Fountain Gate FC - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 28 Sep 2025 21:02:19 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Fountain Gate FC - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Simba yaicharaza Fountain Gate 3-0 https://www.greensports.co.tz/2025/09/26/simba-yaicharaza-fountain-gate-3-0/ https://www.greensports.co.tz/2025/09/26/simba-yaicharaza-fountain-gate-3-0/#respond Fri, 26 Sep 2025 14:41:21 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13955 Na mwandishi wetuSimba imeanza na ushindi mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu NBC kwa kuipa kichapo cha mabao 3-0 Fountain Gate FC mechi iliyopigwa Alhamisi hii Septemba 25, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.Washindi walianza kusaka bao la mapema na juhudi hizo kuzaa matunda dakika ya tano ya mchezo huo kwa bao […]

The post Simba yaicharaza Fountain Gate 3-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba imeanza na ushindi mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu NBC kwa kuipa kichapo cha mabao 3-0 Fountain Gate FC mechi iliyopigwa Alhamisi hii Septemba 25, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Washindi walianza kusaka bao la mapema na juhudi hizo kuzaa matunda dakika ya tano ya mchezo huo kwa bao lililofungwa na Rushine De Reuck akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona iliyochongwa na Jean Ahoua.
Dakika 10 kabla ya timu kwenda mapumziko, Simba waliandika bao la pili mfungaji akiwa Ahoua ambaye alifunga bao hilo kwa pasi ya Yusuf Kagoma na kuzifanya timu ziende mapumziko Simba wakiwa mbele kwa mabao mawili.
Ahous mmoja wa wachezaji walioonesha ubora katika kikosi cha Simba msimu uliopita, pia ndiye aliyetangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
Kipindi cha pili mambo yalizidi kuwa magumu kwa Fountain Gate ambao walipachikwa bao la tatu mfungaji akiwa Jonathan Sowah aliyefunga bao hilo dakika ya 57 kwa pasi ya Elly Mpanzu.
Simba ingeweza kupata mabao mengi katika mechi hiyo kama si ubutu wa safu ya ushambuliaji kwani licha ya kutengeneza nafasi kadhaa lakini umaliziaji ilikuwa tatizo.
Baada ya ushindi huo, Simba sasa inasubiri kucheza mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United ya Botswana, mechi itakayocheza Jumapili ijayo, Septemba 28, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Katika mechi ya kwanza, Simba ikiwa ugenini ilitoka na ushindi wa bao 1-0, mechi ambayo ilikuwa ya mwisho kwa aliyekuwa kocha wao, Fadlu Davids ambaye ameachana na Simba na kujiunga na Raja Casablanca ya Morocco.

The post Simba yaicharaza Fountain Gate 3-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/09/26/simba-yaicharaza-fountain-gate-3-0/feed/ 0
Yanga yaicharaza Fountain Gate mabao 4-0 https://www.greensports.co.tz/2025/04/21/yanga-yaicharaza-fountain-gate-mabao-4-0/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/21/yanga-yaicharaza-fountain-gate-mabao-4-0/#respond Mon, 21 Apr 2025 18:56:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13296 Na mwandishi wetuYanga imeipa kipigo cha mabao 4-0 Fountain Gate FC katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa leo Jumatatu Aprili 21, 2025 kwenye Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa mjini Manyara.Yanga ilianza kuandika bao la kwanza katika dakika ya 38 lililofungwa na Clement Mzize ambaye aliyatumia vizuri makosa ya kipa wa Fountain Gate, John Noble kuipatia […]

The post Yanga yaicharaza Fountain Gate mabao 4-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Yanga imeipa kipigo cha mabao 4-0 Fountain Gate FC katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa leo Jumatatu Aprili 21, 2025 kwenye Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa mjini Manyara.
Yanga ilianza kuandika bao la kwanza katika dakika ya 38 lililofungwa na Clement Mzize ambaye aliyatumia vizuri makosa ya kipa wa Fountain Gate, John Noble kuipatia Yanga bao.
Bao la pili la Yanga lilifungwa na Stephane Aziz Ki ambaye kama ilivyo kwa Mzize naye aliyatumia makosa ya kipa Noble aliyejichanganya wakati akiokoa mpira ulioelekezwa langoni mwake badala yake akamrudishia mfungaji.
Kipindi cha pili kiliendelea kuwa kigumu kwa Fountain Gate baada ya kupachikwa bao la tatu mfungaji akiwa Mzize katika dakika ya 69 akiitumia pasi ya Jonathan Ikangalombo.
Mzize ambaye pia aliibuka mchezaji bora wa mechi hiyo, bao hilo lina maana kubwa kwake kwani sasa amefikisha mabao 13 katika ligi hivyo kuwa kinara akifuatiwa na Jean Ahoua wa Simba mwenye mabao 12 sawa na Prince Dube wa Yanga.
Clatous Chama alikamilisha bao la nne kwa Yanga katika dakika ya 89 akifunga kwa mpira wa adhabu iliyotolewa baada ya Mtenje Albano kumchezea rafu Mzize nje kidogo ya eneo la penalti.
Ushindi huo unaifanya Yanga kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 70 katika mechi 26 ikiiacha Simba nafasi ya pili ikiwa na pointi 57 katika mechi 22.

The post Yanga yaicharaza Fountain Gate mabao 4-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/21/yanga-yaicharaza-fountain-gate-mabao-4-0/feed/ 0
Simba yakwama kuishusha Yanga kileleni https://www.greensports.co.tz/2025/02/06/simba-yakwama-kuishusha-yanga-kileleni/ https://www.greensports.co.tz/2025/02/06/simba-yakwama-kuishusha-yanga-kileleni/#respond Thu, 06 Feb 2025 19:26:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12986 Na mwandishi wetuMatarajio ya Simba kuiengua Yanga kileleni kwa msimamo wa Ligi Kuu NBC yamekwama leo Alhamisi, Februari 6, 2025 baada ya timu hiyo kutoka sare ya bao 1-1 na Fountain Gate FC.Simba ikiwa ugenini Manyara kwenye Uwanja wa Kwaraa imeshindwa kufanya kilichotarajiwa na mashabiki wake na kuambulia pointi moja inayowafanya wabaki nafasi ya pili.Mashabiki […]

The post Simba yakwama kuishusha Yanga kileleni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Matarajio ya Simba kuiengua Yanga kileleni kwa msimamo wa Ligi Kuu NBC yamekwama leo Alhamisi, Februari 6, 2025 baada ya timu hiyo kutoka sare ya bao 1-1 na Fountain Gate FC.
Simba ikiwa ugenini Manyara kwenye Uwanja wa Kwaraa imeshindwa kufanya kilichotarajiwa na mashabiki wake na kuambulia pointi moja inayowafanya wabaki nafasi ya pili.
Mashabiki wa Simba walikuwa na matarajio makubwa kwa timu yao kupata ushindi mwingine wa kuwapa pointi tatu ambazo zingewatoa Yanga kileleni kwa kuwazidi kwa pointi moja.
Matokeo hata hivyo yamekuwa tofauti na Simba inabaki nafasi ya pili na pointi 44 wakati mahasimu wao Yanga ambao ndio mabingwa watetezi wa ligi hiyo wakijinafasi kileleni na pointi zao 45.
Simba walipambana kusaka bao la mapema lakini ukuta wa Fountain Gate ulikuwa mgumu na haikushangaza kwa timu hiyo kupata bao lao katika dakika ya 57, mfungaji akiwa Leonel Ateba kwa pasi ya Ladack Chasambi.
Bao hilo lilianzia kwa mpira wa adhabu uliopigwa kwa haraka na Jean Ahoua na kumkuta Chasambi aliyetoa pasi ya bao jambo ambalo liliwakera wachezaji wa Ken Gold ambao walimlaumu mwamuzi Abel William wakionekana kutoridhishwa kwa namna Ahoua alivyopiga mpira kwa haraka.
Mambo hata hivyo yaliwaharibikia Simba baada ya Chasambi aliyetoa pasi ya bao kujifunga dakika ya 76 wakati akimpa pasi ya nyuma kipa wake Musa Camara lakini akakosea hesabu na mpira kujaa wavuni.
Juhudi za Simba kusaka bao la pili hazikufanikiwa licha ya wenyeji Fountain Gate kubaki 10 uwanjani katika dakika za lala salama baada ya kipa wao, Noble John kupewa kadi ya pili ya njano na kulazimika kutoka nje.
Katika kuhakikisha lango lao linapata ulinzi, Fountain Gate waliamua kumfanya mchezaji wa ndani Hashim Omar kuwa kipa katika dakika zilizobaki lakini Simba hawakuweza kupata bao la pili licha ya kulisaka kwa nguvu nyingi.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo zilizochezwa leo, Dodoma Jiji ililala kwa bao 1-0 mbele ya Pamba FC wakati Prisons iliichapa Mashujaa mabao 2-1 na Azam FC ikailaza KMC mabao 2-0.

The post Simba yakwama kuishusha Yanga kileleni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/02/06/simba-yakwama-kuishusha-yanga-kileleni/feed/ 0
Yanga yaipiga mkono Fountain Gate https://www.greensports.co.tz/2024/12/30/yanga-yaipiga-mkono-fountain-gate/ https://www.greensports.co.tz/2024/12/30/yanga-yaipiga-mkono-fountain-gate/#respond Sun, 29 Dec 2024 22:44:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12535 Na mwandishi wetuYanga imeendelea kutoa dozi kubwa katika Ligi Kuu NBC baada ya kuitandika Fountain Gate FC mabao 5-0 au mkono katika mechi iliyopigwa Jumapili hii Desemba 29, 2024 kwenye dimba la KMC, Dar es Salaam.Dozi hiyo ambayo ni ya tatu mfululizo imesababisha timu hiyo kulivunja benchi zima la ufundi kuanzia kocha mkuu Mohamed Muya […]

The post Yanga yaipiga mkono Fountain Gate first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga imeendelea kutoa dozi kubwa katika Ligi Kuu NBC baada ya kuitandika Fountain Gate FC mabao 5-0 au mkono katika mechi iliyopigwa Jumapili hii Desemba 29, 2024 kwenye dimba la KMC, Dar es Salaam.
Dozi hiyo ambayo ni ya tatu mfululizo imesababisha timu hiyo kulivunja benchi zima la ufundi kuanzia kocha mkuu Mohamed Muya na wasaidizi wake wote.
Kabla ya ushindi huo, Yanga ilitoa dozi nyingine mbili kubwa kwenye mechi za ligi hiyo dhidi ya Dodoma Jiji na Tanzania Prisons ambazo kila moja ililala kwa mabao 4-0.
Yanga ilianza kuandika bao la kwanza dakika ya 16 mfungaji akiwa Pacome Zouzoua ambaye aliitumia vizuri pasi ya Shadrack Boka ambaye naye aliinasa pasi ya Mudathir Yahya.
Mudathir aliiandikia Yanga bao la pili dakika ya 40 kwa mpira uliotokana na kona ya Aziz Ki na kumkuta Prince Dube aliyeurudisha kwa Clement Mzize ambaye naye alimpasia kabla ya kutua miguuni kwa mfungaji.
Katika dakika ya 45 juhudi za Aziz Ki aliyeuwahi mpira ulioonekana kama hauna mwenyewe na kumpasia Mzize aliyempasia Pacome ambaye aliiandiki Yanga bao la tatu.
Dakika nane baada ya kuanza kipindi cha pili, Yanga iliandika bao la nne lililotokana na shuti la Pacome ambaye alitangazwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
Pacome alifumua shuti lililomshinda kipa wa Fountain Gate, John Nobo na kugonga mwamba wa juu kabla ya kurudi uwanjani na beki Jackson Shija kujifunga wakati akiokoa.
Zikiwa zimebakia dakika tatu kabla ya mpira kumalizika, Clement Mzize alihitimisha karamu ya mabao ya Yanga kwa kuandika bao la tano akiitumia pasi ya Salum Aboubakar ‘Sure Boy’.
Kwa ushindi huo Yanga imezidi kuwasogelea vinara wa ligi hiyo Simba baada ya kufikisha pointi 39 ikiwa nafasi ya pili katika mechi 15 sawa na Simba yenye pointi 40.
Wakati Yanga wakifurahia kuisogelea Simba hali ni mbaya kwa Fountain Gate ambao baada ya kipigo hicho walitoa taarifa ya kulivunja benchi zima la ufundi kuanzia kocha mkuu.

The post Yanga yaipiga mkono Fountain Gate first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/12/30/yanga-yaipiga-mkono-fountain-gate/feed/ 0