Garnacho - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 08 Oct 2024 06:35:14 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Garnacho - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Goti lamtoa Garnacho kikosini Argentina https://www.greensports.co.tz/2024/10/08/goti-lamtoa-garnacho-kikosini-argentina/ https://www.greensports.co.tz/2024/10/08/goti-lamtoa-garnacho-kikosini-argentina/#respond Tue, 08 Oct 2024 06:35:12 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11994 Manchester, EnglandWinga wa Man United, Alejandro Garnacho amejitoa katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kinachojiandaa kwa mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2026 baada ya kuumia goti la mguu wa kushoto.Argentina katika mbio za kufuzu fainali hizo itakuwa na mechi mbili dhidi ya Venezuela Alhamisi na dhidi ya Bolivia Jumanne ijayo, mechi ambazo, […]

The post Goti lamtoa Garnacho kikosini Argentina first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Winga wa Man United, Alejandro Garnacho amejitoa katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kinachojiandaa kwa mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2026 baada ya kuumia goti la mguu wa kushoto.
Argentina katika mbio za kufuzu fainali hizo itakuwa na mechi mbili dhidi ya Venezuela Alhamisi na dhidi ya Bolivia Jumanne ijayo, mechi ambazo, Garnacho mmoja wa wachezaji muhimu wa timu hiyo atazikosa.
Garnacho, 20, Jumapili alicheza kwa dakika 90 mechi ya Man United dhidi ya Aston Villa kwenye Ligi Kuu England, mechi ambayo ilimalizika kwa sare ya bila kufungana ingawa ilibainika kuwa hali yake haikuwa nzuri.
Tayari Argentina imetambua kuumia kwa mchezaji huyo na nafasi yake amepewa nyota wa Leicester City, Facundo Buonanotte.
Argentina katika mbio za kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026 inashika usukani katika kundi lake kwa tofauti ya pointi mbili ikifuatiwa na Colombia inayoshika nafasi ya pili.
Garnacho hadi sasa ameichezea timu ya taifa ya Argentina mara saba na alitoa mchango mkubwa kwa timu hiyo kubeba taji la Copa America kwa mara ya 16 katika fainali zilizopigwa nchini Marekani Juni mwaka huu.

The post Goti lamtoa Garnacho kikosini Argentina first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/10/08/goti-lamtoa-garnacho-kikosini-argentina/feed/ 0
Ten Hag ataja sababu ya kumuacha Garnacho https://www.greensports.co.tz/2023/09/27/ten-hag-ataja-sababu-ya-kumuacha-garnacho/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/27/ten-hag-ataja-sababu-ya-kumuacha-garnacho/#respond Wed, 27 Sep 2023 12:44:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7858 Manchester, EnglandKocha wa Man United, Erik ten Hag amesema kwamba alimuweka kando, Alejandro Garnacho (pichani) baada ya mechi mbili za awali kwa kuwa kiwango cha mchezaji huyo hakikuwa juu kiasi cha kutosha.Garnacho alikuwa katika kikosi cha kwanza katika mechi dhidi ya Wolves na Tottenham zilizochezwa mwezi Agosti lakini aliachwa katika mechi tano kabla ya kurudi […]

The post Ten Hag ataja sababu ya kumuacha Garnacho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kocha wa Man United, Erik ten Hag amesema kwamba alimuweka kando, Alejandro Garnacho (pichani) baada ya mechi mbili za awali kwa kuwa kiwango cha mchezaji huyo hakikuwa juu kiasi cha kutosha.
Garnacho alikuwa katika kikosi cha kwanza katika mechi dhidi ya Wolves na Tottenham zilizochezwa mwezi Agosti lakini aliachwa katika mechi tano kabla ya kurudi kikosi cha kwanza jana Jumanne dhidi ya Crystal Palace katika mechi ya Carabao ambayo Man United ilishinda kwa mabao 3-0.
“Utaona katika mechi za mwanzo za msimu tulikuwa tukimpanga lakini mchango wake haukuwa mkubwa kiasi cha kutosha,” alisema Ten Hag akimzungumzia mchezaji huyo ambaye ndio kwanza ana miaka 19.
“Unajua wakati wote hiyo ni hatari kwenye mechi pale anapokuwa hachezi vizuri, ni lazima ajifunze anapofanya kazi yake katika kukaba, ana nafasi yake na wakati wote atakuwa tishio kwa sababu ana sifa zote,” alisema.

“Nafikiri ni jambo la kawaida kwa mchezaji wa umri wake bado ana nafasi ya kuwa bora, kila mtu anampenda, mashabiki wanampenda, timu inampenda, na mimi nampenda lakini ni lazima tumtake awe mwenye kujitoa kwa ajili ya timu,” alisema Ten Hag.


Baada ya kumpa nafasi Garnacho, Ten Hag ameendelea kumfungia mlango, Jodan Sancho ambaye ameondolewa kikosi cha kwanza baada ya kutofautiana na kocha huyo ingawa amewapa nafasi Mason Mount, Raphaƫl Varane na Harry Maguire.

The post Ten Hag ataja sababu ya kumuacha Garnacho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/27/ten-hag-ataja-sababu-ya-kumuacha-garnacho/feed/ 0