Fifa - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 15 Mar 2025 18:59:49 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Fifa - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Trump ahoji nafasi ya Marekani kubeba Kombe la Dunia https://www.greensports.co.tz/2025/03/09/trump-ahoji-nafasi-ya-marekani-kubeba-kombe-la-dunia/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/09/trump-ahoji-nafasi-ya-marekani-kubeba-kombe-la-dunia/#respond Sun, 09 Mar 2025 10:59:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13116 New York, MarekaniRais wa Fifa, Gianni Infantino amekutana na Rais wa Marekani, Donald Trump katika Ikulu ya Marekani na kuzungumzia mipango ya fainali za Kombe la Dunia 2026 huku Trump akihoji kama Marekani itabeba taji la michuano hiyo.Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ijumaa hii kwenye Ikulu ya White House, Trump inadaiwa alimuuliza Infantino kama Marekani itaweza […]

The post Trump ahoji nafasi ya Marekani kubeba Kombe la Dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Rais wa Fifa, Gianni Infantino amekutana na Rais wa Marekani, Donald Trump katika Ikulu ya Marekani na kuzungumzia mipango ya fainali za Kombe la Dunia 2026 huku Trump akihoji kama Marekani itabeba taji la michuano hiyo.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ijumaa hii kwenye Ikulu ya White House, Trump inadaiwa alimuuliza Infantino kama Marekani itaweza kushinda Kombe la Dunia na Infantino akaonesha kuwa jambo hilo linawezekana.
Sambamba na fainali za Kombe la Dunia 2026, Marekani itakuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia kwa Klabu ambazo zitafanyika baadaye mwaka huu.
Awali baada ya Trump kumuuliza Infantino nchi ambazo zinaweza kushinda Kombe la Dunia, Infantino akazitaJa na ndipo Trump alipomuuliza kuhusu Marekani ambayo haikuwa kwenye orodha ya awali ya Infantino.
“Brazil, Argentina, England, Hispania, Ujerumani,” alizitaja Infantino na ndipo Trump alipohoji iwapo Marekani inaweza kuishangaza dunia na kubeba taji hilo.
Katika ufafanuzi wa hoja hiyo, Infantino alimwambia rais huyo wa 47 wa Marekani kwamba nchi yake inaweza kubeba taji hilo kwa msaada wa mashabiki na hata timu yao ni moja ya timu bora duniani.
“Kwa hiyo uwezekano upo?” Alihoji zaidi Trump na Infantino akamjibu hapo hapo, “Hakika nafasi hiyo ipo.”
Trump pia alimuahidi Infantino kwamba ataunda kikosi kazi kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2026 ambazo safari hii zinafanyika Marekani ya Kusini kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1994.
Marekani itakuwa mwenyeji wa fainali hizo ikishirikiana na nchi za Canada na Mexico ingawa nchi hizo kwa sasa zipo katika mzozo unaohusisha mambo ya kodi baada ya Trump kutaka bidhaa za nchi hizo majirani zake zitozwe kodi.
Trump hata hivyo anaamini mzozo wa mataifa hayo kuhusu masuala ya kodi utazifanya fainali hizo ziwe na hamasa zaidi.
Katika historia ya fainali za Kombe la Dunia, Marekani ina rekodi ya kufikia hatua ya nusu fainali mwaka 1930 katika fainali za kwanza katika historia ya michuano hiyo na baada ya hapo Marekani pia ilifikia hatua ya robo fainali mwaka 2002.

The post Trump ahoji nafasi ya Marekani kubeba Kombe la Dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/09/trump-ahoji-nafasi-ya-marekani-kubeba-kombe-la-dunia/feed/ 0
Fifa yazifungia Pakistan, Congo https://www.greensports.co.tz/2025/02/07/fifa-yazifungia-pakistan-congo/ https://www.greensports.co.tz/2025/02/07/fifa-yazifungia-pakistan-congo/#respond Fri, 07 Feb 2025 19:55:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12991 Zurich, SwitzerlandShirikisho la Soka Kimataifa (Fifa) limetangaza kuyafungia kushiriki mashindano ya soka ya kimataifa mashirikisho ya soka ya nchi za Pakistan na Congo Brazaville.Taarifa ya Fifa iliyopatikana Alhamisi hii ilieleza kuwa Shirikisho la Soka Congo Brazzaville (Fecofoot) limefungiwa kwa kile kinachodaiwa kuwa shughuli za uendeshaji soka zimekuwa zikiingiliwa na makundi mengine.Kwa mujibu wa taarifa hiyo, […]

The post Fifa yazifungia Pakistan, Congo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Zurich, Switzerland
Shirikisho la Soka Kimataifa (Fifa) limetangaza kuyafungia kushiriki mashindano ya soka ya kimataifa mashirikisho ya soka ya nchi za Pakistan na Congo Brazaville.
Taarifa ya Fifa iliyopatikana Alhamisi hii ilieleza kuwa Shirikisho la Soka Congo Brazzaville (Fecofoot) limefungiwa kwa kile kinachodaiwa kuwa shughuli za uendeshaji soka zimekuwa zikiingiliwa na makundi mengine.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uamuzi huo wa Fifa umefikiwa baada ya kuwashirikisha viongozi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) waliokwenda Congo kwa ajili ya suala hilo.
Uamuzi wa kuifungia Congo utasitishwa pale baadhi ya hatua zitakapochukuliwa ikiwamo uongozi kukabidhiwa majukumu ya usimamizi wa makao makuu ya shirikisho hilo.
Kwa upande wa Pakistan, shirikisho la soka nchini humo yaani PFF, nalo limefungiwa baada ya kutoifanyia mabadiliko katiba ya shirikisho hilo ili katiba hiyo itoe nafasi ya kufanyika kwa uchaguzi huru na wa kidemokrasia.
Hii si mara ya kwanza kwa Fifa kuifungia Pakistan, iliwahi kufanya hivyo mwaka 2017 na 2021 sababu ikiwa hiyo hiyo ya masuala ya soka kuingiliwa na makundi mengine ingawa adhabu ya mwisho ilifutwa Juni 2022 baada ya kuundwa kwa tume ya usuluhishi ya PFF.
Kwa adhabu hiyo nchi za Pakistan na Congo hazitoshiriki mashindano yoyote ya kimataifa ya soka yanayotambuliwa au kusimamiwa na Fifa na washirika wake.

The post Fifa yazifungia Pakistan, Congo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/02/07/fifa-yazifungia-pakistan-congo/feed/ 0
TFF yawanyooshea kidole mawakala https://www.greensports.co.tz/2024/12/04/tff-yawanyooshea-kidole-mawakala/ https://www.greensports.co.tz/2024/12/04/tff-yawanyooshea-kidole-mawakala/#respond Wed, 04 Dec 2024 06:36:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12324 Na mwandishi wetuShirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa angalizo kwa mawakala wa soka nchini na kubainisha kuwa wanaotambulika ni wale tu wenye leseni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).Taarifa ya TFF iliyopatikana Jumanne hii na kusainiwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa shirikisho hilo, Cliford Ndimbo (pichani) ilitoa tahadhari kuwa mbele ya kamati zake […]

The post TFF yawanyooshea kidole mawakala first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa angalizo kwa mawakala wa soka nchini na kubainisha kuwa wanaotambulika ni wale tu wenye leseni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Taarifa ya TFF iliyopatikana Jumanne hii na kusainiwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa shirikisho hilo, Cliford Ndimbo (pichani) ilitoa tahadhari kuwa mbele ya kamati zake haitotambua uwakilishi wowote wa wakala asiye na leseni.
“TFF haitotambua uwakilishi wowote kwa mchezaji ikiwamo uhamisho na mashauri mengineyo kwa wakala ambaye hana leseni ya Fifa,” ilifafanua taarifa hiyo.
Ndimbo ameibainisha kuwa kwa mujibu wa kanuni za Fifa ni wakala wa shirikisho hilo pekee ambaye anaweza kufanya shughuli za uwakala katika mchezo wa soka.
Tarifa hiyo pia imewataka wanaotaka kufanya shughuli za uwakala kuhakikisha wanafanya mtihani wa uwakala na kufaulu ili wapewe leseni na Fifa. Mtihani wa uwakala wa Fifa hufanyika mara mbili kwa mwaka.
TFF pia imetoa onyo kwa yeyote anayefanya shughuli za uwakala katika soka bila ya kuwa na leseni kuwa shirikisho hilo halitosita kupeleka taarifa za mtu huyo Fifa ili achukuliwe hatua.
Hadi sasa Tanzania ina mawakala wa soka saba tu wanaotambuliwa na Fifa ambao ni Ismail Hassan, Nassir Mjandari, Latifa Idd Pagal, Eliya Samwel Rioba, Benjamin Masige, Erick Mavike na Hadji Shaaban Omar.

The post TFF yawanyooshea kidole mawakala first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/12/04/tff-yawanyooshea-kidole-mawakala/feed/ 0
Klabu Ulaya kuipandisha Fifa kortini https://www.greensports.co.tz/2024/07/24/klabu-ulaya-kuipandisha-fifa-kortini/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/24/klabu-ulaya-kuipandisha-fifa-kortini/#respond Wed, 24 Jul 2024 06:42:23 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11664 London, EnglandKlabu kubwa za soka barani Ulaya kwa kushirikiana na umoja wa wachezaji duniani, wanajipanga kuushitaki uongozi wa Fifa kwa madai ya kutumia vibaya mamlaka yake katika usimamizi wa soka.Mpango huo unashirikisha ligi 39 pamoja na klabu za soka zaidi ya 1,000 kutoka nchi 30 ambazo kwa pamoja zimefikia uamuzi huo kwa kile wanachodai kuwa […]

The post Klabu Ulaya kuipandisha Fifa kortini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
TOPSHOT – FIFA president Gianni Infantino poses with Al Rihla, the official match ball before a press conference during the 72th FIFA Congress in the Qatari capital Doha, on March 31, 2022. – The countdown towards the most controversial World Cup in history really begins tomorrow as the draw for Qatar 2022 takes place in Doha 2022, less than eight months befor the start of the tournament itself. (Photo by FRANCK FIFE / AFP)

London, England
Klabu kubwa za soka barani Ulaya kwa kushirikiana na umoja wa wachezaji duniani, wanajipanga kuushitaki uongozi wa Fifa kwa madai ya kutumia vibaya mamlaka yake katika usimamizi wa soka.
Mpango huo unashirikisha ligi 39 pamoja na klabu za soka zaidi ya 1,000 kutoka nchi 30 ambazo kwa pamoja zimefikia uamuzi huo kwa kile wanachodai kuwa ni kulinda ustawi wa wachezaji.
Kiini cha uamuzi huo inadaiwa kuwa ni malalamiko yanayoendelea kutolewa na mamlaka za ligi na umoja wa wachezaji kutokana na ongezeko la idadi ya mashindano kwenye kalenda ya soka na jinsi jambo hilo linavyowaathiri wachezaji.
Taarifa ya Chama cha Wanasoka Profesheno (Fifpro) ilieleza kuwa kalenda ya soka kimataifa kwa sasa imevuka mipaka, haina mustakabali mzuri kwa ligi za taifa na hatari kwa afya za wachezaji.

“Uamuzi wa Fifa katika miaka iliyopita umeendelea kunufaisha mashindano na kuangalia faida za kibiashara na kupuuza wajibu wake kama bodi ya usimamizi na kuathiri mikakati ya kiuchumi ya ligi za taifa na ustawi wa wachezaji,” ilifafanua taarifa ya Fifpro.


Taarifa hiyo pia iliwalaumu mabosi wa Fifa kwa kushikilia msimamo wao wa kukataa kuzihusisha mamlaka za ligi za taifa na umoja wa wachezaji katika taratibu zake za kufanya maamuzi.
Fifa hata hivyo ilijibu madai hayo kwa kuzituhumu baadhi ya ligi kwa unafiki na kusisitiza kwamba kalenda ya Fifa hupitishwa na baraza la shirikisho hilo ambalo linahusisha wajumbe kutoka kila nchi zikiwamo nchi za Ulaya.
Uamuzi wa kuifikisha Fifa mahakamani unatajwa kuwa ni mpango wa pili wenye lengo la kutikisa mamlaka za shirikisho hilo baada ya ule wa kwanza wa baadhi ya klabu barani Ulaya kutaka kuanzisha Super Ligi kufeli.
Rais wa Fifa, Gianni Infantino alinukuliwa akilalamikia uamuzi wa klabu za Ulaya kutaka kuanzisha Super Ligi kwa lengo la kujitenga na Fifa kuwa ni mkakati ambao haukuwa na nia njema na mendeleo ya soka.

The post Klabu Ulaya kuipandisha Fifa kortini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/24/klabu-ulaya-kuipandisha-fifa-kortini/feed/ 0
Tanzania yashindwa kupanda Fifa https://www.greensports.co.tz/2023/12/01/tanzania-yashindwa-kupanda-fifa/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/01/tanzania-yashindwa-kupanda-fifa/#respond Fri, 01 Dec 2023 19:32:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8706 Na mwandishi wetuTanzania imeendelea kusalia kwenye nafasi ya 121 katika viwango vya ubora wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kwa mwezi Novemba.Katika mwezi huo, Tanzania ilicheza michezo miwili ya kimataifa ambapo ilishinda dhidi ya Niger kwa bao 1-0 kabla ya kufungwa na Morocco mabao 2-0, zote zikiwa ni mechi za kuwania kufuzu fainali za […]

The post Tanzania yashindwa kupanda Fifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Tanzania imeendelea kusalia kwenye nafasi ya 121 katika viwango vya ubora wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kwa mwezi Novemba.
Katika mwezi huo, Tanzania ilicheza michezo miwili ya kimataifa ambapo ilishinda dhidi ya Niger kwa bao 1-0 kabla ya kufungwa na Morocco mabao 2-0, zote zikiwa ni mechi za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026.
Kwa mujibu wa mtandao rasmi wa Fifa uliotoa viwango hivyo vipya, Tanzania imeendelea kusalia katika nafasi hiyo iliyoishikilia tangu mwezi Oktoba, mwaka huu mara ya mwisho kutolewa viwango hivyo vya Fifa.
Kwa Ukanda wa Afrika Mashariki, Jamhuri ya Kidemokdasi ya Congo ni ya 67 ikishuka nafasi mbili, Uganda imeshika nafasi ya 92 nayo pia ikiendelea kuporomoka kwa nafasi mbili wakati Kenya iking’ang’ana katika nafasi ya 110.
Sudan yenyewe imepanda mpaka namba 128 kutoka nafasi ya 130, Rwanda imetoka nafasi ya 140 mpaka 133 na Burundi imetoka namba 142 na kushika namba 139 huku Ethiopia ikishuka kwa nafasi moja ikiangukia nafasi ya 144 na Sudan Kusini ni ya 166 ikipanda kwa nafasi moja.
Kwa Afrika, Morocco imeendelea kuwa kinara ikishika nafasi ya 13 ikifuatiwa na Senegal nafasi ya 20, Tunisia ikipanda mpaka namba 28 kutoka namba 32, Algeria ya 30, Misri ya 33, Nigeria ya 42 wakati Cameroon ya 46 na Ivory Coast ni ya 50.
Kidunia, Argentina inashika nafasi ya kwanza, ikifuatiwa na Ufaransa na England imeshika nafasi ya tatu na kuitoa Brazil ambayo imeangukia nafasi ya tano. Ubelgiji ni ya nne na Uholanzi ni ya sita ikifuatiwa na, Ureno, Hispania, Italia na Croatia inayohitimisha 10 bora.

The post Tanzania yashindwa kupanda Fifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/01/tanzania-yashindwa-kupanda-fifa/feed/ 0
Tanzania yapanda Fifa https://www.greensports.co.tz/2023/10/26/tanzania-yapanda-fifa/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/26/tanzania-yapanda-fifa/#respond Thu, 26 Oct 2023 19:50:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8236 Na mwandishi wetuTanzania imepanda nafasi moja kutoka nafasi ya 122 hadi ya 121 kwenye viwango vya ubora wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kwa mwezi Oktoba vilivyotolewa leo Alhamisi.Huenda kufanya vizuri kwa timu ya taifa kumeipa nafasi hiyo, kwani ilitoka kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Sudan hivi karibuni katika mchezo wa kimataifa […]

The post Tanzania yapanda Fifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Tanzania imepanda nafasi moja kutoka nafasi ya 122 hadi ya 121 kwenye viwango vya ubora wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kwa mwezi Oktoba vilivyotolewa leo Alhamisi.
Huenda kufanya vizuri kwa timu ya taifa kumeipa nafasi hiyo, kwani ilitoka kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Sudan hivi karibuni katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa nchini Saudi Arabia.
Pia, Tanzania ni miongoni mwa mataifa 24 yaliyofuzu kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) itakayofanyika nchini Ivory Coast, mwakani.
Katika ukanda wa Afrika Mashariki, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ni ya 65, Uganda licha ya kutofuzu Afcon inashika nafasi ya 90 ikishuka nafasi moja, ikifuatiwa na Kenya ya 110, Sudan ni ya 130, Rwanda ya 140 na Burundi ya 142.
Ethiopia ya 143 wakati Sudan Kusini ni ya 167, Djibouti imepanda nafasi moja mpaka 189 na Somalia ikishuka nafasi mbili ikidondokea nafasi ya 196.
Kwa Afrika kinara ni Morocco ambayo ni ya 13 duniani, Senegal ya 20, Tunisia imeshuka nafasi tatu na kuangukia ya 32, Algeria ya 33, Misri ya 35, Nigeria ya 40, Cameroon ya 43 na Mali imeshika nafasi ya 47.
Kidunia, Argentina inaongoza ikifuatiwa na Ufaransa, Brazil, England, Ubelgiji, Ureno, Uholanzi, Hispania, Italia na Croatia.

The post Tanzania yapanda Fifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/26/tanzania-yapanda-fifa/feed/ 0
Fifa yaanza uchunguzi bosi aliyembusu mchezaji https://www.greensports.co.tz/2023/08/25/fifa-yaanza-uchunguzi-bosi-aliyembusu-mchezaji/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/25/fifa-yaanza-uchunguzi-bosi-aliyembusu-mchezaji/#respond Fri, 25 Aug 2023 06:31:15 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7530 Zurich, UswisiShirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limetangaza kuanza uchunguzi kuhusu kitendo cha Rais wa Shirikisho la Soka Hispania (REEF), Luis Rubiales kumpiga busu mdomoni mshambuliaji wa timu hiyo, Jenni Hermoso.Jumapili iliyopita, Rubiales alimpiga busu la mdomoni mshambuliaji huyo wakati wachezaji na viongozi wa Hispania wakifurahia ushindi baada ya kuilaza England bao 1-0 na kubeba […]

The post Fifa yaanza uchunguzi bosi aliyembusu mchezaji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Zurich, Uswisi
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limetangaza kuanza uchunguzi kuhusu kitendo cha Rais wa Shirikisho la Soka Hispania (REEF), Luis Rubiales kumpiga busu mdomoni mshambuliaji wa timu hiyo, Jenni Hermoso.
Jumapili iliyopita, Rubiales alimpiga busu la mdomoni mshambuliaji huyo wakati wachezaji na viongozi wa Hispania wakifurahia ushindi baada ya kuilaza England bao 1-0 na kubeba Kombe la Dunia la Wanawake (WWC).
Taarifa ya Fifa ilieleza kuwa shirikisho hilo linaloongoza soka duniani kote litaangalia kama alichofanya Rubiales kinakwenda kinyume na sheria ya 13 ya Fifa inayohusu kanuni za nidhamu na matukio yasiyofaa na yanayokwenda kinyume na fair play.
“Fifa inasisitiza juu ya kujituma bila kusita katika kuheshimu hadhi ya kila mtu na kwa nguvu zote inalaani tabia zozote zinazokwenda kinyume na jambo hilo,” ilieleza taarifa ya Fifa kwa vyombo vya habari.
Taarifa hiyo pia ilifafanua kuwa hatua za kinidhamu zinaweza kuchukuliwa dhidi ya mtu yeyote anayekwenda kinyume na maadili.

“Kumdhalilisha mtu kwa nama yoyote hasa kwa kutumia ishara au hata lugha au kufanya jambo ambalo litauweka mchezo wa soka au Fifa katika mazingira ya ukosefu wa heshima, hatua za kinidhamu zitachukuliwa,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.


Itakachofanya Fifa ni kuchunguza ili kubaini kama alichokifanya Rubiales kinakwenda kinyume na sheria namba 13 inayohusu maadili na kwenda kinyume na mienendo iliyo sahihi na kukiuka kanuni ya fair play.
Rubiales akionekana mwingi wa furaha alimpiga Jenni busu ‘zito’ mdomoni mara baada ya kukabidhiwa medali, ingawa mshambuliaji huyo aliwahi kumtetea bosi huyo wa soka akisema ni tukio lililochangiwa na hali ya furaha lakini pia alisema hakulipenda.
Baadaye Rubiales naye alitaka waliolipa tafsiri mbaya tukio hilo wapuuzwe kwani lilichangiwa na yeye kuwa mwenye furaha isiyo kifani ingawa aliibuka mara ya pili na kuomba msamaha.
Viongozi kadhaa nchini Hispania wakiongowa na Waziri Mkuu, Pedro Sanchez wamelaani tukio hilo wakisisitiza kuwa kitendo cha Rubiales kuomba msamaha hakitoshi huku wengine wakimtaka ajiuzulu.
Wakati huo huo Umoja wa Wachezaji wa Profesheno umeingilia kati ukidai kwamba alichofanya Rubiales hakikubaliki na hakiwezi kuachwa hivi hivi ni lazima hatua zichukuliwe.

The post Fifa yaanza uchunguzi bosi aliyembusu mchezaji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/25/fifa-yaanza-uchunguzi-bosi-aliyembusu-mchezaji/feed/ 0
Kocha Zambia adaiwa kumpapasa mchezaji kifuani https://www.greensports.co.tz/2023/08/04/kocha-zambia-adaiwa-kumpapasa-mchezaji-kifuani/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/04/kocha-zambia-adaiwa-kumpapasa-mchezaji-kifuani/#respond Fri, 04 Aug 2023 09:34:05 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7231 Sydney, AustraliaShirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) linachunguza tuhuma zinazomkabili kocha wa timu ya wanawake ya Zambia, Bruce Mwape (pichani) anayedaiwa kumpapasa kifuani mchezaji wa timu hiyo bila ridhaa yake.Taarifa ya Fifa ilithibitisha kupokea tuhuma hizo ambapo Mwape anadaiwa kumfanyia kitendo hicho mchezaji wake Julai 29 wakati timu ya taifa ya Zambia ikiwa mazoezini nchini […]

The post Kocha Zambia adaiwa kumpapasa mchezaji kifuani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Sydney, Australia
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) linachunguza tuhuma zinazomkabili kocha wa timu ya wanawake ya Zambia, Bruce Mwape (pichani) anayedaiwa kumpapasa kifuani mchezaji wa timu hiyo bila ridhaa yake.
Taarifa ya Fifa ilithibitisha kupokea tuhuma hizo ambapo Mwape anadaiwa kumfanyia kitendo hicho mchezaji wake Julai 29 wakati timu ya taifa ya Zambia ikiwa mazoezini nchini New Zealand.
Wakati Fifa ikieleza kupokea tuhuma hizo na kuzifanyia kazi, Chama cha Soka Zambia (FAZ) kimedai kutopokea malalamiko yoyote dhidi ya kocha huyo aliyeiwezesha Zambia kufuzu fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini New Zealand na Australia.
Mwape anadaiwa kufanya kosa hilo wakati wa mazoezi siku mbili kabla ya mechi ya mwisho ya Zambia ya hatua ya makundi dhidi ya Costa Rica, mechi ambayo Zambia ilishinda kwa mabao 3-1 ikiwa ni ushindi wa kwanza wa timu hiyo kwenye fainali hizo.
Taarifa ya msemaji wa Fifa ilieleza kuwa shirikisho hilo linachukulia kwa nguvu zote tuhuma za ukosefu wa maadili na imeweka wazi taratibu za kufuatwa kwa mtu yeyote katika soka ambaye anataka kuripoti tuhuma hizo.
Katika hatua nyingine, taarifa ya FAZ hata hivyo ilieleza kwamba mazoezi yote ya timu hiyo ambayo tayari imerejea nyumbani, yalirekodiwa na hakuna picha zinazoonesha tukio lolote baya.
FAZ pia walifafanua kwamba timu ya waandishi wa Fifa walikuwa wakirekodi mazoezi ya timu hiyo maarufu Copper Queens.
Kocha Mwape ambaye alikabidhiwa jukumu la kuinoa timu hiyo mwaka 2018, hii si mara ya kwanza kujikuta katika kashfa hiyo, mwaka jana mitandao ya kijamii ilimtaja ikimhusisha na kashfa za kuwafanyia wachezaji wake vitendo vya udhalilishaji kijinsia.
Mara baada ya kuibuka kwa tuhuma hizo FAZ walidai kutopokea rasmi tuhuma zozote dhidi ya Mwape ingawa iliahidi kufanya uchunguzi kama kutakuwa na ushahidi.
Kabla ya Zambia kutolewa kwenye fainali za Kombe la Dunia, Mwape aliulizwa kuhusu tuhuma hizo lakini alikana na aliwahi kuvunja mkutano na waandishi wa habari kwa sababu ya kuulizwa swali hilo zaidi ya mara moja.
Mmoja wa wachezaji wa Copper Queens alinukuliwa akidai kwamba Mwape akimhitaji mchezaji wake kimapenzi, mchezaji huyo hana haki ya kusema hapana.

The post Kocha Zambia adaiwa kumpapasa mchezaji kifuani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/04/kocha-zambia-adaiwa-kumpapasa-mchezaji-kifuani/feed/ 0
Infantino ainadi Super Ligi https://www.greensports.co.tz/2023/07/14/infantino-ainadi-super-ligi/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/14/infantino-ainadi-super-ligi/#respond Fri, 14 Jul 2023 08:02:04 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6960 Abidjan, Ivory CoastRais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) Gianni Infantino amesema ligi ya soka ya timu nane bora za Afrika maarufu Super League ambayo timu ya Simba itashiriki, itaanza Oktoba 20 mwaka huu.Infantino (pichani) ametoa kauli hiyo jana Alhamisi kwenye mkutano mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) uliofanyika mjini Abidjan, Ivory Coast […]

The post Infantino ainadi Super Ligi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Abidjan, Ivory Coast
Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) Gianni Infantino amesema ligi ya soka ya timu nane bora za Afrika maarufu Super League ambayo timu ya Simba itashiriki, itaanza Oktoba 20 mwaka huu.
Infantino (pichani) ametoa kauli hiyo jana Alhamisi kwenye mkutano mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) uliofanyika mjini Abidjan, Ivory Coast na kuongeza kuwa mpango uliopo ni kuiboresha zaidi ligi hiyo.
Mpango wa awali ulikuwa ni kushirikisha jumla ya timu 24 za Afrika lakini baadaye makubaliano yalifikiwa na idadi ya timu kupunguzwa hadi kufikia nane.
“Ligi itahusisha timu nane bora na baadaye itafuatiwa na mpango mkubwa zaidi, ni lazima tuwekeze kwenye klabu za soka za Afrika pamoja na timu za soka za Taifa,” alisema Infantino mbele ya wajumbe wa mkutano huo.
“Ni jukumu na wajibu wetu na kwa kushirikiana wote kwa pamoja tukiwa kama timu tutafanikiwa katika hilo,” aliongeza Infantino.
Kwa mujibu wa CAF, michuano ya Super Ligi itafanyika sambamba na Ligi ya Mabingwa Afrika na kwamba Super Ligi haijaanzishwa kuwa mbadala wa Ligi ya Mabingwa Afrika kama inavyodhaniwa
Kwa upande wake Rais wa CAF, Patrice Motsepe akiizungumzia ligi hiyo alisema kuna ulazima wa kuliboresha soka la Afrika na kulipa nguvu na mvuto zaidi duniani na ligi hiyo imeanzishwa ili kufikia malengo hayo.
Motsepe pia aliwataka viongozi wa mashirikisho ya soka Afrika pamoja na serikali za Afrika kuhakikisha zinawekeza zaidi kwenye mchezo wa soka.

“Tuna imani kubwa kwamba mafanikio tunayoyapata na vipaji vilivyopo Afrika matokeo yanaweza kuwa Afrika kushinda Kombe la Dunia, lakini lazima tutumie fedha kuwafundisha makocha, kufungua akademi na kuhakikisha klabu za soka zinakuwa na rasilimali za kutosha,” alisema Motsepe.


Ukiacha Simba ya Tanzania, timu nyingine zinazotajwa kushiriki ligi hiyo ni Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Petro Atletico (Angola), Al Ahly (Misri), Wydad Casablanca (Morocco), TP Mazembe (DR Congo), Esperence (Tunisia) na Horoya (Guinea).

The post Infantino ainadi Super Ligi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/14/infantino-ainadi-super-ligi/feed/ 0
Fifa yaifungia Al Nassr kusajili https://www.greensports.co.tz/2023/07/13/fifa-yaifungia-al-nassr-kusajili/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/13/fifa-yaifungia-al-nassr-kusajili/#respond Thu, 13 Jul 2023 19:50:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6945 SwitzerlandKlabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia anayochezea Cristiano Ronaldo imepigwa marufuku na Fifa kusajili wachezaji hadi itakapoilipa Leicester City deni lililotokana na usajili wa aliyekuwa winga wa timu hiyo, Ahmed Mussa (pichani).Mwaka 2018, Leicester iliwauzia Al Nassr mchezaji huyo kutoka Nigeria lakini baadaye timu hizo mbili zikaingia katika mzozo wa malipo na ndipo Leicester […]

The post Fifa yaifungia Al Nassr kusajili first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Switzerland
Klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia anayochezea Cristiano Ronaldo imepigwa marufuku na Fifa kusajili wachezaji hadi itakapoilipa Leicester City deni lililotokana na usajili wa aliyekuwa winga wa timu hiyo, Ahmed Mussa (pichani).
Mwaka 2018, Leicester iliwauzia Al Nassr mchezaji huyo kutoka Nigeria lakini baadaye timu hizo mbili zikaingia katika mzozo wa malipo na ndipo Leicester ilipoamua kuwasilisha malalamiko yake Fifa ikidai ilipwe Dola 390,000.
“Adhabu hiyo itafutwa mara tu baada ya kulipwa kwa deni hilo na kuthibitishwa na upande wa mdai,” ilieleza kwa kifupi taarifa ya Fifa.
Klabu ya Al Nassr imejipatia umaarufu dunia katika siku za hivi karibuni baada ya kumsajili winga wa zamani wa Real Madrid na Man United, Cristiano Ronaldo.
Mbali na Ronaldo, Al Nassr pia hivi karibuni imekamilisha usajili wa nyota wa Croastia, Marcelo Brozovic huku kukiwa na habari pia ipo katika mkakati mzito wa kumsajili kwa pesa ndefu nyota wa Chelsea, Hakim Ziyech.
Klabu hiyo hata hivyo haijasema lolote kuhusu deni hilo ingawa ni ukweli kwamba mwaka 2018 ilimsajili winga huyo wa Nigeria kutoka Leicester.

The post Fifa yaifungia Al Nassr kusajili first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/13/fifa-yaifungia-al-nassr-kusajili/feed/ 0