Giggs - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 19 Jul 2023 07:52:23 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Giggs - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Giggs afutiwa kesi ya udhalilishaji https://www.greensports.co.tz/2023/07/19/giggs-afutiwa-kei-ya-udhalilishaji/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/19/giggs-afutiwa-kei-ya-udhalilishaji/#respond Wed, 19 Jul 2023 07:46:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7013 Manchester, EnglandKesi ya udhalilishaji kijinsia iliyokuwa ikimkabili winga wa zamani wa Man United, Ryan Giggs haitoendelea tena baada ya waendesha mashtaka kutangaza kujiondoa katika kesi hiyo.Giggs alitarajia kupanda kizimbani kwa mara nyingine Julai 31 mwaka huu akituhumiwa kwa tabia za ubabe na udhalilishaji dhidi ya aliyekuwa rafiki yake wa kike, Kate Greville, makosa aliyodaiwa kuyafanya […]

The post Giggs afutiwa kesi ya udhalilishaji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kesi ya udhalilishaji kijinsia iliyokuwa ikimkabili winga wa zamani wa Man United, Ryan Giggs haitoendelea tena baada ya waendesha mashtaka kutangaza kujiondoa katika kesi hiyo.
Giggs alitarajia kupanda kizimbani kwa mara nyingine Julai 31 mwaka huu akituhumiwa kwa tabia za ubabe na udhalilishaji dhidi ya aliyekuwa rafiki yake wa kike, Kate Greville, makosa aliyodaiwa kuyafanya kati ya Agosti 2017 na Novemba 2020.
Sambamba na kosa hilo, Giggs pia alituhumiwa kumfanyia ubabe huo dada wa Kate aitwaye Emma baada ya kuzozana naye wakiwa nyumbani kwa Giggs jijini Manchester, tukio analodaiwa kulifanya Novemba 2020.
Giggs hata hivyo alikana makosa yote hayo baada ya kufikishwa katika mahakama ya Manchester, katika kesi ambayo iliendeshwa kwa muda mrefu lakini hitimisho lilichelewa kufikiwa.
Waendesha mashitaka hao waliieleza mahakama hiyo jana Jumanne kwamba wamefikia uamuzi wa kujiondoa katika kesi hiyo baada ya Kate Greville kutoonesha utayari wa kutoa ushahidi na hivyo hawaoni sababu ya kuendelea na mashtaka ya udhalilishaji na ubabe dhidi ya Giggs.
Wakili wa Giggs, Chris Daw alisema mteja wake amepata faraja kwa hatua hiyo na sasa atakuwa na amani baada ya kujikuta katika mapambano kwa takriban miaka mitatu akipambana kusafisha jina lake.
Katika moja ya utetezi wake, Giggs aliwahi kukiri kwamba amewahi kumsaliti mpenzi wake mara kadhaa lakini hakuwahi hata mara moja kumpiga.

Katika miaka yake 23 ya soka la ushindani, Giggs ameichezea Man United katika mechi zaidi ya 900 na kushinda mataji 13 ya Ligi Kuu England (EPL) pamoja na mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Baada ya kuandamwa na kesi ya udhalilishaji, Novemba mwaka jana Giggs alitangaza kung’atuka katika nafasi yake ya ukocha kwenye timu ya Taifa ya Wales.
Giggs alisema kwamba alichukua uamuzi huo kwa kuwa hakutaka kesi hiyo iathiri kwa namna yoyote maandalizi ya timu hiyo iliyokuwa ikijiandaa kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Qatar kati ya Novemba na Desemba 2022.

The post Giggs afutiwa kesi ya udhalilishaji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/19/giggs-afutiwa-kei-ya-udhalilishaji/feed/ 0
Kesi ya Giggs yamponza Gary Neville https://www.greensports.co.tz/2022/09/02/kesi-ya-giggs-yamponza-gary-neville/ https://www.greensports.co.tz/2022/09/02/kesi-ya-giggs-yamponza-gary-neville/#respond Fri, 02 Sep 2022 14:30:26 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2668 Manchester, EnglandMchambuzi wa soka na nahodha wa zamani wa Man United, Gary Neville anatarajia kufikishwa kwa mwanasheria mkuu wa serikali kwa kuingilia uhuru wa mahakama katika kesi ya udhalilishaji kijinsia inayomkabili mchezaji mwenzake wa zamani wa klabu hiyo, Ryan Giggs katika Mahakama ya Manchester.Giggs anatuhumiwa kumpiga kichwa aliyekuwa mpenzi wake, Kate Greville pamoja na matukio […]

The post Kesi ya Giggs yamponza Gary Neville first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Giggs (kulia) na Gary Neville enzi zao wakiwa wachezaji wa Man Utd.

Manchester, England
Mchambuzi wa soka na nahodha wa zamani wa Man United, Gary Neville anatarajia kufikishwa kwa mwanasheria mkuu wa serikali kwa kuingilia uhuru wa mahakama katika kesi ya udhalilishaji kijinsia inayomkabili mchezaji mwenzake wa zamani wa klabu hiyo, Ryan Giggs katika Mahakama ya Manchester.
Giggs anatuhumiwa kumpiga kichwa aliyekuwa mpenzi wake, Kate Greville pamoja na matukio mengine ya udhalilishaji ambapo wakati kesi ikiendelea, Neville anadaiwa kutoa kauli kwenye mitandao ya kijamii, kauli ambazo mawakili wa upande wa mashitaka wanaziona kuwa ni kuingilia uhuru wa mahakama au mwenendo wa kesi.
Neville anadaiwa kutoa kauli ambazo zimetafsiriwa kama ni kuingilia uhuru wa mahakama na ingawa kauli hizo hazijawekwa wazi na vyombo vya habari lakini katika kujitetea kwake, Neville kupitia wakala wake alisema kwamba kauli hizo ziliilenga familia ya Glazer ambayo inamiliki klabu ya Manchester United na si kesi inayomkabili Giggs.
Kwa mujibu wa sheria ni marufuku kuingilia mwenendo wa kesi au uhuru wa mahakama iwe ni kwa kutoa taarifa kwenye mitandao ya kijamii au kwa namna yoyote ile taarifa ambayo itaonekana kuwa na ushawishi au kuhusiana kwa namna yoyote na kesi inayoendelea na adhabu ya kosa hilo ni faini au kufungwa jela kwa miaka miwili.
Akizungumzia alichokifanya Neville, Jaji anayesikiliza kesi hiyo, Hilary Manley alisema kwamba ameamua kulifikisha suala hilo kwa mwanasheria mkuu wa serikali akizihusisha kauli hizo kuwa ni kuingilia uhuru wa mahakama au mwenendo wa kesi.
Ilielezwa mahakamani kwamba mtoaji wa kauli hizo ni mtu maarufu na akaunti yake ya Instagram inafuatiliwa na watu wapatao milioni 1.5 na alichokisema kinaonekana kutoa ushawishi katika kesi ya jinai inayomkabili Giggs na hivyo kutafsiriwa kuwa ni kuingilia mwenendo wa kesi au uhuru wa mahakama.
Giggs amekana mashitaka yote yanayomkabili ikiwamo ya kumpiga kichwa mkewe, kuwa mbabe na udhalilishaji wa kijinsi, matukio ambayo inadaiwa alikuwa akimfanyia Kate wakati wawili hao wakiwa wapenzi kabla ya kutengana.
Kutokana na kesi hiyo, Giggs alilazimika kujiuzulu ukocha wa timu ya Taifa ya Wales kwa kile alichodai kuwa ni kutotaka maandalizi ya timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Dunia yaathiriwe kwa namna yoyote ile na kesi inayomkabili.

The post Kesi ya Giggs yamponza Gary Neville first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/09/02/kesi-ya-giggs-yamponza-gary-neville/feed/ 0
Giggs adaiwa kumpiga kichwa mpenzi wake https://www.greensports.co.tz/2022/08/10/giggs-adaiwa-kumpiga-kichwa-mpenzi-wake/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/10/giggs-adaiwa-kumpiga-kichwa-mpenzi-wake/#respond Wed, 10 Aug 2022 10:48:06 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2302 Manchester, EnglandWinga wa zamani wa Man Utd, Ryan Giggs amefikishwa mahakamani mjini Manchester kwa tuhuma kadhaa ikiwamo kumpiga kichwa mpenzi wake wa zamani, Kate Greville huku pia akidaiwa kuwa mwenye tabia ya kupenda ngono mara kwa mara.Giggs anadaiwa kufanya kitendo hicho Novemba Mosi, 2020 baada ya wawili hao kukorofishana ambapo alimshika Kate mabegani kisha akamuangalia […]

The post Giggs adaiwa kumpiga kichwa mpenzi wake first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Winga wa zamani wa Man Utd, Ryan Giggs amefikishwa mahakamani mjini Manchester kwa tuhuma kadhaa ikiwamo kumpiga kichwa mpenzi wake wa zamani, Kate Greville huku pia akidaiwa kuwa mwenye tabia ya kupenda ngono mara kwa mara.
Giggs anadaiwa kufanya kitendo hicho Novemba Mosi, 2020 baada ya wawili hao kukorofishana ambapo alimshika Kate mabegani kisha akamuangalia usoni, kabla ya kumpiga kichwa.
Katika tukio jingine la ubabe wa Giggs inadaiwa wawili hao walikuwa wakigombea simu baada ya Kate kuiweka simu ya Giggs chumba kingine jambo lililomkera Giggs na akaamua kuichukua simu ya Kate ndipo walipoanza kugombea simu hiyo kabla Giggs hajamlaza chini na kumkaba kisha kuchukua simu hiyo na kuondoka zake wakati wote huo Kate alikuwa akilia kuomba msaada.
Kate pia aliiambia mahakama kwamba Giggs alikuwa akitaka kufanya ngono kila wakati, na wakati mwingine alikuwa akimtumia hovyo ujumbe mfupi na picha zenye maudhui ya ngono kwenye simu
“Hakika haukuwa wakati mzuri kwangu, nilijiona kama mtu ninayetumiwa kumridhisha kwa mahitaji yake ya ngono, haijawahi kutokea wakati asiwe mwenye uhitaji wa ngono.
“Baba yangu aliwahi kumwambia anaumwa saratani, lakini hakuiangalia hata simu, badala yake wakati wote alikuwa akiniambia ninamkera, huku akiniambia niondoke.”
Giggs katika tuhuma nyingine anadaiwa alikuwa akimkera Kate kwa kumwambia yuko kama Stacey Cooke, mke wa zamani wa Giggs ambaye ni mama wa watoto wake wawili na ambaye wameachana sababu kubwa ikidaiwa kuwa ni tabia za Giggs za ubabe na kutotaka kupingwa.

“Alikuwa akinishambulia kwa kuniambia niko kama Stacey ambaye alidai kwamba alikuwa na tatizo la ulevi na aliyafanya maisha yake kuwa ya matatizo, na kuna wakati aliniita kwa jina la Stacey,” alisema Kate.
Kate aliiambia mahakama kwamba kuna wakati alijaribu kumkwepa Giggs kwa kwenda Abu Dhabi na baadaye Dubai na hakuamini kama Giggs angeweza kumkimbia mke wake kwa ajili ya kuwa na yeye,
“Niliamua kumkimbia na kwenda kuishi Dubai, niliona mahusiano haya hayakuwa mazuri kwangu, niliona aibu kwani alikuwa ni mume wa mtu na sikutaka mtu yeyote afahamu.
“Katika hali ya kawaida nilijikuta nikivurugwa na mapenzi yake, alikuwa akinifukuzia na kunitumia ujumbe mfupi, alinishawishi, kuna mambo mengine niliyasikia kuhusu yeye lakini aliyapinga, hali ilikuwa hivyo kwa muda mrefu.
Baada ya vyombo vya habari kujua habari yake na Giggs, Kate aliamua kum-block Giggs lakini ikawa balaa, “kukawa na ujumbe wa email mara kwa mara, niliamua bora iwe tu, nikaanza kuzungumza naye tena.”
Wakiwa pamoja, Kate akajikuta akipewa habari za Giggs kwamba yote aliyokuwa akimwambia ilikuwa kama ahadi tu lakini baadaye watu walikuwa wakimpa za ndani kuhusu Giggs kuhusu mambo ambayo ameonekana akiyafanya.
“Ilikuwa kama watu wawili tofauti, kati ya mtu ambaye aliniambia alivyo na mtu ambaye nilisikia habari zake kwa watu, sikujua niamini kipi, je alikuwa mtu mzuri au mbaya, alikuwa akiniambia ukweli au alikuwa akinidanganya? Nilikaa chini na kujiona kama mtu aliyekuwa akikimbia marathon na kuchoka hadi kushindwa kupumua,” alisema Kate.
Kate pia aliiambia mahakama kwamba Giggs aliwahi kumtumia mke wa mtu picha yake akiwa mtupu na alilijua hilo baada ya mtu mmoja, mume wa huyo mwanamke kumtumia Kate email iliyoambatanishwa na picha ya mtu mwanaume aliyekuwa mtupu akimuuliza kama mtu huyo ni Giggs au la.
Kate aliiambia mahakama kwamba siku ya tukio hilo alikuwa na Giggs Dubai na siku moja kabla Giggs alikuwa katika mzozo kwenye simu kwa dakika 20 wakati huo wakiwa wanapata chakula cha jioni na hapo hapo mtu huyo akasema kwamba asingependa jambo hilo lijulikane kwa kuwa yeye ana watoto.
Baadaye Kate alimfuata Giggs na kumwambia kuhusu jambo hilo, kwanza alibisha hadi alipoangalia kwenye simu na kuona ushahidi kwamba alimtumia mwanamke huyo picha hiyo wiki mbili zilizopita, “Hakuweza kubisha kwa sababu nilikuwa na ushahidi, badala yake akawa mtu mzuri kweli kwangu, Ryan mzuri niliyekuwa naye mwanzo, hata hivyo hali hiyo ilikuwa ya muda mfupi tu, akarudi katika uhalisia wake taratibu.”
Katika tuhuma nyingine, Giggs anadaiwa kumtumia video za ngono Kate huku akimtisha na kumwambia kwamba hataki tena kufanya naye kazi na kwamba anachotakiwa ni kumjibu ujumbe huo au kum-block asipofanya hivyo angewasiliana na bosi wake na kumwambia kwamba hayo ndiyo mambo anayofanya kazini.
Kate anasema kwamba hakutaka hata kuziangalia video hizo, alizifuta haraka, “zinaweza kuwa za kuchekesha lakini zimejaa maudhui ya ngono, niliogopa angeniharibia kazini, nilihisi angeweza hata kutumia email za ofisini kutuma picha hizo.”.
Kate pia aliiambia mahakama kwamba Giggs alikuwa akimlaghai kwenye mahusiano yao kwani alikuwa akijirusha na wanawake wengine wanane tofauti, mambo ambayo Kate aliyabaini baada ya kufungua iPad ya Giggs. “Uhalisia niliokutana nao kwenye iPad ilikuwa ni tukio baya kuliko hata nilivyokuwa nikidhani.
Kate alimtaja mmoja wa wanawake hao kwa jina la Helen ambaye alisafiri na Giggs ndege moja wakati Giggs akielekea Barcelona kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na mwingine alimtaja kwa jina la Zara ambaye alibaini hilo wakati wakielekea Urusi kwenye mechi za Kombe la Dunia 2018.
Katika tuhuma nyingine, Kate alisema kwamba Giggs alikuwa akimpiga mara kwa mara mfano ni siku ambayo alimgaragaza chini wakiwa kwenye chumba cha hoteli na kumkamata kiunoni kwa nguvu na kuanza kumvuta sakafuni wakati huo Kate akiwa amevaa taulo kabla ya kutupa vitu vyake kwenye varanda nje ya chumba walichofikia, hilo likiwa tukio la kwanza la ukatili kufanyiwa na Giggs.
Katika tukio jingine, wakiwa kitandani, Giggs alianza kumpiga mgongoni na kumfanya aanguke, akiwa chini Giggs alichukua laptop na kumpiga nayo kichwani na kumuacha akiwa na majeraha.
Siku nyingine, Giggs alidaiwa kuuvuta kwa nguvu mkoba aliokuwa ameushikilia Kate hadi Kate akaanguka chini, dada yake Kate, Emma alipoingilia kati Giggs alimpiga mdomoni kwa kiwiko.
Giggs ambaye ameichezea kwa mafanikio klabu ya Man Utd, hivi karibuni alitangaza kujiuzulu kuinoa timu ya Taifa ya Wales kwa alichodai kwamba asingependa tuhuma zinazomkabili ambazo tayari amezikana, ziathiri kwa namna yoyote maandalizi ya Wales kwenye fainali za Kombe la Dunia.

The post Giggs adaiwa kumpiga kichwa mpenzi wake first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/10/giggs-adaiwa-kumpiga-kichwa-mpenzi-wake/feed/ 0
Kesi ya Giggs kusikilizwa kwa siku 10 https://www.greensports.co.tz/2022/08/08/kesi-ya-giggs-kusikilizwa-kwa-siku-10/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/08/kesi-ya-giggs-kusikilizwa-kwa-siku-10/#respond Mon, 08 Aug 2022 16:32:30 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2282 Manchester, EnglandKocha wa zamani wa timu ya Wales, Ryan Giggs amefika mahakamani leo akikabiliwa na kesi ya kumdhalilisha, kumshambulia na kumuumiza aliyekuwa mpenzi wake, Kate Greville na mdogo wake Emma Greville tukio analodaiwa kulitenda Novemba Mosi, 2020 akiwa nyumbani kwake.Katika kesi hiyo, Giggs pia anatuhumiwa kuwa kati ya Agosti 2017 hadi Novemba 2020 amekuwa na […]

The post Kesi ya Giggs kusikilizwa kwa siku 10 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kocha wa zamani wa timu ya Wales, Ryan Giggs amefika mahakamani leo akikabiliwa na kesi ya kumdhalilisha, kumshambulia na kumuumiza aliyekuwa mpenzi wake, Kate Greville na mdogo wake Emma Greville tukio analodaiwa kulitenda Novemba Mosi, 2020 akiwa nyumbani kwake.
Katika kesi hiyo, Giggs pia anatuhumiwa kuwa kati ya Agosti 2017 hadi Novemba 2020 amekuwa na tabia zisizo za kiungwana dhidi ya Kate na tayari amekana kuhusika na tuhuma hizo wakati shauri hilo likitarajiwa kusikilizwa kwa siku 10 mfululizo katika Mahakama ya Manchester.
Giggs ambaye pia ni mchezaji nyota wa zamani wa Man Utd, licha ya kukana kuhusika na tuhuma hizo lakini aliamua kujiuzulu nafasi ya ukocha katika timu ya Wales kwa kile alichodai kwamba asingependa kuona kesi yake inaathiri kwa namna yoyote ile maandalizi ya timu ya Taifa ya Wales kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Doha, Qatar, Novemba mwaka huu.
Tangu akamatwe kwa tuhuma hizo Novemba, 2020, Giggs alijiweka kando na timu ya Wales ambapo mechi yake ya mwisho akiwa na timu hiyo ilikuwa ni dhidi ya Bulgaria katika Nations League, mechi ambayo Wales ilitoka na ushindi wa bao 1-0.
Awali kesi ya Giggs ilikuwa ianze kusikilizwa mwezi Januari lakini ilichelewa sababu ikiwa ni janga la Corona ambapo mahakama ililazimika kubadili taratibu zake za uendeshaji kesi na kulazimika kuahirisha baadhi ya kesi.

The post Kesi ya Giggs kusikilizwa kwa siku 10 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/08/kesi-ya-giggs-kusikilizwa-kwa-siku-10/feed/ 0