Fred Mbuna - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 28 Mar 2023 19:30:55 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Fred Mbuna - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Nkoma afutiwa mkataba Yanga Princess https://www.greensports.co.tz/2023/03/28/nkoma-afutiwa-mkataba-yanga-princess/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/28/nkoma-afutiwa-mkataba-yanga-princess/#respond Tue, 28 Mar 2023 12:40:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5618 Na mwandishi wetuUongozi wa Yanga umemteua Fred Mbuna (pichani juu) kuwa kocha mkuu wa timu ya wanawake ya Yanga Princess na kuvunja mkataba na Sebastian Nkoma aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo.Taarifa za kuvunjwa mkataba na kocha huo iliyotolewa leo Jumanne kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo ilieleza kuwa hatua hiyo imefikiwa baada […]

The post Nkoma afutiwa mkataba Yanga Princess first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Uongozi wa Yanga umemteua Fred Mbuna (pichani juu) kuwa kocha mkuu wa timu ya wanawake ya Yanga Princess na kuvunja mkataba na Sebastian Nkoma aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo.
Taarifa za kuvunjwa mkataba na kocha huo iliyotolewa leo Jumanne kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo ilieleza kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya makubaliano ya pande zote mbili.
“Uongozi wa Yanga unamshukuru kocha Sebastian kwa kazi yake kipindi chote alichokuwa akiifundisha timu yetu ya wanawake, kwa sasa benchi la ufundi la Yanga Princess litakuwa chini ya kocha Fredy Mbuna mpaka msimu huu utakapomalizika,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Nkoma aliyetua Yanga mwanzoni mwa msimu huu baada ya kuachana na Simba Queens, anaondoka akiiacha Princess ikiwa nafasi ya nne, ikiwa imeshinda mechi sita, sare nne na kufungwa mechi mbili.
Timu hiyo imekusanya jumla ya pointi 22 wakiwa na tofauti ya pointi saba dhidi ya vinara Fountain Gate Princess wenye pointi 29.
Mbuna ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu ya Yanga, kabla ya hapo alikuwa ndiye msaidizi wa Nkoma katika timu hiyo.

The post Nkoma afutiwa mkataba Yanga Princess first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/28/nkoma-afutiwa-mkataba-yanga-princess/feed/ 0