nayo kumtimua kocha Brendan Rodgers baada ya timu hiyo kufungwa mabao 2-1 na Craystal Palace.
Chelsea imeshuka hadi nafasi ya 11 kwenye Ligi Kuu England (EPL) ikiwa nyuma kwa tofauti ya pointi 12 kutoka timu nne bora za EPL hali inayohatarisha ushiriki wa timu hyo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Anguko la timu hiyo kwenye EPL limesababisha uamuzi huo mgumu kuchukuliwa hasa kwa kuwa takriban Pauni 550 milioni zimetumika kwenye usajili wa wachezaji wapya lakini matokeo yameendelea kuwa mabaya.
Wamiliki wa klabu hiyo wameeleza kusikitishwa na uamuzi wa kumtimua kocha huyo ambaye kwa mara ya kwanza alikabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo, Septemba mwaka jana akitokea Brighton.
Kwa mujibu wa Chelsea, Potter pamoja na kutimuliwa, amekubali kushirikiana na uongozi katika kipindi cha mpito ambapo Bruno Saltor aliyekuwa msaidizi wake akiwa Brighton sasa atabeba majukumu ya kocha mkuu.
Taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa na matajiri wawili wa klabu hiyo, Todd Boehly na Behdad Eghbali ilimsifia Potter, “Tunamheshimu mno Graham kama kocha na binadamu, wakati wote alikuwa akiendesha mambo yake katika ubora na maadili na sote tunasikitishwa na hiki kilichotokea.”
Potter anakuwa kocha wa pili kutimuliwa Chelsea tangu kuanza msimu huu, kabla yake timu hiyo ilikuwa ikinolewa na Thomas Tuchel ambaye alitimuliwa lakini kwa sasa anainoa Bayern Munich ya Ujerumani.

The post Graham Potter atimuliwa Chelsea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/03/graham-potter-atimuliwa-chelsea/feed/ 0
Graham Potter meno nje https://www.greensports.co.tz/2023/03/08/graham-potter-meno-nje/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/08/graham-potter-meno-nje/#respond Wed, 08 Mar 2023 13:35:26 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5438 London, EnglandKocha wa Chelsea, Graham Potter ana kila sababu ya kuwa mwenye furaha baada ya timu yake kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na hivyo kuwa na amani baada ya kupitia kipindi kigumu.Chelsea imekuwa na matokeo mabaya hasa katika Ligi Kuu England (EPL) licha ya usajili mkubwa ambao timu hiyo imeufanya lakini mambo […]

The post Graham Potter meno nje first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Chelsea, Graham Potter ana kila sababu ya kuwa mwenye furaha baada ya timu yake kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na hivyo kuwa na amani baada ya kupitia kipindi kigumu.
Chelsea imekuwa na matokeo mabaya hasa katika Ligi Kuu England (EPL) licha ya usajili mkubwa ambao timu hiyo imeufanya lakini mambo yamekuwa magumu.
Ushindi wa jana Jumanne usiku wa mabao 2-0 dhidi ya Borrusia Dortmund umeibua matumaini mapya na kumpa amani Potter ambaye habari za kutimuliwa kwake zilikuwa zikivuma kwa kasi.
Baada ya matokeo hayo kocha huyo amenukuliwa akisema kwamba bado yupo, kauli ambayo inaweza kutafsiriwa kuwa ataendelea kuwa na timu hiyo baada ya matokeo hayo ya kuvutia.
Katika EPL, Chelsea sasa inashika nafasi ya 10 ikiwa na pointi 34 imepoteza mechi tisa, nyingi kati ya hizo ni mechi za karibuni ambazo zilitishia nafasi ya Potter kiasi cha baadhi ya wachambuzi kuanza kuchambua majina ya makocha ambao wangeweza kuwa mbadala sahihi wa Potter.
Mabao ya Chelsea jana yalifungwa na Raheem Sterling dakika ya 43 na Havert kwa penalti dakika ya 53 na hivyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya kulala kwa bao 1-0 mechi ya kwanza.
Penalti hiyo ilizua utata baada ya picha za VAR kuonyesha kwamba Marius Wolf aliunawa mpira uliopigwa na Ben Chilwell lakini penalti ilipopigwa Havert kwanza alikosa lakini mwamuzi akaamuru irudiwe na ndipo Havert aliponi na kuujaza mpira wavuni.

“Wachezaji walikuwa vizuri na hata mashabiki walikuwa vizuri, tulikutana na timu inayofanya vizuri, katika mechi zilizopita niliona tulikuwa na kila sababu ya kusonga mbele, ni usiku wa kipekee,” alisema Potter baada ya mechi hiyo.


Pengine tangu aondoke Brighton na kutua Chelsea akichukua nafasi ya Thomas Tuchel, hii inakuwa mara ya kwanza kwa Potter kuwa mwenye furaha isiyo kifani baada ya kuwa na wakati mgumu.
Katika mechi nyingine ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Benfica ya Ureno iliibwaga Club Bruges mabao 5-1 na hivyo kufuzu robo fainali kwa jumla ya mabao 7-1.
Michuano hiyo itaendelea tena leo kwa mechi zifuatazo ambazo zitachezwa saa tano usiku…
Bayern Munich v PSG
Tottenham v AC Milan

The post Graham Potter meno nje first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/08/graham-potter-meno-nje/feed/ 0